Marekani imelitungua puto la kichina

πŸ€£πŸ€£πŸ€£πŸ€£πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»
 

Attachments

  • FB_IMG_1675693848572.jpg
    109 KB · Views: 9
Balloon lilikuwa na self destruct mechanism

Balloon lilikuwa na urefu wa ft 200

Debris zimetapakaa sawa na viwanja 15 vya mpira

Wamekuta mabaki ya bomu dogo

Lilizuiwa transmit taarifa tokea lilipoingia anga la marekani

Mabaki yake yana uzito wa zaidi ya ndege ya abiria 70, Embraer
 
Too late. Wachina washasave info. Ila Wachina nao bwana. Wamechemsha, walitakiwa waliset ili lisionekane.
Katika wachangiani wote wewe ndio umetoa komenti ya maana sana.
Kuja watu wanasema walisubiri ili lifike baharini.
Sasa wakati wanasubiri si tayari limeshapeleka taarifa muhimu..
Kulitungua TU hata JWTZ tungeweza.
Cha muhimu walitakiwa walitungue mapema ili kama ni la kipelelezi lisipate habari nyingi muhimu.
Kama ulivyosema" too late"
 
Kwa nini wachina watumie spy balloon wakati wa satellite na stealth jets .......hivi vingefaa zaidi kwenye uchunguzi......
Unawezekana walikuwa wanatafuta sababu ya kudungua kifaa chochote cha west
 
puto lishajizungukia vya kutosha kwenye anga lenu na kukusanya taarifa zake na kumtumia Mchina ndio mnakuja kulilipua halafu mnajitangaza, bora mngelipua kimya kimya.!
Huwa nafurahia sana kusoma comments za sisi wabongo tunavyoyajua mambo ya US kwa ndani zaidi kuliko hata Pentagon na CIA
 
[emoji115]
Kumbe Marekani ni wa hovyo hivi? So hata Rais kila kitu anakikuta kimeshapangwa?

Ulipenda wawe kama Marais wa kwetu,kila anaeingia kutawala anafuta kila kitu cha mtangulizi wake na anaanza upya? Akija mwingine na yeye anafuta vya mtangulizi wake na kuanza upya. Ndiyo maana tutaendelea kuwa hivi hivi kwa miaka mingi ijayo.
 
Huawei mobile anatumia Harmony OS.. Kuna KylinOS, UOS na nyingine nyingi.
 
Huawei mobile anatumia Harmony OS.. Kuna KylinOS, UOS na nyingine nyingi.
Enhe mkuu umejikakamua, emu niambie nani duniani saivi amekuwa convinced kutumia hivyo vijiprogram vya kichina, kwa sababu naona hata rasis wao Xi Jinping anatumia iphone (iOS) pro max 14

Hivyo viprogram ulivyovitaja wameiba mambo mengi toka kwenye Android na iOS na karibuni walitishiwa kuzimwa wakaomba radhi, Hata russia walipotaka kuwekewa vikwazo vya kutumia iOS waliomba poo sana kuiangukia US wanaomba waachiwe watumie simu za iphones
 
Ulishajiuliza ni kwa nini Trump alipiga marufuku wafanyakazi wa ofisi za umma wasitumie Huawei & ZTE? Na majibu kwa upande wa China yalikuwaje?
 
USA ni nchi ya kipekee sana. Watu kutoka nchi mbalimbali wameshika nafasi kubwa na wanatambulika kama raia wa Marekani.
Unaweza ukamkuta mhindi kutoka india lkn ni mkuu wa polisi jimbo fulani.
UK pia, muhindi kawa Waziri Mkuu wao.
 
Marekani muisikie tu...ukitaka kujua kiwango cha ujinga ndani ya taifa hili pitia thread kama hizi!
Wabongo tuna ujuaji mwingi wa maswala ya security ya US kuliko hata CIA wenyewe.
 
Nimepatwa na wasiwasi juu ya uwezo wa teknolojia ya military defence ya USA. Siamini tena kwenye yake wanayotuaminishaga kwamba wao wako zaidi kwenye masuala ya kiulinzi na usalama hasa zile ndege BAT. Puto limekaa siku mbili juu ya mitambo ya nukse za USA. Mmmmmh!



MAGUFULI4LIFE.
 
Huwa nafurahia sana kusoma comments za sisi wabongo tunavyoyajua mambo ya US kwa ndani zaidi kuliko hata Pentagon na CIA
Mbona vitu vyao viko wazi ni wewe ma bando lako?

Au ulitaka wawe wachawi kama jwtz?
 
Jazia
DRC na M23
Mr Slim na DRC
Ruto na Makabaila wenye ardhi kubwa
 
Mbona vitu vyao viko wazi ni wewe ma bando lako?

Au ulitaka wawe wachawi kama jwtz?
Wanakuwekea wazi vile wanavyotaka wewe ujue kwakuwa kwao havina madhara tena.Point yangu ni kuwa mtu anacomment as if anazijua classified Info zote za Security ya US.
 
Mchina na sayansi wapi na wapi?Wawashukuru wazungu kwa kuwafundisha sayansi. China bado sana ,wao wanachojua ni kucopy tu.
Sijui nikujibu nini!! Yaani kwa mawazo yako sayansi inamaanisha nini kwako?? Labda tuanzie hapo-kuna imani/dhana nyingine zinashangaza sana sana.
 
Mchina alivumbua nini?
Waswahili bwana!! Yaani huna hata habari kwamba karatasi unayo tumia hivi sasa wavumbuzi wake walikiwa ni wachina na sio wazungu, pia kalamu na wino wavumbuzi wake ni wachina haya tuje kwenye highly accurate mathematical calculator au tuseme manual komputa (abacus)walikuwa ni wachina na zinafanya kazi mpaka leo, tukija kwenye uvumbuzi wa gunpowder na solid fuel rockets na mizinga wavumbuzi ni wachina vile vile, utangenezaji nguo including silk kwa kutumia manual looms ni uvumbuzi wa wachina, hapo hatujagusia utengenezaji wa saani za chakula, vikombe sourcers,birika za chai etc.

Zipo vile vile manual duplicating machine, unatumia karatasi special na pen una andika alphanumerical charaters zako pamoja na diagrams inclunding graphs and what have you baadae unaweka master kwenye flat surface unatumia wino na roller unatoa copy hata million moja ukitaka. WALIO VIMBUA matumizi ya simaku ni Wachina walizumia kuunda compass kwa ajili ya kuongozea vyombo/Meli kuonyesha mwelekekeo kwenye vyombo vya baharini walikuwa - Haya tuje tuzungumzie masuala ya foundries za ku-forge metal na alloys ukweli ni kwamba mapioneers walikuwa ni Wachina.

Mwisho nataka kuwakumbishe kwa mara nyingine tena kwamba wanadamu wenye IQ kubwa Duniani majority ni wenye asili ya Orientals yaani: Wachina/Wajapan/Wakorea - Wachina walirudishwa nyuma kimaendeleo na kuibiwa uvumbuzi wao na mabeberu walio kuwa wanawavamia mara kwa mara kwa kuendekeza masuala ya vita vita na kuwafsnya Wachina wenyewe kwa wenyewe kuanza kupigana vita wakichonganishwa na mabeberu hao hao ksma mnavyo ona vita Vya Ukraine ni kama ndugu tu lakini wanapigani kwa maslshi ya mabeberu. Ni watu wachache wanao jua kwamba Uchina hapo zamani Uchina ilikiwa imepiga hatua kubwa sana katika masiala ya sayansi hata kuliko hao Wazungu mnao- wasujudu masaa yote!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…