Marekani iliwashitaki wapi Osama Bin Laden, Saddam Hussein? Kwanini Umoja wa Ulaya ulimuua Gadafi kama mnyama? Nani aliwawekea vikwazo?

Corticopontine

JF-Expert Member
Sep 20, 2019
664
1,272
Hawa wanajiita Wanademokrasia ndio waliwaua Sadam, Osama na Abubakar

Waliwashitaki Mahakama gani? Kwanini Umoja wa Ulaya ulimuua Gadafi kama mnyama? Nani aliwawekea vikwazo?
 
Kwani jambazi akikutwa kaua na akatakwa kukamatwa kwa kutumiwa nguvu si huwa anauliwa

Hawa washauwa watu wengi na ushahidi upo wazi
 
Sadam alihukumiwa kunyongwa na mahakama za huko Iraq, Osama alifariki katika harakati za kumkamata ( japo mimi siamini kama USA walikuwa wanamtafuta kweli).
Hawa wanajiita Wanademokrasia ndio waliwaua Sadam, Osama na Abubakar waliwashitaki Mahakama gn?
 
Ndugu itabidi uwe mpole tu. Katika dunia hii hamna taifa linaweza kuweka vikwazo dhidi nchi za magharibi. Labda miaka inayokuja huko mbeleni.
Hata hii platform ya JF unayotumia imeanzia huko kwa hawa jamaa.
 
Ngoja nianze na Osama Bin Laden

Afghanistan ilikuwa katika hali ya vita ya wenyewe kwa wenyewe na miezi michache baada ya kufika kwa Osama kundi la Taliban lilivamia mji mkuu wa Kabul na kutangaza
Emirati ya Afghanistan likaendelea kutawala sehemu kubwa ya nchi.

Katika maeneo yaliyokuwa chini ya serikali ya Taliban Osama aliweza kuanzisha makambi mbalimbali alipopokea na kufunza wanajihadi kutoka nchi mbalimbali. Pamoja na Aiman az-Zawahiri alitoa tamko la fatwa mnamo tar. 23 Februari 1998 waliposema "Kuwaua Wamarekani na wanaoshikamana nao -kama ni wanajeshi au watu raia- ni wajibu wa kila Mwislamu mwenye uwezo wa kuyatekeleza katika nchi yoyote kwa kusudi la kuleta ukombozi wa msikiti wa al Aqsa na Masjid al-Haram (msikiti wa Makka) na kuwafukuza wanajeshi wao kutoka nchi zote za Uislamu ..

Kwa msaada wa Mungu tunamwita kila Mwislamu anayemwamini Mungu kutekeleza amri wa Mungu na kuwaua Wamarekani na kupora pesa zao kila mahali anapoikuta"

Mwaka uleule wa 1998 mabomu mawili yalipuliwa kwenye mashambulio ya kigaidi ya 7 Agosti 1998 katika Afrika ya Mashariki dhidi ya balozi za Marekani huko Nairobi na Dar es Salaam yaliyoua zaidi ya watu 300 na kuwajeruhi maelfu. Serikali ya Marekani ilijaribu kuwashawishi viongozi wa Taliban kuwakabidhi bin Laden lakini hadi 2001 badi hawakufikia mapatano.

Tarehe 12 Oktoba 2000 wanajihadi wa al Qaida walishambulia maonowari USS Cole nchini Yemen. Tarehe 9 Septemba 2001 wapiganaji wa al Qaida walimwua mpinzani wa Taliban
Ahmad Shah Massoud kwa bomu.

Tendo hili lilifuatwa na shambulio la 11 Septemba 2001 katika Marekani lililoua takriban watu 3,000. Marekani ilidai tena Afghanitan imkabidhi bin Laden lakini viongozi wa Taliban walikataa wakadai kuonyeshwa uthebitisho. Rais Bush wa Marekani alijibu kwa kushambulia Afganistan tar. 7 Oktoba 2001; baada ya kutekwa kwa Kabul bin Laden alikimbia kwenye mipango ya milima ya Tora Bora na kutoka huko katika maeneo ya Pakistan kaskazini-mashariki ambako serikali ya taifa ilikuwa na athira ndogo.

Jitihada wa Wamarekani kumkamata zilikuwa bila mafanikio. Inaaminiwa ya kwamba Osama bin Laden aliendelea kujificha nchini Pakistan, labda kwa msaada wa sehemu ya huduma ya usalama ya kijeshi ya nchi hiyo. Alitoa matagazo mbalimbali kwa njia ya kanda za video zilizosambazwa duniani kwa njia ya intaneti.

