unapoishia kuwaza wengine wanaanzia hapo.
ZITO ni mwanachama wa CDM kama wengine hata NYERERE alikuwa mwana CCM hayupo na inadunda,Chacha Wangwe alikuwa mwana CDM,KABOURU,KAFULILA,MKOSAMALI,AKWILOMBE,SHITAMBALA.
chama kipo wanasiasa wanapita tu.
Dk k umezungumza jambo ila sijui ndani yako unadhamira gani Je ni dhamaira ya kumjenga Zitto aau Kumboa Zitto.Kwa kuwa maneno yako kwa namna fulani yeye binafsi Zitto akiyafanyia kazi na kujiangalia pengine unaweza kumsaidia.Kwaa sasa baadhi ya wancdm humu ndani wanakuona wewe kama mnoko fulani,lakini kwa mwanasiasa makini [Ambako mpaka sasa Zitto ajafika kuwa mwanasiasa makini japo analazimisha kuonekana kuwa mwanasiasa makini] maneno yako yangekuwa tiba na yeye kuyatumia kama kioo chake cha kupima jinsi jamii ya waelewa wengine wanamuonaje.
Moja ya tatizo la Mwanasiasa asie makini ni kutokuwa mwepesi wa kusikia mambo hasi [Negative Issues] zinazomuhusu yeye binafsi na utendaji wa mambo yake mazima kwenye mambo ya kisiasa.Wanasiasa makini daima uwa awasikilizi sifa zao utendeaji wao ,kwa kuwa sifa kwao ndio sehemu ya wajibu wao,Mwanasiasa makini daima uwa mwepesi kusikia maadui zake wa kisiasa na wakosoaji [Critics] wake wanasemaje kumuhusu.Kwa kuwa daima wakosaji wanakuonyesha mapungufu yako na kisha mhusika kutumia nafasi hiyo kunyoosha kisha sifa zinaludi palepale kwake kwa kuwa sifa kwake yeye ni wajibu sio kiburi au ujivuni.
Mwanasiasa mashuhuri na waziri mkuu wa Uingereza haijapata kuona Sir Churchill,alikumbana na wakosoaji kibao ndani ya maisha yake wakati wa harakati zake za kisiasa ikiwemo kuwa hana kiingereza kizuri,pata picha mwingereza anaambia hana kiingereza kizuri,kwa kuwa Sir Chuchill mwanzo wa ujana wake aliishi India kama mwakilishi wa serikali ya kikoloni ya waingereza hivyo kuathirika kwenye matumizi ya kizungu chake,pamoja na yote ndiye waziri mkuu bora kupata kutokea ndani ya ardhi hiyo ya markia.
Hivyo yanayosemwa kuhusu Zitto,kama atachukulia kuwa ni majungu na kuwa yeye yuko sawa uwo wote unaosemwa ni wivu wa kike,hakika ndani ya miaka kumi ijayo itakuwa imekula kwake.Zaidi akitaka kuwa Mwanasiasa makini yampasa kweli kubadilika na kuwa REAL MAN,mtu anaetembe kwenye kile anachoamini na si kufanya mambo ndani yake kuna migongo ya watu fulani,yampasa kuwa FREE MAN,kwa kuwa mtu aliye wazi daima ujisimamia,yasemwayo yapo kama hayapo yaja.Kuna jambo moja ambalo daima sijaliona kwa zitto ni mahusiano yake na baadhi ya vijana na watendaji wenzie ndani ya CDM.Ndoto zake haziwezi kufika popote bila ya kujipanga toka chini ukiwa na watu ambao wenye macho [Anawajua] yao wanaweza kuingiza mkono kukusaidia wewe na timu yako kufikia dhamila ya ndani,ikibidi wanauwezo wa kumpa support ya watu kutumika ili kutimiza dhamila yako kama kweli wanaiona ni GENEUINE.
Lakini ili la kujifanya mimi ndio mimi,the youngest CDM .........P Material ndani ya Nchi hakika atatumika vibaya na mwisho wake uenda ukawa mbaya sana na kuathili maono [vision] za vijana wengi sana.Kuachwe kale kauarrogance na stubborness kwa chama chake.Miaka ya tisini na ushee [1994s] kulikuwa na mwanasiasa machachali sana kwa jina la Amani Waridi Kabul hakika leo ni simulizi kwa Watanzania,kiasi kuwa wananchi hata hawana kumbukumbu zake kuwa alichangia sana kuinua CDM.Lakini ndani yake kulikuwa na kale kale katabia ka arrogance na stubborness hatimae ndio hivyo sijua kama yupo Bongo au alishaludi Marekani kufundisha.
Zitto usije ukaludi vyuoni kufundisha watch out,sikia...............jitahidi sana kusikiliza.........Pia tabia ya yeye kuonekana wazi wazi na watu ambao kwa namna nyingine wananchi wa kawaida hasa wana CDM watapokea mwonekano wake huo na wahusika kama USALITI.Na hata mimi binafsi sipendi tabia hiyo kumuona mtu ambae upande wa pili namuona kama opponet [rival] kisha the other side ndani ya timu anaonekana wazi wazi anamawasiliano ya wazi na dhahiri basi ni vyema mhusika akaamua kucheza American Sytle "IF YOU CANT DEFEAT THEM JOIN THEM".
Zitto is to young na anaitajika sana kujipanga na haya mengine ya siju.............kiti na vingora avipe muda miaka ishirini toka sasa,ajipange hata vijana wenzie kwa sasa watamuelewa sana hapo na kumuona kweli kaiva.Hata JK hapo alipo hakufika hivyo amepikwa akapikwa pata picha graduate unatupwa Lindi polini kisha watu wanauchubua,wala hawana time na wewe,wanakutoa hapo wanakurusha sijui Zanzibar wanakupotezea.Hayo yote ndio uzoefu wenyewe uliomfikisha hapo na ndio kiongozi anavyopita na kufundwa.
Tusikulupuke na ujana na mengineyo,daima ujana unatufanya siku zote kuwa over ambitious na kuona kila jambo tunaweza na kumbe mambo mengine hayaitaji nguvu za ujana bali busara za ujuvi wa hali halsi ya Kidunia,ambayo mhusika uwa ameshajifunza kupitia misukosuko kadha wa kadha yakiwemo majaribu ya makusudi ili kumfanya imara na mwenye uwezo wa kuamua mambo muhimu juu ya mamilioni ya watu wanaotegemea uamuzi wake kama ndio jibu kila mwisho la utatuzi wa hatima ya jamii.
Hivyo yanayomjenga Zitto, yasichukuliwe kama chuki kwa baadhi bali kama nafasi adimu ya yeye kujijua na kuona kioo kingine kinamuonaje.