Marekani: Wakutwa wanauza bleach wakidai inatibu UKIMWI

101 East

JF-Expert Member
Feb 25, 2015
1,040
2,121
Watu wanne wa familia moja kutokea jimbo la Florida nchini Marekani wamepatikana na hatia kwa kosa la kuuza dawa ya kuondoa madoa sugu kwenye nguo ‘bleach’ yenye sumu kama tiba ya magonjwa mbalimbali yakiwemo Saratani ya Ubongo, Corona na virusi vya UKIMWI kupitia kanisa lao linaloendeshwa mtandaoni.

Mahakama ya shirikisho la jiji la Miami ilimkuta na hatia Mark Grenon (65) na Watoto wake watatu Jonathan (37) Joseph (35) na Jordan (29) na hatia ya kula njama ya kuwatapeli Raia wa Marekani na kuuza dawa za kuondoa madoa kwenye nguo kuwa kama dawa za kutibu magonjwa.

Shtaka hilo hubeba kifungo cha hadi miaka mitano jela ambapo hukumu yao inatarajiwa kutolewa Oktoba 6, 2023.

Kanisa la Familia ya Bradenton liitwalo ‘Genesis II, Church of Health and Healing’ liliuza kile kilichojulikana kama dawa ya muujiza na uponyaji kufikia thamani ya dola milioni 1 (Tsh Bil 2.4) ambapo Watu hawa waliwaaminisha Raia kuwa dawa hii ni tiba ya 95% ya magonjwa sugu yakiwemo Corona, ugonjwa wa kusahau kwa wazee ‘Alzheimer's’, Saratani ya ubongo, VVU/UKIMWI na vinginevyo waendesha mashtaka walisema kumbe muda wote walikuwa wanauza “chlorine di oxide” ambayo hutumika kama dawa ya kutibu maji na kusafisha nguo. #MillardAyoUPDATES
 
Back
Top Bottom