Mara moja tu.....!

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,808
2,000
MARAMOJA TU poster 3NEW.JPG

View attachment 160771

MARA MOJA TU!

UGONJWA UNAO ANGAMIZA WANAUME WENGI DUNIA YA LEO !
KARIBU KILA MWANAUME AMEPATA KUUGUA UGONJWA HUU, LAKINI WACHACHE WANATOKA SALAMA!

STORY INAKWENDA HIVI:

Peter alikutana na msichana mrembo wa kuvutia Vita, mara moja tu! ndipo balaa lote lilipo anza. Usiku huo alijaribu sana kutumia kinga (condom) lakini hoteli aliofikia usiku huo zilikuwa zimekwisha, na maduka ya mtaani hapo yalikuwa yamefungwa usiku huo.

Baada ya jitihada kali, alirudi chumbani kwake na alipo fika mlangoni, alisita kidogo kabla ya kufungua mlango taratibu na kuchungulia ndani. Alimwona Vita akiwa amelala kitandani akiwa amelalia tumbo huku akiwa amejifunga taulo moja tu! roho yake ilimpasuka na mapigo ya moyo yalienda mbio!

" Nimwache aende! msichana zuri namna hii! haiwezekani!" akawaza "lakini si mara moja tu! hata hivyo ni msichana mzuri, mdogo, ametokea kijijini na wala haja haribiwa na wanaume wa mjini, lazima atakuwa salama"

DAKIKA CHACHE ZA STAREHE ZA MWILI, ZAWEZA KUKULETEA MAUMIVU NA MAANGAMIZI YA MILELE!
mara moja tu! ni filamu pekee inayo zungumzia vishawishi vinavyoweza kupeleka katika mojawapo ya njia kuu za maambukizi ya maradhi ya zinaa hususan VVU!
 

ICHANA

JF-Expert Member
May 10, 2012
4,780
2,000
ni kweli watu wengi wamekuwa na hili tatizo la kusema "mara moja"katika kutenda dhambi na hii mwishowe inawaletea shda
sana

kikubwa ni kuachana na hii kasumba mbaya ya kufanya mambo bila kufikiri madhara yake..tujitambuena tujue dhamani ya maisha yetu
 

akenajo

JF-Expert Member
Oct 21, 2012
1,618
2,000
Hii dhambi ya mara moja tuu nimeishindwa mie mpaka baada ya mwezi ndio eehh hv tulipima?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom