Mtumiabusara
JF-Expert Member
- Nov 18, 2009
- 473
- 40
MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati (EWURA), imepiga marufuku matumizi ya chupa za plastiki (vidumu) kuhifadhi au kubebea mafuta jamii ya petroli, kwa kuwa zina uwezo mkubwa wa kulipuka.
Pia imewataka wauzaji wa nishati hiyo katika vituo vyote vya mafuta nchini, kukataa kuhudumia wateja watakaohitaji petroli bila kuwa na magari yao vituoni kama njia ya kuwaelimisha juu ya athari za matumizi ya chupa au vidumu hivyo
Source: Habari leo
Maoni yangu

- Sisi tunaotumia magenereta kwenye biashara zetu na majumbani tufanye nini?
- Sheria hii inataka kutuaminisha kwamba mwenye gari akiishiwa mafuta ghafla basi ni mzembe. Tuchukulie mazingira kwamba umebakiwa na mafuta kidogo kwenye gari, lakini yanatosha kufika sheli iliyo umbali wa kama KM 25, then unafika na gari yako kwenye sheli hiyo, unakuta mafuta wameishiwa au hawa operate. The next sheli ni KM 25 zingine, uliskume gari mpaka huko?