Mapumziko ya Rais Magufuli Chato ni fundisho

Trump2

JF-Expert Member
May 28, 2017
1,553
2,608
Kwa Mara kadhaa,watanzania tumeshuhudia Mh.RAIS wetu kipenzi cha watanzania akitumia Muda wake mwingi,Nguvu zake na Akili zake zote kuwatumikia watanzania usiku na Mchana.Ameonesha Uzalendo kwa watanzania na Taifa kwa ujumla.

Mh.Rais yupo nyumbani kwake Chato kwa mapumziko mafupi baada ya Ziara na kazi kubwa ya kujenga Taifa.Mapumziko ya Mh.Rais yanatufundisha nini?,Ingalikuwa ni Rais asiye mzalendo wa kweli,Mapumziko haya angeweza kuyafanya nchi za ng'ambo,Marekani,Dubai,Uingereza na Mataifa mengine makibwa yenye Nguvu ya Kiuchumi.

Mh.Rais,kwa kuthamini,Kujali na kutetea maslahi mapana ya kodi za Watanzania,Mh.Rais Yupo Chato kijijini kwake,Amekomaa na Tanzania yake.Najua Jamaa zetu wanatamani sana Mh.Rais asafiri nje ya nchi hata kwa siku moja tu.Lakini Mjomba ni Boda tu Boda.(Home movement).Serikali ya JPM INA sikio la usikivu sana,Kwanini imesikia ?

Vyama vya siasa vilijipatia umaarufu sana kumseama sana Mh.Kikwete na viongozi waliopita kuwa safari zao za nje ya nchi ni Matumizi mabaya ya kodi za watanzania,Chai Ikulu ni Matumizi mabaya ya kodi za watanzania,Semina na walsha ni Matumizi mabaya ya kodi za watanzania,Posho za vikao ni Matumizi mabaya ya kodi za watanzania nk,nk.

JPM,kwa hekima ,unyenyekevu na kwa Sauti ya upole akasema "NIMESIKIA KILIO CHENU" sasa everything STOP.Hakuna safari Nje ya nchi,hakuna posho,hakuna chai ya Ghalama nk,Wakaanza ooooh,Ooooh mbona Rais hasafiri nje jamani!!!!! Oooooh mbona posho hazitoki jamani!!!!!!!,Ooooh Safari za nje wabunge vipi jamani!!!!!!! nk,nk.

"Nimesikia kilio chenu,Sasa ni kila MTU awajibike sawa sawa na Maombi yake" Huyu ndiye Rais anayeendelea kugonga vichwa vya HABARI Duniani nzima kwa utendaji wake,kwa misimamo yake,kwa uzalendo wake,na kwa Uadilifu wake wa hali ya Juu.Lazima tuige mfano wa Kiongozi wetu Mkuu.

Tuendelee kumuombea matashi mema MH.Rais na serikali yake,Tuendelee kuwaombea Viongozi wetu wa chama cha mapinduzi ,Lakini tuendelee kuwaombea pia wale wa upande wa Pili ili waendelee kubatizwa kwa moto.Watanyooka tu.

Mungu Ibariki Tanzania
 
tmp_3268-fb_img_1499868909948-1557722374-jpg.540545
 
Hayo maneno utafikiria labda nchi hii imeshawahi kupata Rais njee ya CCM ina maana kwa maneno hayo unakashifu na kujaribu kuwa vua nguo walio mtangulia ambao ni wazee wenu jaribu kupima kabla ya kuandika kijana wa Lumumba...

Sent from my SM-N910H using JamiiForums mobile app
 
natamani nijue hii tshirt imeandikwa nini..Eniwei tunamtakia mapumziko mema, akitoka huko aje kuendelea kunyoosha majizi
Namshauri Mkuu, kama inawezekana apelekewe Kundi la Watoto, au atembelee yeye mwenyewe katika KUNDI/RUNDO la watoto, hii itampa RELIEF (a PEACE OF MIND + HEART).

Naamini akitoka mapumziko, Nguvu itakuwa ni Zaidi ya SIMBA.

Hapo itakuwa ni KAZI KIPEO CHA PILI..
wa Namba, wataisoma tu...kama hawataki Kujituma kufanya kazi..

Na wamasikio (wale wasikilizaji, kisha kutoa kasoro) Watazidi kunukuu..!!

Ni ushauri tu, akishindwa hilo Mkuu, ashinde kwa muda mrefu AKIOGELEA (Swimmig) kwa saa tatu kwa wiki. katika POOL...!



Sent from my SM-A500F using JamiiForums mobile app
 
fundisho liko wapi sasa hapo? nimeipenda hiyo picha na mjukuu wake,

Sent from my HUAWEI P7-L10 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom