Marekani yakosoa utawala wa Nigeria

Marekani yakosoa utawala wa Nigeria

Bujibuji Simba Nyamaume

Platinum Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
78,144
Reaction score
166,082
Marekani yakosoa utawala wa Nigeria

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Hillary Clinton amekosoa vikali utawala wa Nigeria kwa kutowajibikia majukumu yake vilivyo.
Bi Clinton amesema hali mbaya ya maisha nchini Nigeria imesababisha wananchi wengi na hasa vijana kuhisi kwamba wametengwa na sasa wamekuwa walengwa wa makundi ya kigaidi ambayo yanawasajili na kuanza kuwapa mafunzo ya itikadi kali.
Amezungumzia ongezeko la machafuko na uasi nchini Nigeria na kisa cha raia wa Nigeria Umar Farouk Abdulmutallab, ambaye anadaiwa kuhusika katika jaribio la kuidungua ndege katika anga za marekani mnamo siku ya krismasi.
Bi Clinton na Rais Barack Obama wameweka mbele kampeini ya kuwezesha utawala bora barani Afrika katika agenda yao.
 
Wameanza taratiiiiiibu, baadae utasikia Nigeria inaingia kwenye black list. Ikifika huko nitaanza kuamini kweli Marekani wanafanya haya mambo wenyewe (kama vile kumpandikiza kijana wa kiNigeria kwenye ndege yao akijaribu kuilipua) ili kuhalalisha uvamizi kwa Nigeria

Ngoja tuone
 
Back
Top Bottom