Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 16,818
- 62,030
Kama wengi mnavyoshuhudia yanayojiri nchini. Nchi yetu kwa sasa hivi ipo katika mapito magumu na makali kuelekea mabadiliko. Hapana shaka mabadiliko yanakuja na hakuna mtu wa kuyazuia maana huu ni wakati wake. Yeyote atakayejaribu kuyazuia yatamtupa pembeni au kumsaga tikitiki, maana hili ni tufani kubwa. Kwa wengi mnaofuatilia historia ya mabadiliko tangu enzi za manabii wa Mwenyezi Mungu hadi watu wapigania mabadiliko utaona ufanano mkubwa sana na yanayotokea nchini hasa yakimhusisha Tundu Lissu na chama cha CHADEMA nitaeleza.
1. Lissu kuwekwa Jela ni kama Yusuf alivyowekwa Jela.
Yusufu alifanyiwa fitina, akasingiziwa kesi ya uongo kuwa alitaka kumbaka mke wa kiongozi mkubwa huko Misri. Hatimaye Yusuf alikaa Jela masiku mengi tu kwa sababu ya kesi ya mchongo. Ukisoma Qur'an tukufu juu ya kisa cha Yusufu, Yusufu alimwambia Mwenyezi Mungu kuwa kwa yanayoendelea Misri ni heri akakaa Jela kuliko baadae kuja kujikuta anafanya mambo ya ajabuajabu kwa sababu ya yanayojiri ndani ya Misri. Na Qur'an hiyohiyo inasema kuwa kwa hakika kisa cha Yusufu na nduguze ni kisa chenye mazingatio makubwa sana kwa watu wenye kupenda kutafiti mambo. Ukimuangalia Lissu, kitendo cha kuwekwa ndani kwa kesi ya mchongo, na kitendo cha yeye kuwa tayari kulipa gharama hiyo bila kucompromise kwa kulamba asali, bila shaka hili litupe mazingatio makubwa sana watu tunaopenda kuchunguza mambo. Eventually tunajua ni hatma ya Yusufu, baadae alikuja kuwa kiongozi mkubwa ndani ya Misri.
2. Wanaohama CHADEMA na kisa cha Wana wa Israel wanaotaka kurudi Misri.
Leo operation ya No Reforms no Election ndiyo operation kubwa ambayo inaweza kubadili siasa za nchi hii kwa kuweka pressure kubwa kwa watawala wafanye japo reforms za kuboresha hali ua kisiasa nchini. Operation hii ni kama vile operation ya EXODUS, kuondoka Misri kwenda katika nchi ya ahadi, ni operation ya Musa Kumconfront Pharaoh na kumwambia BWANA asema "LET MY PEOPLE GO". Cha ajabu wakati safari ya kwenda Canaan imeanza, kuna watu katika kundi wanasema Canaan ni mbali sana bora wabaki Misri (Statis quo), Wanasema Japo Pharaoh ni mbaya lakini kule Misri kuna vitunguu, matango, matikiti maji, kwa nini wapate shida njiani kwrnda Canaan wakati Misri japo kuna shida lakini kuna vyakula vizuri?. Hawa ndo hao G55 ambao wamezoea kuibiwa chaguzi lakini wana ndoto ya viti maalumu, wengine wamezoea kuuza viti kipindi cha msimu wa chaguzi, wengine ni mapandikizi ya Pharaoh. Lakini eventually nani alikuja kuibuka kidedea, movement ya Musa au resistance ya Pharaoh?. Hii movement ya CHADEMA kwa sababu ni movement ya haki, inayosimamiwa na watu ambao ni genuine itashinda tu.
