Marry your friend

Marry your friend

Diwani

JF-Expert Member
Joined
Oct 25, 2014
Posts
2,903
Reaction score
3,140
Nimeona ni kazi kumbadili unaekutana nae kama mpenzi wako, kuwa rafiki yako, mapenzi yakiwafanya muwe marafiki kuna uwezekano mkubwa wa kutofanikisha mahusiano, kwa sababu urafiki ni kama msingi/mtaji wa mapenzi

Nimeona si kazi sana kumbadili rafiki/mshikaji/ wako kuwa mpenzi wako, urafiki ukiwafanya muwe wapenzi kuna uwezekano mkubwa sana wa kufanikisha mahusiano, kwa sababu urafiki ni kama msingi/mtaji wa mapenzi....

Nawasilisha
 
Maana yake mtakuwa mshajuana in and out rahisi kumsaidia mwenzako pale anapokuwa down kujua hapa anaigiza na hapa kweli kaumia. Si rahisi ndoa kuvunjika kama kabla ya kuanza mahusiano urafiki ulikuwa wa kushibana. Hata akija kukukwaza kama mke/ mume na hisia zikiisha juu yake, atabaki kuwa rafiki yako.

Japo marafiki nao hugombana na kuwa zaidi ya maadui.
 
Nakuunga mkono kwa 100% kwa sababu mkiwa marafiki bila mipango ya kuoana au kuwa wapenzi mnakuwa na muda wa kujuana vizuri. Hamuambiani uongo wala kufichana raarifa fulani kuhusu maisha yenu kwa sababu hakuna maslahu yoyote kufichana. Kwa mfano kama uliwahi kuzaa, huna kazi ya kudumu, au ukiwahi kuoelewa/kuoa mtawekana wazi kwa kuwa ni marafiki tu. Hata tabia zenu na hobbies yote mtayaweka wazi kwa matendo na maneno. Sasa mnapoamua kuamzisha uchumba na hatimaye mkaonana yaani ndoa yenu itadumu sana kwa sababu mnafahamiana vizuri ni rahisi kuvumiliana.
 
Belinda na Masanja wa CRDB!

Hawa wakioana na wakipata mtoto, huyo mtoto atakuwa chautundu on steroids!
 
Nakuunga mkono kwa 100% kwa sababu mkiwa marafiki bila mipango ya kuoana au kuwa wapenzi mnakuwa na muda wa kujuana vizuri. Hamuambiani uongo wala kufichana raarifa fulani kuhusu maisha yenu kwa sababu hakuna maslahu yoyote kufichana. Kwa mfano kama uliwahi kuzaa, huna kazi ya kudumu, au ukiwahi kuoelewa/kuoa mtawekana wazi kwa kuwa ni marafiki tu. Hata tabia zenu na hobbies yote mtayaweka wazi kwa matendo na maneno. Sasa mnapoamua kuamzisha uchumba na hatimaye mkaonana yaani ndoa yenu itadumu sana kwa sababu mnafahamiana vizuri ni rahisi kuvumiliana.
For sure
 
inategemea na msingi wenu mwanzo mmeuanzaje,

mnaweza mkaanza kama marafiki na msifikie kuwa na pendo lenye nguvu na mnaweza mkaanza kama wapenzi na mkafikia kuwa na pendo lenye nguvu.
But inaonekana kukiwa na urafiki kwanza foundation ya mapenzi yenu inakuwa tofali. Hii naipa nguvu zaidi
 
Back
Top Bottom