Sele Mkonje
JF-Expert Member
- Oct 2, 2011
- 643
- 846
Utafiti wa kitaalamu uliyofanya na wanahistoria bobezi kwenye harakati za siasa za pwani ya Afrika Mashariki wameandika, wametafiti na kuandika sana juu ya Mapinduzi ya Zanzaibar. Hata hivyo kuna nukta kadha wa kadha zinazotatanisha na hazipewi "nguvu" ya akili ya kisomi kwenye kudadavua hoja ya "nani muhusika mkuu" wa mapinduzi yale. Kwa upande mmoja, Mwalimu Nyerere anatajwa sana kuwa ni "mhandisi" wake; na kwa upande mwingine Mwalimu Nyerere anaonekana kama :wakala" wa kufanikisha mapinduzi yenyewe. Kwa utashi wa nani? Na, kwa nini? Haya ni masuala "nyeti" ambayo kwa sehemu kubwa yalishapatiwa majibu kitambo!
Kwa wasomaji makini na wanaofuatilia historia "angavu" ya harakati za siasa za "Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar" wanafahamu kwa nini Mwalimu Nyerere "alimlazimisha" Abeid Karume aingie kwenye "ndoa" iliyoitwa "muungano". Tazama nukta hizi kisha jiulize masuala yenye mchokoo wa kifalsafa na kiutafiti (uchunguzi + mantiki):
- Kabla ya mapinduzi, Mv Khaldun (ya Algeria) ilishusha "silaha" Dar es Salaam na iliagwa na Mwalimu Nyerere;
- Mara kadha wa kadha "Field Marshal" John Okello alionekana Ikulu ya Dar es Salaam hata kabla ya mapinduzi na baada yake;
- Hata Okello alipokosana na Karume alirudishwa Dar es Salaam chini ya "escort" ya POLISI na hata baada yake haikujulikana alipelekwa wapi;
- Jina la Tanganyika lilifutwa na nchi ya Tanganyika kuchukua jina la Tanzania Bara huku "Katiba ya Tanganyika" ilifanywa ndio katiba ya muungano;
- Mamlaka ya Zanzibar yaliwekwa chini ya "kivuli" cha Tanganyika na kuendeshwa bila ya katiba wakati wote wa Abeid Karume hadi alipouawa na nafasi yake kuchukuliwa na Aboud Jumbe;
- Tazama Mwalimu Nyerere alivyomlazimisha Aboud Jumbe kujiuzulu urais wa Zanzibar - tafuta sababu za kina (ilikuwaje na kwa nini?);
- Angalia jinsi Mwalimu Nyerere alivyolazimisha kuunganiswa TANU na ASP na kupatikana kwa CCM;
nimeipenda hii

Mkuu.Ghibuu, unapoamua kudanganya na kupotosha historia ya Zanzibar, basi angalau sema uwongo unaokaribiana na ukweli.
Umedanganya kihusu asilimia ya Waislamu Zanzibar kuwa ni asilimia 100% kwa 100%. Kimahesabu maana yake asilimia ya Wakristo ni 0.00% jambo ambalo si kweli!.
Naomba kukumbusha, hao waarabu unaowashabikia na kuwasujudia, nao ni watu wa kuja tuu huko Zanzibar, Sultan Said Said alitoka zake Oman na kuhashia makazi yake Zanzibar katika karne ya 17. Hapo Zanzibar alipakuta kuna wenyewe ambao ni wenyeji wa asili wa Zanzibar, jee unajua aliwafanya nini?. Unakijua kilicho wakuta?. Unajua ni kwa nini hawatajwi popote?.
Hilo na tuliache. Katika karne ya 18 jee unafahamu Zanzibar ndio ilishamiri kwa biashara ya utumwa?. Jee una taarifa watumwa waliopelekwa nchi za India na nchi za Kiarabu wote walitoka soko la Zanzibar?.
