Mapishi: Biskuti za kahawa


kbm

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Messages
5,144
Likes
268
Points
180
kbm

kbm

JF-Expert Member
Joined Oct 5, 2012
5,144 268 180
Mapishi: Biskuti za kahawa

Pamoja na kuwepo kwa aina nyingi ya biskuti, kumekuwepo na tofauti ya ladha. Hii hutokana na kutofautina kwa viungo kati ya biskuti moja na nyingine.
Hilo ndilo jambo linalozifanya biskuti za kahawa kuwa tofauti na biskuti za aina nyingine.
Mahitaji
Unga wa keki kilo moja
Chumvi nusu kijiko cha chai
Sukari nusu kilo
Siagi robo kilo
Mafuta ya kupikia kiasi
Baking powder kijiko kimoja cha chakula
Vanilla matone matatu
Kahawa vijiko viwili
Vya kujazia
Maji robu tatu kikombe cha chai
‘Icing sugar’ 200g
Siagi gramu 100
Maziwa robo tatu kikombe cha chai
Namna ya kutengeneza
Kwenye bakuli moja kubwa, weka unga wa ngano, chumvi, baking powder na sukari. Changanya vizuri, kisha chukua siagi na anza kukanda.
Weka matone matatu hadi manne ya vanilla. Chukua maji kidogo na weka kwenye mchanganyiko wako, huku ukiendelea kukanda hadi liwe donge gumu.
Funika na uache ukae kwa muda wa saa 12. Ikiwa umekanda usiku unaweza kuuacha hadi asubuhi.
Sukuma kama chapati, kisha kata katika umbo la biskuti. Kata na zipange kwenye bati la kuokea. Oka kwa muda wa dakika 8-12 kwa moto wa kawaida.
Vya kujazia: Chukua donge la kahawa na weka kwenye maji, koroga na kisha weka kwenye sufuria. Weka viungo vingine kama maziwa, siagi na sukari. Injika jikoni acha vichemke. Koroga kwa muda wa dakika tano kwa kutumia mwiko. Ipua na acha vipoe.
Baada ya hapo chota kidogo na tandaza kwenye uso wa biskuti moja na kisha weka nyingine juu yake. Fanya hivyo kwa biskuti zote.
Biskuti zako zipo tayari kwa kuliwa. Unashauriwa kuhifadhi katika chombo chenye mfuniko.

Source: http://www.mwananchi.co.tz/Makala/Mapishi---Biskuti-za-kahawa/-/1597592/1876972/-/item/0/-/12nwp3xz/-/index.html

