Marufuku kumwangalia mwanamke kwa sekunde 14

Marufuku kumwangalia mwanamke kwa sekunde 14

Amavubi

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2010
Posts
30,156
Reaction score
13,267
_90818220_indiastare.jpg

Ni hatia kumwangalia mwanamke kwa sekunde 14 India
Watumiaji wa mitandao ya kijamii wamelalamika kuhusu tamko la afisa mmoja aliyesema kuwa ni kinyume na sheria kumuangalia mwanamke kwa zaidi ya sekunde 14 katika jimbo la Kerala nchini India.

Hakuna sheria kama hiyo nchini India lakini afisa huyo Rishiraj Singh ambaye ni kamshna amesema kuwa kumuangalia mwanamke kwa mda mrefu kunaweza kukutia mashakani.

Watu mitandaoni wanauliza itakuwaje iwapo mwanamume atafunga jicho mara moja na kulifungua akimwangalia mwanamke wakiongezea kuwa huenda bei ya miwani ya kujilinda dhidi ya jua ikapanda.

Lakini wengine wanasema kuwa bwana Signh amezua hoja nzuri sana kuhusu usalama wa wanawake.

''Mtu anaweza kushtakiwa kwa kumuangalia mwanamke kwa sekunde 14'',alisema bwana Singh katika eneo la Kochi siku ya Jumamosi.

Tamko hilo lililofanywa katika kanda ya video limesambaa katika jimbo hilo na kuzua ucheshi miongoni mwa mitandao ya kijamii.
 
Ha ha ha
wakwanza kushtakiwa niko hapa na polisi akiwa mwanamke ,hakimu akiwa mwanamke,magereza pia duh! tutaponea wapi..
Wabantu na hii misambwanda, mkiambiwa msiiangalie mtateswa sana
 
wanawake wenyewe wanapenda sana tuwaangalie......hii sheria inawanyima haki yao ya msingi.
 
Ama kweli wanalengo la kuwatia nguvuni wanaume wengi duh
 
Ni nani atakuwa anaangalia wakati nikimwangalia huyo mwanamke kwa sekunde 14?Ushahidi wake mgumu sana otherwise kila kona zifungwe cctv camera za kunasa footage.Sheria zingine bana.
 
Unamwangalia huku unahesabu, ikifika sekunde ya kumi unaangalia pembeni, unarudi tena unamwangalia mpk sekunde ya kumi..
Unarudia hivyo hivyo
HAPO imekaa njema
 
sawa
Ni nani atakuwa anaangalia wakati nikimwangalia huyo mwanamke kwa sekunde 14?Ushahidi wake mgumu sana otherwise kila kona zifungwe cctv camera za kunasa footage.Sheria zingine bana.
na ule ushahidi wa kukonyeza naona ile sheria iliishia hewani
 
Back
Top Bottom