Mapumziko ya Rais Magufuli Chato ni fundisho

Mapumziko ya Rais Magufuli Chato ni fundisho

Magufuli chapa kazi mzee. Tunakuombea kwa mungu akuongezee ujasiri mala dufu na weredi wa kazi ubarikiwe sana

Sent from my itel_it1503 using JamiiForums mobile app
 
Hongera kuwa msemaji wa rais.

Sent from my TECNO-W3LTE using JamiiForums mobile app
 
Akisikia masamaki ametoka, atakatisha mapumziko.

Sent from my TECNO-C9 using JamiiForums mobile app
Juzi juzi wakati wa kuzindua mradi wa upanuzi (?) wa bandari aligusia juu ya yule mwenye ICD inayotumika kukwepa kodi. Akasema kampuni husika 'ilijiua' wakati fulani lakini ikafufuka kwa jina tofauti. Hakusema kwa nini ilifanya hivyo lakini inaelekea anafahamu. Walio kwenye industry husika wanasema kiwango cha kodi kilichoibiwa na kampuni hiyo na washirika na wafadhili wake kini kikubwa kuzidi nchi ilichopoteza kwenye madini ndani ya makinikia. Nahisi anatumia mapumziko hayo kutafakari hatua za kuchukua. Nimbonyeze: baada ya kusema maneno yale mabango ya matangazo ya kampuni hiyo kwenye barabara ya Mwenge hadi Tegeta 'yameyeyuka'. Sijui kwenye barabara nyingine kama ni hivyo hivyo!
 
Akapumzike ng'ambo kwa lugha ipi ambayo atakuwa anatumia?
Baadhi yetu sisi watanzania ni WAPUMBAVU sana.
Wazungu wanapokuja huku kwetu wanatumia lugha gani?

Sent from my TECNO-Y4 using JamiiForums mobile app
 
tmp_3268-fb_img_1499868909948-1557722374-jpg.540545
Safi sana
 
Huyu ndio aliomsema juzi Ka John....? Mbona Samia hayupo hapo? Alisema hakubakwa!!! Na shule imeishia hapo!!! John buana!!! Hana kosa lakini ka John....wala Mama yake hana kosa! Babu John weeeeeee
 
Eti fundisho! Kipi ambacho hukijui n.a. umefunzwa ?

Sent from my SM-J110H using JamiiForums mobile app
 
Kwa Mara kadhaa,watanzania tumeshuhudia Mh.RAIS wetu kipenzi cha watanzania akitumia Muda wake mwingi,Nguvu zake na Akili zake zote kuwatumikia watanzania usiku na Mchana.Ameonesha Uzalendo kwa watanzania na Taifa kwa ujumla.

Mh.Rais yupo nyumbani kwake Chato kwa mapumziko mafupi baada ya Ziara na kazi kubwa ya kujenga Taifa.Mapumziko ya Mh.Rais yanatufundisha nini?,Ingalikuwa ni Rais asiye mzalendo wa kweli,Mapumziko haya angeweza kuyafanya nchi za ng'ambo,Marekani,Dubai,Uingereza na Mataifa mengine makibwa yenye Nguvu ya Kiuchumi.

Mh.Rais,kwa kuthamini,Kujali na kutetea maslahi mapana ya kodi za Watanzania,Mh.Rais Yupo Chato kijijini kwake,Amekomaa na Tanzania yake.Najua Jamaa zetu wanatamani sana Mh.Rais asafiri nje ya nchi hata kwa siku moja tu.Lakini Mjomba ni Boda tu Boda.(Home movement).Serikali ya JPM INA sikio la usikivu sana,Kwanini imesikia ?

Vyama vya siasa vilijipatia umaarufu sana kumseama sana Mh.Kikwete na viongozi waliopita kuwa safari zao za nje ya nchi ni Matumizi mabaya ya kodi za watanzania,Chai Ikulu ni Matumizi mabaya ya kodi za watanzania,Semina na walsha ni Matumizi mabaya ya kodi za watanzania,Posho za vikao ni Matumizi mabaya ya kodi za watanzania nk,nk.

JPM,kwa hekima ,unyenyekevu na kwa Sauti ya upole akasema "NIMESIKIA KILIO CHENU" sasa everything STOP.Hakuna safari Nje ya nchi,hakuna posho,hakuna chai ya Ghalama nk,Wakaanza ooooh,Ooooh mbona Rais hasafiri nje jamani!!!!! Oooooh mbona posho hazitoki jamani!!!!!!!,Ooooh Safari za nje wabunge vipi jamani!!!!!!! nk,nk.

"Nimesikia kilio chenu,Sasa ni kila MTU awajibike sawa sawa na Maombi yake" Huyu ndiye Rais anayeendelea kugonga vichwa vya HABARI Duniani nzima kwa utendaji wake,kwa misimamo yake,kwa uzalendo wake,na kwa Uadilifu wake wa hali ya Juu.Lazima tuige mfano wa Kiongozi wetu Mkuu.

Tuendelee kumuombea matashi mema MH.Rais na serikali yake,Tuendelee kuwaombea Viongozi wetu wa chama cha mapinduzi ,Lakini tuendelee kuwaombea pia wale wa upande wa Pili ili waendelee kubatizwa kwa moto.Watanyooka tu.

Mungu Ibariki Tanzania
Wala hayuko mapumziko Bali matibabu ya kale kajama lake,,.......
 
Back
Top Bottom