Marando na watuhumiwa wa ufisadi

Marando na watuhumiwa wa ufisadi

To be honest ushiriki wa marando kama wakili wa kesi za watuhumiwa wa ufisadi limewachanganya wengi...mimi ni mwanafunzi wa sheria na nafahamu kwa ufasaha kabisa kwamba mtu hapaswi kuitwa mkosaji mpaka ithibitishwe (na mahakama) beyond reasonable doubts kwamba amekosa.

Albeit, katika siasa za ushindani, c kila jambo hutazamwa kwa utashi wa kisheria(mengine hutazamwa kwa utashi wa kisiasa).kwa mfano katika mdahalo kuhusu sera za vyama vya siasa uliorushwa STAR TV, mimi na wenzangu kadhaa tulirundikana mbele ya runinga tukisubiri hoja nzito kutoka kwa wakili mahili kutoka chama kinachovutia vijana wengi..hakuna aliyeiwaza CUF.

Hakuna aliyetarajia jipya kutoka CCM..Contrary to our expectation,jussa alimuacha marando mbali..moja ya hoja zilizombabaisha marando zat day ni hili suala la kuwatetea mafisadi.nakumbuka jibu lake kwa ufasaha(niko tayari kusahihishwa).."ninaowatetea mimi ni dagaa tu..watuhumiwa wakubwa hawafikishwi mahakamani.wanakiri kwamba wamechukua hela.wanaambiwa wazirejeshwe na kusamehewa''..

Ukitazama jibu la marando kwa kina(hasa kwa walio unbiased)ni kama vile mh.marando anakiri kwamba watuhumiwa anaowatetea ni mafisadi but they r petty..hii ina impact kubwa hasa kama watuhumiwa wale watapatikana na hatia!!!!katika vita ya ufisadi,haijalishi udogo au ukubwa wa fisadi.mpambanaji ni lazima ajidhihirishe kung'oa kila aina ya ufisadi.
 
vilaza bana .... limekaa na dictionary lina kremu .. teh teh teh .... utabakia ngumbaru mpaka mwisho wako
:msela:TEH TEH TEH..Shule za kata at work
 
  • Thanks
Reactions: LAT
:msela:TEH TEH TEH..Shule za kata at work

huwezi kufahamu maana ya kukremu kwani u kilaza ..... aliyekunyima kupata elimu ndiyo amekuponza

nimekugongea like kwa ujinga wako

fold your ignorance ..... !
 
Kwa taaluma yangu ya Sheria,Marando yupo sahihi kwa vile there is the rule that the person is not guilty at untill his guilty have been proved so by competent court of law,na jua kuwa advocate kama Marando ni kinyume cha maadili ya uwakili kubagua wateja wake kwa misingi yeyote, Marando ni kama Daktari hawezi kubagua wagonjwa kwa kisingizio ni jambazi kama ulivyo udaktari ni sawa kabisa na Sheria you suppose not be bias.NDIO MAANA UTAKUTA WANASHERIA SIKU NYINGINE ANAMTETEA JAMBAZI SIKU YA PILI ANAWATETEA WATU WALIOPORWA NA KUDHURUMIWA na hawana cha kumlipa kwa sababu hiyo,

LA PILI tujue wale walioenda mahakamani ni vidagaa tuu hali mapapa na masangara yapo mitaani ya kikata mitaa hivyo bac haki haibagui lazima wote waliohusika wafikashwe mahakamani na wahukumiwe kwa stahili sawa,

Hivi una habari kuwa daktari haruhusiwi kumtibu mkewe, mtotowe, mumewe mama yake au baba yake? Una jua kama wakili hatakiwi kumtetea mmoja kati ya wana familia yake katika kese yoyote? KWA NINI MIIKO ILIWEKWA HIVYO NA WAANZILISHI WA TALUMA HIZO?

Hivyo basi kwa kuwa Mabere Marando chama chake kinajipambanua kupambana na ufisadi katika akili ya utu uzima asingejiingiza katika kese hiyo inamvunjia heshima mbele ya watu makini. LAKINI ,kwa kuwa tuna haki ya kutoa maoni na mitazamo si vibaya tukafundishana hapa ndio mahala pake.
 
To be honest ushiriki wa marando kama wakili wa kesi za watuhumiwa wa ufisadi limewachanganya wengi...mimi ni mwanafunzi wa sheria na nafahamu kwa ufasaha kabisa kwamba mtu hapaswi kuitwa mkosaji mpaka ithibitishwe(na mahakama) beyond reasonable doubts kwamba amekosa.Albeit,katika siasa za ushindani, c kila jambo hutazamwa kwa utashi wa kisheria (mengine hutazamwa kwa utashi wa kisiasa).

Kwa mfano katika mdahalo kuhusu sera za vyama vya siasa uliorushwa STAR TV,mimi na wenzangu kadhaa tulirundikana mbele ya runinga tukisubiri hoja nzito kutoka kwa wakili mahili kutoka chama kinachovutia vijana wengi..hakuna aliyeiwaza CUF.Hakuna aliyetarajia jipya kutoka CCM..Contrary to our expectation,jussa alimuacha marando mbali..

Moja ya hoja zilizombabaisha marando zat day ni hili suala la kuwatetea mafisadi.nakumbuka jibu lake kwa ufasaha(niko tayari kusahihishwa).."ninaowatetea mimi ni dagaa tu..watuhumiwa wakubwa hawafikishwi mahakamani.wanakiri kwamba wamechukua hela.wanaambiwa wazirejeshwe na kusamehewa''.

Ukitazama jibu la marando kwa kina(hasa kwa walio unbiased)ni kama vile mh.marando anakiri kwamba watuhumiwa anaowatetea ni mafisadi but they r petty..hii ina impact kubwa hasa kama watuhumiwa wale watapatikana na hatia!!!!katika vita ya ufisadi,haijalishi udogo au ukubwa wa fisadi.

Mpambanaji ni lazima ajidhihirishe kung'oa kila aina ya ufisadi!!!

Nakubaliana nawe. Hebu soma mfano huu. Kuna padre mmoja mkatoliki alikwenda kuongeza elimu kusomea sheria. Alipata uwakili. Miongoni mwa dhambi zinazopigiwa kelele na kanisa ni pamoja na wizi, uongo, uzinzi.

Ikatokea kesi ya mwizi padre akaenda kumtetea mwizi na kwa kukosa ushahidi mwizi akashinda (japokuwa alliba kweli) ASKOFU WAKE aliposikia habari hiyo akaitwa padre huyo na kukaripiwa kwa nini ametetea uovu unaokatazwa (AMRI KUMI) Hivyo pamoja na uwakili wake marando angemeza pini asubiri kesi nyingine ambazo CDM haina MASLAHI nazo.

Mbona zipo nyingi sana nchi hii.
 
Nimefuatilia mjadala na naona kuna mchanganyiko wa mambo ambayo yaweza kuwa hatuyaelewi au tunayatafsiri vibaya.
Kwanza nakubaliana na Kobello kuwa kazi ya wakili(stand to be corrected) ni kusimamia haki ili itendeke (Fair trial) hata kama mtuhumiwa amethibitika kutenda kosa ili mambo mengine ya kisheria yazingatiwe katika kutoa adhabu.

Mawakili ni weledi sana wa sheria na kama taaluma zingine wanongozwa na sheria, principles na ethics. Moja kati ya Ethics zao ni kulinda public interest iwe katika kikundi au mtu binafsi kwa kuhakikisha haki inatendeka kwa kila raia anayestahili bila kujali itikadi ya kisiasa ya wakili au mtuhumiwa kama wanavyofanya madaktari hospitali.

Profesa Sarungi mtaalamu wa upasuaji alikuwa mkuu wa mkoa wa Pwani, Mbunge mjumbe wa halmashauri kuu ya taifa ya CCM na kada muhimu. Kuna nyakati alilazimika kutumia taaluma yake katika hospitali ya tumbi pale kulipotokea matukio kama ya ajali, au kuhudumia majeruhi wanaotokana na uhalifu kama ujambazi, wizi, fumanizi n.k.

Sarungi hakufanya kazi kama kada wa chama bali mtaalamu anayelinda kiapo chake cha udaktari cha kuhudumia binadamu bila kuangalia jambo lolote bali uninadamu na utabibu kwa kutenda haki.
Court of public opinion ilimhukumu kama mtu, daktari na kiongozi anayejali na kuenzi taaluma yake kwa kuthamini utu.

Popote duniani mtuhumiwa bila kujali wajihi, hadhi au nafasi yake katika jamii analindwa na haki ya kisheria. Wauaji wa Albino ambao wengine hawamudu hata kununua mkate, bado wanahaki ya kuwekewa uwakili na cha kushangaza zaidi ni kuwa mawakili wao wanalipwa na serikali ambayo ni kodi yangu mimi na wewe. Kwa maneno mengine, tunalaani mauaji ya albino na wakati huo huo tunatoa pesa za kuwawekea mawakili.
Court of public opinion inapaswa kutusuta sisi tunaolipia gharama za kumuokoa muuaji au kabla ya kumlaumu wakili.

Tunapoiba pesa za halmashauri au wizara na kisha kuwaambia mawakili siri zetu na wao kututetea hata kama wanajua tumeiba au tumefanya ujambazi, court of public opinion inatupa haki kama ambavyo inapaswa kutoa haki kwa mtuhumiwa mwingine wa fumanizi au ufisadi.

Ni jambo gumu kuwa na mtu asiyefungamana na itikadi ya kisiasa hasa katika kada ya wasomi.
Wapo watakaosema hawafungamani kama ninavyoweza kusema lakini ukweli unabaki mioyoni mwao na wala hatupaswi kusadiki kauli zao.

Mfano, sheria inakataza viongozi wa majeshi kuwa washabiki wa vyama vya siasa. Mwaka jana tumeona kamanda mkubwa wa polisi aliyestaafu miezi 3 tu nakuchukua form za ubunge. Hivi huyu tunaweza kusadiki kuwa alikielewa chama chake katika miezi 3 tu hadi kufikia hatua ya kuchukua form za ubunge kama si kuwa alikuwa kada asiyesema? Sasa tutasemaje tuwe na mawakili neutral, kwa evidence gani.

Marando anapokuwa mahakamani anasimamia haki kama wakili na mtaalamu kwa mtuhumiwa na sio mhalifu na si kama ni mwakilishi wa Chama cha kisiasa kwa mantiki ile ile ambayo Profesa Sarungi anakuwa theatre akimshona nyuzi jambazi.

Profesa kwa wakati ule si mkuu wa mkoa au kada wa chama bali daktari aliyekula kiapo kutoa huduma ya haki kwa binadamu.
Ikifika hapo lazima tujiulize kwanini kuna double standard?
Why court of public opinion is not applicable across the board!

Kisiasa ni kweli hili jambo lina political ramifications hasa kwa nchi zenye wananchi ambao ufahamu wao una limit. Kibaya zaidi ni kuwa hata sisi tunaopaswa kuwaambia kuwa kuna politics na professionalism tunaelekea kuwashadidia waelewe tofauti.Je huku si kuendelea kuwapotosha!!
Tatizo lingine ni sisi kuchomeka siasa kwenye kila jambo hata yale ya kitaaluma na kitaalamu ndiyo maana hata mambo ya megawatts, resuscitation, economy, tumewaachia wao wapange na wasaini mikataba. Sio engineers, doctors au economists.

Tumeruhusu na kukubali wanasiasa kuchomeka siasa katika taaluma na sasa tuneshaingia huko haya ndiyo matokeo yake.

Tunadhima ya kuuambia umma wetu uliochanganywa na siasa za Nape Nnauye kuwa kuwa, alichosema Nape ni political mudsling and confusion, ukweli ni kuwa Marando kama professional hajakiuka Laws, regulations, principles au ethics kwa namna yoyote na kwamba court of public opionion imhukumu kwa kauli na matendo yake kisiasa katika chama chake bila kuchanganya na utaalamu wake kama vile court of public opinion ilivyomuelewa profesa Sarungi alipokuwa ana repea mifupa na kuzuia damu isivuje kwa majambazi.

Ni maoni yangu senti sumuni.

HAPOHAPO! Kama WELEDI anayohaki kabisa kutetea kama alivyowatetea akina Papii Kocha na Wadogo zake wengine wale wadogo wakaachiwa huru. Sheria ilifanya kazi yake, mathalani leo tarehe 07 Septemba Mabere Marando na viongozi wa juu wa CHADEMA wana mkutano wa hadhara pale Mwembe yanga.

Na miongoni mwa hoja ni kuwashambulia watuhumiwa wa ufisadi wakiwemo anaowatetea( Haijathibitika kama ni wakosaji) kwa msimamo wa chama chake( CHAMA KWANZA) ataambiwa ataje ubaya wa ufisadi na akafanya ivyo.

Anaweza kutaja na wahusika kwa majina halafu kesho yake kuna kesi ya wateja wake wanaotuhumiwa kwa ufisadi kama binadamu uso wake atauficha wapi mbele ya wananchi walewale aliokuwa anawahutubia jana yake?

KUNA MSEMO UNA SEMA FEDHA ZAKO NI HARAMU BAKI NAZO.
 
ujinga ndio unao ku cost
IS IT TRUE THAT THE JF IS THE ONLY PLACE WHERE WE CAN DARE TALK OPENLY? mbona tukishindwa kwa hoja tunakuwa wepesi kuandika maandishi yasiyojenga? TUSHINDANE KWA HOJA UKIZIDIWA PUMZIKA TAFUTA FACTS RUDI TENA JAMVINI. matusi hapana bwana. MJADALA UNASAIDIA kupanua fikra na mawazo yetu. chondechonde wana JAMII.
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Hiyo ndio inaitwa rule of law and justice. Mshitakiwa katika nchi yetu ni innocent until proven guilty. Sisi wananchi always tunathink otherwise "Guilty till proven Innocent". Kama ni kosa kwa Marando kutetea washtakiwa wa ufisadi kwa sababu tu ni mjumbe wa cdm, je inakuwaje kwa serikali kuwa na pande mbili katika kesi moja?

Nadhani wengi ntakuwa nimewaacha kidogo, kwenye kesi ya mauaji serikali inasimama kama mshitaki (public), wakati huohuo inawajibika kumwekea wakili ama mawakili mshitakiwa (kama hana uwezo wa kuweka wakili wake), hapo je?

Pia mawakili wanaowatetea washitakiwa wa mauaji nao ni wauwaji? Je, makanisa na misikiti viwatenge kwa kuvunja amri ya Mwenyezi Mungu "usiue".

Je, Mabere Marando kutetea mafisadi naye pia ni fisadi?
 
na mimi naomba nikuulize kaswali kadogo; hivi mh. marando anapokwenda kuwatetea hawa mafisadi anapoulizwa na hakimu kuwa watuhumiwa wake ni wezi, wameiba pesa za epa kwa mfano; huwa anajibu nn? ndio au hapana? yaani kwa niaba ya watuhumiwa marando huwa anakubali au huzikana tuhuma?
Marando," MHESHIMIWA Hakimu mteja wangu X hajahusika na lolote katika shtaka hili la wizi wa mabilioni ya shilingi katika akaunti ya EPA"
Hakimu, " Umeulizwa swali AMEIBA HIZO FEDHA?"
Marando," HAKUIBA MHESHIMIWA HAKIMU" Tukienda Jangwani kesho yake. CCM wezi waameiba fedha za EPA. Ndo nini hiyo?
 
hiyo ndio inaitwa rule of law and justice. Mshitakiwa katika nchi yetu ni innocent until proven guilty. Sisi wananchi always tunathink otherwise "guilty till proven innocent". kama ni kosa kwa marando kutetea washtakiwa wa ufisadi kwa sababu tu ni mjumbe wa cdm, je inakuwaje kwa serikali kuwa na pande mbili katika kesi moja?

Nadhani wengi ntakuwa nimewaacha kidogo, kwenye kesi ya mauaji serikali inasimama kama mshitaki (public), wakati huohuo inawajibika kumwekea wakili ama mawakili mshitakiwa (kama hana uwezo wa kuweka wakili wake), hapo je? Pia mawakili wanaowatetea washitakiwa wa mauaji nao ni wauwaji? Je, makanisa na misikiti viwatenge kwa kuvunja amri ya mwenyezi mungu "usiue".

Je, mabere marando kutetea mafisadi naye pia ni fisadi?
Ukikaa karibu na waridi utanukia muwaridi.
Ukimsaidia mchinja mbuzi kuchuna ngozi bila shaka utanuka ubeberu na utamwagikiwa damu japo kidogo. Na utapewa bakshishi ya uchunaji.
 
Wana JF

Kwanza na-declare interest mm ni mfuasi na mwanachama wa CHADEMA, Hili swala la Marando kuwa wakili wa baadhi ya watuhumiwa wa ufisadi km vile manji na mahalu litakuja kuwa na madhara makubwa sana hapo badae ktk harakati za chama za kuchua dola natambua kabisa ile ni professional yake na ni vigumu aache kazi aliyoisomea kwa muda mrefu, lakini kabla ya kuchua kazi lazima mtu ufanya client assessment.

Kwa kuwa ameamua kuwa ktk siasa na kufanikiwa kuwa mjumbe wa cc ya cdm ni wakati wake muafaka wa kuhakikisha kimoja kati ya professional yake na siasa hakuna kinacholeta madhara kwa kingine. Kwa hiyo moja ya criteria ya kutumika kwake kum-accept client iwe ni asiwe mtuhumiwa wa ufisadi. Nionavyo mm professional yake kwa sasa inaleta madhara ktk siasa si kwake tu bali kwa Chadema kwa ujumla coz ni vigumu sana mtu kupinga ufisadi majukwaani na kuukubali mahakamani na watu wote wakaamua kukuamini ww ni mpiganaji wa kweli wa ufisadi.

Swala kubwa la sisi wana-chadema tunalotakiwa kulielewa ni kwamba asilimia kubwa ya wananchi hawawezi kutofautisha professional na siasa kiasi kwamba point tutakayoitumia kuuelezea uma ya kuwa hii ni siasa na hii ni professional haitaweza kuzaa matunda yeyote. Marando na uongozi wa juu ulitazame hili kwa mapana na marefu ili nguvu iliyokwisha tumika kukifikisha chama hapa isije kupotea kirahisi kisa mtu mmoja ambae ana uwezo wa kuchua kesi zingine na kuendelea na maisha.

Tujiulize swali dogo kwa mfano leo ROSTAM amefikishwa mahakamani kwa tuhuma za wizi wa KAGODA na marando akafanya km anavyofanya kwa wale wa EPA itakuwa sahihi? Au kuwatetea wa EPA itakuwa halali na kumtetea Rostam itakuwa haramu wakati wote ni mafisadi?

Nawasilisha

Jiulize hivi: hapo ulipo ukituhumuwa umeua/lawiti au kubaka mtoto na ukatakiwa upewe hukumu ya kifo au utumikie kifungo cha maisha kama utatiwa hatiani, hutahitaji wakili kwa kutuhumiwa kuua/kulawiti au kubaka?
 
hoja yako ni nzuri sana na ina tahadhali na mtazamo mkubwa sana wa mbele! ninachokiona hapa kuna wana chadema wamekua wavivu wa kufikiria sana! hawaoni hatari ya kuichafua chadema jukwani kupitia hili analolifanya marando! ni bahati mbaya sana wanachadema wameiweka akili yao kw aupande wa kishabiki kwa kila jambo! hili la marando linatia doa kwa chadema katika vita yake ya kupinga ufisadi! ni doa!
Kikwete alpowatetea akina Lowasa Rostamu na Chenge kuwa ni watu safi unakumbuka alishindwa kujibu swali aliloulizwa siku ya tarehe 29 oktoba 2010? Hao ni watu waliokuwa wanahusishwa na ufisadi mkubwa katika nchi hii. Jamani tuangalie yasije kutukuta maswali tutakayoshindwa kuyajibu baadae.
 
Jiulize hivi: hapo ulipo ukituhumuwa umeua/lawiti au kubaka mtoto na ukatakiwa upewe hukumu ya kifo au utumikie kifungo cha maisha kama utatiwa hatiani, hutahitaji wakili kwa kutuhumiwa kuua/kulawiti au kubaka?
hukatazwi kuwekla wakili. Lakini Usithubutu kuweka wakili ambaye pia ni padre utasababisha avuliwe upadre kwa kutetea dhambi hizo.
 
Huyu aliyeleta mada ,asiwe anatupetezea nafasi za kufikiria, je,police anavyomkamata mwizi amwache wananchi wamwue??? au atmlinda tena kwa karibu zaid ili wapate uthibtisho wa wizi wake , Tena inabidi daktari kuwa karibu sana na yule mwizi aliyeumizwa ili wapate ushaid na ijulikane hatima yake ni nini.
 
ni simple logic too! unahubiri la kupinga ufisadi kesho unaenda kisutu kuwatetea mafisadi!
<br />
<br />
personal interests zimesimama kweli...
hakuna mwenye uchungu na tanzania hapa.. njaa tunaendekeza sana watanzania..ushabiki mwingi hata kwenye kasoro tunatetea tu..
 
Mnajuaje kama Marando anataka kuwaingiza shimoni hao watuhumiwa wa Ufisadi....
 
HAPOHAPO! Kama WELEDI anayohaki kabisa kutetea kama alivyowatetea akina Papii Kocha na Wadogo zake wengine wale wadogo wakaachiwa huru. Sheria ilifanya kazi yake, mathalani leo tarehe 07 Septemba Mabere Marando na viongozi wa juu wa CHADEMA wana mkutano wa hadhara pale Mwembe yanga.

Na miongoni mwa hoja ni kuwashambulia watuhumiwa wa ufisadi wakiwemo anaowatetea( Haijathibitika kama ni wakosaji) kwa msimamo wa chama chake( CHAMA KWANZA) ataambiwa ataje ubaya wa ufisadi na akafanya ivyo.

Anaweza kutaja na wahusika kwa majina halafu kesho yake kuna kesi ya wateja wake wanaotuhumiwa kwa ufisadi kama binadamu uso wake atauficha wapi mbele ya wananchi walewale aliokuwa anawahutubia jana yake?
KUNA MSEMO UNA SEMA FEDHA ZAKO NI HARAMU BAKI NAZO.
Kwanza kabisa nitashangaa sana kama Chadema wataitisha mkutano wa kushambulia watu na si dhana ya ufisadi. Wanasiasa makini hawajishughulishi na matukio bali sababu za matukio.

Pili kuna hili suala la uwakili ambalo watu wanadhani ni kuetetea uhalifu. Niliandika kuwa kazi ya wakili ni zaidi ya hapo ikiwa ni pamoja na kusimamia haki ili itendeke. Hebu soma haya maelezo kwanza kabla sijakupa mfano;

Criminala defense lawayer (sio lazima iwe criminal tu inaweza kuwa kesi ya madai n.k) deal with issue sorrounding arrest of his or her client as well as any statement the client may have made. Also deal with substantive issues of the crime with which his or her clients are charged until the prosecutors prove each element of crime beyond reasonable doubt.

Inaposemwa prosecutors prove each element of crime beyond doubt haina maana kumtetea kuwa hakufanya uhalifu, bali kuhakikisha kuwa kila dai lina ukweli na adhabu inayotolewa ina lingana na sheria kama ilivyoandikwa.

Sasa wa EPA ambao mumeshawahukumu,mfano wanaweza kubambikiwa kuwa walihusika na wizi wa Radar n.k na prosecutor.
Intakiwa mwanasheria mwenye ueledi kuweza kumbana mwendesha mashitaka athibitishe bila shaka yoyote juu ya uhalifu huo.

Prosecutor anapomwongoza mwenye mashitaka haina maana anashabikia kesi, ni ili haki ipatikane. Unaweza kufanyiwa uhalifu na ukashindwa kesi pia kwasababu 'technically' hujui sheria. Ndivyo ilivyo kwa washitakiwa pia.

Mfano mtu anaweza kuua na akakamtwa na kila ushahidi wa kimazingira, kisayansi na watu 100 waliomuona na kurekodi tukio hilo. Na mtu huyo akakiri kuwa ameua. Kwa mujibu wa sheria za nchi yetu adhabu iliyopo mbele yake ni kunyongwa.

Miezi 3 baadaye ikagundulika alitoroka hospitali ya wagonjwa wa akili mirembe na aliua siku hiyo hiyo.
Hivi unategemea kuwa mgonjwa wa akili angeweza kusema nina ugonjwa wa akili? Hivi unadhani wakati anakiri alikuwa na akili timamu?
Na unategemea angeweza kujenga hoja ya kwanini aliua ?
Ikifika hapo nani anaweza kisheria kumsaidia kama si wakili. Je adhabu atakayopewa inalingana na haki na mzingira ya tukio? nani anajua kama si wakili.

Kwanini tunazama kufikiri kazi ya wakili ni kutetea tu na tunasahau majukumu mengine! kama kuhakikisha haki na sheria inatendeka kama ilivyoandikwa n.k n.k
 
Kwa hiyo Leo Chadema wakiamua kwenda mahakamani kumshtaki ROSTAM kwa wizi wa kagoda uliochangia kikwete kuingia madarakani 2005 itakawa ni sawa mjumbe wa kamati kuu ya cdm MARANDO kumtetea rostam?
Ni sawa kabisa ka kuwa mwenye jukumu la mwisho la kumtia hatiani mtuhumia ni hakimu au Jaji. Lakini ni watanzania wangapi wanalijua hili, ndio maana hoja ya mtoa mada inabaki na mashiko kutokana na uelea mdogo wa watanzania wengi.
 
Mimi naamini serikali inapaswa si tu kupeleka watu mahakamani, wapeleke watuhumiwa sahihi kwa makosa sahihi. Na hicho hakifanyiki hivi sasa, haingii akilini kuona hukumu za watu waliochukua bil 2, huku "wamiliki" wa kampuni iliyochota bil 40 wakiwa hawajulikani.

Kuna watu watapewa misalaba isiyokuwa ya kwao. Kama wana makosa kweli, serikali ipeleke ushahidi utakaokuwa scrutinized na watu kama Marando, tupate wakosaji wa ukweli, sio waigizaji.
KAMA SERIKALI HAIWAJUI WALIOPORA BIL 40 BOT,BADHI DHAMANA YA UHALIFU ATAIBEBEA RAIS ALIEAPA KUILINDA NA KUITETE NCHI,WATU WAKE NA MALI ZAKE TUTANZA NA KIKWETE KUPOKEA FEDHA ZILIZOIBWA NA KUREJESHWA BILA HATUA KALI KUWACHUKULIA WALIOREJESHA,THEN Mkapa atajua nani aliwaandikia vimemo wakajichotee .kila nikiona watanzania wanavyopata shida,huku kina mkapa wanatesa na mavogo ole wao.kiama chao kipo jirani.
 
amini amini nawambieni, jamii yoote ya watanzania ni corrupted either kimatendo au kimawazo.
na fahamu ya kwamba, tumbo ni bora kuliko nguo! bora USHIBE lakini utembee UCHI,
 
Back
Top Bottom