Mariam Wangwe na Jukwaa la Wahariri | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mariam Wangwe na Jukwaa la Wahariri

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Paparazi Muwazi, Sep 26, 2008.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. P

  Paparazi Muwazi JF-Expert Member

  #1
  Sep 26, 2008
  Joined: Dec 23, 2007
  Messages: 310
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Niliwahi kuandika siku za nyuma mkakati mzima wa Rostam na ule wa Gachuma. Na katika kuandika nikamtaja na mtu mmoja aliyeitwa Mariam Chacha Wangwe. Niliacha kuendelea kuandika kwa heshima ya marehemu. Sasa mke wa marehemu amepanga kuendelea na ile mikakati niliyoieleza wakati ule. Ameanza kwa kujitokeza hadharani kusema kwamba anataka Spika wa Bunge aunde Tume ya kuchunguza kifo cha Wangwe. Amewajia juu CHADEMA kuwa wamekwepa kumzika marehemu mumewe na ameonyesha kuwa viongozi wa CHADEMA wanahusika na utata wa kifo hicho.

  Hata hivyo, mkakati mzima umepata upinzani ndani ya familia kwa kuwa mke mkubwa wa marehemu anamlaumu Mariam kuwa ni kimada aliyepora mume na mali zote za marehemu. Kwa sasa sinafanywa jitihada za hali ya juu na Gachuma kuwaweka sawa watoto wakubwa wa marehemu ambao wameanza kubaini Mariam anawatumia kwa minajili ya kuchota fedha wakati wao hawapi mgao wowote.

  Kwa upande mwingine, bwana Mengi amepata shinikizo toka kwa wamiliki wengine wa vyombo vya habari kupitia MOAT kuwa ahakikishe ripoti ya Jukwaa la Wahariri haitoki kabla ya uchaguzi Tarime kufanyika. Na Mwenyekiti wa jukwaa hilo Sakina Datoo naye ametishiwa kuwa akitoa ripoti hiyo tu, vyombo hivyo vya habari vitamtangaza kuwa anafanya kazi ya kuunga mkono CHADEMA ili ishinde uchaguzi tarime.

  Katika mazingira hayo, inaelekea ripoti hiyo yenye kueleza kama kulikuwa na mapanga au la na inayoeleza ukweli au uwongo kuhusu kupikwa kwa habari sasa itapaswa iwekwe kabatini. Kamba yangu ya kupata habari imekatika baada ya Ballile kuondolewa kuwa mhariri wa Rai. Sasa hajadiliani tena na wenzake na hivyo chanzo changu cha habari kimekwama kupata habari za upande wa pili. Na toka uzinduzi mpya wa magazeti yetu ufanyike mimi na wenzangu watatu wametuhamishia The African ambapo kwa kweli hakuna nyeti za maana.

  PM
   
 2. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #2
  Sep 26, 2008
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Asante PM
  Naona Bi Mariamu ameamua kutumiwa kama Mtikila, akina Sakina Datoo wanabidi waendelee na kazi zao bila kujali mashikizo ya kifisadi, maana wakiwasikiliza hao basi nao watakuwa impartial on the othe side as well

  Ushi
   
 3. C

  Chuma JF-Expert Member

  #3
  Sep 27, 2008
  Joined: Dec 25, 2006
  Messages: 1,330
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Naona ripoti ipo Kwa Sakina Datoo, kwa vyanzo vya Habari ni kuwa Ripoti itatoka baada ya Uchaguzi wa Tarime, ili isiathiri Uchaguzi...

  Sijui kama kuweka ripoti kapuni huku kutasaidia lolote huko tarime....?
   
 4. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #4
  Sep 27, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Huu ndio usanii; kama ripoti iko tayari iwekwe wazi watu waamue wenyewe. Hivi wanafikiri itaathiri uchaguzii kwa namna yoyote ile? Kwa kuificha na kutoiweka wazi lakini kuwaambia watu kuwa ipo tayari hawaoni kuwa tayari wanaathiri uchaguzi?

