Marekani inakaribia kufunga mlango wake karibu nusu kwa Afrika…

Marekani inakaribia kufunga mlango wake karibu nusu kwa Afrika…

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,244
Reaction score
1,213
VCG41N854169152.jpg

Marekani imenyanyua tena "upanga wake wa viza", safari hii ukielekea kwa nguvu zaidi Afrika. Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Marekani vinavyoanika nyaraka za serikali, Rais Donald Trump anapanga kuongeza orodha ya nchi zinazopigwa marafuku raia wake kuingia Marekani katika wiki kadhaa zijazo. Kati ya nchi 36 mpya, 26 ziko barani Afrika! Pamoja na orodha iliyotangazwa mapema mwezi huu, raia wa nchi 36 kati ya nchi 54 za Afrika watakabiliwa na marufuku kamili au nusu kuingia Marekani. Afrika, bara linalochukuliwa kama "bara lenye matumaini", linakaribia kuwa eneo kuu kabisa ambalo Marekani "itakataza kikamilifu".

Sababu za Marekani? Ni za kusemasema tu

Katika kumbukumbu yake, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio alizipa nchi hizo siku 60 za "kujirekebisha" ili kufikia "viwango". Je, viwango ni vipi? Kumbukumbu hiyo haielezi wazi, lakini inataja sababu kadhaa za marufuku hiyo:

"kuunga mkono ugaidi"; vitambulisho visivyo vya kuaminika; rekodi za uhalifu zisizoweza kuthibitishwa; Uuzaji wa uraia kwa watu wasioishi katika nchi hizo; Kiwango cha juu cha wanaokaa Marekani bila viza; kutotoa ushirikiano wa kurudisha raia wanaofukuzwa Marekani, n.k

Ufumbuzi ni nini? Rubio "kwa ukarimu" amependekeza: Nchi hizo zinaweza kukubali kupokea raia wa nchi nyingine wanaofukuzwa na Marekani, au kuchukua nafasi ya "Nchi Salama ya Tatu" kupokea wahamiaji wanaotafuta hifadhi Marekani. Ajabu, mipango ya hila ya Marekani inaonekana hadi kuvuka bahari ya Atlantiki!

Wakati akitangaza orodha ya kwanza ya marufuku ya kuingia Marekani, Trump alitumia tukio la mashambulizi yaliyotokea jimboni Colorado akionyesha "hatari kubwa" ya "wageni wasiokaguliwa". Lakini hali halisi ni kuwa mtuhumiwa alitoka Misri (nchi iliyoko kwenye orodha inayozingatiwa), lakini nchi aliyoishi Kuwait haiko kwenye orodha. Mantiki hiyo ya Marekani imeepuka kabisa na baadhi ya "mashirika".

Wakosoaji wamesema wazi: Kutoka marufuku ya kuingia Marekani kwa raia wa nchi 7 hapo awali, hadi sasa nchi 26 mpya za Afrika, mara nyingi zinazolengwa ni nchi zenye watu weusi, zenye mapato ya chini. "Urithi" uliobatilishwa na Biden, Trump anaonekana kuwa anataka "kuurithi maradufu na kuuendeleza"!

Ni nani anayeathiriwa na kuuzwa zaidi?

Takwimu za Taasisi ya Sera za Uhamiaji Marekani zinaonyesha kuwa: kati ya wahamiaji milioni 44 Marekani, takriban milioni 2 wanatoka nchi za Afrika, nao ndio kikundi kinachokua kwa kasi zaidi hivi karibuni. Wengi wao wana shahada za juu, na ndio kikundi kikubwa zaidi cha wahamiaji kwenye soko la nguvu kazi Marekani. Nigeria, Ethiopia, Ghana, Misri... nchi hizi zilizopo kwenye “orodha inayozingatiwa", ndizo zimepeleka watu wenye ujuzi zaidi Marekani. Wataalamu wanaonya: marufuku hiyo ikitekelezwa, kwa raia wa Afrika ambao hawajapata uraia wa Marekani itakuwa ni kama "amri ya kuwashika" – kuondoka kwao Marekani kunaweza kumaanisha kushindwa kurudi tena, na familia zitavunjika.

