Mapishi ya wine (mbege) hatua kwa hatua

Hazard CFC

JF-Expert Member
Apr 7, 2015
16,616
38,586
Hatua kwa hatua mapishi ya mbege.
Mahitaji kimjini mjini
1. Ndizi mbivu
2.ulezi
3.msesewe
4.mkaaa
5.ndoo walau 4
5. Maji

Chukua ndizi mbivu zilizoivaa kabisa na kulainika sana,zimenyee kwenye chombo kisafi uziponde ponde( hii inasaidia ziive mapema)..zitie kwennye sufuria zichemshe bila maji mpaka pale zitakapobadilika rangi kabisa na kua na rangi kama kahawi,wakati wakuchemsha zikiwa zinaanza kubadilika rangi weka msesewe husaidia baadae pombe yako kua na ukali..ziepua ndizi zako weka kwenye vikontena usijaze hadi juu na ziache kwa siku saba ndizi zichachuke(zikatike).

Chukua ulezi wako uoshe vizurii na kisha weka kwenye viroba(mifuko iliosha sukari au unga) ziache kwenye mifuko zichujike maji hadi kesho yake, zimimine kwenye sakafu safi zitandaze kwa muda kama masaa 12, sikusanye kwa pamoja zinyunyuzie maji yakutosha kisha changanya hakikisha zote zinapata maji yakutosha,zitandaze tena kisha funika kwa siku moja hadi mbili zianze kuota...baada ya kuota siku mbili zifunue na kuziachanisha kisha kazianike zikaule hapo utakua umepata kimea safii kabisaa...

Baada ya siku saba chukua ndizi zako zile changanya kwenye chombo kimoja kikubwa kisha zitie maji inategemea na vipimo vya ndizi zako,kama ulipika ndoo moja tia maji ndoo mbili, ziache kwa masaa kadhaa kisha tafuta chujio locally unaweza tumia viroba hivi vya kuwekea mchelee kuzichuja ndizi zako ili upate ile juice nyekundu kabisaa..

Kasage ulezi wako(kimea) kisha weka maji ya moto mimina unga wako koroga hakikisha unaiva kabisa na kupata uji zitoo uache upoe..

Chukua ile juice yako ya ndizi kwenye chombo safi pipa au jaba mimina humo kisha chukua ule uji wa ulezi changanya pamojaa...hapo unapata togwa safi kabisaa tenga togwa yako kwa wale wasiotumia kilevi wanaweza kunywa..baada ya hatua hiyo weka msesewe wa kutosha uliosagwa koroga kisha funika....

Subiri kwa siku moja pombe yako itakua tayarii.... wingi wa alcohol kwenye pombe yetu inategemea na ndizi zilizotumika,mda ndizi zilivyokaa kwenye uchachushaji,ulezi n.k

December ndio hiyo wadau twendenii zetu moshi tukapate darasa kwa vitendoo,mimi sio mwelezeaji mzuri sana kwa anaetika kujifunza kwa vitendo asisite kunitafuta

Imeletwa kwenu na hazardihoo
 
Bosi maelezo yako hayajitosjelezi mkuu, huo uliouita msesewe Ninini, na ukakatika product gani unga,maji,mbegu ama Ninini? Na niwapi unapopatikana? Na kazi yake Ninini? Na nisipoweka athari zake ninni kwenye mbege.

Kati ya ulezi na ndizi zinazotajikana kuwahi kuandaliwa ninini?
 
Naomba kirikiri hapo ninywe mbege.kwa ulivyoelezea naona ipo tayari kwa ajili ya kunywewa.

Arifu Hama huko tutakupoteza.kijana mzuri kama wewe kutengeneza mbege hapana kwakweli 😅
 
Bosi maelezo yako hayajitosjelezi mkuu, huo uliouita msesewe Ninini, na ukakatika product gani unga,maji,mbegu ama Ninini? Na niwapi unapopatikana? Na kazi yake Ninini? Na nisipoweka athari zake ninni kwenye mbege.