Jee unafahamu watumwa waliopelekwa nchi za Marekani na Ulaya walitoka soko la Afrika Magharibi?,
Unajua kilichowapata watumwa walipelekwa Arabuni na bara Hindi?,
Jee unafahamu baada ya kusimamishwa kwa biashara ya utumwa, watumwa wote waliokuwa sokoni na waliopenda kurejeshwa barani Afrika walirejeshwa?.
Watumwa wa soko la Marekani walirejeshwa nchini Liberia na wale wa Ulaya wakarejeshwa nchini Sierra Leone, jee wale wa soko la Zanzibar walirejeshwa wapi?.
Baada ya kusitishwa kwa biashara ya utumwa hata Zanzibar, jee wajua kuwa watumwa waliikwisha nunuliwa ili wawe huru, ilibidi wagombolewe kwa wanunuzi kurudishiwa fedha zao?, Jee wajua waliowagomboa ni kina nani na watumwa waliogombolewa walipelekwa wapi hapo Zanzibar?,
Jee wajua eneo lilipokuwepo soko kuu la watumwa Zanzibar enzi hizo leo pana nini?.
Majibu ya maswali hayo yatapunguza uwongo na utakatifu wa Waarabu unaowasujudia na kwa kwa vile ndio babu na bibi zako upande wa kikeni, then hakika wee uu mmoja wao?,
Hizo ndio sababu za Nyerere kutaka kupewa utakatifu! kazi kubwa aliyoifanya ni kutaka kuuobdoa uIslam Tangamyika na Zanzibar, lakini kwa hilo hakufaulu. uIslam upo, utakuwepo na ndio dini ya mwanzo na ya mwisho katika dunia hii.
Ukisoma kitabu cha KWAHERI UKOLONI KWAHERI UHURU cha mwandishi Harith Ghassany unakaribia kulia ukijua kwamba kumbe Mapinduzi ya Zanzibar si kama tunavyoyajuwa.Kwa upande mwengine kumbe uongo ni kitu kibaya sana kinacholeta maangamizi katika jamii.
Mwandishi anastahiki sifa kubwa ya kuwa mtafiti aliyebobea.Amehojiana na watu muhimu walioshiriki kuipindua serikali ya Zanzibar ambao wengi wala si wenye kusikika.
Ukisoma hiki kitabu ushahidi uko wazi kuwa mapinduzi yale yalikuwa ya chuki za kikabila na kidini na hayakufanywa na wazanzibari wenyewe.Kumbe Nyerere ndiye aliyesuka na kugharimia mapinduzi yale akikitumia chama cha TANU.
Viongozi wa mapinduzi wao wenyewe hawakujua kipi hasa kilikuwa kikiwaongoza kufanya mapinduzi,ni kumuondoa mwarabu mwenye rangi nyeupe na kumuweka mwafrika wa rangi nyeusi au ni kuwaweka watu wa bara waiongoze Zanzibar.Kauli zao na matendo ni vyenye kujichanganya.
Waliokuwa wakitawala Zanzibar walikuwa ni waislamu lakini hawakutekeleza uislamu,hili ni moja ya kosa lao kubwa.Ubwanyenye na ujinga wa kiutawala ulitoa fursa kwa maadui zao kuwapindua kirahisi.Hata hivyo nguvu ya adui aliyekuwa ndani yao na nje wasingekuwa na uwezo wa kuhimili tena.
Katika mkanganyiko huu walioathirika zaidi bila kosa ni wazanzibari waliotafsiriwa na viongozi wa mapinduzi kwamba wana asili ya kiarabu,wengi wao wakiwa wala hawako kwenye utawala.
Nyerere alipata kusema kuwa udini na ubaguzi ni kama ukoma lakini kwa hakika alitumia ukabila na ubaguzi kujenga udini.
Nyerere kwa Afrika anaweza kuitwa baba wa Mapinduzi.Yeye aliweza kuongoza Mapinduzi ya Zanzibar,akawapinduwa waislamu ndani ya TANU na hupati taabu kuona kwamba yeye alishiriki kumuua Karume kupitia kamanda wake Ali Mahfudh.Nyerere alikuwa na damu ya kimapinduzi tu lakini si kwamba mapinduzi aliyoyafanya yalikuwa yana umuhimu.
Kwa wakristo Nyerere anaweza kuonekana ni shujaa lakini kwa waislamu ni mtu mbaya mno.
Harith Ghassany ni nani na hiki kitabu 'KWA HERI OKOLONI, KWA HERI UHURU' KINAPATIKANA WAPI?

Nipe history,nipe ushahidi usiandikie mate..Nyerere amelipiza walichofanya waarabu kutok Oman Miaka 150 nyuma kwa kuwanyonga masista aw Kikatoliki waliokuwa wameshaijenga Zanzibar Kabla . Asante Nyerere
Nipe history,nipe ushahidi usiandikie mate..
Kwa taarifa yako wakati huo .Lille mnaliita Arab Fort, au Ngome Kongwe, alilijenga Nani? Je weye wajua kuwa Laitwa Portuguese Fort? Enzi hiz o? Nenda Kwenye web ya catholic au wasiliana nami nikupe histori ya zenji, wengi wenu mlikuwa bado Congo Kabla hamjaletwa watumwa
Soma website ya Kanisa katoliki Zanzibar
Salaam aleikum
Utafiti wa kitaalamu uliyofanya na wanahistoria bobezi kwenye harakati za siasa za pwani ya Afrika Mashariki wameandika, wametafiti na kuandika sana juu ya Mapinduzi ya Zanzaibar. Hata hivyo kuna nukta kadha wa kadha zinazotatanisha na hazipewi "nguvu" ya akili ya kisomi kwenye kudadavua hoja ya "nani muhusika mkuu" wa mapinduzi yale. Kwa upande mmoja, Mwalimu Nyerere anatajwa sana kuwa ni "mhandisi" wake; na kwa upande mwingine Mwalimu Nyerere anaonekana kama :wakala" wa kufanikisha mapinduzi yenyewe. Kwa utashi wa nani? Na, kwa nini? Haya ni masuala "nyeti" ambayo kwa sehemu kubwa yalishapatiwa majibu kitambo!
Kwa wasomaji makini na wanaofuatilia historia "angavu" ya harakati za siasa za "Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar" wanafahamu kwa nini Mwalimu Nyerere "alimlazimisha" Abeid Karume aingie kwenye "ndoa" iliyoitwa "muungano". Tazama nukta hizi kisha jiulize masuala yenye mchokoo wa kifalsafa na kiutafiti (uchunguzi + mantiki):Ukitumia "akili" isiyokuwa na "uzezeta" wala "uzimbezimbe" unaweza kupat "mawingu" ya kwa nini Mwalimu Nyerere alikuwa nyuma ya "mapinduzi" ya Zanzibar na kwa nini aliamua kuchukua "nafsi" hiyo! Kama humjui John Okello, tazama picha iliyoambatanishwa na makala haya na ujaribu kutafakari alikuwa nani (na jiulize nani alimlepeleka Zanzibar na kwa nini). Kwa ujumla, Mwalimu Nyerere "alificha" mengi nyuma ya mapinduzi ya Zanzibar na hata "muungano" wenyewe; na siri hizo ndizo zilizokuwa zinamfanya Mwalimu Nyerere kuwa "mkali" na hata kutotamani wananchi wa Tanganyika na Zanzibar kuhoji juu yake! Je, "siri" inaweza kuwa siri hadi mwisho wa "dahari"..tusubiri na tuone kama Tanganyika ya "wadanganyika" na Zanzibar ya "wazanzibara" hawataanika "yaliyofichwa" na kuhifadhiwa na Marehemu Thabit Kombo Jecha na hatimaye kumponza Maalimu Seif Sharif Hamad hadi kufukuzwa CCM na wenzake akina Shaaban Mloo, nk....MUDA UTATUPA MAJIBU!
