lossoJR
JF-Expert Member
- Oct 11, 2012
- 2,710
- 2,387
Kwanza nimshukuru Mungu kwa kuniokoa katika hili. Amen
Ikiwa ni mida ya SAA 5 usiku, nashuka zangu kituoni(Tabata Bima), nikitokea zangu huko Victoria(GEPF) nilikokua nafanya kazi(temporary).
Basi katika matembezi ya kuelekea home pale bima nikamuona binti wa ukweli , yaani ile ukweli isiyo mfano naye pia akija njia nielekeayo mimi, ofcoz raia bado walikuwepo sasa mnaelewa Dar raia mda wote wanashughulika.
Basi bwana, nikapunguza mwendo ili niongozane nae pia ili tujuane(kama mnavyojua wanaume tena), hatimae tukawa tunaongozana nae, baada ya salamu, nikamuhoji mbona watembea usiku huu waelekea wapi?
Akajibu kunaduka nalitafuta,mmh nikamweleza mbona maduka mengi yameshafungwa, akajibu we tulia ntalipata tu, duh basi nikapotezea, nikahoji tena waishi wapi? Akacheka kisha akajibu naishi mbali sana siwezi hata kukuelekeza, nikang'ang'ania kujua but aligoma.
Kwa upande wangu nilikua nakaribia maeneo ninayotaka kula,hivyo nikamwambia twende pamoja tule(ukarimu 1st time), kasema ana mtoto mdogo so anaenda nyumbani hata hilo duka ameahirisha kulitafuta.
Sikujali sana nikamwomba contacts ili nisiendelee kumganda, akafikiria kwa sekunde kadhaa! Lakini ghafla akawa mkali kupita maelezo huku akisema "
Potea haraka machoni kwangu, tena unabahati sana we kijana, nasema unabahati, ondoka haraka na usigeuke, aisee nilisisimkwa sana mwili,mwanaume nikatii amri.
Faster nikaachana nae, hata pale kwenye chakula nilipitiliza, nilipofika kwa mbele nikasema wacha nigeuke ili nione labda zilikua kiki za madada wa town but sikubahatika kumuona tena.
Nilipofika home nilitafakari sana,pia nikajiuliza why alikua anajiapiza sana kwamba, "Tena unabahati sana wewe ". Aisee mpaka nawaogopa sana hasa viumbe, lakini pia nikajifunza si kila mwanamke ni wakusimamisha maana tutakuja beba na matatizo yasiyo na ukomo.
Ila Mungu mwema alinilinda jui ya lile.