Marekani: Brazil itakabiliana na hatari iwapo itaruhusu Huawei kujenga 5G

The Evil Genius

JF-Expert Member
Mar 21, 2014
5,459
17,258
Kwa kile kinachoitwa muendelezo wa Marekani kutumia mkono wake mrefu na wenye nguvu kuiwekea vikwazo kampuni ya Huawei kutoka China, sasa mbinyo huo umeifikia Brazil.

Balozi wa Marekani nchini Brazil ameionya nchi hiyo kua itakabiliwa na hatari iwapo itairuhusu kampuni ya Huawei kujenga mitambo ya teknolojia ya 5G.

Mwezi huu mwanzoni Marekani iliiahidi serikali ya Brazil itafte mbadala wa Huawei na Marekani yuko tayari kulipia gharama za huo mbadala, yaani kati ya Nokia ama Erickson ila sio Huawei.

Brazil ndie mshirika mkubwa wa kibiashara wa Marekani (trading partner) bara la Amerika ya Kusini.

Je, Brazil itaweza kuibishia Marekani? Tusubiri tuone.

Brazil may face 'consequences' if it gives Huawei 5G access, says U.S. ambassador
 
Kwani brazil si ana mkataba wa makubaliano ya biashara kati yake na china,urusi nk na tulisikia warusi wa jf wakisema hakuna kitu kama IMF tena maana wameshakikata mikono😂😂😂

Acha tuone atakaza aende na washkaji zake,au atamsikiliza kaka mkubwa.
 
BRICS - Brazil, Russia, India, China, South Africa. Ukiacha China unadhani hao wengine wanne wako affiliated na nani zaidi kati ya US na China?
 
Hao HUWAWEI watatapika nyongo mwaka huu.

Hivi kwanini wasiende kuweka hiyo 5G yao IRAN, Russia na North Korea, maana kwingine hawataweza.

Kila watakapokanyaga US atawafukuza.
Sijui lini na wapi wataanza na kufanya uwekezaji wao humu duniani, maana naona US kakaba hadi penalt.
 
Ukiona katika mashindano yoyote mtu anacheza rafu za waziwazi hiyo ni dalili za kuanza kuelemewa au kushindwa kabisa.Yani beki unaona forward anakupita unamkumbatia ili muanguke wote hiyo sio fair kabisa...
 
Kuna wajinga humu wanamshangilia mmarekani kwa hatua hiyo bila kujua mmarekani anapambania uchumi wake huku hawa washangiliaji hata uchumi wa kuunga bando la mwezi ambalo ni unlimited hawana sad!
 
Sasa China unaemsifiwa kwa nn nae asiendeleze ubabe? Yeye kulilia tu baada ya kubanwa mbavu, aonyeshe kuwa nae anaweza
 
Masikinii marekani analialia sana,,mchina sio mtu mzuri jamani.

Hawana simu inayoweza shindana na Huawei, oppo wala samsung.
 
Ukiona katika mashindano yoyote mtu anacheza rafu za waziwazi hiyo ni dalili za kuanza kuelemewa au kushindwa kabisa.Yani beki unaona forward anakupita unamkumbatia ili muanguke wote hiyo sio fair kabisa...
Natamani kujua wewe ni chadema au CCM?
 
Natamani kujua wewe ni chadema au CCM?
Huawei wana technology tayari,US anabweka tu hapo. Marekani na nchi zote za magharibi watatumia nguvu na vitisho lakin hali yao na competitiveness ya kampuni zao inaenda ikishuka kila siku . Marekani anataka kushusha Chinese influence duniani lakin hawataweza hata kidogo. Kwa nn? Kila nchi ya ulaya matajiri ndio wanaamrisha serekali zao zifanye nn, iwe kuingia vitani,...ili waweze either kupata rasilimali za bei che au kupata soko. Hizo vita wanatumia silaha za bei ghali ambazo lazima vita ikiisha wanze kuzilipa ndipo nao wapate profit. Sheria za ulaya za minimum wages, environmental regulations, na mambo mengine anawabana sana na kuongeza cost of production. China haijawahi kuvamia nchi yoyote kusaka rasilimali za viwanda vya, Bali hutumia negotiations hata kama watakulaghai lakin ni kukosa umakini kwako. Minimum wages ipo lakin haiko juu kama Western worlds, na hata standard of life siyo expensive kama nchi za magharibi. Environmental regulations zipo China lakin siyo too tight kama Ulaya. US inachofanya ni temporary solutions na si suluhisho la kudumu. Wanaendelea kupigwa tu sehemu nyingi na wataendelea kupoteza soko kwa sababu ya tamaa zao, na gharama kubwa wanazotumia kuendesha vita ili wapate access kwenye rasilimali. Poleni wote ambao mnaunga mkono mabeberu wasiojitambua
 
Kwa kile kinachoitwa muendelezo wa Marekani kutumia mkono wake mrefu na wenye nguvu kuiwekea vikwazo kampuni ya Huawei kutoka China, sasa mbinyo huo umeifikia Brazil.

Balozi wa Marekani nchini Brazil ameionya nchi hiyo kua itakabiliwa na hatari iwapo itairuhusu kampuni ya Huawei kujenga mitambo ya teknolojia ya 5G.

Mwezi huu mwanzoni Marekani iliiahidi serikali ya Brazil itafte mbadala wa Huawei na Marekani yuko tayari kulipia gharama za huo mbadala, yaani kati ya Nokia ama Erickson ila sio Huawei.

Brazil ndie mshirika mkubwa wa kibiashara wa Marekani (trading partner) bara la Amerika ya Kusini.

Je, Brazil itaweza kuibishia Marekani? Tusubiri tuone.

Brazil may face 'consequences' if it gives Huawei 5G access, says U.S. ambassador

As long Raisi wa sasa ni Mu-Israel yule basi huawei wajiandae kupigw akikumbo, Ila mchina akijibu mapigo nauwakika brazil ataka achini kama austarlia anayo haha sasa.
 
Kuna wajinga humu wanamshangilia mmarekani kwa hatua hiyo bila kujua mmarekani anapambania uchumi wake huku hawa washangiliaji hata uchumi wa kuunga bando la mwezi ambalo ni unlimited hawana sad!

Marekani awezi toboa, anachotakiw akwasasa ni kujiunga na mchina tu na sio kupambana
 
Ukiona katika mashindano yoyote mtu anacheza rafu za waziwazi hiyo ni dalili za kuanza kuelemwa au kushindwa kabisa.Yani beki unaona forward anakupita unamkumbatia ili muanguke wote hiyo sio fair kabisa...
Wenye kunielewa mkisoma hii post naamini na nyie mtataka kujua huyu jamaa ni chadema au CCM?
 
Back
Top Bottom