Martial artist tukutane hapa

Mr. Purpose

JF-Expert Member
Nov 12, 2016
1,063
2,000
31Rn%2BclWKNL._AC_SY580_.jpg

Inafahamika kama Nunchaku. Wengine wa mtaani wanaiita Cheni (kila mmoja uipachika jina lake kwa namna yake). Tupeane experience na mbinu mbili tatu.

Uliijulia wapi na ulijifunzia/Fundishwa wapi na kwasasa uwezo wauonaje katika kutumia silaha.

Nianze, binafsi niliiona kwenye movie ya Bruce Lee kisha kuanza kuifuatilia hapo nikiwa dogo sana kisha nilipoanza mafunzo ya martial arts ndipo nilipojitengenezea yangu mwenyewe kwa kuchonga miti miwili urefu wastani kisha nilitumia mnyororo ule wa kufungua mbwa na kuunganisha kwa misumari na kupata hicho kifaa kisha nikaanza jifunza peke yangu kwa kuangalia movie, internet pia ilihusika kidogo

Nilijigonga mara kadhaa kichwani na maeneo mengine pia wakati wa kujifunza hivyo majeraha ya hii kitu niliyapata sana na vilivyo.

Baada ya kufika chuo niliamua kwenda kujichukulia yangu rasmi sasa maana nilikuwa mzoefu tayari. Mpaka sasa ukiacha mikono na miguu yangu, hii ni silaha ya pili ninyoikubali sana na ninayowez tumia muda wowote popote.

Pia matumizi ya fimbo, jambia na visu kwa wastani ila Nunchaku nikikamata nakuwa comfortable sana.

Tupe experience yako mdau. Una experience gani na Nunchaku??
31Rn%2BclWKNL._AC_SY580_.jpg
 
Aladeen04

JF-Expert Member
Sep 6, 2016
2,675
2,000
Aise niliwahi kujipiga nayo kisogoni hii kitu, na mpaka sasa sijapata mwalimu sahihi wote huwa zinatupiga hizi jamaa.
 
Mr. Purpose

JF-Expert Member
Nov 12, 2016
1,063
2,000
Aise niliwahi kujipiga nayo kisogoni hii kitu, na mpaka sasa sijapata mwalimu sahihi wote huwa zinatupiga hizi jamaa.
Mkuu hii kitu nina kovu lake kichwani hadi leo. Anza nayo taratibu kisha spidi na nguvu katika kuizungusha ongeza kadiri uwezo unavyokuwa. Usiikatie tamaa. You tube na vitabu vipo kibao maana najua ilivyo nadra kumpata au hata kumtambua anayeweza haya mambo, wapo ila mtaani tunajificha.
 
Aladeen04

JF-Expert Member
Sep 6, 2016
2,675
2,000
Mkuu hii kitu nina kovu lake kichwani hadi leo. Anza nayo taratibu kisha spidi na nguvu katika kuizungusha ongeza kadiri uwezo unavyokuwa. Usiikatie tamaa. You tube na vitabu vipo kibao maana najua ilivyo nadra kumpata au hata kumtambua anayeweza haya mambo, wapo ila mtaani tunajificha.
Kwa hiyo na wewe mkuu ulijifunzia vitabu tu?
 
BRN

JF-Expert Member
Nov 18, 2013
1,630
2,000
Hongera sana mkuu. Vp tunaweza pata experience yako kidogo mkuu na vijana wajifunze kitu kuhusu hiyo kitu
Ahsante..kwa kuanzia kuna mizunguko ya msingi saba,hapa namaanisha namna ya urushaji wa hiyo silaha na mizunguko hii ili upate mirusho sahihi lazima uizungushe kwenye mikono au mwilini/mgongoni. Ndio maana mnalalamika hapo kwa kupata makovu, jambo la msingi ni kuanza polepole na spidi utaipata tu vile ukianza kuzoe.
Kwa ujumla hivi vitu tunajifunza lakini matumizi yake kwenye mazingira ya kawaida ni nadra sana. Nadra kwa maana vile unavyofahamu haya mambo unakuwa na tabia na muonekano ambao tayari unakutengenezea kinga.
 
Umenena vema boss. Muonekano unabadilika na ukiwa mzoefu ni rahisi sana kuwatambua wanoielewa hii michezo. Jambo la kumshukuru Mungu kadiri unavyozoea na kuelewa sana haya mambo unajikuta mpole sana.
 
Mr. Purpose

JF-Expert Member
Nov 12, 2016
1,063
2,000
Kwa hiyo na wewe mkuu ulijifunzia vitabu tu?
Nilianzia kujifunza kupitia movie. Nilikuwa na mwalimu wa martial arts ila alikuwa anakaza sana mpaka baadhi ya techniques alikataa nifundisha mwanzoni akidai mpaka nifike level fulani, hivyo hata matumizi ya silaha hakunifundisha ndipo kuanza kujifunza mwenyewe kupitia movie.

Vitabu nimeanza kutumia baadae na vimenisaidia pia kuelewa theory na practical side ya hii kitu mpaka sasa nimeiweza sijawahi fundishwa na mtu yeyote matumizi ya silaha hii.
 
semper saratoga

JF-Expert Member
Aug 10, 2015
1,086
2,000
Ni nzuri sana mkuu na ukiizoea ni rahisi sana kutumia katika mapigano halisi. Kusimama na mtu zaidi ya mmoja ukiwa na nunchaku huwa ni jambo la kawaida. Ishu ni wakati wa kujifunza ngumu kuiweza bila kukugonga
Mkuu upande huu wa Mwenge mpaka mapinga kwa uzoefu wako kuna dojo makini wapi?
 
Mr. Purpose

JF-Expert Member
Nov 12, 2016
1,063
2,000
Lini mtapigana...?
Mkuu nikikutana na mtu anarusha na mimi narusha kwa dakika zaidi ya moja, hiyo ndio kupigana. Ila umekutana na mzembe ukamtandika kofi anakuangalia tu na matusi mengi kisha anaondoka hapo sijapigana. Mara ya mwisho kupigana ilikuwa 2014 mpaka leo sijakutana na wa kurushiana, ninaokutana nao wengi maneno mengi ila hawajui sanaa ya mapigano.

Mkuu mara ya mwisho wewe kupigan ilikuwa lini boss??
 
Mr. Purpose

JF-Expert Member
Nov 12, 2016
1,063
2,000
Mkuu upande huu wa Mwenge mpaka mapinga kwa uzoefu wako kuna dojo makini wapi?
Mkuu sina uzoefu sana maeneo hayo boss. Labda kama kuna wazoefu wanaweza kusaidia. Binafsi sijawahi ingia dojo maalum, nimejifunza street kwa miaka yote zaidi ya sita na sparring ndio huwa kipimo cha uwezo wangu so hata ishu ya mkanda na level kiutaratibu sizijui sana kivile.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom