Mapinduzi yafanyika klabu ya simba uongozi waondolewa!!!

Mapinduzi yafanyika klabu ya simba uongozi waondolewa!!!

Naunga mkono mapinduzi despite what. Sijawahi, sina na sitakuwa na imani na Rage katika kuiongoza Simba. Ila sikubaliani na wazo la kumkabidhi timu malkini wa nyuki. Maana hiyo sasa inaonekana sisi ni njaa kali. Tunamkabidhi kwa kuwa ana hela?

Ndio.
Ni njaa.
Tukatae tukubali, njaa inatusumbua.
Na hata timu akipewa Crashwise utumbo utakuwa huu huu.
tukubaliane na ukweli kuwa Sisi washabiki wa Simba tuna njaa.

Ndio maana kuna tofauti kubwa kati yetu na watani zetu ambao hata ukipita pale Jangwani kwenye jengo lao utatamani usimame kisha upigwe picha ukiwa umesimama maeneo yale, kwani AC zinapepea, Vioo vinang'aa, maandhari mazuri.
Tofauti na jengo la KILABU yetu.
 
Yaani Leo hata hiko kikao cha simba nimekipa like juu kwa juu, na nimegawa like kwa watu wote waliokisapoti. Rage nyambafu kwenda tabora kahudumie jimbo, wewe jela ulistahili.


Povu...
Futa mimate hiyo kisha tuachie Rage wetu.
Tulimuweka pale kwa katiba, na katiba ndio itakayomuondoa.

Usikurupuke.
Rage hafukuzwi na genge la wahuni wengine walikuwa wanamung'unya ugolo, wengine wamekaa kama wapo kwenye mabanda ya simema uswahilini, na wengine walikuja pale kwa ajili ya kucheza mziki tu.

Tuachieni Rage wetu.
 
habari ambazo zimetapakaa kwa sasa ni kwamba ule mkutano ulioitishwa na wanachama wa simba umekubaliana kuondoa uongozi uliopo madarakani wa mh.adeni rage kutokana na sito fahamu katika timu hiyo kongwe ya soka hapa nchini.TIMU ITAKUWA CHINI YA MALIKIA WA NYUKI BI,RAHMA AL KHAROOS PAMOJA NA HANS POPE.(PICHA NYINGINE IYO INAANZA SIMBA).
Wanahangaika na RIBOLO.
 
Povu...
Futa mimate hiyo kisha tuachie Rage wetu.
Tulimuweka pale kwa katiba, na katiba ndio itakayomuondoa.

Usikurupuke.
Rage hafukuzwi na genge la wahuni wengine walikuwa wanamung'unya ugolo, wengine wamekaa kama wapo kwenye mabanda ya simema uswahilini, na wengine walikuja pale kwa ajili ya kucheza mziki tu.

Tuachieni Rage wetu.

Mpe dada yako ili uendelee kuwa naye personal. Simba ilikuwepo kabla ya rage na itaendelea kuwepo, kama vp nawe tupa like, kazi ziko nyingi sio lazima aongoze yy. Yaani tungeweka hata jiwe kuliko yule msomali. Acha ujinga ww, nn ugolo watu wanapiga cocaine na wako mjengoni.
 
Ndio.
Ni njaa.
Tukatae tukubali, njaa inatusumbua.
Na hata timu akipewa Crashwise utumbo utakuwa huu huu.
tukubaliane na ukweli kuwa Sisi washabiki wa Simba tuna njaa.

Ndio maana kuna tofauti kubwa kati yetu na watani zetu ambao hata ukipita pale Jangwani kwenye jengo lao utatamani usimame kisha upigwe picha ukiwa umesimama maeneo yale, kwani AC zinapepea, Vioo vinang'aa, maandhari mazuri.
Tofauti na jengo la KILABU yetu.

Mvua ikinyesha utatamani upige picha?
 
[h=1]Aden Rage apinduliwa Simba SC[/h]






[TD="align: right"] Submit Cancel [/TD]


Rating

aden.jpg
Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage.
Na Sosthenes Nyoni, Mwananchi




[TD="align: right"] Submit Cancel [/TD]


Awali uongozi wa Simba ulipiga marufuku mkutano huo usifanyike kwa sababu haukuwa halali, lakini jana wanachama wa Simba walifanya mkutano huo kwenye Hoteli ya Starlight jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wanachama zaidi ya 600


SHARE THIS STORY​
0
inShare​






Dar es Salaam.Mkutano mkuu wa dharura wa wanachama wa Klabu ya Simba umemwondoa madarakani mwenyekiti wao Ismail Rage na kuivunja Kamati ya Utendaji ya klabu hiyo kwa madai ya kukiuka katiba ya klabu yao.

Awali uongozi wa Simba ulipiga marufuku mkutano huo usifanyike kwa sababu haukuwa halali, lakini jana wanachama wa Simba walifanya mkutano huo kwenye Hoteli ya Starlight jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wanachama zaidi ya 600.

Hata hivyo, kwa mujibu wa katiba ya Simba, ni mwenyekiti aliye madarakani kwa kushirikiana na Kamati ya Utendaji ndiye mwenye mamlaka ya kupanga ajenda, mahali na wakati wa kufanyika kwa mkutano mkuu.

Mbali ya kumtimua Rage, mkutano huo pia ulimpendekeza aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya usajili ya Simba, Zacharia Hans Pope na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha ya Simba, Rahma Al Kharoos kuongoza Kamati Maalumu ya kuiongoza Simba hadi pale uchaguzi mkuu wa klabu hiyo utakapofanyika.

Mkutano huo uliokuwa chini ya uenyekiti wa Mohamed Wandi na katibu wake Maulid Said ulikuwa na ajenda iliyojadili mwenendo mbovu wa klabu ya Simba kwenye Ligi Kuu inayoendelea na kutokuwa na imani na viongozi wa Simba.

Akizungumza wakati akifungua mkutano huo uliokuwa na utulivu mkubwa huku ukilindwa na askari polisi wachache, Wandi alimlaumu Rage kwa madai kwamba amekuwa akiiendesha klabu yao bila kufuata katiba.

“Ibara ya 16 kipengele G inasema kutakuwa na mkutano kila baada ya miezi minne kujadili maendeleo ya klabu, lakini haujafanyika mpaka leo.

Alisema,“Ibara ya 22 ya katiba ya klabu ya Simba inatupa wanachama haki ya kuitisha mkutano endapo mwenyekiti na makamu mwenyekiti hawatakuwapo na Ibara ya 19 kifungu cha tatu inatupa mamlaka ya kumwandikisha na kumfukuza mwanachama.”

Baada ya kumaliza kusoma sehemu ya katiba ya klabu ya Simba aliyodai imekiukwa, Wandi aliwataka wanachama wenzake kuamua kama Rage na kamati yake ya utendaji ipewe muda zaidi au iondolewe ndipo wote waliponyoosha mikono juu wakitaka watimuliwe na kuunda kamati ya muda chini ya Hans Pope na Rahma Al Kharoos.

Hata hivyo, Hans pope alikataa kuchukua jukumu hilo akisema “Sijapewa taarifa yoyote juu ya uteuzi huo, hata hivyo siafiki suala hilo kwa vile hawajaomba hata ushauri kabla ya kufikia uamuzi wao.”

Juhudi za Mwananchi kuwapata viongozi wa Simba akiwamo ziligonga mwamba huku simu zao zikiita bila kupokelewa.
 
Mimi nasema SIMBA au YANGA HATA WAFUNDISHWE NA SPECIAL ONE,FERGUSON,WENGER au hata MANCINI kupinduana bila kufuata katiba kutakua pale pale.

Suala la mpira wa bongo ni mfumo mbovu wa viongozi wasiojua nini maana ya uongozi wa soka. Wanakumbatiana na kulewa sifa za mashabiki na wanachama wabovu waliotayari kuona timu zao za nyumbani zinafungwa saa 10 jioni alafu wanachama na mashabiki hao hao saa 3 usiku unawakuta wako bar wanawashangilia Man utd,Arsenal,Chelsea,Barca,Juve n.k.

Sasa unajiuluza hawa wanachama na viongozi hawajifunzi kitu kutoka nje ya Tanzania kuhusu soka!

Kila leo utasikia klabu haina pesa. Kuna vitu vya kufanya ambavyo hatuhitaji kuwa na mabilioni kufanya ila ni akili tu.
 
ARSENAL wameshinda mechi nyingi kwenye ligi ya england kuliko timu yoyote nyuma ya man u we arsenal ipi unayolinganisha na simba?
mimi sio arsenal lakini kwanini alinganishe mbingu na ardhi?
 
Ukiona mgonjwa anatapika dawa ujue mambo yashaharika.
 
i hate Rage!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! anadharau sana na analeta U-ndolanag ndani ya Simba!! hiyo ni michezo siyo Siasa za CCM bwana!! aondoke haraka sana tena sana!! atuachie Club yetu!!
 
Back
Top Bottom