Marekani yataja sababu nne za Obama kuja Tanzania


R.B

R.B

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2012
Messages
6,294
Likes
1,262
Points
280
R.B

R.B

JF-Expert Member
Joined May 10, 2012
6,294 1,262 280
Marekani imetaja sababu nne ambazo zimemfanya Rais Barrack Obama kuijumuisha Tanzania katika ziara yake ya bara la Afrika. Rais Obama amepanga kulitembelea bara la Afrika kuanzia Juni 26 hadi Julai 3, mwaka huu na atazitembelea pia Senegal na Afrika Kusini.

Kiongozi huyo wa Marekani ambaye baba yake mzazi ni mzaliwa wa Kenya, anatarajiwa kuwasili nchini Julai Mosi kwa ziara ya siku tatu. Atakuwa Rais wa tatu wa Marekani kuitembelea Tanzania baada ya Bill Clinton mwaka 2000 na George Bush mwaka 2008.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Balozi wa Marekani, Alfonso Lenhardt alisema sababu ya kwanza ya Obama kuja Tanzania ni kutokana na kuwa mfano wa utawala bora, demokrasia na ushirikishaji wa watu wake wakati wa kufanya uamuzi unaogusa maisha yao ya kila siku.

Alisema kuwa Tanzania ni nchi ya mfano linapokuja suala la uongozi bora na ndiyo maana imekuwa na amani na utulivu kwa muda mrefu ikilinganishwa na nchi nyingi za Kusini mwa Jangwa la Sahara.

“Nchi nyingi za Afrika zinazoizunguka Tanzania zimekuwa na matatizo ya vita vya wenyewe na hata ukosefu wa utawala bora,” alisema Balozi Lenhardt ingawa alidokeza kuwa katika siku za karibuni imekuwa ikikabiliwa na changamoto mbalimbali kutokana na matukio ya uvunjifu wa amani.

Balozi Lenhardt alisema sababu nyingine inayomfanya Rais Obama kuja Tanzania ni kutokana na jitihada za Serikali ya Marekani kutengeneza mazingira mazuri ya uwekezaji na kasi ya ukuaji wa uchumi.

“Rais Obama anakuja kuunga mkono juhudi za Watanzania katika kutengeneza mazuri ya uwekezaji lakini bila kusahau kuwa kasi ya ukuaji wa uchumi wa Tanzania imeivutia Serikali ya Marekani,” alisema.

Balozi Lenhardt alitaja sababu nyingine inayomleta Rais Obama kuwa ni kuisaidia Tanzania kuendeleza fursa mbalimbali za kujiletea maendeleo.

Alisema uendelezaji huo wa fursa una lengo la kuisaidia Serikali ya Tanzania kukabiliana na tatizo la umaskini.

Alisema Marekani ni moja ya nchi zinazoongoza kwa kutoa fedha nyingi za misaada na akisema kwa mfano, mwaka 2012 pekee ilitoa Dola 750 milioni.

Aidha, alisema nchi yake imekuwa ikitoa misaada mingi kupitia Shirika la Millenium Challenge (MCC), ambayo imejikita zaidi katika kusaidia sekta za umeme, maji na miundombinu

Alisema Tanzania inaunga mkono jitihada za Serikali kujitosheleza kwa chakula na inafadhili Mkakati wa Kukuza Kilimo Kusini mwa Tanzania (SAGCOT).

“Tunaunga mkono mpango wa SAGCOT kupitia Mfuko wa Rais wa Marekani unaoitwa `Feed the Future’ lengo likiwa kuifanya Tanzania kupiga hatua katika kilimo,” alisema balozi huyo.

Sababu nyingine ya ujio wa Obama ni kuhimiza haja ya Afrika kutayarisha viongozi wa kizazi kijacho. Ameanzisha programu ya kuandaa viongozi wa kizazi inayoitwa `Young African Leaders Initiative’ na Watanzania watatu, Modesta Lilian Mahiga, Masoud Salim Mohamed na Malula Hassan Nkanyemka walishiriki katika mpango huo na kukutana na kiongozi huyo mwaka 2010.

“Rais Obama anataka kusaidia kuandaa viongozi wa kizazi kijacho wa Afrika kusimamia vizuri rasilimali za nchi,” alisema.Tishio la China

Akizungumzia ushindani na China kuhusiana na fursa za kuwekeza na kuvuna rasilimali za Afrika, Balozi Leinhardt alisema hawana tatizo lolote na hilo kwani dhamira ya Marekani ni kusaidia Tanzania kupiga hatua katika maendeleo ya kiuchumi.

Rais wa China, Xi Jinping aliitembelea Tanzania Machi mwaka huu na ujio wa Obama umetafsiriwa na baadhi ya watu kuwa ni ushindani wa mataifa hayo mawili katika kusaka na kunufaika na rasilimali za Afrika.

Balozi Lenhardt alieleza imani yao ni kuwa China inadumisha urafiki na Tanzania kwa nia ya kuisaidia kuendelea... “Sisi hatuna shida na China, kwani tunaamini wako kwa ajili ya kusaidia. Ilimradi tu wawe na dhamira safi katika kuwasaidia.”

Alipoulizwa kama ziara ya Rais Obama ina lengo la kusaka fursa ya kuvuna rasilimali za Tanzania, balozi huyo aliwataka Watanzania kuacha kuwa na wasiwasi wa kuporwa rasilimali zao.

“Watanzania ni watu wapole na wakarimu ila mna tatizo moja la kuhofia kila jambo. Kila kitu mnachofanyiwa mnaona kuna baya linakuja. Sisi tuna nia njema ya kuwasaidia kuendelea.”
 
njiwa

njiwa

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2009
Messages
11,634
Likes
2,275
Points
280
njiwa

njiwa

JF-Expert Member
Joined Apr 16, 2009
11,634 2,275 280
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Balozi wa Marekani, Alfonso Lenhardt alisema sababu ya kwanza ya Obama kuja Tanzania ni kutokana na kuwa mfano wa utawala bora, demokrasia na ushirikishaji wa watu wake wakati wa kufanya uamuzi unaogusa maisha yao ya kila siku.

Alisema kuwa Tanzania ni nchi ya mfano linapokuja suala la uongozi bora na ndiyo maana imekuwa na amani na utulivu kwa muda mrefu ikilinganishwa na nchi nyingi za Kusini mwa Jangwa la Sahara.ahsante balozi.... wa tanzania wanadanganywa na cdm kwamba hatuna hivi vitu ... shukran za dhati kwa Dr JK
 
Mkoroshokigoli

Mkoroshokigoli

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2012
Messages
14,621
Likes
2,691
Points
280
Mkoroshokigoli

Mkoroshokigoli

JF-Expert Member
Joined Dec 20, 2012
14,621 2,691 280
.....Alipoulizwa kama ziara ya Rais Obama ina lengo la kusaka fursa ya kuvuna rasilimali za Tanzania, balozi huyo aliwataka Watanzania kuacha kuwa na wasiwasi wa kuporwa rasilimali zao.

"Watanzania ni watu wapole na wakarimu ila mna tatizo moja la kuhofia kila jambo. Kila kitu mnachofanyiwa mnaona kuna baya linakuja. Sisi tuna nia njema ya kuwasaidia kuendelea."
salaaale
 
Ng'wamapalala

Ng'wamapalala

JF Gold Member
Joined
Jun 9, 2011
Messages
6,332
Likes
137
Points
160
Ng'wamapalala

Ng'wamapalala

JF Gold Member
Joined Jun 9, 2011
6,332 137 160
Haya mawazo ya Kutoka kwenye corridors of power in Washington ndiyo ukweli wa Tanzania?.

Kuna swali ambalo Rais Kagame alipata kuulizwa na Justin Fox ambaye ni editorial director wa the Harvard Business Review Group pale alipokuwa amekaribishwa na Professor Michael Porter wa Harvard Business School kama guest speaker, na Rais Kagame alijibu na kusema,
If you want to learn anything about a country, I think you need to ask the one who wants to make investment in that country. The one who is thinking about the risks involved. They're thinking about the return. If somebody comes to your country and says, "You know, this is a place to invest," actually that is a good place. You see?

But if you send someone and say, "Go on, look and find for me something that is at fault," in any place in this world somebody will come up with piles and piles to things to report about.
Ninafikiri Watanzania wanaopiga kelele kuhusu ubaya wa Tanzania wanakuwa ni kama wale ambao Rais Kagame anawaelezea katika kundi la pili huku wale wanasema Tanzania ni nchi nzuri ni wale wa kundi la wawekezaji.

Kila mtu na mawazo yake kuhusu ubora wa Tanzania kwa sasa kulingana na jinsi anavyochungulia dirishani.

Is it true, kwamba investors wako katika position nzuri kujua hali halisi ya nchi zaidi ya wananchi?

Ni kweli kuwa malalamiko mengi ya Watanzania ni sawa na mtoto kwa wazazi wake ambaye hatosheki hata ukimpa au kumnunulia kitu gani?.

Is it true kwamba binadamu hatosheki?. Ni kweli Watanzania hawatosheki?

What's Tanzania in a NAKED eyes of Watanzania wengi compare with Investors and Foreigners
 
Capt Tamar

Capt Tamar

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2011
Messages
9,044
Likes
7,117
Points
280
Capt Tamar

Capt Tamar

JF-Expert Member
Joined Dec 15, 2011
9,044 7,117 280
“Rais Obama anataka kusaidia kuandaa viongozi wa kizazi kijacho wa Afrika kusimamia vizuri rasilimali za nchi,” alisema
HAPA NINA SHAKA NAPO
Baada ya kugundua kuwa kuna tabaka la ma young Waitara,wenye guts za kusema NO kwa issue isiyo na maslahi kwa taifa sasa wameamua kutengeneza tabaka la wamarekani wa kitanzania,watakaosimamia Pipe za kunyonyea uchumi kwa niaba ya waamerika,TWENDE KAZI
 
mdeki

mdeki

JF-Expert Member
Joined
Mar 28, 2011
Messages
3,304
Likes
48
Points
145
mdeki

mdeki

JF-Expert Member
Joined Mar 28, 2011
3,304 48 145
Jamani naombeni kuuliza eti anaetakiwa kusema nchi ina maendeleo au inaendelea ni mgeni au mwenyeji(mtanzania mwenyewe)?
 
Mama Mdogo

Mama Mdogo

JF-Expert Member
Joined
Nov 21, 2007
Messages
2,900
Likes
504
Points
280
Mama Mdogo

Mama Mdogo

JF-Expert Member
Joined Nov 21, 2007
2,900 504 280
Marekani imetaja sababu nne ambazo zimemfanya Rais Barrack Obama kuijumuisha Tanzania katika ziara yake ya bara la Afrika. Rais Obama amepanga kulitembelea bara la Afrika kuanzia Juni 26 hadi Julai 3, mwaka huu na atazitembelea pia Senegal na Afrika Kusini..............Sababu nyingine ya ujio wa Obama ni kuhimiza haja ya Afrika kutayarisha viongozi wa kizazi kijacho. Ameanzisha programu ya kuandaa viongozi wa kizazi inayoitwa `Young African Leaders Initiative’ na Watanzania watatu, Modesta Lilian Mahiga, Masoud Salim Mohamed na Malula Hassan Nkanyemka walishiriki katika mpango huo na kukutana na kiongozi huyo mwaka 2010. “Rais Obama anataka kusaidia kuandaa viongozi wa kizazi kijacho wa Afrika kusimamia vizuri rasilimali za nchi,” alisema.

Tishio la China

Akizungumzia ushindani na China kuhusiana na fursa za kuwekeza na kuvuna rasilimali za Afrika, Balozi Leinhardt alisema hawana tatizo lolote na hilo kwani dhamira ya Marekani ni kusaidia Tanzania kupiga hatua katika maendeleo ya kiuchumi.

Rais wa China, Xi Jinping aliitembelea Tanzania Machi mwaka huu na ujio wa Obama umetafsiriwa na baadhi ya watu kuwa ni ushindani wa mataifa hayo mawili katika kusaka na kunufaika na rasilimali za Afrika.

Balozi Lenhardt alieleza imani yao ni kuwa China inadumisha urafiki na Tanzania kwa nia ya kuisaidia kuendelea... “Sisi hatuna shida na China, kwani tunaamini wako kwa ajili ya kusaidia. Ilimradi tu wawe na dhamira safi katika kuwasaidia.”

Alipoulizwa kama ziara ya Rais Obama ina lengo la kusaka fursa ya kuvuna rasilimali za Tanzania, balozi huyo aliwataka Watanzania kuacha kuwa na wasiwasi wa kuporwa rasilimali zao.

“Watanzania ni watu wapole na wakarimu ila mna tatizo moja la kuhofia kila jambo. Kila kitu mnachofanyiwa mnaona kuna baya linakuja. Sisi tuna nia njema ya kuwasaidia kuendelea.”
Loooh, katika population ya Tanzania yenye watu milioni 44 ni vijana watatu tu wameweza kutayarishwa kuwa viongozi wa kizazi kijacho!!! Loooh, kumbe Wamarekani wanatuoina sisi kuwa ni wakarimu sana (kila mtu tunamkaribisha bila kujali atatusaidia au la, tunataka thawabu toka kwa Muumba wetu); hata hivyo Wamarekani wanatuona tumejaa hofu kuhusu kila jambo. Kwa nini tuko wakarimu na hapo hapo tuko waoga??? Why?? Sina jibu na nimechoka!!!
 
Capt Tamar

Capt Tamar

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2011
Messages
9,044
Likes
7,117
Points
280
Capt Tamar

Capt Tamar

JF-Expert Member
Joined Dec 15, 2011
9,044 7,117 280
American is a traitors,wanaelewa wazi kuwa apart from valuables(suti tano, etc)hata sifa za uongo zinatosha kabisa kuwaliwaza viongozi mbumbumbu wa kiafrika na wakavuta usingizi moroooro,huku maliasili ikiendelea kutokomea, Leihardt kazi yake ni kumlainisha mkuu jk,na kutuaminisha kuwa marekani haina nia nyingine yoyote zaidi ya kutusaidia,kwa undugu gani tulionao? When the deal is too good>think twice.
 
nyabhingi

nyabhingi

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2010
Messages
13,531
Likes
11,238
Points
280
nyabhingi

nyabhingi

JF-Expert Member
Joined Oct 12, 2010
13,531 11,238 280
anayetaka kukuibia lazima atakupumbaza na sifa za kijinga,obama ni mwizi wa rasilimali za afrika kama marais wote waliomtangulia..eti uchumi unakuwa!mbona watu wanazidi kuwa masikini,bei ziko juu.
obama ain't no black.
 
Iron Lady

Iron Lady

JF-Expert Member
Joined
Mar 4, 2008
Messages
4,071
Likes
153
Points
160
Iron Lady

Iron Lady

JF-Expert Member
Joined Mar 4, 2008
4,071 153 160
mmarekani hajawahi kumsaidia mtu bila kutaka kumuibia chochote. hana wema huo kuna analolitafuta.
 
Centrehalf

Centrehalf

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2013
Messages
509
Likes
1
Points
0
Centrehalf

Centrehalf

JF-Expert Member
Joined Jun 9, 2013
509 1 0
Haiwezekani mtu wa nje atangulie kujua maendeleo ya uchumi wetu kabla hatujauona sisi wenyewe.nisawa na mtu kukwambia umeshiba wakati hujala.
 
Iron Lady

Iron Lady

JF-Expert Member
Joined
Mar 4, 2008
Messages
4,071
Likes
153
Points
160
Iron Lady

Iron Lady

JF-Expert Member
Joined Mar 4, 2008
4,071 153 160
wajanja sana watu hawa, wameshajua udhaifu wetu wanatambaa nao.
nyerere alishasema tuwe nao makini sana.
 
Rapherl

Rapherl

JF-Expert Member
Joined
Jun 20, 2012
Messages
3,426
Likes
1,592
Points
280
Rapherl

Rapherl

JF-Expert Member
Joined Jun 20, 2012
3,426 1,592 280
Kwanini watuandalie viongozi?!
 
Ritz

Ritz

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2011
Messages
42,249
Likes
4,700
Points
280
Ritz

Ritz

JF-Expert Member
Joined Jan 1, 2011
42,249 4,700 280
Tunashukuru sana balozi kwa kutoa ufafanuzi na kutambua kama Tanzania ni nchi ya amani tofauti tunavyopotoshwa na Chadema.
 
mpinga shetani

mpinga shetani

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2010
Messages
3,268
Likes
43
Points
145
mpinga shetani

mpinga shetani

JF-Expert Member
Joined Nov 22, 2010
3,268 43 145
Tunashukuru sana balozi kwa kutoa ufafanuzi na kutambua kama Tanzania ni nchi ya amani tofauti tunavyopotoshwa na Chadema.
hivi mauaji ya akina Mwangosi, mateso ya Ulimboka, kibanda etc. ni sehemu ya utawala bora?
 
bily

bily

JF-Expert Member
Joined
Apr 5, 2012
Messages
8,054
Likes
4,147
Points
280
bily

bily

JF-Expert Member
Joined Apr 5, 2012
8,054 4,147 280
alfonso naye tatizo anapenda sana kuropoka kwenye tv na vyombo vya habari kwani sababu anazotaja ni danganya toto kwanini asiende kenya au sudan ata central africa kama kweli wanataka kuandaa viongozi wa kiafrika katika suala zima la kidemokrasia
 

Forum statistics

Threads 1,275,220
Members 490,932
Posts 30,536,026