Mapishi – Ndizi Mshare na Nyama | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mapishi – Ndizi Mshare na Nyama

Discussion in 'JF Chef' started by Mamndenyi, Aug 19, 2011.

 1. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #1
  Aug 19, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,049
  Likes Received: 6,494
  Trophy Points: 280
  Mapishi – Ndizi Mshare na Nyama


  ndizi mshare.jpg


  Mapishi yetu ya leo yatakuwa ni ndizi mshare (wengi wanapenda kuziita ndizi moshi) na nyama ya ng'ombe.
  Mahitaji
  · Ndizi Mshare mbichi 16
  · Nyama ya ng'ombe 1/2 kilo
  · Vitunguu maji vikubwa 2
  · Nyanya 1
  · Pili pili hoho 1
  · Karoti 1
  · Mafuta ya kupikia kijiko kikubwa 1
  · Chumvi kiasi
  Matayarisho
  1. Osha nyama vizuri na kata kata vipande vidogo unavyopendelea na kisha uichemshe hadi iive. Nyama yenye mafuta kidogo na mifupa kidogo inafaa sana kwa ndizi.
  2. Menya ndizi zako vizuri na kuzikata katikati kwa urefu na kisha kwa upana (mshazari), kisha zioshe na kuweka kwenye sufuria yenye maji masafi.
  3. Katakata vitunguu, nyaya, karoti na pilipili hoho.
  4. Chukua sufuria yako ya kupikia weka ndizi kiasi kisha weka nyama na supu yake, na vitu vyote ulivyokatakata weka pamoja (vitunguu, nyanya, hoho na karoti) kisha weka na ndizi zilizobaki kwa juu. Hakikisha supu inatosha kuivisha ndizi, kama ni kidogo sana ongeza maji ya moto kidogo. Hakikisha ndizi hazizami zote kwenye supu.
  5. Bandika jikoni kwa moto wa kiasi na zikichemka, geuza na kisha weka mafuta ya kupikia (na nazi tui la kwanza ukipenda). Acha zichemke hadi ziive kabisa bila kuwa na kiini katikati.
  6. Epua na andaa meza tayari kwa kula.
  Enjoy!
   
 2. m

  ma jery Senior Member

  #2
  Aug 19, 2011
  Joined: Jun 15, 2011
  Messages: 171
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  eeka mama ulya shambuura maa
   
 3. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #3
  Aug 19, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  <br />
  <br />
  khee! ndo lugha gongana nini..
   
Loading...