MARA: Baba ampa mimba mtoto wake, abaka wengine wawili

MARA: Baba ampa mimba mtoto wake, abaka wengine wawili

Nyanswe Nsame

Senior Member
Joined
Jul 9, 2019
Posts
166
Reaction score
182
Baba ampa mimba mtoto wake, abaka wengine wawili

MTU mmoja, Meshack Michael mkazi wa eneo la Nyamakokoto mtaa wa Mbulumatare halmashauri ya mji wa Bunda mkoani Mara anashikilia na Jeshi la Polisi mkoani Mara kwa tuhuma za kumpa ujauzito mtoto wake wa umri wa miaka 13.

Pia Michael anatuhumiwa kuwabaka watoto wake wawili wa kuwazaa kwa nyakati tofauti ambao ni wanafunzi wa shule ya msingi Balili wilayani humo.

Mama mzazi wa watoto hao Gaudensia Meshack amesema mmewe amekuwa akiwafanyia watoto wake vitendo hivyo kwa muda mrefu.

Amesema kuwa kuna kipindi alishawahi kunfumania akiwa kitandani na mtoto wake na alipomkuta mmewe aliomba msamaha.

"Nilishawahi kumkuta kitandani na mtoto wangu na nilipowakuta walishtuka na mme wangu huyu akaomba msamaha na mimi nilimsamehe kwa kuwa mimi ni mtu wa dini na namna tulivyolelewa.

"Ukiangalia hii amekuwa akiwafanyia watoto wetu watatu na mmoja alishampa ujauzito," amesema Gaudensia.

Gaudensia ameiomba Serikali kumchukulia hatua kali za kisheria mme wake ili kuwa fundisho kwa watu wengine hatua ambayo itasaidia kukomesha vitendo hivyo katika jamii.

Mkurugenzi wa Shirika lisilo la kiserikali la kutetea Haki za wanawake na watoto la KIVULINI ,Yassin Ally ameishauri Serikali kuwa, pindi shule zitakapo funguliwa ni vyema wanafunzi wakapimwa ujauzito na magonjwa mengine.

Amesema kuwapima ujauzito na magonjwa mengine itasaidia kuwabaini watoto waliopata mimba na kuweza kuwasaidia.

Afisa maendeleo ya jamii wa mji wa Bunda Bonji Bugeni ameiomba jamii kuwafichua wale wote wanaowafanyia vitendo vya ukatili watoto wadogo.

Amesema jamii inapaswa kuacha kufumbia macho vitendo hivyo na badala yake wanapaswa kutoa taarifa kwa vyombo husika ili kuwakamata na kuwachukulia hatua.

Mkuu wa wilaya ya Bunda ambae pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya humo, Lidya Bupilipili amekiri mtu huyo kushikiliwa na Polisi na kuitaka jamii kuacha vitendo vya ukatili wa kingono kwa watoto.

"Yaani kitendo hiki kimenisikitisha sana, baba anabaka watoto wake hadi na mwingine amempa mimba, hali hii haikubaliki tutamshughulikia ipasavyo," amesema Bupilipili.

Mkoa wa Mara wenye makabila 26 ni mkoa kinara unaoongoza kuwa na vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto kwa asilimia 78.
 
2d4c32811c4c5e81c34c195f67194252

Mama mmoja anayejulikana kwa jina la Gaudensia Michael, mkazi wa Nyamakokoto Halmashauri ya Bunda, Mkoani Mara, amesema kuwa siku ya kwanza aliyomfuma mume wake kitandani na mwanaye, aliamua kusamehe kwa kuamini kuwa kitendo hicho cha baba kuwaingilia wanaye kisingeendelea tena.

Gaudensia ameyabainisha hayo alipokuwa akizungumza na EATV, wakati mume wake akipelekwa katika kituo cha Polisi kilichopo wilayani humo kwa tuhuma za kuwabaka wanaye 2 kwa nyakati tofauti na huku mwanaye mwingine wa miaka 13 akimpa ujauzito, na kuiomba Serikali iingilie kati suala hilo kwa kuwa yeye hana jambo la kufanya tena.

“Kuna siku nilimkuta chumbani kitandani na mtoto, nikamuuliza nini kimekupungua mbona wanawake wengi sana, akaniambia mke wangu nisamehe, basi nikaachana na hilo suala kumbe likawa endelevu, mimi nakaa na wanangu kumbe ni wake wenzangu, kwa hili naomba Serikali inisaidie yamenitokea jamani na sina cha kufanya” amesimulia Mama wa watoto hao.

Yassin Ally ni Mkurugenzi wa Shirika la Kutetea Haki za Wanawake na Watoto la KIVULINI, amesema shule zitakapofunguliwa ni vyema wanafunzi wote wakapimwa ujauzito na magonjwa mengine, huku Afisa Maendeleo ya Jamii wa Mji wa Bunda, Bonji Bugeni, akiitaka jamii kuwafichua wanaowafanyia vitendo vya ukatili watoto.


Chanzo Eatv.tv
 
Wazazi, kabla hujaruhusu Binti yako aolewe, hakikisha akili ya mkweo (mume wa Binti yako ina utu au ubinadamu).

Sidhani kama kuna mzazi atafurahi kuona wajukuu zake wanaishi maisha ya unyanyasaji wa kijinsia.

I hate gender violence to both parts, men and women.

Kasie Platinumz.
 
Sichangii lolote linapotokea Kanda pendwa kwani wamejaliwa kila aina ya laana! Sijui kangi atamwitaje huyu poti? Malaika au roho wa upako?
 
  • Thanks
Reactions: Auz
Kama mimi ni huyo mama nilivyomkuta Mara ya kwanza nisingemsamehe.
Kingeeleweka.
Bora wewe unayesema ungekuwa ndo huyo mama, usingemsamehe huyo bazazi lakini mimi ningekuwa kwenye mamlaka, ningemtia ndani na huyo mama akakae angalau kwa wiki moja ili atie adabu.

Yaani seriously anakiri kwamba huyo mumewe ilikuwa ndo mchezo wake na amekuwa akifanya hhivyo kwa muda mrefu na ameshawahi kumkuta redhanded!!

Hapo inaonesha hiyo mimba ndo imebumburua kila kitu halafu sasa ajifanye kuiomba serikali imchukulie hatua kali! Watoto watatu, wote wadogo anawagonga, hivi inawezekana wote hawakuwa wanamwambia let alone siku alipomfumania!!!

Hata huyo Jesus aliyesema samehe 7x70 kama kweli alisema, I believe wala hakumaanisha kwa mambo ya kishenzi kama haya.
 
Back
Top Bottom