3. Usaliti wa Mbowe kama Brutus kwa Juliasi Kaizari (Et tous Brutus?)
Leo Chama kiko katika vita ya kupigania maslahi mapana ya umma, lakini wakati huo kinaingiziwa mgogoro wa kukiua na kukimaliza kabisa (Existential threat). Kundi la Mwenyekiti mstaafu linaleta fujo, linafanya uasi ndani ya chama, kundi kubwa la watu waliokuwa wanamuunga mkono mwenyekiti mstaafu linafanya vurugu, vitimbi na kila aina ya hila kuiua taasisi iliyojengwa kwa machozi jasho na damu. Mwenyekiti msataafu amekaa kimya, haongei chochote. Mwenyekiti wa sasa yuko jela, lakini haonyeshi solidarity na wanachama wenzao kumtetea mwenyekiti wao. Hii inanikumbusha kisa cha muasisi wa dola ya Urumi Julias Kaizari alipotengenezewa fitna ya kumalizwa, akaja kushangaa na mtu wake aliyemuamini sana aitwaye BRUTUS naye yumo katika njama. Wakati Julias Kaizari amewekwa mtu kati akashangaa kumuona na BRUTUS kuwa naye yumo katika njama, Julius Kaizari akamuuliza HIVI KWELI NA WEWE BRUTUS? (ET TOUS BRUTUS?). Na sisi Watanzania tunamuuliza Mbowe (ET TOUS MBOWE?).
4. Kisa cha mzalendo Patrice Lumumba na Wasaliti akina Mobutu Seseseko
Patrice Lumumba, alikuwa mpambanaji, mzalendo wa kweli wa Kongo, alikuwa na dhamira njema. Alikuja kusalitiwa na watu aliowaamini akina Mobutu Seseseko. Akina Mobutu waliweka mbele maslahi binafsi na si Taifa, wakasaidiwa na Watesi wao (Wakoloni wakiwemo wabelgiji) wakageuka manamba wa kusaidia Kongo kuendelea kuwa shamba la bibi in exchange ya vyeo, fedha na ulua feki. Leo hii hawa G55 wanasaliti course nzima kwa ajili ya vyeo vichache, kwa ajili ya pesa. Akina Lissu ni mrengo wa akina Lumumba wanaangalia Mustakbsli wa Taifa la kesho, lakini hawa G55 hawana tofauti na akina Mobutu. Wao ukombozi wa Watanzania siyo priority, wao wanajiwaza wao peke yao.
5. Yuda Iskariot na Vipande 30 vya fedha.
Pamoja na kuaminiwa na Yesu Kristo, na kumfanya kuwa miongoni mwa inner circle yake, lakini Yuda aliona kuwa vipande 30 vya fedha ni bora kuliko mission ya Yesu, na ni bora kuliko heshima aliyopewa na Yesu akamsaliti. Hawa wanaoisaliti CHADEMA ya leo ni mfano wa "Mayuda Iskariot" wengi tu ambao historia imewashuhudia. Ni kweli watapata hizo fedha, lakini kamwe hazitokuwa na baraka, hazitowafaa chochote, kiufupi hazina wema ndani yake kwa sababu ni pesa za hila, dhulma na ulaghai mtupu.
MWISHO.
Watawala watake wasitake mabadiliko nchi hii hayakwepeki. Ulaghai una mwisho, na hakuna fedha zisizo na ukomo za kununua watu. Udhaifu hauondolewi kwa kufanya mambo dhaifu zaidi.
Huwezi kupambana na sauti za wananchi, huwezi kupambana na jumuia za kimataifa, huwezi kupambana na Ukweli uliowazi kuwa mifumo ya uchaguzi nchini ni mibovu na katiba yetu ni mbovu. Huwezi kupambana na historia ya mabadiliko nchini tangu enzi za Jaji Francis Nyalali hadi Tume ya mabadiliko ya katiba ya Jaji Warioba
Lissu na Heche wanadhamiri safi, wangetaka kugombea ubunge wangefanya lakini hawajafanya kwa dhamiri njema na hilo ndilo litakalowapa ushindi.
Nimalizie kwa kuwaambia watawala wa nchi hii kama maandiko yalivyosena kumwqmbia Pharaoh LET MY PEOPLE GO, na mimi nawaambia LET TANZANIANS BE FREE!