Vicoba vinamilikisha wanawake uchumi
Kwa muda mrefu kumekuwa na kilio kikubwa cha wanawake kuwa nyuma kimaendeleo hali iliyosababisha kuwepo kwa harakati mbalimbali za kumkomboa mwanamke.
Miongoni mwa harakati hizo ni kuanzishwa kwa Benki za Kijamii Vijijini (Vicoba) ambazo ni muunganiko wa hiari wa watu wa eneo moja wenye nia moja na kuunganisha nguvu zao, raslimali zao na mawazo yao ili kuweza kutengeneza chombo cha pamoja cha kuwaletea maendeleo.
Nchini Vicoba vilianza rasmi mwaka 2002, hadi sasa vimeenea Tanzania nzima huku wanachama wengi wa vikundi hivyo wakiwa ni wanawake.
Kuwepo kwa Vicoba kumesaidia kumgusa kila mwananchi kuanzia wa kipato cha juu hadi wa kipato cha chini.
Scolastica Kevela ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Vicoba Tanzania, katika mahojiano na gazeti hili anasema kuwa miaka ya nyuma mila potofu zilisababisha wanawake kukandamizwa na kuonekana kama hawastahili kumiliki uchumi.
“Zamani mwanamke alikuwa hata akitaka kwenda kukopa benki au kwenye taasisi zingine za fedha anashindwa kwa sababu mali nyingi zilikuwa zikimilikiwa na mwanamume na kumfanya mwanamke aishi katika hali ya unyonge,”anasema Kevela.
Anasema kuwa mila hizo zilisababisha wazazi wengi kujali zaidi watoto wa kiume hasa katika upande wa elimu hali iliyowafanya watoto wa kike waendelee kuwa nyuma kimaendeleo, hata kwenye ajira na kujiona wao ni wanawake wa nyumbani.
Makamu huyo wa rais Vicoba, anasema kuwa baada ya kuanzishwa kwa Vicoba mwaka 2002, wanawake wengi wamekuwa na mwamko na kujiunga kwenye vikundi hivyo, ambavyo vimewawezesha kumiliki uchumi, hata kinababa wengi kuingia kwenye Vicoba.
“Tuliona wanawake wengi wananyanyasika kutokana na kukosa sifa ya kukopesheka kwa kukosa dhamana, lakini kupitia Vicoba wameweza,”anasema.
Anasema kwamba kupitia Vicoba mtu anaweza kukopa na kurejesha mkopo bila tatizo kwani riba ni nafuu na wanachama wa kikundi husika hukubaliana wenyewe katika kupanga riba.
Pia anasema wanashirikiana na Shirika la Kazi Duniani (ILO) kutoa mafunzo ya ujasiriamali kwa wanawake na vijana walioko kwenye vikundi vya Vicoba ili wajue namna ya kufanya biashara na kutumia vizuri mikopo wanayoipata.
“Tunafanya hivi kwa sababu mtu akipata mkopo bila kuwa na elimu ya awali ya ujasiriamali atatumia tofauti na malengo yaliyokusudiwa,”anasema.
Anasema kuwa wanawake ndiyo watendaji wakuu wa familia na kwamba idadi ya wanawake katika vikundi vya Vicoba ni kubwa ukilinganisha na wanaume.
Akieleza mchango wake katika kuwainua wanawake Scola anaeleza kuwa amekuwa akitumia muda mwingi kuhamasisha jamii hasa wanawake kujiunga kwenye vikundi na kuanzisha Vicoba ili kuweza kujikwamua kiuchumi.
Uhamasishaji huo umekuwa ukiufanyika kupitia mikutano au kwenda moja kwa moja kwenye makundi maalumu kama ya watu wenye ulemavu, kwenye masoko, mama ntilie na kampuni Dar es Salaam na mikoa mingine.
“Muda mwingi nautumia kutoa elimu ili isaidie jamii hasa wanawake kwani kama mtu anakopa na hajui akafanye nini hilo ni tatizo. Tumeshuhudia sehemu nyingi watu wakishindwa kurejesha mikopo na kunyang’anywa mali,”anasema.
Mwanamke huyo anaeleza kuwa kipato vikubwa vinawezesha kaya kuboresha uwezo wao kupitia elimu bora, afya, lishe na malazi na kuiwezesha Serikali kukusanya mapato kwa ajili ya utoaji wa huduma mbalimbali.
Anabainisha kwamba kwa sasa kuna Vicoba vya kaya, balozi, tawi, kata, wilaya, mikoa na taifa na kimataifa.
“Hivi sasa tuna ushirikiano na Marekani kwenye Jimbo la South Caroline kupitia Chuo cha Benedict kwenye mji wa Colombia na tuna mwaliko wa kwenda huko mwaka huu,”anasema.
Miongoni mwa mafanikio yaliyopatikana tangu kuwepo kwa Vicoba ni kuongezeka kwa ajira, kupatikana kwa mitaji, riba nafuu, kuondoa umaskini, kuwawezeaha wanawake kupata elimu ya ujasiriamali na kuweza kujitambua. Pia anasema kwamba Vicoba vimesaidia katika mapato ya nchi ambapo zaidi ya Dola za Marekani 30 milioni hukusanywa kwa mwaka kama kodi na kuingia katika mfuko wa Serikali.
“Hata manyanyaso ndani ya nyumba yamepungua kwa sababu wanawake sasa wana vipato vyao na wana uwezo wa kufanya uamuzi katika masuala mbalimbali ya maendeleo ndani ya familia,”anasema akiongeza:
“Lengo letu ni kuwa na Vicoba endelevu vyenye vikundi vingi sehemu mbalimbali.”
Kevela ana Shahada ya Uzamili ya Utawala aliyoipata Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) na pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Udalali ya Yono

Source: SCOLASTICA KEVELA: Vicoba vinamilikisha wanawake uchumi - Makala - mwananchi.co.tz
 

Forum statistics

Threads 1,273,558
Members 490,428
Posts 30,484,982