  Tarime, kuna vyama vitashindwa na kuna chama kitashinda. Hili halihitaji ripoti. Tatizo ni kuwa kwa kuficha ripoti inaoonekana wanataka chama fulani kishinde na vyama vishindishwe.

  Hivi walipounda hiyo tume yao walikuwa hawajui kuwa kuna uchaguzi? Si wangesubiri hadi baada ya uchaguzi kuunda tume hiyo?
   
 5. H

  Habarindiyohiyo JF-Expert Member

  #5
  Sep 27, 2008
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 263
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  ..........ndiyo hiyo

  Kwa nini tusianzishe Petition ya "Sakina Toa Ripoti"? Hawa wahariri wamezoea kuishinikiza serikali kuweka mambo wazi. Vipi ya kwao yanawashinda? Sasa wakikakaa nayo, chama kimoja kikashindwa kwa uwongo kuendelea kushamiri si watakuwa wamekubali kutumiwa na chama kingine dhidi ya chama hicho? Hapa kucheka na kulia zote ni kelele tu. Afadhali waamue kucheka. Afadhali waamue kusimamia ukweli tu, na kuutoa ukweli katika siku walizoahidi. Kwanza waliahidi wiki mbili tu. Sasa yameshapita mawiki mengi bado wanataka kuongeza mengine. Shame on you Kubenea, Jesse Kwayu and Sakina Datoo.
   
 6. NgomaNzito

  NgomaNzito JF-Expert Member

  #6
  Sep 27, 2008
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 561
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35

  Kubenea tunahitaji hii ripori kwenye gazeti lako next week otherwise credibility yako itapungua kwenye jamii yetu. Therefore u have one option to publish report au umeshaingizwa kwenye payrol ya mafisadi

  Pia tunahitaji maelezo toka kwa IGP iweje FFU walioko tarime wanapewa Chakula na maji na kuni toka kwa Peter Zacharia anyegombea udiwani?na Gachuma
   
 7. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #7
  Sep 27, 2008
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Nimemuona Mama Wangwe akiongea jana.Aliyo ongea ni ya msingi kabisa, kwamba iundwe kamati ya kuchunguza kiini cha kifo cha mume wake.Ni sawa kabisa, kwa vile sio siri kwamba kifo cha mume wa mama huyu, yaani Wangwe, kiligubikwa na utata mwingi.Hakuna mpaka sasa anayeelewa bayana kifo hiki kilisabishwa na nini,labda wauwaji wake, kama kifo hicho ni cha mauaji.Kwa hiyo ingekuwa busara kabisa kama serikali ingeunda tume kuchunguza kifo hicho.Hii ingeondoa hisia nyingi zilizojengeka kwenye jamii yetu kwa sasa kuhusiana na kifo hicho.Tumeona kamati nyinyi zikiundwa ambazo kimsingi hazikuwa na sabababu yeyote kwa vile hata matokeo ya uchunguzi wake yanafahamika.Hakuna siri kwamba hili lina utata wa kweli,serikali iliundie tume.
   
 8. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #8
  Sep 27, 2008
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Mkewe marehemu Wangwe atoboa (Gazeti la Majira)

  Na Gladness Mboma

   
 9. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #9
  Sep 27, 2008
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  PM,

  Huyo mama kafiwa na bwanake, hata angelikuwa mama mwingine yeyote kwenye hili atatapatapa tu katika kutafuta ukweli.

  Unless una uhakika sana na unayoyasema, naona kumshambulia huyu mama anayeomboleza kifo cha bwanake ni kumuonea bure.

  Binafsi naamini Wangwe alikufa kwa ajali, lakini pia simshangai huyu mama akiamini tofauti. Sio mke wa kwanza kuamini tofauti kwenye haya mambo ya vifo kwenye ajali. Hata pale Twin Tower kuna familia wanaamini tofauti mpaka leo. Kifo cha Diana, yule Fayed bado anaamini mtoto wake aliuawa na establishment.

  Hii dhana ya kufikiri kila mtu anatumiwa naona inatupeleka kwenye taifa la wajinga, taifa la watu wasio na mawazo yao binafsi.