Kwa Marekani, sio tu itapoteza mawasiliano ya watu, bali pia fursa kubwa za ushirikiano.

Mkurugenzi wa Mradi wa Dunia ya Kusini katika Taasisi ya Washauri Bingwa ya Quincy Marekani Sarang Shidore ametoa onyo kali kuwa marufuku ya viza ni kama "kujenga ukuta". Anaikumbusha Marekani kuwa "Afrika ni muhimu sana kwa Marekani kwa sababu ina maliasili nyingi, masoko yanayokua na idadi kubwa ya watu wenye vipaji." Je, Marekani inataka kukataza uhamiaji wa watu huku ikitawala peke yake masoko ya maliasili barani Afrika? Hakuna jambo zuri kama hilo duniani!

Kufunga mlango ni sawa na kupoteza siku zijazo

Kwa kutumia jina la "usalama" na "kufuata kanuni", serikali ya Marekani inatumia marufuku ya viza kama silaha, lakini inachofanya kwa kweli ni "kujifungia ndani kama kwenye kuta" na kujidhuru wakati ikidhuru wengine. Inaharibu maisha na matumaini ya mamilioni ya watu wa kawaida, inasababisha kujitenga na bara lote la Afrika lenye uwezo mkubwa, na kuacha fursa ya ushirikiano wa watu wenye vipaji, masoko na maliasili muhimu.

Hata hivyo, athari mbaya zaidi ni kwamba, kutoka ushuru wa upande mmoja hadi vikwazo vya viza, ukuta inaojenga Marekani kwa kasi unaonyesha waziwazi kiburi, upendeleo na mawazo yake finyu, na kupeleka fursa kwa mikono yake miwili kwa wenzake ambao wanafungua milango yao na kuwatendea watu kwa usawa. Mapema mwezi huu, China ilitangaza kuondoa kabisa ushuru wa bidhaa kutoka nchi 53 za Afrika zenye uhusiano nao wa kidiplomasia, na kuonesha kwa vitendo namna ya kujenga pamoja jumuiya yenye mustakabali wa pamoja kati ya China na Afrika katika hali zote. Nchi za Afrika zinaona yote haya, na mioyoni mwao wana kipimo.
 
Hivi TZ ilikuwa confirmed hakuna visa? Ukanda huu ni Kenya na Rwanda tuu confirmed hawana zuio
 
afrika > 60% ni muslim, shida iko hapo, too much suffrering …
 
Ila hua nikimuangalia trump, ni hamnazo kabsa.
  • Ni mbaguzi
  • ni mbinafsi
Pia ana maamuzi anayojua yey tu, cjui hana washauri!

Kipindi cha corona aliduwaa jins magufuri anavopambana zid ya covid-19 na uchumi.
 
Hivi TZ ilikuwa confirmed hakuna visa? Ukanda huu ni Kenya na Rwanda tuu confirmed hawana zuio
Ilikuwa njiani kupigwa ban, ila imeshajisalimisha.

Tanzania ni nchi ya ajabu sana, ni mbinde kwa Mmatumbi jupata passport, lakini ndiyo nchi ambayo waarabu, Wahindi na Wasomali wana passport zake kwa wingi kuliko wamatumbi wenyewe.

Ukitaka upate passport kirahisi nenda uhamiaji ukiwa unatafuna tambuu au pilipili au ongea kwa lafudhi ya kutema makohozi (Kisomali) hapo utahudumiwa kama VIP.

Wasomali wanakuja huko bongo , wanafungua maduka ya ya kuuza mapazia na used computers Kariakoo , hayo maduka ni vijiwe/mitandao ya kupokelea ndugu zao kuwatafutia passport na nauli za kwenda nchi za Ulaya na Marekani. Wanashinda wanazurura kariakoo na Arusha kwa miezi mitatu hadi 6 wengine hadi miaka 5, baada ya hapo mtandao wao unakuwa uneshawafanyia michakato ya passport na vibali wanaondoka nchini kama wabongo.

