Marekani yataja sababu nne za Obama kuja Tanzania

Ngoja nijikumbushe kidogo

RichardBrunwick

Recommend

26 January 2012 2:33pm

Tanzania's Kikwete is one of the most pathetic African leaders of our times. He is a peacetime leader for a country known to be one of the richest in the world in terms of natural resources, yet he leades the world with begging. Foreign companies have known Tanzania to be a free land in which you can go in and take all you can without being asked a question. I really don't get the mind set of its leaders especially their prsident Mr. Kikwete, a Muzungu worshiper. Having worked with the UNDP in that country for 8 years, I realized how inneficient and corrupt the country's leadership is. His ministers that requested bribes from BAE have never been tried despite the damning evidence against them. British TAX payers must stop funding this man's corruptin and foreign trips. His human rights record is horrible. Mr. Kikwete had no business of going to Davos to ask for foreign aid. Already his country is the world third leading foreign Aid dependant nation. He should be embarassed to say to the world that people are poor. His people living "hand to mouth " is his own is own ignorance and stupidity.That is hiw own problem, Brits are having their own problems he must realize that. We cant bankroll his foreign trips. He should make good use of his country's wealth. Instead of letting his corrupt officials and foreigners loot his country, he needs to think before letting himself be a global loughing stock. I read in one of the regional (kenyan) publication the mockery nature related to his frequent foreign trips. Palestinian, Haiti, Lebanon, Somalia and even Rwanda economies are more robust that of Tanzania. We must question the nations that welcomes this "Joker's" request for AID. He needs to be on a "no-fly" list so he can be serious. Hopefully the billionaires questions what he has done with the Money he has received for decades. The Arab spring should turn into the African summer and get rid of the Kikwete likes

SIO MIMI JAMANI,MSINIUE
 



ahsante balozi.... wa tanzania wanadanganywa na cdm kwamba hatuna hivi vitu ... shukran za dhati kwa Dr JK
Hivi Mwalimu Nyerere alikuwa mwongo aliposema hakuna MJOMBA toka nje atakayekuja kuwaletea maendeleo? Mimi sina imani na wachina na wamarekani ...hawaji kutusaidia wamekuja kutengeneza faida kama Enzi zile za mababu zetu walivyokuja na Germany East Africa Company leo wanakuja na MNCs or Multinational Companies to equally exploit our resources be it minerals, gas, animals ect...huo ndio ukweli!!
 
Haya mawazo ya Kutoka kwenye corridors of power in Washington ndiyo ukweli wa Tanzania?.

Kuna swali ambalo Rais Kagame alipata kuulizwa na Justin Fox ambaye ni editorial director wa the Harvard Business Review Group pale alipokuwa amekaribishwa na Professor Michael Porter wa Harvard Business School kama guest speaker, na Rais Kagame alijibu na kusema,


Ninafikiri Watanzania wanaopiga kelele kuhusu ubaya wa Tanzania wanakuwa ni kama wale ambao Rais Kagame anawaelezea katika kundi la pili huku wale wanasema Tanzania ni nchi nzuri ni wale wa kundi la wawekezaji.

Kila mtu na mawazo yake kuhusu ubora wa Tanzania kwa sasa kulingana na jinsi anavyochungulia dirishani.

Is it true, kwamba investors wako katika position nzuri kujua hali halisi ya nchi zaidi ya wananchi?

Ni kweli kuwa malalamiko mengi ya Watanzania ni sawa na mtoto kwa wazazi wake ambaye hatosheki hata ukimpa au kumnunulia kitu gani?.

Is it true kwamba binadamu hatosheki?. Ni kweli Watanzania hawatosheki?

What's Tanzania in a NAKED eyes of Watanzania wengi compare with Investors and Foreigners

Watanzania tutosheke kwa kipi tulichopewa? na hao investors wanaoona hapa ni mahali pa zuri wameona hivyo leo? mbona hakuna meaningful investment imefanyika hapa? alafu hakuna mtu amewalalamikia wamarekani au anawaogopa wasibebe mzigo ambao hawajatwishwa, sisi tunawalalamia viongozi na serikali yetu.

Kama kuna msaada tunahitaji na ninamna ya kuidhibiti serikali yetu ili iweze kutimiza wajibu wake, hiki ndio kilio chetu.
 
Hivi Mwalimu Nyerere alikuwa mwongo aliposema hakuna MJOMBA toka nje atakayekuja kuwaletea maendeleo? Mimi sina imani na wachina na wamarekani ...hawaji kutusaidia wamekuja kutengeneza faida kama Enzi zile za mababu zetu walivyokuja na Germany East Africa Company leo wanakuja na MNCs or Multinational Companies to equally exploit our resources be it minerals, gas, animals ect...huo ndio ukweli!!


1 ) ndio nyerere alikuwa mwongo

2) huwaamini wachina lakini huyu ambaye mnamuita baba yenu wa taifa ndiye aliyekuwa kipenzi cha wa china... hadi akaturithisha philosophy za wachina ujamaa na kujitegemea .... yalipomshinda na kuona nchi inateketea akamuachia alhaji ally hassan mwinyi .. leo hii unatumia computer , aunaangalia TV sababu ya kazi nzuri aliyofanya mwinyi ...

 
tujiulize wote ambao wamekua na urafiki na marekani wameishia wapi kama si pabaya.Pia kwa nini anasema hawana nia mbaya na sisi na kutuasa juu ya urafiki wetu na China.Tuangalie hapo.
 
Ha ha haa ha, leo hii ndiyo unasema haukubaliani na balozi wa Marekani wakati kila siku unajisifia ubalozi wa Marekani umekichukuwa kitabu chako cha ugaidi na kukupa mialiko pentagon, kitabu chako kimewafurahisha.

CC: gombesugu, THE BIG SHOW, Ami, Boko haram,

Shariff Ritz,

ahaha!!...yaani hawa jamaa ni pumba tupu wanapokua lile jukwaa lao la Crusade, mawazo na fikra zao zoote wanaweka kando,na wakirejea huku kwengine ndo kama tunavyoona malalamiko hayaishi!?ahaha!!...poor Yericko!

Ahsanta.
 
Hivi ameshindwa kwenda kenya kwao au kaamua tu kuwapotezea? Wenzie wana kiu nae sana basi tu. Hivi si nchi yetu ndio tuseme ina mvuto eh! Toba, mungu tusaidie, wamarekani wanatuambia tusiogope wanataka kutusaidia loh! si kama mtoto unavyomwambia atulie anavyochoma sindano kwamba haiumi, na sisi ndio vile tunaddanganywa live poh!
 
Hadanganyiki mtu hapa.

Obama afanye assignment ifuatayo kwanza ndipo tuweze kumuelewa: asimamie fedha zilizofichwa Uswiss zirudi (maana hatuhitaji mtu amwage mapesa kwenye MCC na SAGCOT halafu ziishie Uswiss) halafu amwambie JK apeleke bungeni mikataba yote inayohusiana na raslimali zetu (huo ndio utawala bora na ushirikishwaji). Nje ya hapo ni bepari kama bepari wengine (Mwalimu alikata mirija ya mabepari ndiyo maana wakasubiri akafa wanakimbizana kuja tz, kwanini wasije wakati wa Mwalimu? Kwani kulikuwa hakuna umaskini na raslimali??)
 
Mauaji ya Mwangosi yamesababishwa na Chadema baada ya kukataa kutii sheria bila shuruti.

Sheria nyingi sana tulizonazo na namna ya utekelezaji wake ni ushahidi wa ukosefu wa utawala bora.
 
Marekani imetaja sababu nne ambazo zimemfanya Rais Barrack Obama kuijumuisha Tanzania katika ziara yake ya bara la Afrika. Rais Obama amepanga kulitembelea bara la Afrika kuanzia Juni 26 hadi Julai 3, mwaka huu na atazitembelea pia Senegal na Afrika Kusini.

Kiongozi huyo wa Marekani ambaye baba yake mzazi ni mzaliwa wa Kenya, anatarajiwa kuwasili nchini Julai Mosi kwa ziara ya siku tatu. Atakuwa Rais wa tatu wa Marekani kuitembelea Tanzania baada ya Bill Clinton mwaka 2000 na George Bush mwaka 2008.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Balozi wa Marekani, Alfonso Lenhardt alisema sababu ya kwanza ya Obama kuja Tanzania ni kutokana na kuwa mfano wa utawala bora, demokrasia na ushirikishaji wa watu wake wakati wa kufanya uamuzi unaogusa maisha yao ya kila siku.

Alisema kuwa Tanzania ni nchi ya mfano linapokuja suala la uongozi bora na ndiyo maana imekuwa na amani na utulivu kwa muda mrefu ikilinganishwa na nchi nyingi za Kusini mwa Jangwa la Sahara.

“Nchi nyingi za Afrika zinazoizunguka Tanzania zimekuwa na matatizo ya vita vya wenyewe na hata ukosefu wa utawala bora,” alisema Balozi Lenhardt ingawa alidokeza kuwa katika siku za karibuni imekuwa ikikabiliwa na changamoto mbalimbali kutokana na matukio ya uvunjifu wa amani.

Balozi Lenhardt alisema sababu nyingine inayomfanya Rais Obama kuja Tanzania ni kutokana na jitihada za Serikali ya Marekani kutengeneza mazingira mazuri ya uwekezaji na kasi ya ukuaji wa uchumi.

“Rais Obama anakuja kuunga mkono juhudi za Watanzania katika kutengeneza mazuri ya uwekezaji lakini bila kusahau kuwa kasi ya ukuaji wa uchumi wa Tanzania imeivutia Serikali ya Marekani,” alisema.

Balozi Lenhardt alitaja sababu nyingine inayomleta Rais Obama kuwa ni kuisaidia Tanzania kuendeleza fursa mbalimbali za kujiletea maendeleo.

Alisema uendelezaji huo wa fursa una lengo la kuisaidia Serikali ya Tanzania kukabiliana na tatizo la umaskini.

Alisema Marekani ni moja ya nchi zinazoongoza kwa kutoa fedha nyingi za misaada na akisema kwa mfano, mwaka 2012 pekee ilitoa Dola 750 milioni.

Aidha, alisema nchi yake imekuwa ikitoa misaada mingi kupitia Shirika la Millenium Challenge (MCC), ambayo imejikita zaidi katika kusaidia sekta za umeme, maji na miundombinu

Alisema Tanzania inaunga mkono jitihada za Serikali kujitosheleza kwa chakula na inafadhili Mkakati wa Kukuza Kilimo Kusini mwa Tanzania (SAGCOT).

“Tunaunga mkono mpango wa SAGCOT kupitia Mfuko wa Rais wa Marekani unaoitwa `Feed the Future’ lengo likiwa kuifanya Tanzania kupiga hatua katika kilimo,” alisema balozi huyo.

Sababu nyingine ya ujio wa Obama ni kuhimiza haja ya Afrika kutayarisha viongozi wa kizazi kijacho. Ameanzisha programu ya kuandaa viongozi wa kizazi inayoitwa `Young African Leaders Initiative’ na Watanzania watatu, Modesta Lilian Mahiga, Masoud Salim Mohamed na Malula Hassan Nkanyemka walishiriki katika mpango huo na kukutana na kiongozi huyo mwaka 2010.

“Rais Obama anataka kusaidia kuandaa viongozi wa kizazi kijacho wa Afrika kusimamia vizuri rasilimali za nchi,” alisema.



Tishio la China

Akizungumzia ushindani na China kuhusiana na fursa za kuwekeza na kuvuna rasilimali za Afrika, Balozi Leinhardt alisema hawana tatizo lolote na hilo kwani dhamira ya Marekani ni kusaidia Tanzania kupiga hatua katika maendeleo ya kiuchumi.

Rais wa China, Xi Jinping aliitembelea Tanzania Machi mwaka huu na ujio wa Obama umetafsiriwa na baadhi ya watu kuwa ni ushindani wa mataifa hayo mawili katika kusaka na kunufaika na rasilimali za Afrika.

Balozi Lenhardt alieleza imani yao ni kuwa China inadumisha urafiki na Tanzania kwa nia ya kuisaidia kuendelea... “Sisi hatuna shida na China, kwani tunaamini wako kwa ajili ya kusaidia. Ilimradi tu wawe na dhamira safi katika kuwasaidia.”

Alipoulizwa kama ziara ya Rais Obama ina lengo la kusaka fursa ya kuvuna rasilimali za Tanzania, balozi huyo aliwataka Watanzania kuacha kuwa na wasiwasi wa kuporwa rasilimali zao.

“Watanzania ni watu wapole na wakarimu ila mna tatizo moja la kuhofia kila jambo. Kila kitu mnachofanyiwa mnaona kuna baya linakuja. Sisi tuna nia njema ya kuwasaidia kuendelea.”
kama tungekuwa na tabia ya kudai haki zetu kama wananchi wa Mtwara kungekuwa hakuna Amani,Amani tuliyonayo ni kwa sababu tunakubali kuzulumiwa
 
Sikubaliana hata chembe na hoja za balozi Alfonso Lenhardt

Huu ni ulaghai wa kifikra wa USA kama walivyozoea,

Kibaya zaidi watawala wetu nao wanavimba vichwa kwa kusanifiwa kizandiki!

Tanzania sio mfano wa utawala bora barani Afrika kama asemavyo balozi Alfonso Lenhardt

Juzi tu ripoti ya UN imeleza kuwa Tanzania imeingia kwenye nchi kumi bora duniani kwa ukiukaji wa haki za binadamu ikiwemo haki ya waandishi wa habari,

Halafu leo anatokea mumiani mmoja kama USA awasifu watawala nao wakakenua meno bila kujua resource zetu zinateketea!
Ni lugha tuu ya kijanda kwa CCM wanaoogopa sana kukosolewa..wanaweza hata ua watu km hawatatoa kauli ya kuwasifia km ...."...... kwa uongozi uliotukuka wa JK.". Mbowe did the same ghafla akawa super hero among magambaz.

Huyo balozi angendeelea anaweza kuwa alitaka sema kitu equivalent na "ktk waovu umefanya uovu kidogo umelega kushindana na somalia, sudan,lubya, chad,Niger etc ...angalau umewapita Kenya na Eritrea"..Mara zote pongezi huwa zinabase ktk hiyo misingi..ila wanaweka sawa ili pasitokee mahali mahali CCM wakaruka juu ya meza na kuanza sera za mabeberu.Si umesikia kauli za JK baada tuu ya Kagame kuongea?Walishaanza kuja beba watanzania wakawapiganie,ila tukiwa ndani si wenzetu.

hizo ndizo lugha tricky za west ambazo wengi duniani huwa hawazielewi, badala yake hushsngaa hiyo mifano ikitwa tena miovu.
 
Mauaji ya Mwangosi yamesababishwa na Chadema baada ya kukataa kutii sheria bila shuruti.

wewe unafikiri kigaidi...kuwa asiyetaka kutawaliwa basi ni mkosefu..asiyekupenda(ingawa anaweza kuwa pi ahakuchukii) ni adui.hembu kaazime hata kichwa km kutumia natural reflex ndio kunakufikisha hapa.
 
this is a controversial tour? why defending it so too much? wenyeji tumesema hatutaki kutembelewa kwann mgeni alazimishe?
 
hivi mauaji ya akina Mwangosi, mateso ya Ulimboka, kibanda etc. ni sehemu ya utawala bora?

nitajie nchi ambako watu hawafi wala kuuawa. Marekani kwenyewejuzi juzi tu mtu kutoka Chencya aliua jee tuseme ni serikali ya Marekani ndiyo iliyomuua? Watanzania wengine ni wa ajabu sana kila kukicha lawama tu zisizo na maana. Nani alikuambia Ulimboka kama aliteswa na serikali. Je, Kibanda naye ameteswa na serikali? Je yule akari aliyemua Mwangosi naye altumwa na serikali? Kama ndivyo mbona amefikishwa mahakamani?.
 
Wana jf tujitokeze kwa wingi kumlaki mgeni wetu obama
 
Back
Top Bottom