Mapokezi ya dhahabu: Wakenya si kama sisi, watakuja kutueleza ukweli ni upi

Haya mambo yatia mashaka, iweje majuzi tu Rais wa nchi hiyo ametoka kufanya ziara kwenye eneo lenye utajiri mkubwa wa madini na kuna tetesi pamoja na kupewa wale tausi pia alisindikizwa na madini .
Hizi kiki sasa zimekuwa too much.
 
Haya mambo yatia mashaka, iweje majuzi tu Rais wa nchi hiyo ametoka kufanya ziara kwenye eneo lenye utajiri mkubwa wa madini na kuna tetesi pamoja na kupewa wale tausi pia alisindikizwa na madini .
Hizi kiki sasa zimekuwa too much.
Madini yalikamatwa mwaka jana.. Ysmerudishwa mwaka huu
 
Wakenya tambueni kuwa siasa za Tanzania ni tofauti na za huko kwenu, sisi Tanzania Demkrasia ilishazikwa na tukaisahau, tumebaki na siasa za kiini macho, leo huku kwetu hakuna uchaguzi huru wa viongozi kupitia sanduku la kura isipokuwa kuna uporaji wa kura kwa kupitia polisi na nec.
Hivyo mumuonye mapema Uhuru asiige siasa za huku atakuja kuwaletea shida kwenye siasa zenu ambazo kwazo mmeshapiga hatua sana kwenye mambo ya kidemokrasia.
Hivi kweli ndege hiyo hiyo iliyo tua hivi karibuni chato tena hiyo hiyo imetua Dar ikiwa na madini ya wizi?
Majuzi tu tumesikia huko kwenu Kenya mkiingia kwenye mgogoro wa biashara ya dhahabu feki.
Kueni makini sana na siasa za Tanzania, hizi ni zetu inabidi tuzizoe kwa hii miaka mitano inatosha 2020 tutachana nazo.
 
Kuna mtu kunidokezea kwamba ile ilikuwa ni mbinu na propaganda ya kuwatoa Watanzania kwenye suala la Mchangao wa nyongeza ya Mishahara yaani Statutory Annual increments na Madaraja kwa watumishi wanaostahili kupandishwa vyeo na Madaraja. Changa la macho kama kawaida hiyo ni funika
 
Wanasema izo dhahabu zimekamatwa miaka kumi na tano iliyopita hapo ndio nimechoka. Sijui walikuwa wanasubiri nini muda wote uo kuzirudisha
 
Mimi naomba niseme nitakuwa wa mwisho kuamini moja kwa moja hili tukio na nitajipa muda kwanza kabla ya kusifu na kupongeza.

Vile vile naamini kama kuna jambo nyuma ya pazia,basi ni swala la muda tu kabla ya media za Kenya kuanza kuweka hadharani ukweli wa mambo kama walivyofanya kwenye ile kashifa ya kampuni ya Indo Power Solution kwenye sakata zima la koroshow.

Wazungu wana msemo: "once bitten,twice shy".

Alafu pengine hii sijui ni namna ya kujaribu kuonyesha kuwa mahusiano yetu hayana mushikeri yoyote licha ya yaliyotokea siku za nyuma kama ile habari ya kuchoma vifaranga na matamshi ya yule mbunge wa Kenya kwa maana ya kufanya damage control?

Naomba niishie hapa.
Mkuu Salary Slip, ule upande wako umeishiwa hoja za kuupamba, sasa unaanza kuweka mafuta ya taa kwenye kuni kavu, ili iweje?
 
Ufisadi kenya tunaujua sana, swali hapa ni:
Jee hiyo dhahabu kweli ilikuwa 35kg tuu?

Jee hizo pesa zilikuwa hizo tuu?

Ama wajanja walisha kata zao.
Hadithi yenyewe haina background hata kidogo. Kawaida tulitarajia kurudishwa nyuma mpaka pale ambapo MTU anakamatwa uwanja was ndege Nairobi na hizi kilo za dhahabu. Magazeti ya Kenya hayakuandika habari ya hili tukio.? Magazeti ya Tanzania hayakuandika kihusu hili tukio kubwa kama hili?
 
Maneno ya Jaguar yamesaidia indirectly kurudisha urafiki mzuri wa awali wa Kenya na Tanzania.. Ila Kenyans ni marafiki ila ni kuwa nao macho, mtoto wa nyoka ni nyoka..!! Usifikie urafiki wa kukaribishana chumbani au jikoni, mwisho sebuleni plse
 
Basi kesho magazeti yote hii ndio itakuwa habari.Cha ajabu,baadhi ya mambo ya hovyo hovyo ya awamu hata kuyaandika hawaandiki.
Siku hizi wapinzani wakiongea hoja za msingi, Wahariri ama wanazipotezea au kuzipa uzito mdogo.Na tangu watishwe baada ya kuripoti press conference moja ya Zitto siku za nyuma,uogo na hofu imewazidi mpaka kero!!
Exactly magazeti redio hayafanyi research za habari wao ni kutwanga tu
 
Dhahabu imekamatwa miaka kumi na tano nyuma.mhhh
Walikuwa wanasubiri nini muda wote huo?ama kweli movie zingine kama za za
Bwakila ankooo ndio tunaonyeshwa wale watanzania wanaoambia sio wajinga
 
Back
Top Bottom