Marehemu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Marehemu

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Edmund, Feb 8, 2011.

 1. E

  Edmund Senior Member

  #1
  Feb 8, 2011
  Joined: Jul 17, 2009
  Messages: 122
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Baba yangu alifariki mwaka jana mwezi wa saba, katika harakati za kufuatilia mali zake tukakuta kumbe nyumba moja imeshauzwa kwa Mpangaji anaekaa humo ndani kitambo tu. baada ya kupekua nyaraka za marehemu hatukukuta hata chembe ya "document" kuonyesha kuwa imeuzwa, Lakini katika zile hati za mauzo kati ya Marehemu yaani BABA na Mnunuzi yaani yule (Mpangaji). kuna mashahidi wa3 yaani Mununuzi, Mkewe na mtoto wao, kwa upande wa muuzaji alikuwepo pekee yake pamoja na Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa eneo husika

  JE, ni kweli haya yatakuwa mauzo halali kisheria.
   
 2. Lutala

  Lutala JF-Expert Member

  #2
  Feb 8, 2011
  Joined: Jun 17, 2010
  Messages: 845
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Siyo mauzo halali kisheria kwa kuwa mume, mke na mtoto ni kitu kimoja
   
 3. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #3
  Feb 8, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,319
  Likes Received: 22,164
  Trophy Points: 280
  Hapo mmeuziwa mbuzi kwenye junia na wala sio gunia:sad::sad::bump:
   
 4. Dreamliner

  Dreamliner JF-Expert Member

  #4
  Feb 8, 2011
  Joined: Jan 17, 2010
  Messages: 2,034
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Hiyo ni DHURUMA na WIZI
   
 5. d

  daisy Senior Member

  #5
  Feb 9, 2011
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 139
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Kuna information ambazo hujadisclose ili uweze kupatiwa ushauri mzuri wa kisheria.
  Kwanza huu mkataba wa mauzioano umefanyika lini na mbele ya nani nikimaanisha kwamba umeshuhudiwa na wakili au la.
  pili,kama marehemu baba yako alikuwa na mke na mke wake hajasaini hayo makubaliano hilo ni tatizo lingine,
  Tatu, wewe kama na ndugu zako pia wapo inaonekana hamkuwa na mahusiano mazuri kifamilia kwani kama ni kweli marehemu baba yenu aliuza kwaniani hakuwashirikisha?
  Nne,ili kuchukua hatua zozote za kusheria kuhusiana na mali za marehemu inabidi kuwe na msimamizi wa mirathi ya marehemu. kwahiyo kama bado hamjaenda mahakamani kufungua shauri la mirathi inabidi mfanye hivyo kwanza. na kabla ya kwenda mahakamani mfanye kikao cha ukoo ili wote kwa pamoja mkubaliane ni nani katika familia mnayemuamini ili mmpendekeze jina lake na alafu ndo aende kortini kuidhinishwa kisheria.

  hebu fanyia kazi hayo mamboo machache kwanza.
   
 6. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #6
  Feb 9, 2011
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Ndugu yangu umeraise issue tatu za msingi ambazo napmba ufafanuzi:
  1. Ina maana kama ninataka kuingia mkataba je, ni lazima niingie mkataba mbele ya wakili au shahidi?
  2. Kama mali ni yangu na iko kwa jina langu sina uhuru wa kuuza mpaka nimshirikishe mke wangu?
  3. Je ni lazima kushirikisha watoto endapo nataka kuuza mali zangu?
   
 7. E

  Edmund Senior Member

  #7
  Feb 9, 2011
  Joined: Jul 17, 2009
  Messages: 122
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  NAOMBA KUFAFANUA
  1. Mkataba wa kwanza ulikuwa mwaka Juzi mbele ya Marehemu Mzee, Mnunuzi na Mkewe tu kwa Tsh 3,000,000/= na mwingine mwaka Jana mwanzoni mbele ya Marehemu, Mnunuzi, Mkewe, Mtoto wa Mnunuzi pamoja na Mwenyekiti serikali za Mitaa,

  2. Hakuna saini ya Mke wa Marehemu wala Mtoto yeyote wala ndugu wa Marehemu.

  3. sidhani kama tulikuwa hatuelewani kwani kipindi tulikuwa tukiishi kama famili moja hapahapa Dar.

  4. Kikao cha ukoo tayari kimeshafanyika na Mke wa Marehemu ndiye Msimamizi wa Mirathi.
   
 8. d

  daisy Senior Member

  #8
  Feb 14, 2011
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 139
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Kwa ufupi ni kwamba ni vizuri kuandika mkataba mbele ya wakili kwa sababu zifuatazo:
  1. wakili ataweleza mambo muhimu kisheria yanayoufanya mkataba uwe na nguvu ya kisheria (legally enforceable) mfano je mnaoingia kwenye mkataba ndio wahusika nikimaanisha kama kila mmoja wenu ana uwezo wa kufunga mkataba kisheria inaitwa capacity to contract, wote mna akili timamu(sound mind), ni watu wazima (you have attained age of majority), lengo la mkataba ni halali au haramu( legality or illegality of the subject matter), na mengine mengi ambayo yasipozingatiwa mwisho wa siku upande mmoja unaweza kujikuta unapoteza haki zake.

  2. uandishi wa mkataba pia ni jambo la kuzingatia. lawyers wanafahamu namna nzuri za kuweka maneno japo mengi yanakuwa na utata lakini yakitafsiriwa kisheria yanaleta maana iliyokusudiwa.

  Kumhusisha mke wako hata kama mali ipo kwa jina lako ni jambo la kisheria siku hizi hasa mikataba ya mauzo ya ardhi na nyumba. Kwani kumekuwa na kesi nyingi sana kina mama wakienda mahakamani kupinga mauzo ya namna hiyo kwa madai ya kutoshirikishwa na kwamba the property is a matrimonial ( mali iliyopatikana katika ndoa).

  Pia kushirikisha watoto ni vizuri for future events kama ivyo mzee anafariki watoto hamna habari ya kinachoendelea kuhusu mali za baba yenu

  Natuamini umenipata Ngambo ngali.   
Loading...