Maridhiano escrow scandal?

KILLAKIJO

Member
Oct 12, 2014
90
95
Ni kufikia muafaka pande mbili kila moja kukubali kupoteza haki yake. UKAWA have agreed mafisad papa endelea ibia watz?
 

Mgibeon

JF-Expert Member
Aug 7, 2011
8,878
2,000
Ukimchunguza sana bata hutomla.... nimejifunza kujifikiria mimi kwanza na familia yangu bila kujali impact zake kwa jamii na taifa kwa ujumla.. there is no the so called patrionite in this poor country with rotten leadership.... forsake..!!!!
 

Kashishi

JF-Expert Member
Apr 11, 2010
1,103
2,000
Ukweli ni kuwa hakuna maazimio yeyote ya maana yalioafikiwa zaidi ya 'ujing*a na upumba*u' mtupu tu. Bunge zima ni kama limepoteza dira na mtazamo. Wabunge hawawezi kujenga umoja wala maafikiano na maazimio juu ya masuala ya 'wizi' ulio wazi namna ile. Wabunge wanachagua eti nani ni mwizi wa kumwajibisha na yupi ni mwizi wa kumwachia...that's not fair!

Cha kujiuliza ni kuwa hayo yote ile iweje au kwa faida ya nani?
 

GeniusBrain

JF-Expert Member
Nov 3, 2010
4,320
1,195
nawapongeza sana ZITTO , Kafulila na Ukawa kwa hatua waliyofikia katika kulimaliza sakata la escrow japo binafsi sijaridhika na maazimio kwakuwa bado naona yamewaacha huru mafisadi wote bila kujali ushahidi wa wazi wa wizi wao wa karne. kwangu mimi binafsi bongo imeandika historia ya kuwaacha huru majangili ya taifa hili na kubariki wizi uliokubuhu wa kodi za walalahoi. na nawaza kuwa sasa hakuna chombo kinachoweza kuwajibisha wezi hata wakamatwe red handed.na labda wanaowaza na wanaoendelea kuiba pesa ya umma sasa wataona kumbe poa tu kuiba mabilioni na hufanywi chochote! ni mtazamo tu!

Mbona unajipinga mwenyewe? Unawapongeza na huku unasema mafisadi wameachwa huru, yaonyesha ni jinsi gani hujui kuandika thread
 

tajirijasiri

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
2,823
2,000

Mbona unajipinga mwenyewe? Unawapongeza na huku unasema mafisadi wameachwa huru, yaonyesha ni jinsi gani hujui kuandika thread
Kwanza mtoa mada anajikanganya mwenyewe!! Kwanza hajui maazimio yaliyofikiwa!! Pili hajui anachokiandika kina mantiki IPI! Kwa kumsaidia maridhiano ya Upinzani na Serikali yamependekeza kwamba wooote walihusika wawajibishwe kwa kutenguliwa nyazifa zao za utumishi wa Umma wakiwemo Muhongo, Werema na Katibu Mkuu nishati na madini. Mabenki yaliyotakatisha Fedha za Escrow yatangazwe kama money laundering Banks, Bunge liwatengue Uongozi wa Kamati za Bunge akina Chenge na wenzake, Waliochota Fedha za Escrow PCCB, Polisi na Vyombo vya usalama viwachukulie hatua n.k. sasa hapo mtoa mada anataka nini tena!
ANA TEZI KWENYE UBONGO AU?
 

afwe

JF-Expert Member
Oct 29, 2010
4,085
2,000
Ukweli ni kuwa hakuna maazimio yeyote ya maana yalioafikiwa zaidi ya 'ujing*a na upumba*u' mtupu tu. Bunge zima ni kama limepoteza dira na mtazamo. Wabunge hawawezi kujenga umoja wala maafikiano na maazimio juu ya masuala ya 'wizi' ulio wazi namna ile. Wabunge wanachagua eti nani ni mwizi wa kumwajibisha na yupi ni mwizi wa kumwachia...that's not fair!

Cha kujiuliza ni kuwa hayo yote ile iweje au kwa faida ya nani?
Pole sana! Bila shaka inauma. Ungekuwa china nadhani wangehukumiwa kunyongwa kwa wizi ingependeza
 

Kashishi

JF-Expert Member
Apr 11, 2010
1,103
2,000
Ukweli ni kuwa hakuna maazimio yeyote ya maana yalioafikiwa zaidi ya 'ujing*a na upumba*u' mtupu tu. Bunge zima ni kama limepoteza dira na mtazamo. Wabunge hawawezi kujenga umoja wala maafikiano na maazimio juu ya masuala ya 'wizi' ulio wazi namna ile. Wabunge wanachagua eti nani ni mwizi wa kumwajibisha na yupi ni mwizi wa kumwachia...that's not fair! Cha kujiuliza ni kuwa hayo yote ile iweje au kwa faida ya nani?
Pole sana! Bila shaka inauma. Ungekuwa china nadhani wangehukumiwa kunyongwa kwa wizi ingependeza
Na hata sisi WaTanzania yatupasa sasa tufike mahali tukubali kubadilisha mfumo wetu kwa kuijenga 'China' yetu wenyewe. Kwani hata Wachina walifika mahali wakajitengeneza mfumo uliweza kuwatumikia vema kwa kuziba mianya ya kufanya ufisadi.
 

Columbus

JF-Expert Member
Nov 5, 2010
2,004
1,195
Na hata sisi WaTanzania yatupasa sasa tufike mahali tukubali kubadilisha mfumo wetu kwa kuijenga 'China' yetu wenyewe. Kwani hata Wachina walifika mahali wakajitengeneza mfumo uliweza kuwatumikia vema kwa kuziba mianya ya kufanya ufisadi.
Jamani mbona hii issue tumeshaelewa ugumu wa maamuzi uko wapi? Mnyika aliweka wazi pale Bungeni kuwa ofisa mmoja wa ikulu anayeitwa Rajab Gurumo ambaye ana uhusiano wa karibu na mkuu wa nchi naye kavuta fedha kwenye account ya Tegete Escrow kiasi cha Tsh. 800,000,000/=
Hii inauma sana kuona watanzania tunaongezewa bei ya umeme kila mara kumbe ni katika kuongeza fungu la wezi wachache serikalini,tusubiri muda utaamua!
 

anjo

JF-Expert Member
Jun 13, 2009
299
195
Mimi naona wametumia busara baada ya kuona viongozi wamegoma kujiuzuru.
Pili, hata kama Waziri Mkuu hakutajwa kwenye report ya mwisho hata yeye mwenyewe na sisi wote tunajua kuwa anatakiwa kuwajibika kwa kushindwa kulinda maslahi ya serikali yake na Umma. Anapaswa kujitafakari na kuchukua maamuzi ya kulinda heshima yake na ya nchi nzima.
Hata sisi ambao hatukuweza kwenda shule tunafahamu hicyo.
Mhe. Pinda, kwa heshima, tunaomba upishe kazi imekushinda.
 

Super Sub Steve

JF-Expert Member
Jul 9, 2011
15,238
2,000
Hivi inawezekanaje escrow iwe na maridhiano halafu katiba isiwe na maridhiano.Inawezekanaje chenge kutuandikia katiba? Hapa naona kuna umuhimu wa kusema No to katiba pendekezwa.kwenye escrow ni hela za wafadhili ndo zimefanya CCM wakubali maridhiano.
 

pixel

JF-Expert Member
Jun 22, 2012
1,631
1,500
Mleta mada unapotosha,hakuna maridhiano ya escrow scandal.maridhiano ni juu ya maazimio ya bunge.Mimi nawapongeza sana ukawa,laiti kama ukawa wangetoka nje au kukataa maridhiano,ccm wangewaacha wezi wote.kumbuka Nyie watanzania mmewachagua wabunge wengi wa ccm,sasa wewe rafiki yangu unaadhani ikipigwa kura kiongozi gani pale wa serikali angewajibishwa?UKAWA wakitoka nje mnawalaumu,nyie watanzania ndio tatizo.maneno mengi na lawama wakati hata kura huwa hampigi.kufeni tu.
 

Trueblue

Member
Nov 10, 2014
30
0
Unajua Hata Mimi Nimeshangaa. Tumeshasikia Hoja Na Mijadala Mingi Na Wala Maridhiano Hayakupewa Nafas.Leo Kuna Nini Hata Makinda Awe Considerate Kias Kile Au Ndo Mashinikizo Ya Wahisan.Nafkr Mlungula Ulitembea Kufikia Compromise.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom