Marekani yawawekea vikwazo waendesha mashitaka (ICC)

Kuna uwezekano huu uongozi wa Trump umeweka record kwa kuwekea watu wengi vikwanzo kwa muda mfupi.
 
Marekani yatangaza vikwazo dhidi ya mwendesha mashitaka mkuu wa ICC
Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Mike Pompeo alitangaza jana kuwa Marekani imeweka vikwazo dhidi ya mwendesha mashitaka mkuu wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC Fatou Bensouda kwasababu ya ofisi yake kuendelea na uchunguzi wa watu wa Marekani.

Pompeo alisema aliyeongezwa pia katika orodha ya vikwazo ni Phakiso Mochochoko mkuu wa idara ya sheria ya ICC, anayehusika na ushirikiano na hisani, kwa kutoa msaada kwa Bensouda za taarifa mbali mbali. Mwanadiplomasia huyo wa ngazi ya juu wa Marekani ameiita mahakama hiyo ya uhalifu wa kivita, ambayo Marekani haihusiki nayo, kuwa ni taasisi iliyovurugika na yenye ufisadi wa hali ya juu

Mwezi Juni , rais wa Marekani Donald Trump alitoa amri ya rais inayoweka vikwazo vya kiuchumi dhidi ya maafisa wa ICC wanaohusika katika uchunguzi wa vikosi vya jeshi la Marekani kwa uwezekano wa uhalifu wa kivita nchini Afghanistan.
Halafu ndio Lissu anawategemea eti wamsaidie kupata urais kwa kudhani watashitaki viongozi wetu huko ICC wakati wao wamepigwa biti kuwachunguza wamerekani walioua watoto wasio na hatia huko uarabuni, wamebaka, wamelawiti leo hii hao Icc ambao Lissu anawategemea wameufyata kwa marekani na wanawekewa vikwazo!! Mwaka huu machadema mkileta vurugu za kingese mtatembezewa kichapo na hakuna cha ICC wala baba yake na ICC
 
Acheni ubwege, Trump siyo mwalikishi wa wamarekani, wengi wanamuona kama mgonjwa wa akili na walishasema; anao wanaomuunga mkono, lakini ni wachache!
 
Kwamba kuna mtu mwenye akili timamu anaamini USA wanatetea haki na usawa au kwamba hata bepari yoyote anarafiki?
Bepari anaangalia maslahi yake nukta hakuna zaidi.
Ukiona unaurafiki mkubwa na hao ujue wanakutumia na wanakula kwa kukutumia.
Ukitwambia wanapigania haki tutakushangaa sana kwamba uwezo wako wa kufikiri ni mdogo kiasi hicho.

Sent from my Infinix X603 using JamiiForums mobile app
 
Marekani imewawekea vikwazo waendesha mashitaka Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) siku kadhaa baada ya mahakama hiyo kuidhinisha uchunguzi kuhusu tuhuma za uhalifu wa kivita unaodaiwa kutekelezwa na Marekani nchini Afghanistan. View attachment 1557370View attachment 1557371View attachment 1557372

WALE MASHABIKI WA USA NA WASHIRIKA WAKE, NA KUAMINI KUWA JAMAA WAPO SAHIHI KWA KILA KITU KUNA, JAMBO KUBWA SANA LA KUJIFUNZA HAPA
Wanawaita watetezi wa haki za binaadam (USA) ambao wanaogopa kuhukumiwa na ICC kutokana na makosa yao.Ingekuwa nchi nyingine USA na washiriki wake wange shinikiza mpaka vikwazo kwa hiyo nchi.

Siku dunia ikisema wafanye uchunguzi vita ya Iraq,Pakstan,Yemen,Libya wanaweza wakabaki midomo wazi kwa idadi ya vifo ya watu wasio na hatia.

Ila USA wana perfume yao ya kupulizia mauaji yao inaitwa "collateral damage".
 
ww toka umezaliwa uliwahi sikia wap nchi imeuzwa? an dhuyo anaesema ma beberu cjui nn ni ktu gan anafanya bila hao ma beberu? pesa anazo dai n zetu anaenda kukopa kwa hao ma beberu, miundominu almost 98% inajengwa na hao ma beberu in short we depend kwa kila ktu kwa hao ma beberu! kumbuka mbaazi kipind ana wadanganya watu walime then kilichotokea nn baada ya india kutokuhitaj mbaazi nn alizifanyia hizo mbaazi au aliwaambia nn watu? achen kudanganywa kama watoto et anasema yeye hatoi ahadi za uongo hahaha achen basi Tanznania ya viwanda umeiona wap ww? ni kipind gan uhuru wa kujieleza umepotea toka taifa lianzishwe kama siyo hiki kipind? there is alot of things vinaenda ndivyo sivyo JAMAA ANATAKA KUIGA CHINA ILA HATOWEZA HATA KIDOGO AND CHINA KWENYEWE N TAJILI BUT RAIA NI MASKINI THAT WHY MA KAMPUNI MENG YANA OPERATE CHINA SABABU NI CHEAP LABOUR IKIWEMO NA VINGNENVYO KAMA CHEAP ELECTRICITY! INCHI KAMA JAPANI IMEJIKITA KWENYE MAENDELEO YA WATU HALI HIYO IMEPELEKEA NCHI PAMOJA NA WATU KUENDELEA KULIKO KUJIKITA MAENDELEO YA VITU THEN RAIA WANABAKI NYUMA NI UJINGE! I REAL SUPPORT LISU SEMA WACHACHE MTAELEWA NINI HII NCHI IME LACK
 
Niujinga kujilinganisha na marekani. Hii nchi hata wakiweka vikwazo wanajiweza.sisi tuna nini?
 
Marekani imewawekea vikwazo waendesha mashitaka Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) siku kadhaa baada ya mahakama hiyo kuidhinisha uchunguzi kuhusu tuhuma za uhalifu wa kivita unaodaiwa kutekelezwa na Marekani nchini Afghanistan. View attachment 1557370View attachment 1557371View attachment 1557372

WALE MASHABIKI WA USA NA WASHIRIKA WAKE, NA KUAMINI KUWA JAMAA WAPO SAHIHI KWA KILA KITU KUNA, JAMBO KUBWA SANA LA KUJIFUNZA HAPA


nchi nyingi tu zmeacha kua na mahusiano na USA , ni lissu tu amebaki mtetezi wao
 
Mwendesha mashitaka wa ICC Fatou Bensouda

Marekani imewawekea vikwazo maafisa wakuu katika mahakama ya kimataifa kuhusu uhalifu wa kivita ICC akiwemo kiongozi mkuu wa mashitaka Fatou Bensouda.

Waziri wa masuala ya kigeni nchini humo Mike Pompeo alishutumu mahakama hiyo kwa kujaribu kuwashtaki raia wa Marekani.
Mahakama hiyo iliopo mjini Hague kwa sasa inachunguza iwapo vikosi vya Marekani vilifanya uhalifu nchini Afghanistan.
Marekani imeikosoa mahakama hiyo tangu ilipoanzishwa na ni miongoni mwa mataifa mengi ambayo hayajatia saini mkataba wa raia wake kushtakiwa na mahakama hiyo.

Balkess Jarrah , wakili mkuu katika shirika la haki za kibinadamu la Human Rights Watch alishutumu vikwazo hivyo kama aibu kwa Jukumu la Marekani kutoa haki kwa waathiriwa wa uhalifu.

Hatua ya Bw Pompeo iliashiria "upotoshaji wa vikwazo vya Marekani, unaolenga kuwaadhibu wanyanyasaji, na badala yake kuwalenga wale wanaoshtaki uhalifu wa kivita", alijibu ujumbe wa twitter.

Ikiwa mahakama ilioanzishwa kupitia azimio la Umoja wa Mataifa 2002, ICC inachunguza na kuwashtaki wale wanaohusika na mauaji ya kimbari, uhalifu dhidi ya binadamu na uhalifu wa kivita, kuingilia kati iwapo mataifa yameshindwa kuwachukulia hatua waliohusika.

Je, mahakama ya kimataifa kuhusu uhalifu wa kivita ni ipi?
Azimio hilo lilipitishwa na mataifa 123, ikwemo Uingereza.
Lakini Marekani pamoja na China india na Urusi zimekataa kujiunga nayo , huku baadhi ya mataifa ya Afrika yakiishutumu kwa kuwalenga sana viongozi wa Afrika.

Je, vikwazo hivyo ni vipi?
Rais Donald Trump alitoa agizo mwezi Juni, ambalo linaruhusu Marekani kuzuia Mali ya wafanyakazi wa ICC na kuwazuia kuingia katika taifa hilo.

Akiwahutubia wafuasi wake siku ya Jumatano, bwana Pompeo alisema kwamba bi Bensouda na Phakiso Mochokochoko, mkuu wa Idara ya Mamlaka, na kitengo cha Ushirikiano, walipaswa kuwekewa vikwazo kupitia agizo lake.

Akiishutumu mahakama hiyo kama taasisi iliofeli na fisadi , alisema kwamba wale wanaoendelea kuwaunga mkono maafisa hao pia wanahatarisha kuwekewa vikwazo.

Wizara hiyo pia ya Marekani pia imezuia utoaji wa visa kwa wafanyakazi wa ICC wanaohusika na juhudi za kuwachunguza wanajeshi wa Marekani.

