Marangu Coach imefikia hatua hii

Hismastersvoice

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
18,712
22,296
Jana Jumatano 04/10/2023 basi la Marangu Coach liliondoka Dar es Salaam asubuhi kama kawaida na abiria wakiwa na matarajio ya kufika Moshi kwenye saa 10 hivi bila kujua lililo mbele yao, basi lilipofika wilaya ya Bagamoyo likaharibika ikabidi spea iagizwe toka Moshi iletwe Bagamoyo! Akili mbovu.

Spea haikuletwa kwa ndege wala ungo, Moshi siyo Dar masaa yalipita Mungu Mkuu ikafikishwa na basi likatengenezwa na kuendelea na safari, likaingia mkoa wa Tanga likaharibika tena na likatengenezwa na kuendelea na safari, mpaka saa nne usiku basi lilikuwa wilaya ya Same! Usingizi ukanipata nikazimika na sijui Moshi liliingia saa ngapi ila lilifika salama, hiyo ndiyo Marangu Coach.
 
Tuliposema mabasi ya kichina ni hovyo tulishambuliwa tukaambiwa hatuendi na wakati, huo upuuzi hutausikia Kilimanjaro Express, wale gari zao nyingi kama siyo zote ni toughened and trusted Scania.
 
Tuliposema mabasi ya kichina ni hovyo tulishambuliwa tukaambiwa hatuendi na wakati, huo upuuzi hutausikia Kilimanjaro Express, wale gari zao nyingi kama siyo zote ni toughened and trusted Scania
Mkuu gari yeyote inahitaji matengenezo ya mara kwa mara ili yasitokee hayo hata Scania pia zinaharibika nyingi tu tatizo la Marangu ni Mmiliki kufariki naona wahuni wanaendesha Kampuni wanavyotaka...mbona hiyo ishu hakuna Shabiby, Ester na mengineyo ambao wamejaza Mchina...
 
Mkuu gari yeyote inahitaji matengenezo ya mara kwa mara ili yasitokee hayo hata Scania pia zinaharibika nyingi tu tatizo la Marangu ni Mmiliki kufariki naona wahuni wanaendesha Kampuni wanavyotaka...mbona hiyo ishu hakuna Shabiby,Ester na mengineyo ambao wamejaza Mchina...
Scania reliability yake ni 99% hayo mengine ni <80% unasafiri na hofu
 
Tuliposema mabasi ya kichina ni hovyo tulishambuliwa tukaambiwa hatuendi na wakati, huo upuuzi hutausikia Kilimanjaro Express, wale gari zao nyingi kama siyo zote ni toughened and trusted Scania

Tema Mate Chini, Kilimanjaro Moja Ya Tisa Alfajiri Kuna Siku Tuliondoka Saa Kumi Na Moja Bado Wana faults maana gari ilikuwepo pale na hatukubadilishiwa
 
Jana Jumatano 04/10/2023 basi la Marangu Coach liliondoka Dar es Salaam asubuhi kama kawaida na abiria wakiwa na matarajio ya kufika Moshi kwenye saa 10 hivi bila kujua lililo mbele yao, basi lilipofika wilaya ya Bagamoyo likaharibika ikabidi spea iagizwe toka Moshi iletwe Bagamoyo! Akili mbovu.

Spea haikuletwa kwa ndege wala ungo, Moshi siyo Dar masaa yalipita Mungu Mkuu ikafikishwa na basi likatengenezwa na kuendelea na safari, likaingia mkoa wa Tanga likaharibika tena na likatengenezwa na kuendelea na safari, mpaka saa nne usiku basi lilikuwa wilaya ya Same! Usingizi ukanipata nikazimika na sijui Moshi liliingia saa ngapi ila lilifika salama, hiyo ndiyo Marangu Coach.
... tena mshukuru siku hizi safari ni 24-hrs. Ingekuwa mwezi uliopita kurudi nyuma mngegandishwa pale Msata hadi kukuche ndio mruhusiwe!
 
Jana Jumatano 04/10/2023 basi la Marangu Coach liliondoka Dar es Salaam asubuhi kama kawaida na abiria wakiwa na matarajio ya kufika Moshi kwenye saa 10 hivi bila kujua lililo mbele yao, basi lilipofika wilaya ya Bagamoyo likaharibika ikabidi spea iagizwe toka Moshi iletwe Bagamoyo! Akili mbovu.

Spea haikuletwa kwa ndege wala ungo, Moshi siyo Dar masaa yalipita Mungu Mkuu ikafikishwa na basi likatengenezwa na kuendelea na safari, likaingia mkoa wa Tanga likaharibika tena na likatengenezwa na kuendelea na safari, mpaka saa nne usiku basi lilikuwa wilaya ya Same! Usingizi ukanipata nikazimika na sijui Moshi liliingia saa ngapi ila lilifika salama, hiyo ndiyo Marangu Coach.
Spea inatoka Kilimanjaro halafu gari imeharibikia Bagamoyo?

Dah, mmiliki atakuwa kada mwenzangu wa CCM😀😆
 
Back
Top Bottom