Elections 2010 Marando amgeukia Jaji Mkuu

Tanzania is a society of lawlessness ila itawatokea puani kwani panapokosekana haki kinachofuatia ni mtutu tu maana watanzania si malaika. Watamzame kinachoendelea msumbiji ndio watafahamu nini kiko ndani ya mioyo ya watanzania
 
Naona kila mtu anajitumbukiza kumtetea JK na chama cha CCM tena bila haya ili mkuu asije wasahau ktk ufalme wake.
Si unajua JK ni mzee wa kulipa fadhila kama ile ya TIDO mhando kuzima matangazo Jangwani naona this time atamtoa ukurugenzi atampeleka ikulu
 
upumbavu wamtu utaujua kwenye maneno yake,
mtu mpumbavu ni mpumbavu tu hata angekuwa na elimu gani,
bahati mabya upumbavu hauondolewi kwa elimu,
naamu basi ni heri ujinga kuliko kuwa mpumbavu, huyu jaji.....sijui anatafuta nini
 
Hivi Serikali ilikata rufaa kupinga hukumu ya Zombe kama walivyokuwa wamenuia?


My friend, hapa kwetu issue ikisemwa si lazima ifanyiwe kazi. Mangapi tumesikia yakisemwa lakini mpaka leo ukiuliza unaambiwa mipango inaendelea vizuri na eti tuwe wavumilivu. Ukiwauliza watakwambia wameshaanda kila kitu hivyo mda wowote wata-appeal
 
Mi sishangai kwani ni kada wa kutupwa na kwa kufanya hivyo analipa fadhila za kupelekwa Marekani kwenye matibabu. Ni aibu kuwa na mfumo wa kiubabaishaji watu wanakutana nyuma ya mlango na kupanga matokeo...Tazama mgombea binafsi/huru. Bila katiba huru itakayoainisha mchakato wa uteuzi wa wakuu wa mihimili ya dola na taasisi muhimu katika kamii tutaendelea kushuhudia mazingaombwe kila kukicha. Angalia Tume ya Uchaguzi walivyojaa wastaafu. Ndo yale yale ya Richmond hatua hazichukuliwi na mijadala inafungwa kwa maslahi ya chama kwakuwa waliiba wakubwa, tazama Rada, tazama Meremeta na Tangold. Kama ingekuwa kiongozi katika ngazi za Halmashauri ndio kafanya hivyo nadhani kelele zake tungezisikia mpaka chini ya ardhi kwa hatua ambazo zingechukuliwa....sielewi kwanini wanatumia resorces nyingi kuzuia haki kwa kupitia makada kwenye mahakama
 
Huyu Jaji Mkuu wetu ni mmojawapo wa watu wanaostahili kuzomewa kila wanapopita Tanzania. Hukumu aliyosimamia ya mgombea binafsi iliondoa kabisa heshima ya Mahakama Tanzania.

Mtu Mzee na heshima zake kwanini anaogopa kuwa huru? Kila atakapoongea sasa atazidi kuwakasirisha Watanzania. Heri ajikalie kimya, asubiri Slaa akomboe nchi toka mikono ya wabakaji, wasafirishaji wa wa nyara za serikali, wezi wa fedha za EPA, na wafanyabiashra wakubwa wa dawa za kulevya.
 
Back
Top Bottom