- Kabla ya mapinduzi, Mv Khaldun (ya Algeria) ilishusha "silaha" Dar es Salaam na iliagwa na Mwalimu Nyerere;
- Mara kadha wa kadha "Field Marshal" John Okello alionekana Ikulu ya Dar es Salaam hata kabla ya mapinduzi na baada yake;
- Hata Okello alipokosana na Karume alirudishwa Dar es Salaam chini ya "escort" ya POLISI na hata baada yake haikujulikana alipelekwa wapi;
- Jina la Tanganyika lilifutwa na nchi ya Tanganyika kuchukua jina la Tanzania Bara huku "Katiba ya Tanganyika" ilifanywa ndio katiba ya muungano;
- Mamlaka ya Zanzibar yaliwekwa chini ya "kivuli" cha Tanganyika na kuendeshwa bila ya katiba wakati wote wa Abeid Karume hadi alipouawa na nafasi yake kuchukuliwa na Aboud Jumbe;
- Tazama Mwalimu Nyerere alivyomlazimisha Aboud Jumbe kujiuzulu urais wa Zanzibar - tafuta sababu za kina (ilikuwaje na kwa nini?);
- Angalia jinsi Mwalimu Nyerere alivyolazimisha kuunganiswa TANU na ASP na kupatikana kwa CCM;
- Tazama Mwalimu alivyokuwa "mkali" pale G55 walivyodai "Hoja ya Tanganyika" na hatimaye kulimaliza kisiasa kundi lile; na
- Angali (kwa makini) muundo wa uongozi wa kisiasa (na kijeshi) unavyopangwa (kwa stratejia) juu ya nafasi ya Zanzaibar kwenye vyombo vya Ulinzi na Usalama.
nurdin Moh'd, je, huyu Mwandishi Harith Ghassany unamfahamu? Jina lake halisi ni nani? Ni mzaliwa wa wapi? Ana umri gani? Hivi sasa anaishi wapi? Ujumbe wake umeelekezwa kwa watu wa aina gani? Duniani kuna watu na watu...wapo watakaodai wamefanya kazi kubwa kumbe maisha yao yote wanahangaika kusukuma ukuta ambao hata hivyo hausogei hata chembe. Hadithi za Alfu Lela Ulela zinasisimua, zinafurahisha na hata kusikitisha lakini mwisho wake ni kama ndoto tu, unapoamka unajikuta pale pale. Akina Harith Ghassany wapo wengi, wanatumbua kwa kuuza vitabu, kwa kuteka nyoyo za wapenzi, kwa kuwaamsha mori wafuasi, lakini mwisho wa siku malengo yao hayafikiwi wala hawafanikiwi, kwa nini lakini? Penye ukweli, uwongo haudumu hata ukipakwa rangi...hapo hamna ujanja!Watanganyika mambo haya hawataki au niseme hawapendi kuyasikia,wao wapo wapo tu wala hawataki kujua tanganyika yao inaelekea wapi.
Samaki utamjua tu hata atiwe kwenye frizer anatoa harufu,,, duh kazi kweli kweliinurdin Moh'd, je, huyu Mwandishi Harith Ghassany unamfahamu? Jina lake halisi ni nani? Ni mzaliwa wa wapi? Ana umri gani? Hivi sasa anaishi wapi? Ujumbe wake umeelekezwa kwa watu wa aina gani? Duniani kuna watu na watu...wapo watakaodai wamefanya kazi kubwa kumbe maisha yao yote wanahangaika kusukuma ukuta ambao hata hivyo hausogei hata chembe. Hadithi za Alfu Lela Ulela zinasisimua, zinafurahisha na hata kusikitisha lakini mwisho wake ni kama ndoto tu, unapoamka unajikuta pale pale. Akina Harith Ghassany wapo wengi, wanatumbua kwa kuuza vitabu, kwa kuteka nyoyo za wapenzi, kwa kuwaamsha mori wafuasi, lakini mwisho wa siku malengo yao hayafikiwi wala hawafanikiwi, kwa nini lakini? Penye ukweli, uwongo haudumu hata ukipakwa rangi...hapo hamna ujanja!
Watanganyika mambo haya hawataki au niseme hawapendi kuyasikia,wao wapo wapo tu wala hawataki kujua tanganyika yao inaelekea wapi.