Kuna dalili ya kwamba aliishi kwa siri tangu mwaka 2006 katika mji wa Abbottabad kwenye nyumba alipouawa mwaka 2011.

Nitarejea mkuu.....
 
Saddam Hussein Abd al-Majid al-Tikriti

28 Aprili 1937 - 30 Desemba 2006 ) alikuwa Rais wa Iraki , kuanzia tarehe 16 Julai 1979 hadi mwaka wa 2003 , pia waziri mkuu wa Iraki kati ya 1994 na 2003.
Alipanda ngazi ndani ya serikali na chama cha
Baath kama makamu wa rais aliyemtangulia
Ahmad Hasan al-Bakr . Baada ya kupewa cheo cha rais aliua wapinzani wengi na kuimarisha
utawala wake.
Akaanzisha vita mbili :

Vita kati ya Irak na Uajemi ( 1980 - 1988 ) aliyoanzisha baada ya kuona jeshi la Uajemi lilidhoofishwa kutokana na mapinduzi ya
Ayatollah Khomeini, na baadae alishindwa kufikia shabaha zake, akalazimishwa kukubali
mkataba wa kusalimu amri na Uajemi.
Vita ya Ghuba ya 1990/91 alipoamuru jeshi la Iraki kuvamia nchi jirani ya Kuweit. Kisha hatua hii ilijibiwa na amri ya Umoja wa Mataifa Wairaki waondoke tena, walipokataa jeshi la kimataifa lililoongozwa na Marekani lilifukuza Wairaki katika Kuwait.
Ndani ya Iraki alipigania upinzani wa sehemu kubwa za wananchi hasa katika kampeni dhidi ya Wakurdi kaskazini mwa Iraki wakati wa vita dhidi ya Uajemi na dhidi ya Washia wa Iraki Kusini baada ya vita ya Ghuba.
Saddam Hussein aliondolewa madarakani wakati wa uvamizi wa Iraki na Marekani katika vita ya pili ya ghuba mwaka 2003. Alienda mafichoni kwa miezi kadhaa, akakamatwa na kupelekwa mbele ya mahakama ya Kiiraki iliyompa adhabu ya kifo kwa jinai dhidi ya
binadamu na hasa kesi 148 za mauaji zilizothibitishwa mahakamani.
Alinyongwa Desemba 2006 katika kambi la kijeshi mjini Al Kadhimiya nchini Iraki.
 
Abu Bakr al-Baghdadi

Huyu baba aliyesakwa sana na nchi mbalimbali za dunia, alichukuliwa kama mhusika mkuu wa mauaji na mateso ya aina mbalimbali nchini Iraq na Syria na mashambulizi mabaya katika nchi kadhaa.
Abu Bakar al-Baghdad alikuwa kiongozi aliyejitangaza rasmi mnamo mwaka 2014 na kuongoza kwa mkono wa chuma watu milioni 7 nchini Iraq na Syria.
Abu Bakar al-Baghdad alofariki dunia baada ya kujilipua mwenyewe kwa mkanda uliojaa vilipuzi wakati akikimbilia katika shimo lililochimbwa kwa usalama wake. Watoto wake watatu walikufa pamoja naye.
 
beberu jingine hili.

tusaidie kazi ya mahakama ya The Heague ni zipi kuhusiana na uharifu wa kivita endapo mtashabikia risasi na mabomu ndio iwe hukumu?
Kwani jambazi akikutwa kaua na akatakwa kukamatwa kwa kutumiwa nguvu si huwa anauliwa

Hawa washauwa watu wengi na ushahidi upo wazi
 
nakutogirwe sana nkoi.
Abu Bakr al-Baghdadi

Huyu baba aliyesakwa sana na nchi mbalimbali za dunia, alichukuliwa kama mhusika mkuu wa mauaji na mateso ya aina mbalimbali nchini Iraq na Syria na mashambulizi mabaya katika nchi kadhaa.
Abu Bakar al-Baghdad alikuwa kiongozi aliyejitangaza rasmi mnamo mwaka 2014 na kuongoza kwa mkono wa chuma watu milioni 7 nchini Iraq na Syria.
Abu Bakar al-Baghdad alofariki dunia baada ya kujilipua mwenyewe kwa mkanda uliojaa vilipuzi wakati akikimbilia katika shimo lililochimbwa kwa usalama wake. Watoto wake watatu walikufa pamoja naye.
 
Ngoja nianze na Osama Bin Laden

Afghanistan ilikuwa katika hali ya vita ya wenyewe kwa wenyewe na miezi michache baada ya kufika kwa Osama kundi la Taliban lilivamia mji mkuu wa Kabul na kutangaza
Emirati ya Afghanistan likaendelea kutawala sehemu kubwa ya nchi.

Katika maeneo yaliyokuwa chini ya serikali ya Taliban Osama aliweza kuanzisha makambi mbalimbali alipopokea na kufunza wanajihadi kutoka nchi mbalimbali. Pamoja na Aiman az-Zawahiri alitoa tamko la fatwa mnamo tar. 23 Februari 1998 waliposema "Kuwaua Wamarekani na wanaoshikamana nao -kama ni wanajeshi au watu raia- ni wajibu wa kila Mwislamu mwenye uwezo wa kuyatekeleza katika nchi yoyote kwa kusudi la kuleta ukombozi wa msikiti wa al Aqsa na Masjid al-Haram (msikiti wa Makka) na kuwafukuza wanajeshi wao kutoka nchi zote za Uislamu ..

Kwa msaada wa Mungu tunamwita kila Mwislamu anayemwamini Mungu kutekeleza amri wa Mungu na kuwaua Wamarekani na kupora pesa zao kila mahali anapoikuta"

Mwaka uleule wa 1998 mabomu mawili yalipuliwa kwenye mashambulio ya kigaidi ya 7 Agosti 1998 katika Afrika ya Mashariki dhidi ya balozi za Marekani huko Nairobi na Dar es Salaam yaliyoua zaidi ya watu 300 na kuwajeruhi maelfu. Serikali ya Marekani ilijaribu kuwashawishi viongozi wa Taliban kuwakabidhi bin Laden lakini hadi 2001 badi hawakufikia mapatano.

Tarehe 12 Oktoba 2000 wanajihadi wa al Qaida walishambulia maonowari USS Cole nchini Yemen. Tarehe 9 Septemba 2001 wapiganaji wa al Qaida walimwua mpinzani wa Taliban
Ahmad Shah Massoud kwa bomu.

Tendo hili lilifuatwa na shambulio la 11 Septemba 2001 katika Marekani lililoua takriban watu 3,000. Marekani ilidai tena Afghanitan imkabidhi bin Laden lakini viongozi wa Taliban walikataa wakadai kuonyeshwa uthebitisho. Rais Bush wa Marekani alijibu kwa kushambulia Afganistan tar. 7 Oktoba 2001; baada ya kutekwa kwa Kabul bin Laden alikimbia kwenye mipango ya milima ya Tora Bora na kutoka huko katika maeneo ya Pakistan kaskazini-mashariki ambako serikali ya taifa ilikuwa na athira ndogo.

Jitihada wa Wamarekani kumkamata zilikuwa bila mafanikio. Inaaminiwa ya kwamba Osama bin Laden aliendelea kujificha nchini Pakistan, labda kwa msaada wa sehemu ya huduma ya usalama ya kijeshi ya nchi hiyo. Alitoa matagazo mbalimbali kwa njia ya kanda za video zilizosambazwa duniani kwa njia ya intaneti.

Kuna dalili ya kwamba aliishi kwa siri tangu mwaka 2006 katika mji wa Abbottabad kwenye nyumba alipouawa mwaka 2011.

Nitarejea mkuu.....

Mkuu Ungeanzia 1979 wakati Soviet army walipovamia Afghanistan na mpaka USA kumtumia Osama kwa mapambano dhidi ya Soviet na kupelekea jeshi la soviet kupoteza watu 15,000
Hilo moja
Kwa hiyo Osama alikuwa ni kamanda aliesomea USA na kuajiriwa na wao
Hapo ndio naendeleza historia yako

Kuhusu Iraq uzuri nilikuwa huko tangu vita ya inaanza yaani 22/September 1980 na mpaka inaisha na uvamizi wa Saddam huko Kuwait pia nilikuwepo

Ila mengi yamesemwa na ukweli upo kwa wengi walioshuhudia au kuwepo
Ni hayo tu
 
Tatizo wewe umesoma maandishi ya wamarekani, Osama katengenezwa na wamarekani kapewa mipango na wao ya kuunda Taliban na akaiteka Afghanistan, we jiulize nani huwa anawauzia hayo makundi ya Kigaidi kama Taliban, Isil, Alshababu, Bokoharam nk, na je kwanini USA na Washirika wake hawawekei vikwazo wale wanaowauzia hayo makundi zana za kivita?
Ngoja nianze na Osama Bin Laden

Afghanistan ilikuwa katika hali ya vita ya wenyewe kwa wenyewe na miezi michache baada ya kufika kwa Osama kundi la Taliban lilivamia mji mkuu wa Kabul na kutangaza
Emirati ya Afghanistan likaendelea kutawala sehemu kubwa ya nchi.

Katika maeneo yaliyokuwa chini ya serikali ya Taliban Osama aliweza kuanzisha makambi mbalimbali alipopokea na kufunza wanajihadi kutoka nchi mbalimbali. Pamoja na Aiman az-Zawahiri alitoa tamko la fatwa mnamo tar. 23 Februari 1998 waliposema "Kuwaua Wamarekani na wanaoshikamana nao -kama ni wanajeshi au watu raia- ni wajibu wa kila Mwislamu mwenye uwezo wa kuyatekeleza katika nchi yoyote kwa kusudi la kuleta ukombozi wa msikiti wa al Aqsa na Masjid al-Haram (msikiti wa Makka) na kuwafukuza wanajeshi wao kutoka nchi zote za Uislamu ..

Kwa msaada wa Mungu tunamwita kila Mwislamu anayemwamini Mungu kutekeleza amri wa Mungu na kuwaua Wamarekani na kupora pesa zao kila mahali anapoikuta"

Mwaka uleule wa 1998 mabomu mawili yalipuliwa kwenye mashambulio ya kigaidi ya 7 Agosti 1998 katika Afrika ya Mashariki dhidi ya balozi za Marekani huko Nairobi na Dar es Salaam yaliyoua zaidi ya watu 300 na kuwajeruhi maelfu. Serikali ya Marekani ilijaribu kuwashawishi viongozi wa Taliban kuwakabidhi bin Laden lakini hadi 2001 badi hawakufikia mapatano.

Tarehe 12 Oktoba 2000 wanajihadi wa al Qaida walishambulia maonowari USS Cole nchini Yemen. Tarehe 9 Septemba 2001 wapiganaji wa al Qaida walimwua mpinzani wa Taliban
Ahmad Shah Massoud kwa bomu.

Tendo hili lilifuatwa na shambulio la 11 Septemba 2001 katika Marekani lililoua takriban watu 3,000. Marekani ilidai tena Afghanitan imkabidhi bin Laden lakini viongozi wa Taliban walikataa wakadai kuonyeshwa uthebitisho. Rais Bush wa Marekani alijibu kwa kushambulia Afganistan tar. 7 Oktoba 2001; baada ya kutekwa kwa Kabul bin Laden alikimbia kwenye mipango ya milima ya Tora Bora na kutoka huko katika maeneo ya Pakistan kaskazini-mashariki ambako serikali ya taifa ilikuwa na athira ndogo.

Jitihada wa Wamarekani kumkamata zilikuwa bila mafanikio. Inaaminiwa ya kwamba Osama bin Laden aliendelea kujificha nchini Pakistan, labda kwa msaada wa sehemu ya huduma ya usalama ya kijeshi ya nchi hiyo. Alitoa matagazo mbalimbali kwa njia ya kanda za video zilizosambazwa duniani kwa njia ya intaneti.

Kuna dalili ya kwamba aliishi kwa siri tangu mwaka 2006 katika mji wa Abbottabad kwenye nyumba alipouawa mwaka 2011.

Nitarejea mkuu.....
 
Mkuu Ungeanzia 1979 wakati Soviet army walipovamia Afghanistan na mpaka USA kumtumia Osama kwa mapambano dhidi ya Soviet na kupelekea jeshi la soviet kupoteza watu 15,000
Hilo moja
Kwa hiyo Osama alikuwa ni kamanda aliesomea USA na kuajiriwa na wao
Hapo ndio naendeleza historia yako

Kuhusu Iraq uzuri nilikuwa huko tangu vita ya inaanza yaani 22/September 1980 na mpaka inaisha na uvamizi wa Saddam huko Kuwait pia nilikuwepo

Ila mengi yamesemwa na ukweli upo kwa wengi walioshuhudia au kuwepo
Ni hayo tu
Mkuu, kwakuwa sikutaka kumchosha huyu asie ijuwa historia, basi nikiona nianzie tu hapo kati ili tusichoshane tu... Maana nilikuwa tayari nimefika nusu Whatever-Vant kubwa....
 
Back
Top Bottom