Marketing Strategy | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Marketing Strategy

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Anfaal, Mar 4, 2011.

 1. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #1
  Mar 4, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Unainua simu yako bila kujali upo nchi au nchi ya nje unaamua kumpigia jamaa yako aliopo TIGO wakati unasubiri muito wa simu, ghafla unasikia kwa kuchagua nyimbo bonyeza moja.
  Huu na mitindo mingine mibaya imekuwa ndio strategy ya tigo. Inakera saana kwa wale wapiga simu. Maana mie ndiye ninayepiga kisha naambiwa nibonyeze moja, wanajua natumia mtandao gani. Hii ni strategy inayochefua saana. Bahati mbaya wanasahau kuwa marketing advertisement should be attractive na iwe clear. Sina hakika kwa wale wasiofahamu kabisa kiswahili, huenda wakadhani ni voice mail. Hivi kweli huo ndio mwisho wa kufikiri? Hivi core business ya tigo ni hizo nyimbo au ni simu? Kuna haja ya kujipanga na kufanya mambo katika hali inayoonyesha kuwa watu wapo serious. Sina hakika kama upuuzi huu unapatikana maeneo mengine.
   
 2. Mutensa

  Mutensa JF-Expert Member

  #2
  Mar 4, 2011
  Joined: Feb 20, 2009
  Messages: 426
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Mkuu mimi suala zima la RBT (ring back tone), sijakubaliana nalo jinsi linavyoendeshwa kwenye makampuni yote ya simu nchini. Kwa mawazo yangu, mpiga simu ndiye anatakiwa kujichagulia wimbo ambao atakuwa anausikiliza wakati anapopiga simu. Sasa hawa ”wataalamu” wameset kiasi kuwa kila anayekupigia anasikiliza wimbo uliouchagua wewe na sio wanaoupenda wao. Watu wana vionjo tofauti, hivyo huwezi kujua kama unawaburudisha au kuwachosha wanaposikiliza ujumbe fulani.
   
 3. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #3
  Mar 5, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mtu anayepiga simu, hahitaji kutoshelezwa na mziki uitao kwenye simu. Anahitaji kuongea na muhusika wa upande wa pili maana ule uitao hata hauwezi kuitwa mziki zaidi ya kuwa ni kero. Wao kama wanaona hii biashara ya muziki inawalipa ni bora wawauzie hizo tune wenye simu ili wakipigwa wao ndio wasikie muito wa kimuziki na si kuhamisha kelele hizo kwa mpigaji ambaye anaona ni usumbufu. Hizi standard zetu sijui tunaokota wapi maana watu hawafikirii adha hii.
   
Loading...