Uzi maalumu wa kumpongeza Rais Samia kwa miaka miwili akiwa madarakani

Nyabukika

JF-Expert Member
Jun 15, 2022
1,402
942
Tukielekea kilele cha miaka miwili ya Rais Samia Suluhu Madarakani amefanikiwa kufungua mikutano ya hadhara kwa vyama vya upinzani maana walikua wakitamani kwa muda mrefu sana na watanzania tulijiandaa kusikia ajenda nyingi walizokua wameanda kwa zaidi ya miaka 5 lakini mambo yamekua tofauti kabisa

Sasa wapinzani hawana ajenda tena maana Rais Samia Suluhu amefanya maendeleo katika sekta zote hajaacha gepu la kuwapa wapinzani ajenda maana. Amefanisha kuboresha sekta ya elimu kupitia ujenzi wa madarasa na shule mpya pamoja na samani zake, Ameboresha miundombinu hadi vijijini ameanza kufanyia kazi katiba mpya, huduma za afya zimeboreshwa hadi vijijini, pia amefanikisha upatikanaji wa maji hadi vijijini.

Ndani ya miaka miwili ya Mama ameupiga mwingi kila sekta hadi wapinzani wanakosa ajenda wanabaki kulaumu bodaboda.
 
KUSHUKURU NI UUNGWANA, ASANTE MHE.RAIS SAMIA SULUHU HASSAN.

Amon Nguma

Tarehe 19 March 2023 tumetimiza miaka miwili ya uongozi wa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Tumefika miaka miwili kwa mafanikio makubwa na matumaini ni makubwa zaidi kwa siku za usoni.

Mafanikio ni makubwa yaliyopatikana katika miaka miwili, yafuatayo ni kwa uchache:

(1) Kulinda tunu ya amani, umoja na mshikamano. Katika kipindi chote Mhe. Rais ameonesha dhamira yake njema ya kulifanya taifa kuwa na amani na mshikamano ikiwa ni turufu ya maendeleo ya taifa lolote lile. Asante Mhe. Rais kwa kudumisha tunu za taifa letu.

(2) Kuendeleza na kuanzisha miradi mikubwa na ya kimkakati yenye tija katika taifa letu. Katika kipindi cha miaka miwili ya Mhe. Rais Samia, tumeona miradi mikubwa ikienda kwa kasi.

Mfano, mpaka sasa, bwawa la Nyerere (Stiglers) limekwisha jazwa maji, uzinduzi wa vipande vinne vya SGR (Makutupora-Tabora-Isaka-Mwanza-Kigoma), kukamilika kwa meli ya MV Mwanza, daraja la Tanzanite, uanzishwaji wa ujenzi wa bandari ya kisasa ya uvuvi-Kilwa ambayo itatumia bilioni 266.7, bandari hii itakayochochea shughuli uvuvi katika Bahari ya Hindi na kutoa ajira nyingi kwa wananchi, kukuza sekta ya anga kwa kujenga viwanja vya ndege ikiwemo cha kimataifa cha Msalato-Dodoma pamoja na viwanja vinavyojengwa kila mkoa sanjari na ununuzi wa ndege mpya tano zinazowasili mwaka huu nchini.

Kwa miradi michache hii kati ya mingi, shukrani Mhe. Rais Samia kwa uongozi unaogusa maisha ya Watanzania.

(3) Asante Mhe. Rais kwa kuifanya sekta ya afya na huduma kuwa za kisasa.

Tangu kuasisiwa kwa taifa letu ni katika kipindi hiki ambapo sekta ya afya imeshuhudia mapinduzi makubwa ya miundombinu na teknolojia ikiwemo - kuongeza vitanda vya ICU kutoka 258 vilivyokuwepo mpaka 1000, ukamilishaji wa hospitali ya rufaa ya kanda ya kusini, hospitali za rufaa katika mikoa ya Katavi, Geita, Mara, Songwe na Shinyanga zenye vifaa na mitambo ya kisasa, uzinduzi wa teknolojia ya kisasa ya upasuaji ubongo pasipo kufungua fuvu, ununuzi wa mitambo ya kisasa (X-Ray 62, CT-Scan 32, MRI 7, mashine za uchunguzi wa moyo 7 na fluoroscopy 2) lengo ni kuleta huduma karibu na wananchi kwa gharama nafuu ikilinganishwa na ilivyokuwa awali, ununuzi wa mitambo 19 ya kuzalisha hewa tiba (oksjeni) ambayo imesimikwa katika hospitali mbalimbali za mikoa na kanda, na ni serikali hii hii ambayo imeajiri watumishi wa kudumu zaidi ya 10000 katika kipindi kifupi ili wakatoe huduma kwetu wananchi. Asante Mhe. Rais Samia kwa kazi kubwa na nzuri kwenye sekta ya afya.

(4) Shukrani na hongera Mhe. Rais kwa kufanya mapinduzi ya kilimo.

Katika kipindi kifupi tumeona mabadiliko makubwa katika sekta ya kilimo kuanzia kwenye bajeti, bajeti ya mwaka huu zaidi ya bilioni 750 ikiwa ni kubwa zaidi kuliko zilizopita, uwezeshaji wa mbegu za kisasa kwa wakulima, ununuzi wa usafiri na vifaa kwa maafisa ugani kwa kilimo zaidi ya 7000, utolewaji wa mbolea ya ruzuku kwa wakulima, utafutaji wa masoko ya uhakika ya mazao ya wakulima, uanzishwaji wa mashamba (block farming) miradi ya umwagiliaji, pamoja na mradi mkubwa wa kilimo kwa vijana kupitia mradi wa (BBT) ambapo mafunzo yameshaanza na mashamba yameshaandaliwa. Shukrani na hongera Mhe. Rais kwa kufanya mapinduzi ya kilimo.

(5) Uendelezaji wa mahusiano ya kimataifa na diplomasia wa uchumi.

Katika kipindi kifupi Mhe. Rais ameonesha uwezo wake mkubwa wa kidiplomasia kwa kuendeleza na kuboresha zaidi mahusiano ya Tanzania na mataifa mengi, jambo ambalo limeendelea kufungua fursa katika taifa letu, ikiwemo masoko ya bidhaa za Tanzania, hususani mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi ambayo yameleta tija kubwa kwa wakulima, pamoja na kuvutia uwekezaji na utalii nchini, ambapo ajira nyingi zimezalishwa.

(6) Shukrani Mhe. Rais Samia kwa mambo mengi uliyolifanyia taifa letu, ikiwemo:
  • Kulinda haki za binadamu, demokrasia na utawala bora.
  • Kutangaza vivutio vya uwekezaji na utalii kupitia The Royal Tour.
  • Kutoa vibali vya ajira na kuajiri watumishi katika sekta ya umma pamoja na ajira nyingine kupitia uwekezaji na miradi.
  • Kuboresha huduma na miundombinu ya utoaji haki na usimamizi wa sheria kwa ujenzi wa mahakama katika maeneo mbalimbali nchini.
  • Kuinua sekta ya sanaa na michezo kwa uwezeshaji wa kisera, kifedha na wataalamu.
  • Ujenzi wa madarasa zaidi ya 20,000 katika kipindi cha miaka miwili.
  • Ukamilishaji wa Ikulu ya Chamwino pamoja na ujenzi wa mji wa serikali Dodoma.
  • Vita dhidi ya rushwa, ufisadi na uzembe.
Asante Mhe. Rais Samia kwa mengine mengi ambayo hayajaorodheshwa hapa.

Kushukuru na kupongeza pindi mtu anapotimiza wajibu wake kufanya kitu kizuri ama kuleta matokeo chanya ni uungwana. Na kwa uungwana huo, asante na hongera Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa mambo makubwa na mazuri uliyolifanyia taifa letu kama kiongozi mkuu wa nchi yetu.

Tulipo ni pazuri, na tunapokwenda matumaini ni makubwa zaidi chini ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

#MiwiliNaSamia
#KaziIendelee
Samia-Suluhu-Hassan-time100-2022.jpg
 
Habari Wadau..

Kwa wale wapenzi na mashabiki wa Rais Samia na good wishers Leo tunafurahi mafanikio yeko.



Hongera sana mheshimiwa Rais ,kazi umeiweza Kwa sekta zote tukisema tuorodheshe hapa jukwaani hapatatosha..

Ila Kwa kutumia mfano mmja tuu wa TRA inatosha kutoa reflection ya kinachoendelea kwenye sekta zote..

Wakati unaingia Madarakani ulikuta kiwango Cha Juu kabisa Cha Makusanyo ya TRA Kwa mwezi ilikuwa Tilioni 1.2 mwaka 2021 lakini Sasa mwaka 2023 ni shilingi Tilioni 2.01.Ongezeko la Bil.800 ndani ya miaka 2 tuu ya Uongozi wako..

Mapesa yoote hayo yamekuwa reflected kwenye utitiri wa miradi kwenye sekta zote Nchi nzima.

Tukifanya ulinganisho wa awamu ya 5 Kwa mfano,ilichukua miaka 5 kuongeza bil.400 yaani 2015/16 Makusanyo Kwa mwezi ylikuwa bil.800 na Mwaka 2020/21 yalikuwa Tilioni 1.2..

Wewe mheshimiwa Rais umetumia miaka 2 tuu kuongeza Bil.800 Kwa sababu ya sera nzuri za kuifungua Nchi na kuimarisha biashara na uwekezaji.Asiyeona haya ni mchawi..

Hongera Kwa Uongozi wako imara na wenye maono, na kazi iendelee 👇
20230319_081021.jpg
 
MHE. BAHATI NDINGO ASIFU UTENDAJI KAZI WA RAIS SAMIA, "RAIS SAMIA AMETENDEA HAKI SEKTA ZOTE"

Mbunge wa Jumuiya ya Wazazi Taifa Mhe. Bahati Ndingo katika Maadhimisho ya Miaka Miwili ya Kishindo ya Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkoa wa Mbeya.

Mhe. Bahati Ndingo amesifu na kumpongeza Rais Samia kwa utendaji mzuri kwa kila Sekta hususani Sekta ya Kilimo, kwani tangu tupate Uhuru, bajeti ya Kilimo imeongezeka mara mbili zaidi.

Katika Sekta ya Afya, Rais Samia ameendelea kuboresha Sekta ya Mama na Mtoto. Pia Sekta ya Elimu. Kila Sekta Mama ameitendea haki.

"Sisi kama wana Mbeya tunao wajibu wa kuyaongelea mambo makubwa ambayo anayafanya Mheshimiwa Rais wetu na Mwenyekiti wetu wa Chama Cha Mapinduzi" - Mhe. Bahati Ndingo.

Sherehe hizo zimefanyika katika Mkoa wa Mbeya na mgeni rasmi alikuwa ni Ndugu Mohamed Said Mohamed (DIMWA), Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar.
WhatsApp Image 2023-03-18 at 17.38.09.jpeg
WhatsApp Image 2023-03-18 at 17.39.39.jpeg
WhatsApp Image 2023-03-18 at 17.37.53.jpeg


#WatanzaniaTumekuelewa
#IlaniInatekelezwa
#KaziIendelee
 
Nampongeza sana mheshimiwa ila naomba waziri wa ujenzi atufafanulie ni kwanini fly over ya changombe ni mbaya sio kama ya kijazi imepindapinda haina usalama iko kama watoto wanajijengea kwa udongo tatizo ni mkandarasi au tatizo ni malipo au supervision hivi hili watu wote hawalioni

Hata liwango cha barabara ya mwendokasi iliyojengwa magomeni kimara iko na ubora wa hali ya juu kuliko hii ya karume mpka changombe shida iko nani katuloga waswahili. Value for money haionekani kabla hata mradi haujaisha
 
Tukielekea kilele cha miaka miwili ya Rais Samia Suluhu Madarakani amefanikiwa kufungua mikutano ya hadhara kwa vyama vya upinzani maana walikua wakitamani kwa muda mrefu sana na watanzania tulijiandaa kusikia ajenda nyingi walizokua wameanda kwa zaidi ya miaka 5 lakini mambo yamekua tofauti kabisa

Sasa wapinzani hawana ajenda tena maana Rais Samia Suluhu amefanya maendeleo katika sekta zote hajaacha gepu la kuwapa wapinzani ajenda maana. Amefanisha kuboresha sekta ya elimu kupitia ujenzi wa madarasa na shule mpya pamoja na samani zake, Ameboresha miundombinu hadi vijijini ameanza kufanyia kazi katiba mpya, huduma za afya zimeboreshwa hadi vijijini, pia amefanikisha upatikanaji wa maji hadi vijijini.

Ndani ya miaka miwili ya Mama ameupiga mwingi kila sekta hadi wapinzani wanakosa ajenda wanabaki kulaumu bodaboda.
Weka namba ya simu yako haraka hapa unateuliwa kuwa katibu wa ccm wa kijiji
 
Nampongeza sana mheshimiwa ila naomba waziri wa ujenzi atufafanulie ni kwanini fly over ya changombe ni mbaya sio kama ya kijazi imepindapinda haina usalama iko kama watoto wanajijengea kwa udongo tatizo ni mkandarasi au tatizo ni malipo au supervision hivi hili watu wote hawalioni

Hata liwango cha barabara ya mwendokasi iliyojengwa magomeni kimara iko na ubora wa hali ya juu kuliko hii ya karume mpka changombe shida iko nani katuloga waswahili. Value for money haionekani kabla hata mradi haujaisha
Kawaulize maccm wenzako
 
Hii picha kuna watu wakiitazama wanatamani dunia irudi nyuma.

Kufuatia uungwana wa viongozi wa cdm na ccm leo hii tumeanza kuona utangamano halisia ktk maisha yetu ya kila siku.

Jiwe alitaka watanzania tuishi kama wahutu na watusi kabla ya mwaka 1994.

Mungu mkubwa katuepusha hilo na sasa tunaishi kama ndugu wa familia moja.

Wana cdm wamejumuika na wana ccm kwenye shughuli za kitaifa bila kujali itikadi zao za siasa.

Itazameni hii picha mtaelewa nini nimemaanisha .
Screenshot_20230319-164418_Instagram.jpg
 
Nchi ilikuwa uchumi wa kati, mche wa sabuni ulikuwa 2,000 maharage yaliuzwa 1,200, unga wa mahindi uliuzwa 1000, nondo na bati .......
Msilete mapicha ya kulambishwa asali. RIP MAGUFULI
Wakati jiwe anaingia madarakani alikuta sukari kilo moja sh 1800 lkn akaipandisha hadi sh 3000 hiyo mbona husemi wewe sukuma gang?
 
Back
Top Bottom