Binafsi hata mimi sioni maana ya kugawa fedha kwa mchezaji mmoja wakati wapambanaji ni wengi.
Sema hata anaefanya utumbo huo kichwani hakuna kitu, hata TFF wanashindwa kuelewa hii kitu inajenga ubinafsi uwanjani ili kila mtu aonekane mwamba.
Viongozi wa TFF wengi wao ni wanafiki wakubwa na halafu wanamuogopa na kumnyenyekea huyo Mkuu wa mkoa wakiamini kuwa kinachooekana ni ukaribu wake kwa JPM 'kutawasaidia' wao....Binafsi nasema kwa moyo wa dhati kabisa TFF wamefanya kosa kubwa mno la kimkakati kumteua huyo mkuu wa mkoa kwenye kamati inayoitwa sijui ya uhamasishaji wa Taifa stars...hana sifa hizo...anaigawa Taifa Stars....katika mazingira haya Taifa Stars haitafika mbali...uwepo wake kwenye Taifa stars unawafanya hata Watanzania kugawanyika katika kuishangilia timu...Kwa kuliona hilo yeye mwenyewe alipaswa kujiondoa kwenye Taifa Stars kwani TFF hawana ubavu wa kumuondoa kwani ni watu wa kujipendekeza....Wachezaji ni kitu kimoja ...ushindi wa timu ni wa wachezaji wote...huwezi kumpa mchezaji mmoja sh. milioni 10 eti kwa kuwa alidaka penalti...vipi kuhusu waliofunga penalti...kama unataka kumpa fedha fanya hivyo kisiri siri bila kutangaza...fanya hivyo personal...Binafsi nilipokuwa naongoza mpira nilikuwa nafanya hivyo lakini kimya kimya kwa wale wanaonesha juhudi kubwa uwanjani..Ukigawa fedha hadharani kwa mchezaji mmoja unawa=demotivate wengine...
Nakumbuka upo mwaka Yanga ilimsajili mchezaji mmoja aitwaye Elisha John kutoka Coastal Union ..alikuwa ni kiungo yule nadhani namba sita kama sijakosea na alikuwa timu ya taifa...viongozi wa Yanga wakawa wanammwwagia fedha waziwazi huyo Elisha John..wachezaji wengine wa Yanga wakaona isiwe noma...wakati wa mechi wachezaji wengine wa Yanga wakawa wanampasia mipira mingi huyo Elisha ili afunge yeye aliye kipenzi wa baadhi ya viongozi wa Yanga ...Mazingira yale yakamshinda Elisha kwani aliondoka Yanga baada ya kukaa pale nadhani siyo zaidi ya miezi sita..., ...
Poleni TFF kwa kutoona mbali kuhusu suala la uendeshaji wa Taifa Stars...poleni sana kwa kweli...TFF imejaza kwenye kamati watu wanaopenda sifa na wapigaji dili...wengine hawana hata sifa .