Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 4,393
- 14,500
Inadaiwa kuwa kuna mpango wa siri unaohusisha baadhi ya taasisi muhimu za kisiasa nchini, zikiwemo Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Dawati la Siasa Ikulu na baadhi ya wanasiasa maarufu G-55, unaolenga kukipa chama cha CHAUMMA upendeleo maalum kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.
Taarifa hizo ambazo bado hazijathibitishwa rasmi zinadai kuwa Chaumma kinapangiwa kupewa asilimia 7 ya kura za urais kwa njia isiyo ya kawaida ili kukidhi masharti ya kupata ruzuku ya serikali kwa vyama vya siasa. Inadaiwa kuwa ruzuku hiyo itatumika kuwalipa baadhi ya waliowahi kuhudumu ndani ya sekretarieti ya Chadema kupitia kundi la G 55, kwa viwango sawa vya mishahara waliyoizoea.