Mahakama ya ICC ilisema kuwa haitazuiwa na vitisho vya Marekani kufanya majukumu yake
Maelezo ya picha,
Mahakama ya ICC ilisema kuwa haitazuiwa na vitisho vya Marekani kufanya majukumu yake
Wakati Rais Trump alipotoa agizo hilo la rais mwezi Juni, mahakama ya ICC ilipuuzilia mbali kile ilichokitaja vitisho zaidi na vitendo vya kulazimisha, dhidi yake.

''Shambulio lolote dhidi ya ICC pia linawakilisha shambulio dhidi ya waathiriwa wa uhalifu , wengi ambao mahakama hiyo inawakilishi matumaini yao ya mwisho ili kupata haki'', ilisema taarifa yake.

Je, Fatou Bensouda ni nani?
Kama waziri wa haki wa zamani nchini Gambia, taifa analotoka, bi Bensouda alitarajiwa kumrithi Luis Moreno Ocampo kama mkurugenzi wa mashtaka katika mahakama hiyo baada ya kuhudumu kama kaimu wake wakati wote huo.

Awali aliwahi kuhudumu kama mshauri mkuu wa masuala ya kisheria katika jopo la mahakama inayoungwa mkono na Umoja wa mataifa ambayo iliwahukumu viongozi wakuu wa mauaji ya kimbari nchini Rwanda 1994.

Huku akihusika katika kupanua uchunguzi wa ICC ili kuangazia mizozo kwengineko hatua iliomfanya kuadhibiwa na Marekani, Afrika ndio lengo lake kuu.

Mahakama ya kimataifa imekuwa ikikosolewa vikali hivi karibuni na Marekani
Maelezo ya picha,
Mahakama ya kimataifa imekuwa ikikosolewa vikali hivi karibuni na Marekani.

Kesi zote za ICC zimekuwa zikiangazia viongozi wa Afrika na kiongozi mmoja wa wapiganaji kutoka nchini DRC , Thomas Lubanga, alikuwa mtu wa kwanza kuhukumiwa kwa uhalifu wa kivita na ICC 2012.

Lakini Bensouda pia alishindwa na misururu ya kesi, ikiwemo kuwachilia huru kwa aliyekuwa rais wa Ivory Coast Lauirent Gbabgo aliyeshtakiwa kwa mashtaka ya uhalifu wa kivita 2019 na kuondolewa kwa mashtaka ya uhalifu dhidi ya binadamu dhidi ya rais wa Kenya Uhuru Kenyatta 2014.

Je, ICC inachunguza nini?
Mahakama ya ICC ilianza kuchunguza madai ya uhalifu wa kivita yaliotekelezwa nchini Marekani na mengine katika mzozo wa Afghanistan mapema mwaka huu.

Kulingana na Mchakato wa sheria ya ICC, mahakama hiyo inaweza kutoa waranti za kukamatwa kwa washukiwa wanaolazimika kuwasili mbele ya mahakama hiyo inapopata ushahidi wa kutosha na kuwatambua.

Bwana Pompeo aliapa kuwalinda Wamarekani dhidi ya Mahakama ya ICC
CHANZO CHA PICHA,AFP
Maelezo ya picha,
Bwana Pompeo aliapa kuwalinda Wamarekani dhidi ya Mahakama ya ICC

Baadaye itaamua iwapo kuna ushahidi wa kutosha kwa kesi kusikilizwa. Wakati huo, Bwana Pompeo aliapa kuwalinda Wamarekani, akiitaja mahakama hiyo kuwa taaisi isiowajibika inayojifanya kuwa bodi ya kisheria. Ripoti ya 2016 kutoka kwa ICC ilisema kwamba kulikuwa na sababu za kutosha kuamini kwamba jeshi la Marekani liliwatesa washukiwa katika eneo moja la siri linalosimamiwa na shirika la CIA. Afghanistan ni mwananchama wa mahakama hiyo lakini maafisa wameonesha pingamizi yao kuhusu uchunguzi huo.

Shukrani kwa bbc
 
Halafu hawa ndio kina Lissu wanawategemea watasimamia haki Tanzania wakati wao wenyewe waharifu wanalinda maslahi yao na awapo tayari kumuacha mtu ayaingilie hata ikiwezekana kuua millions poa tuu hili wachukue.
 
Nchi 68 za wanachama wa ICC wamesema wanaisupport ICC ktk tuhuma hizi zinazo ikabili USA.

Source;Star TV.

Ngojea tuone kiranja wa dunia kama atasimamishwa mbele ya pilato wa ICC.
 
Back
Top Bottom