Uzalendo wa Kitanzania
JF-Expert Member
- Mar 8, 2020
- 4,252
- 9,311
Kheri anayekunywa pombe asubuhi kwani anaingiza mapato serikalini kuliko yale makundi ya vijana machokoraa wanaozurula nao kila siku ili wawashangilie na kukata viuno kwenye mikutano yao.Wadau hamjamboni nyote?
#HABARI Mkuu wa Mkoa wa Singida Halima Dendego amepiga marufuku wananchi wa mkoa huo kuanza kunywa pombe asubuhi badala ya kufanya shughuli za maendeleo na za kiuchumi hali ambayo inaweza kusababisha kudumaa kwa shughuli za kiuchumi kwa wananchi...
Kulima bila ya kuongelea ni shughuli.Unapigaje masanga asubuhi ,ni mnazi badala ya chaiii!
Na kingine. Nchi haiongozwi kwa matamko ya majukwaani. Nchi ina sheria. Bar zinajulikana zinafunguliwa saa ngapi. Maduka ya kuuza pombe nayo hivyo hivyo. Badala wajenge mifumo wao wanakazania kupanda majukwaani kugeuka sheria.Mtu mwenye shughuli zake hawezi kuacha kuzifanya akaenda kunywa pombe,ukiona mtu anakunywa pombe asubuhi basi ujue keshamaliza kazi zake au hana kazi ya kufanya na hela anayo hivyo viongozi waache kujifanya manyapala kwenye maisha ya watu.
Wao wadhibiti watumishi wao wasiingie kazini wakiwa na kilevi na atakayekwenda kinyume achukuliwe hatua za kinidhamu lakini sio kupangia kila mtu kwa sababu kila mtu ana njia zake za kupata pesa na yeyote atakayebainika ni mhalifu hatua za kisheria zifuate mkondo wake vinginevyo kila mtu ashinde mechi zake.