Mataifa kama Somalia, Yemen, Iran, Burundi na Rwanda (Kwa Rwanda wale wapo associated na Jeshi hasa kule East Congo), Wengi hutumia passport za Tanzania. Tanzania ni hub yao, kukaa huko bongo hadi miaka 7 wakitengeneza attachments na Tanzania ili wajulikane kuwa ni watanzania waweze kupata Visa. Networks zao zipo hadi serikalini na kwenye Idala.
 
Ilikuwa njiani kupigwa ban, ila imeshajisalimisha.

Tanzania ni nchi ya ajabu sana, ni mbinde kwa Mmatumbi jupata passport, lakini ndiyo nchi ambayo waarabu, Wahindi na Wasomali wana passport zake kwa wingi kuliko wamatumbi wenyewe.

Ukitaka upate passport kirahisi nenda uhamiaji ukiwa unatafuna tambuu au pilipili au ongea kwa lafudhi ya kutema makohozi (Kisomali) hapo utahudumiwa kama VIP.

Wasomali wanakuja huko bongo , wanafungua maduka ya ya kuuza mapazia na used computers Kariakoo , hayo maduka ni vijiwe/mitandao ya kupokelea ndugu zao kuwatafutia passport na nauli za kwenda nchi za Ulaya na Marekani. Wanashinda wanazurura kariakoo na Arusha kwa miezi mitatu hadi 6 wengine hadi miaka 5, baada ya hapo mtandao wao unakuwa uneshawafanyia michakato ya passport na vibali wanaondoka nchini kama wabongo.

Mataifa kama Somalia, Yemen, Iran, Burundi na Rwanda (Kwa Rwanda wale wapo associated na Jeshi hasa kule East Congo), Wengi hutumia passport za Tanzania. Tanzania ni hub yao, huwezi kukaa huko bingo hata miaka 7 wakitengeneza attachment na Tanzania i wajulikane kuwa ni watanzania. Networks zao zipo hadi serikalini na kwenye Idala.
Mkuu hao uliowataja wanasaidiana na kupeana habari so kama mmoja ana network basi ujue wote watanufaika. Na rushwa pia inachangia hii kumzungusha mtu kupata passport ni kujenga mazingira ya rushwa. Hapo kwenye kutafuna tambuu mkuu 🤣
 
Ilikuwa njiani kupigwa ban, ila imeshajisalimisha.

Tanzania ni nchi ya ajabu sana, ni mbinde kwa Mmatumbi jupata passport, lakini ndiyo nchi ambayo waarabu, Wahindi na Wasomali wana passport zake kwa wingi kuliko wamatumbi wenyewe.

Ukitaka upate passport kirahisi nenda uhamiaji ukiwa unatafuna tambuu au pilipili au ongea kwa lafudhi ya kutema makohozi (Kisomali) hapo utahudumiwa kama VIP.

Wasomali wanakuja huko bongo , wanafungua maduka ya ya kuuza mapazia na used computers Kariakoo , hayo maduka ni vijiwe/mitandao ya kupokelea ndugu zao kuwatafutia passport na nauli za kwenda nchi za Ulaya na Marekani. Wanashinda wanazurura kariakoo na Arusha kwa miezi mitatu hadi 6 wengine hadi miaka 5, baada ya hapo mtandao wao unakuwa uneshawafanyia michakato ya passport na vibali wanaondoka nchini kama wabongo.

Mataifa kama Somalia, Yemen, Iran, Burundi na Rwanda (Kwa Rwanda wale wapo associated na Jeshi hasa kule East Congo), Wengi hutumia passport za Tanzania. Tanzania ni hub yao, huwezi kukaa huko bingo hata miaka 7 wakitengeneza attachment na Tanzania i wajulikane kuwa ni watanzania. Networks zao zipo hadi serikalini na kwenye Idala.
Ni kweli suala hili Serikali inapaswa kulifatilia kwa karibu sana.
 
Mazoea ya tabu yake kujitegemea ndio suluhisho, lakini ulafi na tamaa za kujipendekeza kwa wamarekani ndio umetufikisha hapo
 
Back
Top Bottom