mara yangu ya kumfahamu Mtikila! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

mara yangu ya kumfahamu Mtikila!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mgen, Sep 26, 2012.

 1. mgen

  mgen JF-Expert Member

  #1
  Sep 26, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 15,148
  Likes Received: 1,882
  Trophy Points: 280
  Sintasahau siku yangu ya kwanza kumfahamu Mtikila!Ilikuwa hivi;Nilipanda basi kutokea G/mboto kueleke posta, kufika tazara trafic police akatusimamisha kwa madai kwamba gari ni mbovu iende kituoni hivyo abiria wote shukeni! Wakati tunajiandaa kushuka akajitokeza mtu mmoja mfupi huku amekasirika na kumwambia yule police hapa hashuki mtu! Unaiona hii ticket? Huu ni mkataba kati yangu na mwenye basi kunipeleka posta. Na wewe kama police kazi yako ni kulinda huu mkataba, kwa nini unataka kuvunja mkataba? Yule police alipofahamu kwamba anaongea na Mtikila akamgeukia dereva na kumwambia wapeleke posta kisha ulete gari kituoni ikaguliwe! Ndipo alipo muongeza hasira Mtikila na kumwambia yule police! We we si ulisema gari mbovu? Hujui kwamba lazima hii gari ifanye kazi ili alipe kodi.Ili na wewe upate mshahara?Wakati police anabung'aa bung'aa akamtupia donge jingine kuwa nyie police badala ya kujifunza sheria mnajifunza kulinda mafisadi na kupiga virungu walalahoi, huku akimuamuru dereva endesha gari na kumuacha yule police pale haamini!My take; raia tunapoelewa haki zetu lazima police watuheshimu!
   
 2. ligendayika

  ligendayika JF-Expert Member

  #2
  Sep 27, 2012
  Joined: Aug 31, 2012
  Messages: 1,175
  Likes Received: 50
  Trophy Points: 145
  Mi sijawahi kumuona namsikia kupitia media lakini huyu jamaa ni mtu anaesimamia vitu anavyovijua na kuviamini kuna wachungaji wachache sana ambao huwa wana misimamo kama ya huyu jamaa. ni makini kwa misimamo yake ebu wachungaji wengine fuateni mazuri ya Mtikila ni kichwa, sio kuyumbishwayumbishwa tu.

  • :frusty:
   
 3. mgen

  mgen JF-Expert Member

  #3
  Sep 27, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 15,148
  Likes Received: 1,882
  Trophy Points: 280
  Mkuu, ni kweli tupu! Nakumbuka issue yake mojawapo; alisherehekea kifo cha Nyerere na kushtakiwa! Yeye alijibu kwamba kwa muda mrefu amemuoba Mungu wake Nyerere afe, nyie mlikuwa mnamuomba Mungu wenu apone Mungu wangu amenijibu amekufa! Hivyo siwezi kuwa mnafiki budi nisherehekee! Kilicho tokea mahakama badala ya kujibu hoja ikaamuru Mtikila apimwe akili yake kama ipo sawa!
   
 4. Shoo Gap

  Shoo Gap JF-Expert Member

  #4
  Sep 27, 2012
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 236
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Ninadhani pamoja na madhaifu yake kama alivyo mwanadamu yeyote, tuna mambo mengi ya kujifunza kwa Mch. Mtikila. Ikiwezekana kiandikwe kitabu cha maisha ya Mtikila na issue kadhaa kama hizi ziwekwe ndani. Tusisubiri akishatutoka(Ingawa ninamwomba Mungu ampe maisha marefu) ndo tuanze kutoa kauli za kumuenzi na kumtunukia nishani kadhaa.
   
 5. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #5
  Sep 27, 2012
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Tatizo la Mtikila hakawii kubadilika.
   
 6. Thegreatcardina

  Thegreatcardina JF-Expert Member

  #6
  Sep 27, 2012
  Joined: Mar 29, 2009
  Messages: 396
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 45

  Hii ya kusheherekea kifo cha Nyerere ilileta gumzo kweli. Mpaka watu walihoji mbona ndugu zetu Wajaluo wanasherehekea kwa kucheza muziki misiba yao na hakuna polisi wanakwenda kuwazuia? Iweje kwa Mchungaji Mtikila?
   
 7. mgt software

  mgt software JF-Expert Member

  #7
  Sep 27, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 10,716
  Likes Received: 1,626
  Trophy Points: 280
  kesi yake ya mwaka 1992 alishinda kirais; aliuliza hivi; wakati gani uliniona kikiwa kwenye gari? Shuhuda nikuwa mita 6; gari lilikuwa linasukumwa na watu wangapi S. Kama kumi; walikuwa wakiimba mtikila mtikila; Akageuka kwa hakimu akimu naomba tutoke nje litafutwe gari lolote uingie na watu kumi wakusukume na mtu huyu akae mita sita alafu shuhuda aimbe mtikila mtikila, akimu akafanya hivyo, shuhuda akaulizwa kwa umbali wako unaweza kuona mtu aliyendani ya gari ? s. hapana , je wewe ulipoimba mtikila mtikila uliimanisha kuwa ndiye aliyeko kwenye gari s. hapana, kesi ikaisha hivyo kwamba waliokuwa wanaimba ni kwa furaha yao wala hakuwepo yeye.
   
 8. Shark

  Shark JF-Expert Member

  #8
  Sep 27, 2012
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 20,046
  Likes Received: 7,257
  Trophy Points: 280
  Mtanganyika Original,

  Mwanzilishi wa neno "Gabachori"
   
 9. mgen

  mgen JF-Expert Member

  #9
  Sep 27, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 15,148
  Likes Received: 1,882
  Trophy Points: 280
  Mkuu, Sikumbuki ni mwaka gani Lakini alishtakiwa kwa kesi ya kuwagomea police kuweka alama za vidole! Siku ya kesi alimuuliza mwendesha mashtaka ni kwa muda gani ukiweka alama za vidole zinaxpire mwendesha mashtaka akawa hajui! Ndipo Mtikila akamsaidia kujimu kwamba ni miaka 100 na kumpa rejea, ndipo alipomjulisha kuwa nimesha chukuliwa alama za vidole dodoma, msimbazi.... Zimexpire lini mpaka mchukue nyingine?Kesi ikaisha kwa ushindi wake!
   
 10. BASIASI

  BASIASI JF-Expert Member

  #10
  Sep 27, 2012
  Joined: Sep 20, 2010
  Messages: 3,090
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Ahaaahaaaa mkuu ujamjua huyoo niulize mie
  nilikuwa nasali nae kanisa moja pale shule ya jamhuri mpwa ..sasa basi pastor wa lile church linaitwa fullsalvation church akaanza kwenda marekani kila mwaka mara mbili mpaka tatu akisema amepata wadhamini wakanisa akawa akija anakuja na plan za makaratasi kanisa litakuwa hivi miradi itakuwa hivi..nk sas basi wakshangaaa mbona anaendelea kwend anje anarudi asemi ameleta nini...akanzisha mapinduzi ndan ya kanisa akahamia shule ya uhuru nae akajiita mchungaji...baada ya mud alile kanisa mchungaji akabadilisha jina likaitwa foundation ya mtu kule marekani ijulikanayo ark foundation church unaweza google arkfoundation ...washarika wakashtuka mbona hivi frm fullsalvation church -arkfoundation gafula watot wa pastor wakaishia wote marekani loh kanis likaishia hapo wakahamia kwa mtikila ....alipoaribu kule ni pale mweka hazina wa kanisa alipoteua ndg gojia yaani mkewe hapo ndipo watu wakakimbia maana hata kanisa walilohama mweka hazina alikuwa mchungaji na ukisikika unaongelea uchaguzi unafukuzwa na yeye kanisa lake likafia hapo mwosha uoshwa
   
 11. BASIASI

  BASIASI JF-Expert Member

  #11
  Sep 27, 2012
  Joined: Sep 20, 2010
  Messages: 3,090
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Huyo ndie rev
  christopher mtikilla
   
 12. mgen

  mgen JF-Expert Member

  #12
  Sep 28, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 15,148
  Likes Received: 1,882
  Trophy Points: 280
  Sina haki ya kuhukumu kiumbe dhaifu yale niliyo yaona kwake ndio ninachokishuhudia!
   
Loading...