Sa 7 mchana
JF-Expert Member
- Dec 30, 2018
- 4,975
- 9,721
Ulikua ni muendelezo wa msimu wa fiesta unayofanyika karibu kila mwaka, utofauti wa msimu huu mwingine ni kuwa msimu uwo wa fiesta ndio kilizaliwa kichanga ambacho sasa kimekua na tayari kinajitegemea kinaitwa FURSA.
Timu ya fursa sijui iliongozwa na nani ila Marehemu Ruge Mutahaba nae alikuwepo, Ilizunguka maeneo mbali mbali kwenye jiji nililokuwepo bila kificho na kujaribu kuweka bayana baadhi ya fursa ambazo zinapatikana kwenye sekta mbalimbali kama rasharasha tu ila lengo kuu ilikua kutukaribisha kwenye tukio kuu la Fursa lillikua linaenda kufanyika katika moja ya kumbi maarufu jiji hapo.
Long story short, kwenye mengi aliyozungumza Marehemu Ruge, moja lilikua ni kuwepo kwa uhitaji mkubwa wa vipindi vya televisheni hasa katika vituo vya kurushia matangazo vya ndani. Hakuishia hapo aliongezea kwa kusema uhaba uwo upo mpaka nje ya nchi, kwamba ushakutana na vituo vikubwa Africa vipo nchini kutafuta maudhuhi kutoka kwa wazalishaji wa ndani na kuondoka bila mafanikio. Mwamba akachangiza kwa kusema tuchangamikia fursa, vijana tusilale... Bhana wewe si nikasema mwamba ndio huyu.
Mwananenu nikazama chimbo kutengeneza maudhuhi ya pekee kabisa, ambayo mpaka muda wa nachapisha bandiko hili bado haijaruka hata ya kufanana nayo.
Miaka mitano nyuma kutoka mwaka huu, Mchongo wangu mkononi nikaanza kugonga milango ya vituo vyetu vya habari. Nikaanza na kituo pendwa cha burudani kwa vijana Clouds Media, Nikaambulia maneno matupu ya siyo eleweka vivyo hivyo EATV, EFM. Kipindi hicho Wasafi TV ilikuwa bado haijatinga kwa hewa.
Mpaka leo nashindwa kuelewa ni kwamba
1. Marehemu alikuwa anafurahisha genge kwa kusema yale
2. connection ndiyo iliyonikwamisha
3. Sikukutana na watu sahihi kwenye malango yale
Mwenye connection anakaribishwa