demigod
JF-Expert Member
- Jan 2, 2015
- 8,288
- 15,238
Jana nilipata nafasi ya kukaa na mzee Kilomoni pale maeneo ya Msondo Bar kariakoo.
Katika piga piga story na Mzee yule nikaamua kuanza kufanya kazi ya upelelezi hata bila yeye Kujua, kwanza kabisa katika jitihada za kuanzisha story zihusuzo soka ikabidi nijifanye kuwa mimi ni shabiki wa Msimbazi. Nikaanza kwa kumuuliza, Mzee unaonaje mafanikio yetu simba sc kwenye msimu ulioisha?
Akajibu "Tume advance kidogo, ila tumezembea pakubwa kwa kuwahata ligi ilipaswa tuwe tumechukua" akaongezea kwa kusema "Msimu huu watani zetu hawakuwa vizuri sana, tungeweza kuishikiria uongozi wa alama zile nane, basi ungekuwa msimu mkubwa sana kwetu".
Nikamdokeza lingine! hili lilihusu suala la Rufaa ya simba. Akasema "Kuhusu ile rufaa! Mhhh sijui kama kutakuwa na mabadiliko yeyote haswa kwenye sualala ubingwa ambao umekuwa lengo kuu". Alionyesha nia ya kutotaka kuongea zaidi kuhusu hili.
Tukiwa tunaendelea na mengine nikaamua kugusia suala la Mama mmoja maarufu sana miaka ya 2013 pale simba.
Rahma Al Kharoosi aka "MALKIA WA SIMBA".
Basi Mzee Kilomoni akacheka sana: Akasema "Unajua nini! umenikumbusha suala fulani aisee".Nikauliza suala gani hilo? akasema "Ule msimu tulipoteza ubingwa kwa sababu ya yule Mama"
"Yule Mama alinekana kuwa ni mpigaji tu tangu awali, nilijitahidi kumminya sikio Mwenyekiti wangu AR kwa wakati huo, ila alionekana kuwa kinyume na mimi - nadhani zile pesa za yule Mama zilikuwa zinamtoa sana mate.
Mimi nikaamua kungoja muda uweze kutuambia, Nakumbuka msimu huo tulikuwa tunashiriki klabu bingwa barani Afrika kwa kuwa msimu uliopita wa mwaka 2011/12 tulikuwa mabingwa, basi yule Mama (sijui mlikuwa mnamuita Malkia wa Nyuki akaichukua simba ili ikaweke kambi Oman. Basi timu ilivyofika Omani haikuwa imepangiwa hata Hotel Maalumya kufikia .Ilibidi msafara mzima ufikie nyumbani kwake. (Hiikitu watu wengi hawajui, viongozi wengi walipenda iwe siri) Basi ikabidi hata uwanja wa mazoezi nao uwe shida, maana tulikuwa tukipokezana na timu tatu yaani mbili za daraja 2 na simba pia. Ile haikuwa kambi ya manufaa maana ni bora tungebaki tu \dar".
Anaendelea "Nakumbuka wachezaji kwa muda wa wiki moja walikuwa wakilala kwenye makochi ya sebule ya yule mama na wengine walikuwa wakitandikiwa mito kwenye sakafu. Kwa kuwa nilikuwa miongoni mwa msafara ilinibidi nifuatilie sababu nikaambiwa Hotel iliyofanyiwa Booking ilikuwa inafanyiwa ukarabati hivyo ilitupasa tungoje, basi wiki nzima ilitumalizikia nyumbani mwa yule Mama...Nakumbuka pia Kocha Lewig kwa kutumia pesa zake akakodi gest house peke yake. Kuhusu la hii kambi watu wengi hawajui kilichotokea huko Muscat."
Nikamuuliza Oman mliweka kambi kwa ajili ya nini? akasema "Tulikuwa kwenye msimu wa CAFCL kwa kuwa tulipoteza mechi ya nyumbani dhidi ya Recreativo Del LIBOLO kwa bao moja, tulihitaji kambi tulivu ili game ya marudiano Angola tuweze kupindua matoke, Ndani ya moyo wangu nikawa na shaka kubwa kuhusu hiyo kambi, kwakuwa sikuwa na sauti kubwa ilinibidi kuwa Kimya!, Tulianza safari ya kutoka Oman kwenda Angola, yule mama naye akaambatana na sisi kuelekea angola.
Cha kushangaza ile mechi tulipoteza bao 4 kwa bila, baada ya mpira kuisha yume mama aliingia vyumba vya Wachezaji na kuanza kuwatupia wachezaji matusi ...Ati kwanini wamepoteza mchezo ikiwa yeye amegharamikia Gharama zote za kambi kule Oman, kwa hasira yule mama akaondoka hata bila kuachia timu uhakika wa kurudi Bongo, basi ilitubidi tuongee na viongozi wa Bongo ili watume mkwanja wa kuisafirisha timu kurudi Bongo.Yule mama alirudi Oman na mpaka sasa hivi sijamuona tena. Nilisikiaga alikorofishana na Rage baada ya Rage kusikia yaliyotokea kambini Oman na Kuitelekeza timu Angola."
Basi Mzee Kilomoni alionekana kupokea simu na kusogea pembeni na kuongea kwa muda mrefu sana...na mimi nikaona isiwe taabu, nikamuonyesha ishara ya kumuaga naye akajibu NIKASEPA!