Kati ya ulezi na ndizi zinazotajikana kuwahi kuandaliwa ninini?
Kuna mti unaitwa msesewe unachonga magome yake unaanika then unasaga...unapatikana sana uchagani kule

Ulezi unaweza kuaandaa siku yoyote ila ndizi ni ndani ya siku saba
 
Hatua kwa hatua mapishi ya mbege.
Mahitaji kimjini mjini
1. Ndizi mbivu
2.ulezi
3.msesewe
4.mkaaa
5.ndoo walau 4
5. Maji

Chukua ndizi mbivu zilizoivaa kabisa na kulainika sana,zimenyee kwenye chombo kisafi uziponde ponde( hii inasaidia ziive mapema)..zitie kwennye sufuria zichemshe bila maji mpaka pale zitakapobadilika rangi kabisa na kua na rangi kama kahawi,wakati wakuchemsha zikiwa zinaanza kubadilika rangi weka msesewe husaidia baadae pombe yako kua na ukali..ziepua ndizi zako weka kwenye vikontena usijaze hadi juu na ziache kwa siku saba ndizi zichachuke(zikatike).

Chukua ulezi wako uoshe vizurii na kisha weka kwenye viroba(mifuko iliosha sukari au unga) ziache kwenye mifuko zichujike maji hadi kesho yake, zimimine kwenye sakafu safi zitandaze kwa muda kama masaa 12, sikusanye kwa pamoja zinyunyuzie maji yakutosha kisha changanya hakikisha zote zinapata maji yakutosha,zitandaze tena kisha funika kwa siku moja hadi mbili zianze kuota...baada ya kuota siku mbili zifunue na kuziachanisha kisha kazianike zikaule hapo utakua umepata kimea safii kabisaa...

Baada ya siku saba chukua ndizi zako zile changanya kwenye chombo kimoja kikubwa kisha zitie maji inategemea na vipimo vya ndizi zako,kama ulipika ndoo moja tia maji ndoo mbili, ziache kwa masaa kadhaa kisha tafuta chujio locally unaweza tumia viroba hivi vya kuwekea mchelee kuzichuja ndizi zako ili upate ile juice nyekundu kabisaa..

Kasage ulezi wako(kimea) kisha weka maji ya moto mimina unga wako koroga hakikisha unaiva kabisa na kupata uji zitoo uache upoe..

Chukua ile juice yako ya ndizi kwenye chombo safi pipa au jaba mimina humo kisha chukua ule uji wa ulezi changanya pamojaa...hapo unapata togwa safi kabisaa tenga togwa yako kwa wale wasiotumia kilevi wanaweza kunywa..baada ya hatua hiyo weka msesewe wa kutosha uliosagwa koroga kisha funika....

Subiri kwa siku moja pombe yako itakua tayarii.... wingi wa alcohol kwenye pombe yetu inategemea na ndizi zilizotumika,mda ndizi zilivyokaa kwenye uchachushaji,ulezi n.k

December ndio hiyo wadau twendenii zetu moshi tukapate darasa kwa vitendoo,mimi sio mwelezeaji mzuri sana kwa anaetika kujifunza kwa vitendo asisite kunitafuta

Imeletwa kwenu na hazardihoo
Mbona umesahau kutenga sambo

Sent from my SM-J500F using JamiiForums mobile app
 
Bosi maelezo yako hayajitosjelezi mkuu, huo uliouita msesewe Ninini, na ukakatika product gani unga,maji,mbegu ama Ninini? Na niwapi unapopatikana? Na kazi yake Ninini? Na nisipoweka athari zake ninni kwenye mbege.

Kati ya ulezi na ndizi zinazotajikana kuwahi kuandaliwa ninini?
Msesewe baada ya kuchanganya ukezi ulopikwa kwenye ndizi ulokamua (hiyo siku ya pombe kamili sasa)kama sukari inakhwa imezidi ndio unatia huo msesewe kama vijiko 2 hivi ili kuongeza uchungu fulani

Sent from my SM-J500F using JamiiForums mobile app
 
Bosi maelezo yako hayajitosjelezi mkuu, huo uliouita msesewe Ninini, na ukakatika product gani unga,maji,mbegu ama Ninini? Na niwapi unapopatikana? Na kazi yake Ninini? Na nisipoweka athari zake ninni kwenye mbege.

Kati ya ulezi na ndizi zinazotajikana kuwahi kuandaliwa ninini?
Msesewe Ni mti mchungu mno ukiukata unatoa maziwa maziwa unatoa vitunda vya kijani size ya zabibu!
Jina la kisayansi unaitwa rauvoflia caffra ingia Google utauona
 
Naufaham mkuu, nilikua nataka mleta mada aende ndani kidogo, nijuavyo Mimi sio kiungo Cha lazima kwenye maandalizi ya mbege.

Mbege iliobora chanzo chake kikuu Ni ule uchanganyaji wa ndizi zilizo pikwa na maji. Pindi maji yakiwa kiasi kidogo mbege inayatarajiwa huwa bora sana
images%20(4).jpg
 
Similar Discussions

4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom