Common Folk
JF-Expert Member
- Nov 8, 2023
- 878
- 3,920
RANGO!
You hate death wapi weweeee.. watu wengi wanatekwa na kupotezwa kila uchwao, huumizwi. Mzee Kibao alitekwa na kuuwawa, hukusikitika. Uliishia kukejeli.
You hate death wakati ulizuia hoja ya utekaji kujadiliwa? Mdude ambaye alitekwa jimbo kwako, hujawahi hata kutoa pole. Unaumizwa na vifo vya watawala.
27.08.2024 ulipiga marufuku mjadala wa utekaji - hoja ambayo iliwasilishwa kwa dharura. Ulisema utekaji haiwezi kuwa hoja ya dharura kujadiliwa. Loh!
You hate death wakati huo unasema hakuna utekaji isipokuwa kuna matukio ya watu kutoonekana? Watu hawaonekani kwamba wanakwenda wapi?
Nduguyo anaamka anakwenda katika mapambano ya maisha, unaambiwa alipotea. Unangoja siku, wiki, miezi na hata miaka... Ni bora angekufa ukamzika.
Mamlaka zinajibu kwa kiburi. Spika anayeongoza baraza la uwakilishi wananchi anazuia wabunge wa mbogamboga wasijadili hoja muhimu ya utekaji.
19.09.2019 ukiwa na mbogamboga wenzako mlishiriki igizo la kuizika CHADEMA. Ulibeba jeneza lenye bendera ya CHADEMA na msalaba ukiwakejeli.
Hilo lilikuwa tusi kwa wakristo wanaotumia msalaba katika imani zao. Kwa kiburi tu, hukuwahi kuomba radhi popote pamoja na kwamba wakristo walilalamika.
Unachukia kifo? Unachukia vifo vya viongozi na watawala. Au ndiyo ndiyo tafsiri ya “maiti inatisha ikiwa inatoka ndani ya mlango wa nyumbani kwenu”.
RANGO, you don't hate death. You probably fear death. A fear of death is a sign that you fear your existence will be meaningless. Death absolutely terrifying.