  Nimesoma maelezo ya huyo mama kwenye gazeti la Majira na kwa kweli sioni cha ajabu alichosema zaidi ya kuhangaika kujaribu kutafuta ukweli. Si ajabu hata wewe ungelikuwa mtoto wake Wangwe ambaye maisha yako yote yamesimama baada ya kifo chake, ungeishia kuanza kutafuta mchawi hivyo hivyo.

  Huyu mama anatakiwa kuonewa huruma na sio kuingizwa kwenye vijembe vya siasa.
   
 10. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #10
  Sep 27, 2008
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Watu tunapenda sana siasa kila kitu siasa tuu

  Mbowe kama angelitumliwa Tarime harafu uchaguzi mdogo unafanyika Ilala hapo kweli ndio mtu angesema inafichwa kwa sababu ingewachanganya wapiga kura ama ingekua na maslahi ya chama fulani.

  LAkini saizi watu wa Tarime itawachanganya vipi?? ili kukipa maslahi chama fulani kivipi?? Maana hiyo ripoti kwao ni uchafu tu fulani, MAANA wao wanafahamu vyema kuliko hiyo ripoti ya kwamba Mbowe alikimbizwa ama hakukukimbizwa Wao ndio wenda ndio walio toa maelezo ktkt ripoti hiyo harafu eti ripoti hiyo baadae ije iwachanganye.NON SENSE.

  Hivi Mbowe anatua lini na HELKOPITA yake akafanye maangamizi ya angani huko Tarime??
   
 11. P

  Paparazi Muwazi JF-Expert Member

  #11
  Sep 27, 2008
  Joined: Dec 23, 2007
  Messages: 310
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35

  Kama wewe ni msomaji mzuri wa habari zangu ni kuwa nilianika mikakati ya huyu mama kabla mumewe hajafa. Niliandika vitu vyote alivyofanya wakati huo. Niliacha kuandika mara baada ya Chacha kufariki kwa matumaini kuwa ataacha mikakati yake na Rostam. Sasa yuko mbali na Rostam lakini ameingia katika timu mpya ya Gachuma na Makamba.

  Lakini anafanyia mambo yake yote Dar esa salaam kwa kuwa akienda Tarime yatamkuta ya Mtikila. Huyu Tarime wanamtuhumu wa kumhamisha chacha Dar es salaam na kumfanya amuache mke wake wa ndoa wa miaka zaidi ya kumi aliyezaa naye watoto watatu.

  Kwa watu wenye umri mkubwa kiasi mtakumbuka huyu mama alipomwacha yule Mzee wa Kiarabu baada ya kufilisika. Wakati huyo huyu binti alikuwa mdogo tayari lakini akiwa shangingi hapa Dar es salaam.

  Pamoja na fedha awamu ya kwanza ambazo alipewa na Gachuma wakati wa msiba Tarime na hivyo kufanya familia ya Wangwe kuwa mstari wa mbele kunyanyua mabango ya kuhusisha CHADEMA na kifo hicho. Mama huyo sasa ameahidiwa na Makamba kuwa atamsaidia mirathi ya marehemu ikiwemo magari mawili na fedha za ubunge wake apatiwe yeye.

  Huyu alikataa arobaini isiwe nyumbani kwake badala yake akaipeleka nyumbani wka Profesa Wangwe mjumbe wa NEC ya CCM ili vigogo wa serikali wamtambue kuwa ndie mke rasmi wa marehemu.

  Huyu tulipomhoji kwenye press ya yake kwanini anasema viongozi wa CHADEMA hawakutoa salamu za pole wakati ambapo anajua kuwa Mbowe akiwa Afrika Kusini alituma salamu za pole na alipofika Tanzania alitoa pole akiwa Tarime na salamu zake za pole zikarushwa na ITV mara baada ya kuondoka msibani baada ya munkari wa wanafamilia akiwemo yeye, akasema kuwa yote hayo hayajayaona.

  Tukamuulizie pia ni kwanini arobaini ya marehemu alikataa isiandaliwe na CHADEMA badala yake akampa jukumu hilo Profesa Wangwe na hatimaye CHADEMA kama chama hakikualikwa kwenye arobaini hiyo, alijibu kwa ukali kuwa yeye kama mke wa marehemu alikuwa na mamlaka ya kufanya hivyo kwa kuwa msiba na suala la kifamilia. Aidha kuhusu kushiriki wa CHADEMA, alisema siku mbili kabla ya arobaini aliwatumia SMS wabunge wa CHADEMA kuwaalika kwenye arobaini na siku moja kabla ya arobaini alipeleka kadi ya mwaliko kwa Mbowe ili naye ashiriki.

  Anasema baada ya kupeleka kadi hiyo alijibiwa kuwa Mwenyekiti Mbowe alikuwa akiendesha kikao cha Kamati Kuu ya chama kilichokuwa kikifanyika siku hiyo.

  PM
   
 12. Single D

  Single D JF-Expert Member

  #12
  Sep 27, 2008
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 459
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Huyu mama naye atapondwa mawe kichwani kama Mtikila.Hizi rushwa zitawamaliza kabisa.
  Leo hana imani na polisi na hakubaliani na uchunguzi wa polisi ki vipi?Mbona hawalaumu mashemaji zake waliotangazia umma kuwa ni ajali wala hakuuwawa na wamejiridhisha kabisa?We know this is nothing more than political game.
  Huyu mama ni sawa na Yuda iskariote aliyemsaliti Yesu.Hana jipya arudi Tabora akafanye biashara
   
 13. P

  Paparazi Muwazi JF-Expert Member

  #13
  Sep 27, 2008
  Joined: Dec 23, 2007
  Messages: 310
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kubenea alikuwa Mwenyekiti wa Kamati,ameshamaliza kazi yake na kukabidhi wa Mwenyekiti wa Jukwaa Sakina Datoo ndio mwenye mamlaka ya kuitoa. Ni Kama Bomani alivyokabidhi ripoti kwa Kikwete. Hapa wa kubanwa ni Sakina ambaye tayari ameshatishwa na kutishika. Wamekubaliana na Mengi kuwa ripoti itoke baada ya uchaguzi ili kuepuka kuonekana wanaisaidia CHADEMA kumbe watakapoitoa baada ya uchaguzi wataonekana pia waliamua kuacha kuitoa ripoti kuisaidia CCM. Hili ni jaribio kubwa kuliko yote ambalo jukwaa hilo limewahi kupata

  PM
   
 14. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #14
  Sep 27, 2008
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280

  Wewe toa hoja zako na sio kutumia mambo binafsi ya kujenga hoja zako,

  Wewe unashangaa Msiba kufanyika kwa kaka wa marehemu ?? Acha uhuni ndugu yangu Je tukisema wewe ndio unatumiwa sio huyo mama anayetumiwa tutakua tumekosea??

  Wewe hujui baadhi ya mila zetu Baba wa familia anapokua hayupo KAKA mkubwa ama mtu mmoja mwenye heshima huteuliwa na familia na ndiye ana act kama BABA MPYA wa FAMILIA??

  Ama wewe hujui baadhi ya mila zetu Mwanamke hana ushauri wowote na ndugu wa marehemu wanaume ndio wanaamua nini wafanye na kwa wakati gani??
  Unashaanga nini Arobaini kuwa kwa kaka wa marehemu?? Ama kwako CHADEMA/CCM ni bora sana kuliko udugu wa DAMU?
   
 15. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #15
  Sep 27, 2008
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Hakuna kitu wanachi wa Tarime wanajua vyema kuliko hiyo ripoti inavyojua ya kua mbowe alikimbizwa au lah ,hivyo hiyo ripoti haitaisadia kwa namna yoyote ile Chadema wala ccm.
   
 16. P

  Paparazi Muwazi JF-Expert Member

  #16
  Sep 27, 2008
  Joined: Dec 23, 2007
  Messages: 310
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Wakati wa maziko, shughuli iliandaliwa na familia kwa ushirikiano na CHADEMA, chama mfiwa na Zitto Kabwe akateuliwa kuingia kwenye kamati.

  Wakati wa maandalizi ya arobaini, CHADEMA haikushirikishwa kwa namna yoyote badala yake walishirikishwa CCM, NCCR, CUF na TLP.

  Mimi kama mwandishi naenda mbali zaidi kuuliza maswali kuhusu yote haya ninayoona ili nisiandike tu nilichoona au kuambiwa, niandike kilivyo. Ndio maana ya habari za uchunguzi.

  Msiba ulikuwa Kimakorere, lakini arobaini ilifanyika kwa Profesa DSM. Hii ni kwakuwa kule pamoja na kuwa alibaki Kaka wa Marehemu Bwana Keba lakini pia alikuwa Mke mkubwa. Na uzito usingekuwepo kama DSM. Tulipopewa nakala ya Risala ya Wanandugu, wengine tuliisoma katika jicho la uchambuzi na kuwauliza maswali mengi pale pale.

  Kwa kweli kuna siasa nyingi katika huu msiba zinazofanywa na vyama vyote.

  PM
   
 17. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #17
  Sep 27, 2008
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Lakini
  WEWE si ndio yule uliyetuletea habari ya kwamba MAREHEM WANGWE ndio ilikua INJINI ya kuimaliza chadema .
  Na ukatueleza kua msaidizi wake alikua MZIRAI na ukasema profesa aliyekua anamchua MAREHEMU CHACHA kuingamiza chadema ni KABURU wakati RA ndio mdhamini mkuu.
  Na ukabainisha kua CHADEMA waliliona hilo na kuamua kumuondoa CHACHA ambaye ni mfitinishi,FISADI ,MWONGO na mwenye marafiki zake wote CCM
  Na ukaendelea kuhoji kwanini CHACHA hapatani na wapinzani wote na kusema kwanini marafiki zake wote ni CCM?

  Naomba kukuuliza ni WEWE Aliyesema maneno hayo ama ni mwingine?
   
 18. P

  Paparazi Muwazi JF-Expert Member

  #18
  Sep 27, 2008
  Joined: Dec 23, 2007
  Messages: 310
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Ni mimi. Na kazi yangu ni kuleta habari za uchunguzi kama zilivyo. Hebu vuta habari zangu hapa zisomwe upya. Niliyaandika yote haya, na hata haya anayoyafanya Mariam nilishayaandika mengine kabla hata Chacha Wangwe hajafariki. Ni mimi mtu wa kwanza kabisa humu kutaja jina la Mariamu Wangwe kabla hata hajaanza kuandika na vyombo vingine vya habari.

  Hila hayo ya kwamba marafiki zake WOTE ni CCM sijalisema popote. Usinisingizie.

  PM
   
 19. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #19
  Sep 27, 2008
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280

  Naam kama ulisema hivyo Na leo unaandika hivi kwa hiyo Unamaa MARIAM anaendeleza Pale mumewe Chacha alipoishia??

  Na hata hivyo mtu huru hawezi kukuelewa wewe maana ukisoma maandiko yako wakati Wangwe yupo hai na unayoandika saizi kuhusu HATOKUELEWA kabisa.
  Sana sana atahitimisha WEWE NDIO UNATUMIWA na sio yule mama.

  Wangapi umesikia wanapofiwa wanaenda kwa waganga kutafuta mchawi??
   
 20. C

  Chuma JF-Expert Member

  #20
  Sep 27, 2008
  Joined: Dec 25, 2006
  Messages: 1,330
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  RIPOTI ITOLEWE watu wajue kipi kilichochunguzwa, then tutakapoiona wananchi tutachuja,...then waandishi walioandaa hio ripoti waweke vyeti vyao hadi vya Form 4 tuvione...Maana uandishi Njaa umeshamiri kila ENEO.....

  Nafikiri Bro Kubenea atakuwa kaingizwa ktk huu MTEGO bila Kujua...na hapo ndipo utakuwa mwisho wake....au aje aikane hio ripoti kabla haijatolewa!!!
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...