Mara ya kwanza ugenini, visa na vituko

Mara ya kwanza ugenini, visa na vituko

Duuu! Ulitisha mkuu, napata picha yako kama 'mzee wa kukurupuka' wa futuhi
 
ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha

mkuu hiki ni kichekesho nimecheka mpaka tumbo linauma aisee

yaani aibu naona mimi
Pamoja sana.
 
You made my day...

Anyway...hata mimi ni mgeni hapa kibaruani.
 
Kufukia sawasawa maana ile mijaruba ya Salawe,Solwa,Didia si mchezo kuilima.
 
Ndiyo matatizo ya watu wamjini, huwa wanashani kila mtu anatosheka kipimo chao
 
Nimezaliwa katika familia duni mkoani Shinyanga.Nilifeli darasa la saba,mbaya zaidi nikafeli vibaya mno kidato cha nne (Elimu ya watu wazima, alimaarufu masomo ya jioni). Wakati nikisubiri matokeo, bibi yangu anayekaa Mwanza aliniomba nikamtembelee wakati nikisubiri matokeo.

Niliondoka na salfeti langu kama la Ommy Dimpoz,lenye fulana niloyamalizia shule, Kasuruali pamoja na lifulana lingine jeusi lililopauka ambalo lilikuwa na shingo pana yakutosha kupitisha vichwa vya watu watatu (nilikuwa nikiipenda sana nguo hii). Nilipokelewa vizuri sana na baada ya kufika nyumbani, niliandaliwa maji ya kuoga, kisha nikaambiwa nijongee sebuleni kupata chakula.

Kufika mezani nilikuta hotpot tatu, sahani za udongo na vibakuli, 1 Ilikuwa na ugali laini mkubwa kiasi, 2 ilikua na nyama iliyokuwa inanukia vizuri mno, 3 ilikuwa na mchicha wenye mapambo (karoti).

Nilichofanya nilichukua mchicha nikachanganya na nyama, nikauchungulia ule ugali nikuona naumudu peke yangu bila usaidizi. Nikautwanga wotee, nikabuguia nyama zotee na mchicha. Vikabaki vimchuzi mchuzi nikainua hotpot nikavinywa.

Kabla sijaweka hotpot chini,mjukuu wa kike wa yule bibi akaingia,nikasikia akiambiwa "P chakula kiko mezani muachieni mjomba na dada".

Jicho lilinitutumka kama kitenesi, chakula cha mtu tatu nimekiteketeza alone, aibu gani hii. Nililoa jasho la fedheha, nikawa mdogo kama punje ya ufuta.

Je wewe ni masahibu yapi yalikukuta ugenini?
Kisa umekiandika kwa staili nzuri sana ya kuvutia. Numekipenda hiki kisa cha ugenini.
 
Kisa umekiandika kwa staili nzuri sana ya kuvutia. Numekipenda hiki kisa cha ugenini.
Acha tu mkuu,ile ilikuwa shule tosha.Vijana wetu,watoto wpewe fursa za kutembelea sehemu nyingine ili kujua upande mwingne watu wanavoishi.Kama uwezo upo lakini.
 
hahah! una mambo wewe
Unasound kama yule mjukuu wa bibi nakumbuka alipenda kumwambia dada yake mgeni mwenyewe hana hata pozi ingawaje mwishoni alitokea kunikubali sana na mpaka leo ni mabestee vibaya munoo.
 
Unasound kama yule mjukuu wa bibi nakumbuka alipenda kumwambia dada yake mgeni mwenyewe hana hata pozi ingawaje mwishoni alitokea kunikubali sana na mpaka leo ni mabestee vibaya munoo.

teh! Basi sawa
 
alivyokula hapo ugenini hicho chakula cha watu watatu ndivyo alivyokuwa akila kwao kijijini! kijijini maisha safi sana asikwambie mtu aisee!!

Alikuwa hajastaarabika wala hana "table manners", utaanzaje kula kabla ya wenyeji na wewe ni mgeni? ni punguani tu afanyae hivyo.
 
Back
Top Bottom