Mapishi ya biriani

Mapishi ya biriani

Nanasi kwenye kikali? Sijawahi ona live.
Mie nachanganyaga na energy japo kuna siku ilitaka kuniletea kashda, kidogo niimbiwe parapanda.
Cheap energy drink ni mbaya mfano mo energy,Azam energy sio nzurii labda ZILE energy drink expensive kidogo.
Energy drink sio nzurii Sana naziogopa maana zinakataga usingizi pombe ikiisha kichwani.
Jarib hata nanasi ya AFIYA utaona io cocktail yake.

Kuna ambao huchanganya na maziwa fresh 😀 dunia hii Ina maajabu mengi mengi sanaa
 
Mahitaji ya Kupika Biriani
Viambato vya Msingi
Wali (mchele wa Basmati) – Vikombe 3
Nyama ya mbuzi, kuku, au nyama nyingine yoyote – Kilo 1
Vitunguu maji – 3 vikubwa (katwa mviringo na kukaangwa hadi rangi ya dhahabu)
Nyanya – 4 (saga hadi ziwe laini)
Mtindi wa asili – Vikombe ½
Kitunguu saumu na tangawizi ya kusagwa – Vijiko 2 vya supu
Mafuta ya kupikia au samli – Vikombe ½
Chumvi – Kiasi cha ladha
Viungo vya Biriani
Binzari ya pilau (cumin) – Kijiko 1 cha chai
Mdalasini – Vipande 2
Hiliki – Mbegu 5
Karafuu – Mbegu 5
Paprika au pilipili ya unga – Kijiko 1 cha chai
Binzari manjano (turmeric) – Kijiko ½ cha chai
Majani ya mint au coriander – Kiasi cha kupambia
Hatua za Kupika Biriani
1. Kuandaa Nyama
Osha nyama vizuri na uikate vipande vya wastani.
Weka nyama kwenye sufuria, ongeza mtindi, tangawizi na kitunguu saumu, nyanya, na viungo vya biriani (binzari ya pilau, hiliki, mdalasini, karafuu, na paprika).
Changanya vizuri na acha ichemke kwa moto wa wastani hadi nyama iwe laini na mchuzi uwe mzito.
2. Kuandaa Wali
Osha mchele na uuweke kwenye maji safi kwa dakika 30 ili ulainike kidogo.
Chemsha maji mengi kwenye sufuria na ongeza chumvi na binzari manjano kwa ladha na rangi nzuri.
Weka mchele na upike hadi uwe karibu kuiva lakini usiutoe kabisa (unapaswa kuwa na ukoko kidogo).
Chuja maji ya wali na uweke pembeni.
3. Kukaanga Vitunguu
Kwenye sufuria tofauti, kaanga vitunguu hadi viwe vya rangi ya dhahabu. Hii itaongeza ladha na muonekano wa kuvutia kwenye biriani yako.
4. Kupanga Biriani
Katika sufuria kubwa, pakiza tabaka za mchanganyiko wa nyama na wali.
Anza na tabaka ya mchuzi wa nyama, kisha funika na wali, na endelea kupangilia hadi viambato vyote viishe.
Nyunyiza vitunguu vya kukaanga na majani ya mint au coriander juu kwa ajili ya harufu nzuri na ladha.
5. Kukamilisha Kupika Biriani
Funika sufuria vizuri na ipike kwa moto wa chini kwa dakika 20 hadi 30. Hii husaidia viungo na ladha kuchanganyika vizuri.
6. Kuhudumia
Tumikia biriani ikiwa moto na usindikize na kachumbari, mchuzi wa nyama, au maziwa ya mgando.
Vidokezo vya Mafanikio
Chagua mchele wa ubora mzuri: Mchele wa Basmati hutoa biriani yenye muonekano mzuri na ladha ya kipekee.
Epuka wali kupitiliza kuiva: Wali wa biriani unapaswa kuwa na ukoko kidogo ili usikunjike unapochanganywa.
Tumia moto mdogo mwishoni: Hii husaidia wali na mchuzi kuiva vizuri bila kuungua.
Viungo vya biriani ni muhimu: Viungo vinachangia harufu nzuri na ladha tamu ya biriani.
Faida za Biriani
Mlo wa kukaribisha wageni: Biriani ni chakula kinachoheshimiwa kwenye hafla mbalimbali.
Mchanganyiko wa ladha: Inakutanisha ladha ya nyama, wali, na viungo vya asili kwa namna ya kipekee.
Inaweza kubadilishwa kulingana na upendeleo: Unaweza kutumia mboga badala ya nyama kwa biriani ya mboga.
Hitimisho
Kupika biriani ni sanaa ambayo inahitaji uvumilivu na upendo lakini matokeo yake ni mlo wa kipekee na unaofurahisha.

Kwa kufuata hatua hizi rahisi unaweza kupika biriani nyumbani kwa ladha nzuri kama ya mgahawani.
👏👏👏👏👏
Asante sana kwa maelezo.
Mwachiluwi uje sasa utoe diko kesho.
Sema biriani lina process kama sijui kitu gani!

Yaani unaweza ghahiri kula.
 
Mwanzo nilihisi hivyo nikaenda kununua pale kwa nino ijumaa morocco hali ikawa ivyo ivyo pilau ina uhafadhari tofauti na birian
Ndio ivo wanaripua tu
Wakishaweka marangi ndio wanaona washapika biriani
Pia mchele wa basmat upo kwa grade. Mchele utaopika wewe nyumbani kilo elfu 5 au elfu 6 sio sawa na wa hizo restaurant wanaokoteza tu Michele ya kuitwa basmat kumbe hamna kitu
 
Cheap energy drink ni mbaya mfano mo energy,Azam energy sio nzurii labda ZILE energy drink expensive kidogo.
Energy drink sio nzurii Sana naziogopa maana zinakataga usingizi pombe ikiisha kichwani.
Jarib hata nanasi ya AFIYA utaona io cocktail yake.

Kuna ambao huchanganya na maziwa fresh 😀 dunia hii Ina maajabu mengi mengi sanaa
Maziwa kwenye pombe kali?
Sijawahi sikia wala ona
Kweli dunia ina maajabu.

Energy inanipaga shida sana sema ndio hivo sina la kufanya.
Na nikinywa inanipelekesha hoi, sema napenda kale ka stimu kake ndio maana wakati mwingine inakuwaga ngumu kuiacha.
Ila ya maziwa sijawahi kuona, mbali ya kusikia pia
 
Mbona zanzi 😊

Huyo jamaa anachanganya pombekali na maziwa ntaweka ushahidi wa pichaa.
 
👏👏👏👏👏
Asante sana kwa maelezo.
Mwachiluwi uje sasa utoe diko kesho.
Sema biriani lina process kama sijui kitu gani!

Yaani unaweza ghahiri kula.
Madam B hujaona mkate wa kingazija (mkate wa gudugudu) unavyopikwa wee utablow
Mkate huo unapikwa siku nzima 😂😂😂
Katika kukua kwangu nimemuona mamaangu kaupika mara 1 tu.
Ila ukishapikwa unaweza kukaa zaidi ya mwezi mmoja upo fresh hauharibiki
 
Tobaaaa!!!
Siku nzima unapika mkate?
Gudugudu?
Sijawahi hata kuusikia.
Kweli vyakula na vitafunwa viko vya aina nyingi.
Ni kama mkate wa kawaida au upoje upoje huo?
 
Cheap energy drink ni mbaya mfano mo energy,Azam energy sio nzurii labda ZILE energy drink expensive kidogo.
Energy drink sio nzurii Sana naziogopa maana zinakataga usingizi pombe ikiisha kichwani.
Jarib hata nanasi ya AFIYA utaona io cocktail yake.

Kuna ambao huchanganya na maziwa fresh 😀 dunia hii Ina maajabu mengi mengi sanaa
Maziwa hayakatiki?
 
Tobaaaa!!!
Siku nzima unapika mkate?
Gudugudu?
Sijawahi hata kuusikia.
Kweli vyakula na vitafunwa viko vya aina nyingi.
Ni kama mkate wa kawaida au upoje upoje huo?
Kwa sura upo kama mkate wa sembe
Lkn kuna unga wake special unapikiwa sijui unaitwa uwanga. Then unawekwa na spices na sukari yake inaunguzwa inakuwa brown. Then unapikwa kama pudding, yaani sufuria ndani ya sufuria ya maji. Kwa moto mdogo mdogo. Inakuwa kazi ya kuongeza maji tu kwenye sufuria ya nje. Sasa ile sauti inayotoka wakati unapikwa ndio hio gudugudu
Hio mikate sio aghlab kuiona inauzwa kama vitafunwa. Ni upishi wa ki Comoro
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom