[h=3]Marais wa Tanzania na Teknolojia[/h]
Fikra ya kwanza iliyotujia ni kwamba Tanzania ni nchi pekee duniani yenye maraisi wawili, hivyo tukaona ngoja tuwaulize hawa kama wanawajua, kwa vile hawa kiswahili kinawapiga chenga tukavuta iPad Mini na k-tune lugha ya mkoloni na kuisalimia Mazungumzo yalikwenda hivi:
Gajetek Habari: "Hi Siri"
Siri: "Hello There, Gajetek"
Mhh, tukajua ehe Siri anatuelewa pamoja na lafudhi yetu ya kibongo bongo, likafuata swali
Gajetek Habari: Who is the president of Tanzania
Siri: This Might Answer your question, Siri ikavuta kadi yenye jibu sahihi: Jakaya Kikwete.
Ah Siri alitukonga nyoyo.
Tukavuta Nexus, tuka-swap kifungo cha Home kwenda juu Google Now ikafunguka, tukatoonya kifungo chake, mazungumzo yakaanza bila ya salamu, maana Google Now haitaki mbwembwe:
Gajetek Habari: Who is the President of Tanzania"
Google Now: "The President of Tanzania is 'Jakaya Ki-quit'"
Kisha Google Now ikavuta kadi na kuandika Jina la Rais wetu kwa Usahihi kabisa Jakaya Kikwete, totauti na vile lilivyotamkwa kizungu Ki-Quit wakati inaongea. Tulicheka sana, lakini tukapata faraja pia. Mheshimiwa katika picha yake amevaa miwani na tai imetulia kabisa
Swali la Pili kwa Google Now:
Gajetek Habari: "Who is the President of Zanzibar"
Google now kimnya, ikafikiri fikiri pale baada ya muda ikakata tama ikaingia kwenye Google Search na kutuletea matokeo ya Search tu.
Hapa kidogo tukavunjika moyo. Tukasema ngoja tuvute iPad Mini huenda itajibu:
Gajetek Habari: Who is the president of Zanzibar"
Siri nayo kimnya, baada ya kungaa ngaa ikaniuliza mimi
Siri: Would you like me to search the web?
Nilikasirika nikaizima na ikawa ndio mwisho wa mazungumzo. Tukashangaa kwamba kumbe wanateknolojia hawajui kwamba Zanzibar nako kuna Rais!!!
Sisi katika Gajetek siasa si mchezo wetu, sisi na gajeti na gajeti na sisi. Lakini leo katika kucheza na gajeti zeetu tukaamua kufanya maongezi na wasaidizi wetu wa virtual wawili kuona kama wanatambulika. Wasaidizi hao ni Google Now wa Samsung Galaxy Nexus na Siri wa iPad Mini.Fikra ya kwanza iliyotujia ni kwamba Tanzania ni nchi pekee duniani yenye maraisi wawili, hivyo tukaona ngoja tuwaulize hawa kama wanawajua, kwa vile hawa kiswahili kinawapiga chenga tukavuta iPad Mini na k-tune lugha ya mkoloni na kuisalimia Mazungumzo yalikwenda hivi: