Mapinduzi ya Zanzibar na Nyerere

Alwaz

JF-Expert Member
Apr 29, 2010
7,055
10,723
Ukisoma kitabu cha KWAHERI UKOLONI KWAHERI UHURU cha mwandishi Harith Ghassany unakaribia kulia ukijua kwamba kumbe Mapinduzi ya Zanzibar si kama tunavyoyajuwa.Kwa upande mwengine kumbe uongo ni kitu kibaya sana kinacholeta maangamizi katika jamii.
Mwandishi anastahiki sifa kubwa ya kuwa mtafiti aliyebobea.Amehojiana na watu muhimu walioshiriki kuipindua serikali ya Zanzibar ambao wengi wala si wenye kusikika.

Ukisoma hiki kitabu ushahidi uko wazi kuwa mapinduzi yale yalikuwa ya chuki za kikabila na kidini na hayakufanywa na wazanzibari wenyewe.Kumbe Nyerere ndiye aliyesuka na kugharimia mapinduzi yale akikitumia chama cha TANU.
Viongozi wa mapinduzi wao wenyewe hawakujua kipi hasa kilikuwa kikiwaongoza kufanya mapinduzi,ni kumuondoa mwarabu mwenye rangi nyeupe na kumuweka mwafrika wa rangi nyeusi au ni kuwaweka watu wa bara waiongoze Zanzibar.Kauli zao na matendo ni vyenye kujichanganya.

Waliokuwa wakitawala Zanzibar walikuwa ni waislamu lakini hawakutekeleza uislamu,hili ni moja ya kosa lao kubwa.Ubwanyenye na ujinga wa kiutawala ulitoa fursa kwa maadui zao kuwapindua kirahisi.Hata hivyo nguvu ya adui aliyekuwa ndani yao na nje wasingekuwa na uwezo wa kuhimili tena.
Katika mkanganyiko huu walioathirika zaidi bila kosa ni wazanzibari waliotafsiriwa na viongozi wa mapinduzi kwamba wana asili ya kiarabu,wengi wao wakiwa wala hawako kwenye utawala.

Nyerere alipata kusema kuwa udini na ubaguzi ni kama ukoma lakini kwa hakika alitumia ukabila na ubaguzi kujenga udini.
Nyerere kwa Afrika anaweza kuitwa baba wa Mapinduzi.Yeye aliweza kuongoza Mapinduzi ya Zanzibar,akawapinduwa waislamu ndani ya TANU na hupati taabu kuona kwamba yeye alishiriki kumuua Karume kupitia kamanda wake Ali Mahfudh.Nyerere alikuwa na damu ya kimapinduzi tu lakini si kwamba mapinduzi aliyoyafanya yalikuwa yana umuhimu.
Kwa wakristo Nyerere anaweza kuonekana ni shujaa lakini kwa waislamu ni mtu mbaya mno.
 
Kwa wale waliosoma hicho kitabu naomba tujadili kwa faida ya wale ambao hawajakisoma.
 
Harith Ghassany ni nani na hiki kitabu 'KWA HERI OKOLONI, KWA HERI UHURU' KINAPATIKANA WAPI?
 
Waislamu huwa hawana jema toka kwa Mkristo hata siku moja, hata kama ukiwalamba nyuma watakudharau tu! Huwezi ukawasikia wanamlalamikia Dikteta Iddi Amin Dada wa Uganda pamoja na maovu yake yote simply kwa sababu alikuwa mwislamu! Similrly kwa magaidi kama akina Osama bin Laden, pamoja na unyama wote wanaofanya, kwao ni mashujaa! Hata hivyo si ajabu kwa sababu asili ya chuki waliyo nayo iko moja kwa moja ndani ya Quran (death manual)!
 
Hata huyo aliyesoma kitabu hicho unaona mawazo yake yanajichanganya. Hivyo siamini kuwa kitabu hicho kinaweza kutoa mwanga mpya kuhusu mapinduzi ya Zanzibar, labda kwa mtu kama yeye ambaye anaonekana alikuwa hajafuatilia haswa namna yalivyotokea mapinduzi yale.
 
Buchanan

Hiki kitabu kinazungumzia mapinduzi yaliyotokea nchini mwetu nafikiri ni bora kukijadili kama kilivyo na kupinga yale ya uzushi yaliyoainishwa humo ndani ili kuhakikisha hakuna kudanganyana.
 
Kwa wale waliosoma hicho kitabu naomba tujadili kwa faida ya wale ambao hawajakisoma.

Hakuna faida humo, ni chuki tu! Mapinduzi yalifanywa kwa uongozi wa John Okello toka Uganda, wala Nyerere wa watu hakutia mkono! Hawakuthubutu kusema hayo akiwa hai, baada ya mzee wa watu kufariki ndio wanachonga. Pamoja na hayo sasa hivi si hayupo? Au wanaogopa kivuli chake?
 
waheri Ukoloni, Kwaheri Uhuru!
Harith Ghassany
info@kwaherikwaheri.com
SOMA HAPA KWANZA
Usambazaji wa kitabu hichi kwa mfumo wa Free Electronic Downloading unafanyika chini ya mkataba wa Creative Commons Attribution-NonCommercial-ShareAlike 3.0 ambao uko chini ya Sharia za nchi ya Marekani.
Kwa mujibu wa Mkataba na Sharia hii, mtu anayekichukuwa kitabu hichi kupitia mfumo huu ana uhuru pia wa kukigawa, kukirudufu na kukisambaza chini ya masharti yafuatayo:
Kulitaja jina la mwandishi wa kitabu kwa njia isiyohalalisha matumizi • binafsi ya kitabu
Kutokitumia kwa makusudi ya kibiashara wakati kinauzwa katika mfumo • wa kitabu
Kutokubadilisha, kugeuza, au kuongeza chochote kwenye kitabu hichi•
Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: Creative Commons — Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States
Kitabu hichi kinatolewa bure katika mfumo huu ili msomaji anufaike na baadaye naye akipendekeze kwa mwenzake ili hatimaye ujumbe wa kusimamisha amani uliomo kitabuni uwafikie walio wengi.
Hata hivyo, mwandishi wa kitabu hiki anafahamu kwamba raha hasa ya kitabu ni kuwamo mikononi mwa msomaji, maana kitabu ni miongoni mwa vitu adhimu na vikongwe kabisa katika urathi wa mwanaadamu.
Kwa hivyo, licha ya kutolewa fursa hii ya mfumo wa kukisoma bure kitabu hichi kupitia kwenye mtandao, ni matarajio ya mwandishi kuwa wako watakaopendelea wawe nacho mikononi na kukisoma kwa nafasi zao.
Kwa vile walengwa wa mfumo huu wa Free Electronic Downloading ni Wazanzibari na Watanganyika wa kawaida, basi ipo haja kwa wale wenye uwezo, wakiwa ndani ama nje ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kutoa mchango wa kuvinunua vitabu ama kupitia mtandao wa kitabu, Goodbye Colonialism, Goodbye Freedom! Zanzibar and the Afrabia Revolution, au moja kwa moja kutoka Self Publishing and Book Printing Solutions - Books, EBooks, Photo books and Calendars at Lulu.com na kuwafikishia walimu na wanafunzi walioko kwenye skuli na vyuo vya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Skuli, vyuo, maktaba, taasisi na watu binafsi wanaweza kumuandikia moja kwa moja mwandishi kupitia mtandao wa kitabu Goodbye Colonialism, Goodbye Freedom! Zanzibar and the Afrabia Revolution ikiwa watahitaji kupata msaada wa wafadhili watakaojitokeza kusaidia. Wafadhili ambao hawatopenda majina yao kujulikana, wamuarifu mwandishi. Majina yao yatahifadhiwa na mwandishi anatanguliza shukrani za dhati kwa ukarimu wao.
Mwandishi pia anatanguliza ombi na shukrani maalum kwa watakaoweza kusaidia kuviwezesha vituo vya mitandao vilivyopo Tanzania Zanzibar na Tanzania Bara kutoa muda maalum wa huduma za mtandao kwa bei nafuu kwa ajili ya wale watakaopenda kukisoma, kukichukua na ama kukihifadhi kitabu hiki kwenye vyombo vyao.
Kuanzia hivi sasa, Kwaheri Ukoloni, Kwaheri Uhuru! kimo machoni mwako. Fungua kurasa zake, zama na zamia kwenye bahari yake na ibuka na lulu zilizomo ndani yake.
Mnakaribishwa nyote-walio karibu na walioko mbali.
 
Utangulizi
Kutoka nusu ya pili ya karne ya ishirini mpaka kuingiya karne ya ishirini na moja, Zanzibar imekuwa ikisifika kwa mambo matatu yenye umuhimu mkubwa wa kijamii na wa kisiasa: kupatikana kwa uhuru wa Zanzibar tarehe 10 Disemba 1963, kupinduliwa dola huru ya Zanzibar tarehe 12 Januari 1964, na kuungana na Tanganyika tarehe 26 Aprili 1964.
Kitabu hichi kinasajili majadiliyano ambayo hayajapata kutolewa, kwa njia rasmi au zisizokuwa rasmi, na kikundi maalumu cha wazee waliyokuwa wanachama wa Afro-Shirazi Party (ASP) na wa Tanganyika African National Union (TANU) katika kuyafanikisha yale yenye kujulikana rasmi kama ni Mapinduzi ya Zanzibar ya tarehe 12 Januari 1964. Kitabu piya kinatumiya marejeo ya daraja la kwanza ya kihistoria ambayo ni maandishi ya nyaraka za kitaifa za maofisa waliyoyashuhudiya mapinduzi au waliokuwa karibu sana na waliyoyashuhudiya. Kushuhudiya jambo kuna daraja.
Mchango wa wazee khasa waliyohusika na waliyokuwa mstari wa mbele kwenye Mapinduzi kunaziba pengo kubwa la kihistoria na ni dira na ramani mpya kwa wananchi wa Zanzibar na wa Tanganyika, kwa Wazanzibari waliyoko ughaibuni, na kwa wenye kufuatiliya masuala ya umoja na muungano wa nchi za Kiafrika. Piya ni mchango muhimu baina ya uhusiyano wa Waafrika na Waarabu ambao mwaka 1990 Profesa Ali A. Mazrui aliubatiza jina la Afrabia akimaanisha uhusiyano mkongwe na maalumu baina ya Waafrika na Waarabu na kubashiriya makundi mawili ambayo yamo katika safari ya mfungamano wa kuwa kitu kimoja.6
Zanzibar na Tanganyika, Tanzania, ziko kwenye njiya panda kuelekeya kunako mfungamano na zimekabiliwa na uamuzi mkubwa na wa haraka wa ya imma kuifuwata njiya ya amani na neema au kuifuata njiya ya ghadhabu na yenye kupoteza dira.
Usomaji wa maneno, udadisi wa maana, na uwelekezaji wake kwenye daraja za juu za ufahamu ndizo pekee zenye uwezo wa kutowa makusudiyo na maana ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa Zanzibar, kwa Tanganyika, na kwa mustakbal wa
Utangulizi
xix
Zanzibar na Tanganyika-Muungano.
Tatizo la Zanzibar, Unguja na Pemba, au la Waafrika Waislam, ni tatizo ambalo lina picha ndogo na picha kubwa. Picha kubwa ni ustaarabu na khasa wa Dola ya Zanzibar ambao ni tishio kwa wale ambao bila ya kutambuwa wamefundishwa na kuamini kuwa wao wana haki zaidi Zanzibar kuliko hata Wazanzibari ambao hawana kwao kwengine isipokuwa Zanzibar.
Na kwanini tatizo likawa na Zanzibar, na si na Tanga, au Mafia, au Kilwa, au Lamu, lakini likawa na Zanzibar na Mwambao wa Kenya? Sababu ni Dola ya Zanzibar ndiyo dola pekee iliyo kongwe (mbali na Ethiopia) kuliko zote Afrika chini ya jangwa la Sahara ambayo iliupata uhuru wake tarehe 10 Disemba 1963. Kuukataa uhuru wa Zanzibar kutoka kwa Muingereza ni kukataa kuwepo kwa Dola ya Zanzibar na ustaarabu wa Waafrika Waislam wa karne juu ya karne. Na ni kuyakataa piya Mapinduzi ya 1964. Mapinduzi yangelikuja kama si uhuru wa Zanzibar wa tarehe 10 Disemba 1963?
Jan P van Bergen wa Uholanzi ameelezeya kwa ufasaha kuwa "Kutokeya ulipoanza, Ukristo umekuwepo kwenye bara la Afrika, Masri, Libya, na Afrika ya Kaskazini, na labda Ethiopia. Lakini hakuna kumbukumbu yoyote katika Zama za Giza (Dark Ages) ya kuingiya kwa Ukristo sehemu za kusini, si kwa kupitiya njiya ya baharini au ya barani. Kuingiya kwa Ukristo Tanzania ni jambo la miaka ya karibuni."7
Ukifananisha na Afrika Magharibi, kufaulu kwa uenezaji wa Ukristo Afrika Mashariki kulisababishwa na "uhaba wa nguvu za Uislamu, uhaba wa Dola zenye nguvu na zilizojiandaa kuuzuwiya Ukristo, na rukhsa aliyoitowa Sayyid Said wa Zanzibar kwa mamishionari kuanza kufanya kazi zao, ambazo ni kinyume na imani yake ya Kiislamu, na upeo wa kipropaganda wa Livingstone Uingereza na nchi za Ulaya." 8
Tukirudi nyuma zaidi na katika mwaka kama wa 975, anaelezeya mtafiti Bergen, "wakimbizi wa kidini na wa kisiasa kutokeya Persia na Arabia walianzisha miji midogo katika pwani ya Afrika Mashariki. Miji hiyo baadaye ilikuwa na kuwa miji mikubwa ya kibiashara, na dini kubwa ya ukanda wa pwani ikawa dini ya Kiislam…Kuowana kwa Waarabu, Wafarsi, Washirazi na Waafrika kukazaa kabila la mchanganyiko la Waswahili, na ustaarabu wa Kiafrika wa Kiislam."9
Vipi udugu wa mtiririko wa zaidi ya karne kumi za ustaarabu, mila, na dini moja, utaweza kuvunjwa na miaka isiyozidi khamsini ya fitina zinazotokana na hadithi za kubuni za dhiki na dhuluma za utumwa? Juu ya yote yaliyotokeya na kufanyika ndani ya fitina za miaka michache, Wazanzibari wengi sana wamekuwa wakisononeshwa na kuwaombeya dua watu wa Zanzibar watuliye nafsi zao na Zanzibar ijirejeshee hishma na hadhi yake. Haya ya Zanzibar ni mfano wa yale aliyoyaelezeya msomi Eqbal Ahmad kuhusu mpasuko wa India:
Haiwezekani kukosa njia za kujiepusha na kufarikiyana kwa jamii mbili zinapoishi
Utangulizi
xx
pamoja kwa miaka mia saba. Sifahamu kwa nini uongozi wa India, wa Kiislam na wa Kihindu, pamoja na Gandhi, wakashindwa kuhakikisha uendelezaji wa mtitiriko wa jamii mbili, moja ya Kihindu ya pili ya Kiislam, kuweza kuishi kwa pamoja. Kulikuwa na mivutano katika mahusiano yao kama kunavyokuwepo mivutano kwenye mahusiano yoyote yale. Muhimu zaidi ni makundi mawili haya yameishi kwa kutegemeyana na ndani yake kumezaliwa mambo mengi sana. Ustaarabu mpya umezaliwa. Lugha mpya ya Urdu imechomoza kutokana na mchanganyiko wa nini Waislam wameleta na walichokikuta Bara Hindi…Kutengana kungeliweza kuepukika kama alivyotabiri mshairi na mwandishi mkubwa Rabindranath Tagore ingelikuwa harakati za India zilizo dhidi ya ubeberu zingeliutambuwa umuhimu wa kujitenga na ideolojiya ya uzalendo (nationalism). Tuliupinga ubeberu wa Magharibi lakini katika kufanya hivyo tukaukumbatiya uzalendo wa Magharibi mzima mzima.10
Uongozi wa Zanzibar na wa Tanganyika, pamoja na Mwalimu Nyerere, ungeliweza kuhakikisha uendelezaji wa mtiririko wa makarne ya jamii mbili zilizouzaa ustaarabu wa Waafrika Waislam, lugha ya Kiswahili, na mengi mengineyo. Mtengano ulioletwa kwa makusudi na mapinduzi ya 1964 ulisababishwa na mrengo wa kisiasa wa kizalendo wa Pan-Africanism ambao chimbuko lake limetokana na Waafrika waliyosoma na kulelewa Ulaya. Matatizo pia yaliletwa na khofu ya mrengo wa kizalendo wa Pan-Africanism kuja kutawaliwa na mrengo wa Pan-Arabism ambao ulikuwa ndiyo mrengo wa Masri ya Rais Gamal Abdel Nasser, rafiki wa chama cha Zanzibar Nationalist Party kilichokuwa kikiongozwa na Zaim (kiongozi) Sheikh Ali Muhsin. Ni jambo la kushangaza vipi mirengo ya kizalendo ya viongozi wakubwa wa Afrika, Julius Kambarage Nyerere na Gamal Abdel Nasser imalizikiye na mauwaji ya halaiki na kuguswa na sumu ya fitina za utumwa.
Mara nyingi Zanzibar imejaribu kujipatiya utulivu na haikuweza kufaulu. Haya yalitokeya kabla ya Mapinduzi na yakajaribiwa tena baada ya Mapinduzi na zaidi kwenye Miafaka ya hivi karibuni. Wakati wa Mwenye Enzi Mungu kutaka ulikuwa bado haukufika na pia kwa sababu ya mashindano ya kisiasa baina ya Wazanzibari wenyewe kwa wenyewe yanayotokana na tabia ya kutoaminiyana.
Miaka arubaini na sita yameutiya umoja wa umma wa Kizanzibari wenye dini, mila, na kuingiliyana kwa kuowana, ndani ya mtego wa upotoshaji wa historia ya nchi ya Zanzibar. Kwa mujibu wa Bwana Abdulshakur:
Ukweli ni uvamizi ulikuwa ni tukio tu lakini yaliyofuata mavamizi hayo ulikuwa ni mlolongo maalum uliojengwa kiitikadi katika kumpotosha Mzanzibari na utambulisho (identity) wake. Mipango ya kumgeuza na kumpotosha Mzanzibari [mweusi na mweupe] ilianza kwa bahati tukiwa wadogo maskulini. Mengi yalitupata na mengi tukayashuhudia lakini kama watoto, mengi tuliyaona kwa jicho la kitoto pia.Tukitafakari leo kwa kutizama nyuma tulikotoka tunaweza kuona kuwa yote hiyo ilikuwa ni mipango yenye nia na madhumuni maalumu.11
Utangulizi xxi
Lililotoswa na kuzoweleka ndani ya akili za wengi ni kuwa mapinduzi ya Zanzibar yalikuja kuondowa dhiki na dhuluma za kikundi cha mabwanyenye wa Kiarabu wachache dhidi ya Waafrika walalahoi waliyo wengi. Kitabu hichi kinahoji kwa ushahidi kuwa mapinduzi ya Zanzibar yalikuwa na lengo la kuubomowa uhusiano mkongwe baina ya Waafrika na Waarabu na kuuweka uhusiano huo chini ya udhibiti wa nguvu za kiutawala za Tanganyika.
Kama alivyosema Eqbal Ahmad, hakuna uhusiano usiokuwa na matatizo yake na uhusiano wa zaidi ya miaka elfu mbili baina ya Waafrika na Waarabu uliyozaa ustaarabu, lugha, na dini ya Kiislam ilyozikaribisha na kuzihishimu dini nyengine Zanzibar, ushindwe kuundeleza mtiririko wa jamii hizo mbili kuweza kuishi kwa udugu na ujirani mwema.
Kwa mujibu wa mchoraji maarufu na bingwa wa lugha ya Kiswahili na habari za Waswahili, Profesa Ibrahim Noor Shariff:
Hakuna mgongano wowote wa mtu kuwa Mwarabu na wakati huohuo akawa Mwafrika kama vile hakuna mgongano wowote wa mtu kuwa Mbantu au Mmasai akawa pia ni Mwafrika.12
Wakati akizungumziya mapinduzi ya Zanzibar, Profesa Ali A. Mazrui aliandika:
Kwa maana ya uzalendo wa Kizanzibari, Jamshid bin Abdalla na Ali Muhsin walikuwa Wazanzibari zaidi kuliko John Okello lakini kwa maana ya uzalendo wa Kiafrika, John Okello alikuwa Muafrika zaidi kuliko Jamshid bin Abdalla na Ali Muhsin.13
Jambo lilokuwapo wakati ule wa nyuma ni kuwa Zanzibar si nchi ya Kiafrika kwa sababu ilikuwa na utawala wa Kisultani ambao ni wa asili ya Kiarabu na wa Kiislam. Na si hivyo tu ulikuwa utawala uliotanguliwa na tawala nyengine kongwe za Kiislam katika Pwani ya Afrika Mashariki na ushawishi mkubwa ndani ya bara la Afrika Mashariki na Kati ambazo pia zilikuwa zina asili ya mchanganyiko wa Kiarabu na wa Kiafrika. Hilo halikuwa jambo geni kwa Afrika Mashariki na Kati ziliyoko chini ya Jangwa la Sahara. Tatizo lilikuja pale wakoloni wa Kizungu walipoona wazi kuwa kuna mahusiyano mazuri na makubwa baina ya Zanzibar yenye ushawishi Afrika Mashariki na Kati na nchi za Kiarabu za Kaskazini ya Afrika ambazo zilikuwa dhidi ya Wakoloni wa Kizungu.
Inafaa ikakumbukwa kuwa "nchi kumi (10) za Kiarabu ziko ndani ya bara la Afrika, na thuluthi moja ya umma wa Kiarabu inaishi Afrika, na aslimia 72% ya ardhi za nchi za Kiarabu ziko Afrika na kuwa dini ya Kiislam ni dini iliyotapakaa katika bara la Afrika kuliko dini yoyote nyengine."14
Wapenzi wa matumizi ya neno "Muafrika" katika Afrika Mashariki hawana
xxii Utangulizi
budi kuuzingatiya ushahidi wa kihistoria au ushahidi wa viini vya DNA vya miaka ya hivi karibuni wenye kuthibitisha kuwa Waafrika Wakristo na Waislam walikuwa kitu kimoja kwenye kuupendeleya mrengo wa uzalendo wa Kiafrika uliyotokana na Waafrika ambao waliishi nchi za Ulaya wakati Afrika ilipokuwa ikitawaliwa na Wakoloni wa Kizungu. Na hata baadhi ya Waarabu pia walitumbukiya ndani ya mrengo huo.
Lakini haina maana kuwa hisiya za kidini zilikuwa hazipo. Ukristo ambao ulikuwa ndiyo dini ya Wakoloni wa Kizungu ulikuja kufananishwa na sifa zote za Muafrika Mkristo aliyeonewa na aliyekosewa na dhuluma za kihistoria, na Waarabu Waislam wakapewa sifa zote mbovu kuwa wao ndiwo waliyoleta uovu wa biashara ya utumwa Afrika. Uchafu wote ukapelekwa Bagamoyo kwenye Uislam na usafi wote ukapelekwa Arusha kwenye Ukristo. Tanganyika ikageuzwa kuwa ndiyo msalaba wa kuisulubu Dola ya Zanzibar bila ya kujali hali ya mchanganyiko wa kidamu baina ya watu wa pande hizo mbili.
Yaleti siku ifike Katiba ya Zanzibar na ya Tanganyika zikapinga kwa maneno na kwa vitendo ubaguzi wa binaadamu yoyote yule kwa misingi ya kikabila, asili, au dini na kuwalinda na kuwapa zawadi watu binafsi au taasisi zitakazowaanika na kuwawajibisha bila ya kuwaoneya haya mafisadi wa kiasili, kidini na wa kiuchumi. Yasije yakawa yale ya Tom Mboya alipomuambiya Sheikh Abdillahi Nasser wa Kenya "rudi kwenu Oman!" na Sheikh Abdillahi akamjibu Mboya "na wewe rudi kwenu Sudan!" Mboya akajibu "angalau Sudan iko Afrika!" na Sheikh Abdillahi akamjibu "hata hivyo. Sudan bado ni memba wa Arab League! (Jumuiya ya Waarabu)." 15
Suala la ubaguzi Afrika limedharauliwa sana kutokana na imani kuwa mtu mweusi hawezi kuwa mbaguzi au kaburu kwa sababu ya historia ndefu ya kubaguliwa, kuuzwa, na kutumbikizwa ndani ya ukoloni. Chembelecho Mwalimu Nyerere, mbaguzi ni mbaguzi tu hata akiwa ni Muafrika mweusi.16 Muhimu binaadamu kujitambuwa na kushikiliya kutambuliwa kuwa ni binaadamu bila ya kuwaoneya haya wabaguzi wa Kiafrika kwa sababu ni weusi.
Nadhariya ya Kitunguu na Mlango Uliyofungwa
Nilifanya mahojiano mengi na kuzisajili sauti za wazee wa Mapinduzi ya Zanzibar lakini baadaye nikaamuwa nisizitumiye kwenye kitabu hichi kwa sababu niligunduwa kuwa nimekamata ganda kavu la kitunguu lililo karibu na nje. Nadhariya ya kitunguu imenisaidiya kufahamu kuwa kitunguu cha mapinduzi ya Zanzibar kina tabaka maalumu na chache mno. Mikono ya Mapinduzi huenda ikawa mingi lakini vichwa vya mapinduzi ni vichache sana. Hilo ni jambo la kawaida. Hakuna nafasi ya watu wengi kwenye jambo la siri kama la kupanga mapinduzi.
Utangulizi xxiii
Mapinduzi ya Zanzibar yana tabaka au vikundi tafauti vya kijamii na vya kisiasa ndani ya Zanzibar, Tanganyika, na nje ya Zanzibar na Tanganyika. Kuna maelezo ya dhahiri kukhusu Mapinduzi na piya yaliyojificha juu ya tukiyo hilo hilo. Maelezo ya dhahiri ni kuyaweka Mapinduzi ya Zanzibar ndani ya mabano ya visiwa na kutamka kuwa hakukuwa na mkono wa nje kwenye kuyafanikisha mapinduzi hayo. Maelezo yaliyojificha ambayo ni muhimu zaidi kwa mustakbal wa Zanzibar yanakubali kuwa Mapinduzi ya Zanzibar yalikuwa na wenyewe, na wenyewe hao walikuwa vichwa vya juu vya Mapinduzi na hawakuwa wanakindakindaki wa Kizanzibari. Wazanzibari wenyeji ambao hawakushirikiyana na vichwa vya mapinduzi kutoka nje hawakuaminiwa kupewa siri ya mipango ya mapinduzi na siri hiyo haikuwa kuingiya Bomani, au Ziwani kwenye vituo vya polisi na silaha.
Majiko ya Mapinduzi yalikuwa machache lakini nguvu zake ambazo ndizo zilokuja kuamuwa wapi Zanzibar ielekee hazikuwa nguvu za Wazanzibari wenyeji. Kwa vile majiko yalikuja kupinduwana msomaji anatakiwa awe makini kuelewa wapi kuna migongano ya maelezo na wapi kuna migongano ya majiko. Jiko asiliya la ndani la Mapinduzi ya Zanzibar lilipinduliwa siku tatu tu baada ya Mapinduzi kutokeya baada ya mikono ya mapinduzi ambayo kisiasa ilikuwa ikicheza mchezo baina ya jiko asiliya la Mapinduzi na baadaye kumkabidhi uongozi Mzee Karume.
Kitabu pia kinahoji kuwa hakukuwa na Kamati ya Watu 14 kabla ya tarehe 12 Januari 1964 iliyokaa kitako peke yao na Mzee Karume kupanga mipango ya Mapinduzi ya Zanzibar. Kamati hiyo iliundwa na kupewa jina hilo baada ya kupinduliwa jiko la kwanza la akina marehemu Abdalla Kassim Hanga, Saleh Saadalla Akida, na Abdulaziz Twala. Waliyojiita baadaye kuwa ni Kamati ya Watu 14 walikuwa ni vijana wa Afro-Shirazi Party Youth League (ASPYL) ambao wakichukuwa miongozo yao kutoka kwa akina Saleh Saadalla. Lakini kwa sababu Hanga, Saadalla, na Twala walikuwa ni viongozi wasomi na wakiupinga uongozi wa Mzee Karume, vijana wa ASPYL ambao takriban wote hawakusoma walikuwa karibu zaidi na Mzee Karume. Mapinduzi yalipofaulu vijana wakamkabidhi uongozi Mzee Karume siku chache tu baada ya mapinduzi ya akina Hanga kufanikiwa.
Kuna sababu tafauti zilizowafanya wazee waamue kusimuliya kwa undani simulizi za Mapinduzi ya Zanzibar. Kuna waliyotaka kuisajili historia inayopoteya. Kuna waliyotanabahi kuwa Mapinduzi hayakuwaleteya faida walizo-kuwa
wakizitarajiya. Wapo wenye hisia kuwa wakati umefika wa kubadilisha serikali kwa njia ya kura za wananchi badala ya kutumiya mtutu wa bunduki. Kuna wanaohisi wamedhulumiwa na wametupwa wao na kizazi chao baada ya kazi kubwa waliyoifanya katika Mapinduzi. Ni dalili ya msemo maarufu wa Mwalimu Nyerere kuwa upinzani [mabadiliko] khasa Tanzania yatatoka ndani
ya chama hichihichi na uongozi huuhuu wa CCM na si nje yake kwa sababu
xxiv Utangulizi
hakuna njiya ya kuyafahamu Mapinduzi na Muungano nje ya ASP, TANU na CCM.
Na piya katika wazee wapo ambao wanataka kuiona Zanzibar na Tanganyika zinazoheshimu historia itakayomtowa binaadamu kutoka jela ya yaliopita na yasiyojulikana, na kuelekeya kunako Zanzibar na Tanganyika zenye mapenzi, umoja, na neema za maisha mazuri kwa kila mwananchi. Zaidi ya yote ni kugubikwa na kusahaulika kwa kumbukumbu za Mapinduzi ambazo kukosekana kwake kwa nusu karne kumezipotezeya Zanzibar na Tanganyika nafasi za kujikwamuwa.
Mfumo wa Kitabu
Muundo wa kitabu hichi ni wa simulizi kuhusu Mapinduzi ya Zanzibar ya 1964. Asilimiya kubwa sana ya kitabu ni simulizi za wazee waliyoshiriki au walioyashuhudiya Mapinduzi kwa undani wake. Kiwakati asilimiya kubwa ya mahojiano ya simulizi ziliyomo ndani ya kitabu yalifanyika kuanziya katikati ya mwaka 2004 na mwisho wa mwaka 2009.
Usajili wa mahojiyano ya muda mrefu ya awali ambayo hayamo ndani ya kitabu yalikuwa na akina marehemu Ali Omar (Lumumba), Othman "Bapa", na wenginewo ambao hawakutaka majina yao kutajwa. Kutokana na nadhariya ya kitunguu nilikuja kuamuwa kuwa mahojiyano ya baada ya mwaka 2004 na kuendeleya yalikuwa yana umuhimu mkubwa zaidi katika kuisajili na kuiweka sawa historia ya mapinduzi ya Zanzibar kuliko ya kabla yake.
Ni vigumu kuyatoleya tarehe mahojiano niliyoyafanya ndani ya nyakati tafauti na ambayo nimeyapanga chini ya mtiririko wa maudhui na milango tafauti. Na kwa vile baadhi ya wazungumzaji hujitokeza kwenye mlango zaidi ya mmoja nimeona hakuna haja ya kumjuulisha tena msomaji ni nani anayezungumza endapo wasifu wake ulikwisha kutolewa huko nyuma. Kuna sehemu chache sana ambazo mahojiyano yalifanywa na zaidi ya mtu mmoja ndani ya wakati mmoja.
Kwa kifupi kitabu kinaanza na maelezo na simulizi ya vipi ndoto ya uhuru wa Zanzibar ilivyozimwa kwa siri nzito ya Mapinduzi na kinamalizikiya na tafsiri ya nyumba ya Afrabia ambayo inatowa picha ya mustakbal mwema wa Zanzibar na wa Tanganyika. Huenda msomaji kutoka Zanzibar, Tanganyika, na kokote kule duniani, aliyekuwa akisononeshwa na suala la Zanzibar akaweza kuuona mwangaza nje ya pango la upotoshaji wa historia. Msomaji wa aina hiyo ni sawa na yule mama aliyotoka ndani ya pango lenye giza huku amebeba ndoo ya maji ya hikma juu ya kichwa chake. Hapana shaka uamuzi wa mwisho na muhimu utakuwa ni wako msomaji.
Kitabu hichi kina mfumo wa binaadamu mwenye hamu na kiu ya kuisaidiya Zanzibar, ikiwa yuko ndani au nje ya Zanzibar, lakini hawezi kufanya hivyo bila ya kwanza kuandaliwa mazingira ya kikatiba na ya kimaisha ambayo yatamvutiya
Utangulizi xxv
kuweza kufanya hivyo. Hichi si kitabu cha siasa ingawa kwa mtizamo wa kijuujuu kinaweza kuonekana kuwa ni kitabu cha kisiasa na cha wanasiasa. Ni kitabu cha wenye dira na ushujaa wa kumchaguwa kiongozi na uongozi ambao utakuwa na sifa na uwezo wa kuituliza Zanzibar na Tanganyika kwa kuufuta upotoshaji wa fitina ya historia ambayo ndiyo mzizi wa shari ya chini kwa chini ndani ya muungano. Muhimu zipatikane nguvu kazi za Wazanzibari na Watanganyika waliyozagaa duniani ili wasaidiye kuutekeleza mkakati wa kuuinuwa uchumi wa Zanzibar na Tanganyika na kuziweka nchi zao kwenye daraja bora zaidi.
Baina ya milango mitatu ya mwanzo na mitatu ya mwisho, katikati kuna milango kumi na tano iliyokusanya simulizi za wazee kuhusu mapinduzi ya Zanzibar. Asilimia kubwa sana ya simulizi hizo zinatoka kwa wazee waliyopinduwa na simulizi mbili kutoka kwa marehemu Sheikh Ali Muhsin juu ya Mapinduzi ya 1964 na Shirikisho la Afrika Mashariki.
Kivitendo, mchango wangu katika kazi hii ni kuandaa minhaji ya utafiti (methodology); kuwasaka na kuwapata wazee; kuisajili na kuiweka sawa historia ya Mapinduzi na kuwakumbusha wazee dhamana zao za kukisaidiya kizazi kipya kufahamu na kuyaondowa matatizo ya Zanzibar, baina ya Zanzibar na Tanganyika na baina ya Waafrika na Waarabu; kuandaa masuala yaliyomuongoza mtafiti ndani ya midani ya utafiti na nyaraka za kitaifa; kukaa na wazee kwa muda mrefu; kuwafanyiya mahojiyano na kuyasajili katika vilimbo vya kunasiya sauti; kuyaandaa majadiliyano katika milango na kwa lugha ya Kiswahili ambayo ndiyo iliyotumiwa na wazee wengi; kuwapiga picha baadhi ya wazee kwa rukhsa yao na kuzipiga picha sehemu muhimu za midani ya utafiti; pamoja na uchapishaji wa kitabu hichi.
Niliweza kuwachaguwa wazee niliyowahoji kwa kuzifuatiliya dalili tafauti kutoka midani ya utafiti na nyaraka za kitaifa za Kiingereza na za Kimarekani na muhimu zaidi kutoka kwa wazee wenyewe kunijuulisha na wanamapinduzi wenzao. Msomaji ataweza kuwatambuwa baadhi ya wazee wanaozungumza na wanaozungumzwa baina ya maelezo yao ya ndani ya kitabu. Kuna baadhi ya wazee nimewagubika wasijulikane kwa sababu hawakutaka kujulikana kwa hivi sasa. Wako wazee muhimu ambao wanayajuwa mengi zaidi kuliko yaliyomo ndani ya kitabu lakini sikuwafuatiliya kwa sababu nilifahamu kuwa walikuwa na uzito wa kuzungumza kwa sababu wanazozijuwa wao wenyewe.
Masuala ya Kujiuliza
Wazee wengi wenye kusimuliya simulizi za Mapinduzi ya Zanzibar ni wazee ambao wamebobea kwenye historia ya Mapinduzi. Ni wazee waliyokaa kitako mara nyingi na kukongeshwa kwenye viti vyao kwa fikra na mawazo ya muda mrefu ambayo hawajawahi kuwakabidhi watoto na wajukuu zao.
Kitabu kinauliza masuala matatu ya msingi. Jawabu za masuala hayo zilimezwa
xxvi Utangulizi
na nyangumi aliyeamuwa kuzamiya au aliyezamishwa kwa makusudi kwenye bahari ya historia kwa zaidi ya miaka 46. Masuala ambayo msomaji wa kitabu hichi anafaa kuyazingatiya kwa umakini mkubwa ni haya yafuatayo:
1) Ufunuo wa Mapinduzi ya Zanzibar ndani ya kipindi cha maridhiyano baina ya Wazanzibari utaweza kuisaidiya Tanganyika kuisitisha mivutano iliyojitokeza kwa kuukaribisha mfungamano ndani ya Zanzibar ambayo ni sehemu ya pili ya Muungano wa Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar?
2) Umoja wa maridhiyano baina ya Wazanzibari wenyewe kwa wenyewe, baina ya Wazanzibari na Watanganyika, na baina ya Waafrika Weusi na Waarabu Waafrika, utakuwa na faida gani kubwa za kisiasa na za kiuchumi kwa wananchi walio wengi wa Afrika Mashariki na Kati?
3) Madola makubwa ya Magharibi yalishiriki katika upangaji na utekelezaji wa Mapinduzi au waliyasaidiya kwa kuzidharau kwa makusudi taarifa za kiusalama walizokuwa nazo kwa sababu Mapinduzi na Muungano ilikuwa ni mihimili miwili yenye maslahi na wao zaidi kuliko maslahi ya Wazanzibari, ya Wazanzibari na Watanganyika, na ya Waafrika na Waarabu?
Yapo masuala mengi yaliyo muhimu ambayo hayakupewa haki yake na kitabu hichi. Kwa mfano, nini chanzo cha fedha zilizotumika kuyagharimiya Mapinduzi ya Zanzibar? Inatosha kumnukuu Bwana Godfrey Mwakikagile ambaye kwenye kitabu chake Nyerere and Africa: End of an Era anakiri kuwa katika mada alizozungumza kwa lugha ya Kiswahili na Kiingereza na mtoto mkubwa wa Mwalimu Nyerere, Andrew Nyerere, moja wapo ni "viongozi kama Mfalme Haile Selassie, Dk. Kwame Nkrumah waliyagharimiya kifedha Mapinduzi ya Zanzibar."17
Ufuatiliyaji wa chanzo cha fedha zilizotumika katika kuyagharimiya mapinduzi ya Zanzibar unahitajiya kufanyika ikiwa chanzo chenyewe ni serikali ya Tanganyika, au Kamati ya Ukombozi ya Umoja wa Nchi Huru za Kiafrika (OAU) au vyanzo vyenginevyo. Iko haja ya kujiuliza kama kuna ushahidi wowote Msalaba Mwekundu kuwaondosha Waarabu ilikuwa kwa ajili ya kuyasaidiya Mapinduzi au la.
Kwa mujibu wa Frieder Ludwig, mwandishi wa kitabu Church & State in Tanzania: Aspects of a Changing Relationship, 1961–1994 "Mapinduzi ya Zanzibar yalipokelewa vizuri na Wakristo waliyokuwa wakiishi Zanzibar." Ludwig amemnakili Mmishionari mmoja aliyemnakili mama mmoja mtu mzima akisema "Nilishindwa kujizuwiya kukumbuka vipi Bwana wetu alisema ‘Nimeyaona mateso ya watu wangu-na nikampeleka Musa kuwakombowa'-na sasa amemleta John Okello kutukombowa…Si Kamishna wa Polisi [Edington Kisasi] peke yake, bali
Utangulizi xxvii
Makamishna wa Gereza na Kazi ni wanachama wenye bidii katika kikundi cha dini yetu".18 Suala la kujiuliza, ni jee, Kanisa lilimuunga mkono Mwalimu Nyerere katika kuipinduwa Zanzibar? Misikiti pia ilishiriki? Na viongozi wa Kiislamu wa TANU walikuwa na mchango gani katika kuipinduwa Zanzibar?19 Wazee wengi waliyohojiwa na mwandishi wa kitabu hichi ni Waislam, ingawa uongozi mkubwa ulikuwa kwa mwenyewe Nyerere na madola makubwa yaliyomuunga mkono. Lakini hata akina Oscar Kambona pia walikuja kuangushwa na Mwalimu Nyerere ingawa alikuwa Mkristo Muanglikani.
Kuna masuala ya msingi kuhusu mchango wa Mzee Abeid Amani Karume katika Mapinduzi ya 1964 na Muungano ambayo ni muhimu sana kuwekwa sawa kwa faida ya historia na zaidi kwa faida ya Zanzibar. Kwa mfano msomi maarufu Tanzania, Profesa Issa G. Shivji ameandika juu ya mahusiyano ya Mzee Karume na Muungano:
Maelezo rasmi yanarudia ….kuwa Karume alikuwa ni mwenye shauku kubwa juu ya Muungano. Hivyo ni mbali na ukweli ulivyo. Kama kuna kitu ambacho Wazanzibari wanamtukuza Karume nacho, mbali ya utawala wake wa kidikteta, ni Uzanzibari wake na upinzani usiyotetereka wa kukataa kuingizwa ndani ya Muungano na kuipoteza haki ya Zanzibar ya kujiamuliya mambo yake wenyewe. Kwa mfano, Smith, ambaye alikuwa hana kizuizi cha kumfikiya Nyerere na maofisa wengine wakati wa utafiti wake, anataja kuwa tishiyo la Nyerere la kuwaondowa askari wa polisi wa Tanganyika visiwani ndiyo lililomfanya Karume aukubali Muungano. Lakini alikuwa anasitasita mpaka dakika ya mwisho.20
Au angaliya namna R. K. Mwanjisi, ambaye aliwahi kuwa Seketeri wa Bunge, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Tanganyika, kwenye kitabu chake kiitwacho Abeid Amani Karume anavyoelezeya matukio ya "Siri za Mapinduzi". Kati ya nukta 46 za matukio ya Mapinduzi, Mwanjisi anaelezeya kunako nukta ya kwanza kuwa "Mwishoni mwa mwaka mwaka 1963 au mwanzoni mwa mwaka 1964 iliundwa ‘Kamati ya Mapinduzi ya watu 14'. Nukta 14 inaelezeya kwa ‘Sultani akaelea baharini siku nzima ya tarehe 12 na kesho yake. Meli yake ikakataliwa kutua Mombasa. Ndipo iliporuhusiwa kuingia Dar es Salaam na Serikali ya Tanganyika baada ya kuombwa na Mwingereza.' Nukta ya 15 inasema: ‘Tarehe 12 Mwalimu Nyerere na Bwana Kambona waambiwa mambo yaliyotokea Unguja [Zanzibar].' "21
Kwa hiyo Mwalimu Nyerere na Oscar Kambona hawakujuwa kitu kuhusu Mapinduzi ya Zanzibar mpaka pale yalipotokeya. Ina maana walikuwa hawana taarifa yoyote kabla ya siku hiyo. Piya hakuna popote pale ambapo Mwanjisi anaelezeya na kwa ushahidi kuwa Mzee Karume alihusika na upangaji wa Mapinduzi ya 1964. Maelezo rasmi juu ya wahusika wakuu wa Mapinduzi ni Kamati ya Watu 14 ambayo ni ya viongozi ambao hawaonekani kuwa walikuwa na kiongozi.
xxviii Utangulizi
Jambo moja muhimu ambalo Mwanjisi aliligusiya ni pale alipoandika:
Madola ya Magharibi yanaamini kwamba ati Mapinduzi ya Unguja na Pemba yameendeshwa na Wakomunisti, hii ni dharau ile ile ya kusema kuwa Mwafrika hawezi kutenda kitu cho chote chenye maana! Pia ni kuwapa Wakoministi sifa wasiyostahili kupata.22
Wakati umefika wa kukaa na kujiuliza masuali mazito ya nafsi zetu na wapi tunataka kwenda. Hukumu ni ya wasomaji wenye kuyapima mambo kwa kutumiya vipaji vyao na uhuru wao wa kufikiri bila ya kupendeleya hata kama ukweli utakuwa unawagusa wale ambao wanawapenda. Bado kuna kuingiya ndani ya nyumba, vyumba na vipembe. Mwenzangu una akili na moyo wako mwenyewe. Jiulize mwenyewe. Jijibu mwenyewe. Wazee wameshatusaidiya mpaka hapa. Sasa tujisaidiye wenyewe palipobakiya kwa kujihami kidini, kihaki, kiakili, kukilinda kizazi kipya na kuilinda Zanzibar na Tanganyika (Tanzania) pamoja na kuutengeneza upya uhusiano mkongwe baina ya Waafrika na Waarabu kwa kuwaleteya maisha mazuri zaidi wananchi wa pande mbili za Muungano.
Lakini lengo muhimu na kubwa zaidi liwe lenye kutizama mbele. Hilo ndilo la muhimu zaidi. Lengo ni kuufuta ujinga wa kuidanganya dunia na kuinyang'anya Zanzibar sifa zake kama ni nchi. Kama tutakavyoona huko mbele, Mzee Karume hakushiriki katika mipango ya Mapinduzi na wala hakuupenda Muungano kama ukweli unavyopotoshwa na wenye kutaka kuupa uhalali kwa kumtumiliya kisiasa baada ya kufa kwake. Kama tutakavyokuja kuona baadae piya, alijaribu kuirudishiya Zanzibar sifa zake kama ni nchi na matokeo yake alijibiwa "wakati wake bado haujafika" na baada ya miezi michache akauliwa.
Mzee Jumbe na Maraisi waliyofuatiliya wa Zanzibar pamoja na aliyekuwa Waziri Kiongozi, Maalim Seif Sharif Hamad, piya walijaribu kwa njia zao kuirudishiya Zanzibar sifa zake kama ni nchi na wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuuzidisha muamko wa Wazanzibari katika kuiteteya nchi yao na katika kuiteteya na kuinusuru Zanzibar ndipo itakaponusurika Tanzania.
Tukitaka kurudishana nyuma hatutokosa la kulitafuta na kuwapata wa kuturudisha nyuma, na khasa kikundi kidogo cha wahafidhina wa Kizanzibari pamoja na wahafidhina wenziwao kutoka Tanganyika watakaotaka kumrudisha chui ndani ya zizi la ng'ombe badala ya kumtimuwa.
Upinzani mkubwa wa kitabu hichi utatoka kwenye jumuiya zisizo za kiserikali kama pale Zanzibar au Tanzania zinapotaka kujiunga na Jumuiya ya Nchi za Kiislam (OIC). Jumuiya hizo hazimo ndani ya mikono ya Waislam na zinamiliki zaidi ya asilimia 95% ya vyombo vya habari pamoja na bodi za wahariri wa magazeti, televisheni na vituo vya redio. Vyombo hivyo vya habari vitauelekeza umma na madola makubwa duniani kwenye khofu zisizo kuwa na msingi kwa kusema kuwa Zanzibar sasa inataka kugeuzwa kuwa Dola ya Kiislam. Niya na
Utangulizi xxix
lengo litakuwa ni kuwatiya khofu za chini kwa chini na za wazi wazi wananchi na madola makubwa kuwa kuja juu kwa Zanzibar ni kuja juu kwa ugaidi. Au wataamuwa kukaa kimya na kuzipa kasi fitina za miaka 46 katika jamii na taifa na watapima muamko wa kijamii kabla kutekeleza mipango yao ya muda mrefu kwa Zanzibar na Tanganyika.
Tutarajiye kupaliliwa ngojera za "biashara ya utumwa wa Waarabu" na kuiunganisha fikra ya Afrabia na kuvunjika kwa Muungano wa Jamhuri ya Tanzania. Upande wa umma ambao ungelipendeleya kuiunga mkono fikra ya mfungamano wa Afrabia utakabiliwa na hatari mpya kwa sababu ungali dhaifu kiuchumi, kisiasa, na haumiliki vyombo vingi vya habari, au kupeyana khabari kwa njiya na mikakati mipya.23
Inatosha neno "Arabia" ndani ya neno "Afrabia" (Afrika na Arabia) likafyatuwa upinzani mkali kama ule uliyoonekana dhidi ya OIC. Inatosha pia kwa baadhi ya watu kuchagazwa na jina na asili ya mwandishi ambaye ana damu za makabila mengi tu yakiwemo makabila kadhaa ya Kiarabu, ya Kimanyema na ya Kimwera, nk. Inatosha pia kutowa mfano wa tukiyo liliyotokeya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 2001 wakati mwanafunzi wa ilimu ya Sayansi ya Jamii alipokuwa anatowa hoja ndani ya semina ya darasa. Mwanafunzi huyo alikuwa akinukuu sentensi kutoka kipindi cha Profesa Ali Mazrui cha The Africans: A Triple Heritage. Wakati mwanafunzi huyo alipokuwa akimnukuu Profesa Mazrui, Profesa mmoja Mkristo wa ilimu ya sayansi ya jamii ambaye alikuwa mwalimu wa hiyo semina alikurupuka kwa hamaki na kusema "…kwa nini unamnukuu Ali Mazrui…yeye hata si Muafrika. Ni Mwarabu!"24
Kitabu hichi ni cha kuwailimisha wale ambao wamejazwa khofu dhidi ya Waarabu na Waislam au dhidi ya Waafrika na Wakristo. Lengo ni kuwa, hatimaye kitabu kituletee mapatano ya haraka na mashirikiyano baina ya Wazanzibari, baina ya Wazanzibari na Watanganyika, na baina ya Waafrika na Waarabu. Wenye kuogopa mfungamano wa Wazanzibari na wa Waafrika na Waarabu hawana uwezo wa kuuzuwiya kwa sababu kipindi cha uhusiano mkongwe wa zaidi ya miaka elfu mbili ni kirefu sana kuliko huu muda mfupi wa miaka arubaini na sita uliyogubikwa na guo la khadaa.
Kwa hakika kwa hali ya leo ya Zanzibar na ya Tanganyika, kitabu hichi ni bishara njema. Kwa mujibu wa mwandishi Bwana Mohamed Said "mazungumzo ya wazee yaliyomo ndani ya kitabu ni kama watu wanaotubu ili wapate msamaha. Jinsi wanavyozungumza utadhani wametiwa kitu waseme yote wautue mzigo." Na wewe msomaji, popote ulipo, huenda ukautuwa mzigo wako pia na ukawa na moyo uliyotuliya na wenye matumaini makubwa katika mustakbal mzuri wa Zanzibar, Tanganyika, na wa Afrika Mashariki na Kati
 
Buchanan

Hiki kitabu kinazungumzia mapinduzi yaliyotokea nchini mwetu nafikiri ni bora kukijadili kama kilivyo na kupinga yale ya uzushi yaliyoainishwa humo ndani ili kuhakikisha hakuna kudanganyana.

Hicho kitabu watunzi walimuuliza Nyerere, Okello, Karume na wengine juu ya Mapindizi ya Zanzibar au ni one sided story? Je, kuna document zozote mithili ya zile za WikiLeaks juu ya tukio zima au ni masimilizi ya wazee wanaokunywa kahawa kule Mji Mkongwe?
 
Kitabu kinapatikana hapa, na pia utapata kumjua nani Harith, soma uondoe giza la moyo.
http://www.lulu.com/product/ebook/kwaheri-ukoloni-kwaheri-uhuru-zanzibar-na-mapinduzi-ya-afrabia/11072610
 
Hata huyo aliyesoma kitabu hicho unaona mawazo yake yanajichanganya. Hivyo siamini kuwa kitabu hicho kinaweza kutoa mwanga mpya kuhusu mapinduzi ya Zanzibar, labda kwa mtu kama yeye ambaye anaonekana alikuwa hajafuatilia haswa namna yalivyotokea mapinduzi yale.

Mtoa hoja kama hajui kujieleza sio kuwa kitabu hakikujieleza vizuri.

Kitabu hicho kimewanukuu moja kwa moja

Comrade aliyepanga kuuliwa Karume

Waliopindua moja kwa moja

Watu wa Hizbu wanaojihesabu wamepinduliwa

Kiongozi wa chama cha wafanyakazi Tanganyika alopeleka wafanyakazi wa mikonga Zanzibar

Waliopelekwa Zanzibar kusaidia ASP kwa uchaguzi hadi mapinduzi.

Waliouliwa watu wao wakati Wa mapinduzi nk

Kambona ametajwa kuhusika na Mkello pamoja na wanamapinduzi wengine waliopokea silaha kutoka kwake

Pamoja na hayo kuna documents nyingi sana zilotumika

Cables and reports za balozi za uingereza, Algeria, CIA, Umoja wa Mataifa


Hicho kitabu watunzi walimuuliza Nyerere, Okello, Karume na wengine juu ya Mapindizi ya Zanzibar au ni one sided story? Je, kuna document zozote mithili ya zile za WikiLeaks juu ya tukio zima au ni masimilizi ya wazee wanaokunywa kahawa kule Mji Mkongwe?
 
Hakuna faida humo, ni chuki tu! Mapinduzi yalifanywa kwa uongozi wa John Okello toka Uganda, wala Nyerere wa watu hakutia mkono! Hawakuthubutu kusema hayo akiwa hai, baada ya mzee wa watu kufariki ndio wanachonga. Pamoja na hayo sasa hivi si hayupo? Au wanaogopa kivuli chake?
We Buchanan ni mtu wa kupinga pinga uislamu tu kila siku.Lakini safari hii nakushauri hichi kitabu ukitafute kwa gharama yoyote na ukisome huenda ukaona yale uyapendayo wakifanyiwa waislamu yako humo ndani,utafurahi tu.
John Okello ;yule mchonga mawe alitumika tu kufanikisha ajenda ya siri halafu wabaguzi wakamwita ni mganda na wakamfukuza.
 
nnakiweka kidogo kidogo

Mlango wa Kwanza
Siri Nzito
Mtawaliwa siku zote anataka kumuigiza mtawala katika maumbile yake, mavazi yake, kazi zake na yote yanayokhusiana na hali yake na dasturi zake. -Ibn Khaldun
Mapinduzi Tanganyika na Kenya
Picha kubwa ya Mapinduzi ya Zanzibar ya 1964 haiwezi kufahamika bila ya kuyafahamu ijapokuwa kwa mukhtasari mfupi mapinduzi ya kabla yake yaliofanyika Tanganyika, na baadaye Kenya. Mapinduzi ya Tanganyika, ya Zanzibar, na ya Mwambao wa Kenya ni mifano ya mapinduzi ya kalamu na ya umwagaji damu.
Tanganyika iliupata uhuru wake tarehe 9 Disemba 1961 na Waislam wa Tanganyika walikuwa na mchango mkubwa sana katika kuupiganiya uhuru huo. Hayati Julius Kambarage Nyerere alitowa mchango mkubwa na yeye mwenyewe alikiri hivyo kwenye hotuba yake ya kuwaaga wazee aliyoitowa Dar es Salaam katika mwezi wa Novemba mwaka 1985. Kwa mara ya kwanza Mwalimu alielezeya namna alivyopokelewa, kujuulishwa na kusaidiwa sana na wazee wa Kiislamu wa Dar es Salaam. Kwenye shughuli za TANU yeye alikuwa ni Mkristo peke yake na mara nyingine alikuwepo John Rupia.
Muhimu pia na kwa mara ya kwanza Mwalimu alisikika akisema kwenye hotuba hiyo kuwa hata jina la Tanganyika African National Union (TANU) lilifikiriwa na kuundwa na akina marehemu Abdulwahid Sykes walipokuwa askari Burma katika vita vya pili vya dunia.1
Historia iliyofichwa ya mchango wa Waislam katika kuupiganiya uhuru wa Tanganyika imeandikwa na kuelezwa kwa ufasaha mkubwa na mwandishi maarufu wa Tanzania Bwana Mohamed Said kwenye kitabu chake kwa lugha ya Kiingereza, The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924–1968), na kwa Kiswahili Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes (1924–1968) Historia Iliyofichwa Kuhusu
Mlango wa Kwanza
2
Harakati za Waislam Dhidi ya Ukoloni wa Waingereza katika Tanganyika. Kitabu hicho ni muhimu sana kwa wanaotaka kufahamu vipi Waislam waliupiganiya uhuru wa Tanganyika na namna walivyopinduliwa kwa mapinduzi baridi kwanza kabla ya kupinduliwa kwa Dola ya Zanzibar tarehe 12 Januari 1964. Kilele cha mapinduzi ya Tanganyika ni kudhoofishwa nguvu za umma wa Kiislamu pale ilipovunjwa East African Welfare Muslim Society (EAMWS) na zilipozimwa juhudi za kuanzisha Chuo Kikuu cha Kiislam mwaka 1964.2
Bwana Mohamed Said pia amefafanuwa katika kitabu chake Uamuzi wa busara wa Tabora namna gani uongozi wa Waislam kutokeya African Association mpaka kuundwa kwa TANU walivyopinduliwa kwa mapinduzi ya kalamu. Baraza la Wazee la TANU ambalo Mwenyekiti wake alikuwa marehemu Mzee Suleiman Takadiri lilipinduliwa chali kwa kazi iliofanywa na kiongozi na viongozi wa Kiislam waliouweka mbele uzalendo wa Kiafrika kuliko mafundisho ya dini yao. Chanzo cha mapinduzi hayo yalikuwa masharti matatu yalioikabili TANU katika kushiriki uchaguzi wa kwanza wa Tanganyika wa kulichaguwa Baraza la Kutunga Sheria. Mkutano wa TANU wa Tabora wa tarehe 21–26 Januari 1958 uliamua kuingiya uchaguzi wa kibaguzi wa kura tatu ambao ulikuwa na masharti matatu magumu:
1) Ili Mwafrika aweze kupiga kura alitakiwa awe na kipato cha pauni mia nne za Kiingereza kwa mwaka.
2) Awe na kiwango cha elimu ya darasa la kumi na mbili.
3) Na awe ameajiriwa katika kazi maalumu.3
Uamuzi wa busara wa Tabora haukuwanasa Waingereza kama ulivyowanasa Waislam wa Tanganyika ambao wengi wao hawakuweza kuwachaguwa viongozi wao kwa sababu uchaguzi wa kura tatu "ulikuwa ukizuia uongozi wa kuchaguliwa kuingia kwenye madaraka."4
Kwa upande mwengine, Kenya kabla ya kupata uhuru wake tarehe 12 Disemba 1963, siku mbili baada ya uhuru wa Zanzibar, ilikuwa imegawanyika sehemu mbili: Koloni la Kenya, au bara, na Himaya ya Kenya, au Mwambao. Sheikh Abdillahi Nassir ni mmoja kati ya viongozi wa Mwambao ambaye alihudhuriya mkutano wa Mwambao uliofanyika Lancaster House, London, baina ya tarehe 8–12 Machi mwaka 1962.
Anaelezeya Sheikh Abdillahi kwenye kanda iitwayo "Mwambao: Historia ya Pwani ya Afrika Mashariki," kuwa Himaya ya Kenya ilikuwa ni nchi kabla ya Koloni la Kenya kuwa ni nchi kwa miaka isiyopunguwa 1,300, na namna chuki za uzalendo wa Kiafrika zilivyowaathiri Waislam na khasa chuki za kikabila na propaganda ya utumwa na Uarabu.5
Sehemu hizo mbili za Kenya, Koloni la Kenya na Himaya ya Kenya au Mwambao, zikawa ni nchi moja ya Kenya kwa makubaliyano ya mabadilishano ya barua baina ya Waziri Mkuu wa Kenya, Mzee Jomo Kenyata na Waziri Mkuu
Siri Nzito
3
wa Zanzibar Bwana Mohammed Shamte walizoandikiyana London tarehe 5 Oktoba 1963. Barua zote mbili zilikubaliyana juu ya mambo matano yafuatayo:
1) Uhuru wa kuabudu wa watu wa dini zote katika sehemu hiyo utalindwa kwa mujibu wa dini zao; na khasa wale raia wa Sultani na vizazi vyao, ambao ni wa dini ya Kiislamu, watahakikishiwa uhuru wao wa kuabudu katika nyakati zote na hifadhi za nyumba na sehemu zote za dini yao.
2) Uwezo wa Kadhi Mkuu na Makadhi wengine wote kuhukumu kwa sharia ya Kiislamu utahifadhiwa kufuatana na sharia ya Kiislamu katika kesi zote za ndoa, talaka na mirathi.
3) Katika zile sehemu ambazo wakaazi wake wengi ni Waislamu, watawekwa, kila inapowezekana, Maafisa Utawala (Mabwana Shauri) Waislamu.
4) Watoto wa Kiislamu, kwa kadri inavyowezekana watasomeshwa lugha ya Kiarabu katika kudumisha dini yao ya Kiislamu kwa vile lugha hii ndiyo lugha ya dini yao. Ule msaada wa fedha unaotolewa kuzisaidia skuli za msingi za Kiislamu katika hilo jimbo la Mkoa wa Pwani utaendelea. Hautakatwa.
5) Umilikaji wa ardhi kutokana na mikataba iliyokwisha kusajiliwa utatambulikana na kukubalika wakati wote. Mwenendo huohuo utaendelea na kuhifadhiwa katika kusajili mikataba mipya ya kumiliki ardhi isipokuwa tu pale itakapokuwa ni lazima kuchukua ardhi kwa masilahi na faida ya umma; lakini papo hapo wale wenye ardhi zao watabidi kulipwa fedha.6
Kwa mujibu wa Sheikh Abdillahi, makubaliano hayo baina ya Serikali ya Zanzibar na Serikali ya Kenya hayakutimizwa na amethibitisha namna nguvu za umma zilivyoporwa na umuhimu wa kujenga muamko wa kuelewa badala ya muamko wa hamasa. Mfano mkubwa ambao ameutowa Sheikh Abdillahi am-bao ni kinyume na makubaliano waliyotiya sahihi Mawaziri Wakuu wa Zanzibar na wa Kenya, ni kunyanganywa Waislam, wa makabila yote, Taasisi muhimu sana ambayo ikijulikana kwa jina maarufu la Mombasa Insititute of Muslim Education (MIOME) ambayo ilikuwa ni:
baraka kubwa kwa Waislam wa Afrika Mashariki. Hapa ndipo mustakbal wa vizazi vya Waislam vinapewa mafundisho katika masomo ya ufundi chini ya Maprofesa mabingwa ambao wameajiriwa na Serikali kutoka Ulaya. Sir Phillip Mitchell ambaye alikuwa ni Gavana na sasa ni Mwenyekiti wa Baraza la Waendeshaji wa Taasisi alikuwa ndiyo nguvu ya usukumaji wa Taasisi [MIOME]. Mtukufu Sultan wa Zanzibar alitowa mchango wa Shs. 2,000,000/- kutoka mfuko wa Colonial Welfare Fund, Mtukufu Aga Khan alichangiya Shs. 2,000,000/-: Mtukufu Sheikh Mkuu wa jamii ya Kibohora amechangiya Shs. 1,000,000/-; na Sheikh Khamis Mohammed bin Juma [El Mutwaji] amekodisha ekari 34 na nusu za ardhi nzuri na kwa muda mrefu kwa matumizi ya Taasisi, na kwa bei khafifu kwa kila mwaka.7
Mbali ya Muslim Teachers' Training College iliyokuwepo Kibuli, Kampala, Uganda, Khamisi Sekondari ya Mombasa, Muslim School ya Soroti, ya Jinja, na kadhalika.
Iliyovunja rekodi zote na ambayo marehemu Sheikh Ali Muhsin akiamini kuwa ndiyo moja kati ya sababu za kupinduliwa Zanzibar, ilikuwa ni fikra na mipango
4 Mlango wa Kwanza
ya kuanzisha Chuo Kikuu Cha Kiislam cha Afrika Mashariki na Kati. Kwa mujibu wa Sheikh Ali Muhsin, Chuo hicho kilikuwa na lengo la kuwafundisha Waislam kutoka sehemu zote za Afrika Mashariki na Kati. Mwandishi wa ramani wa Chuo hicho alikuwepo Zanzibar mapinduzi yalipotokeya na alisaidiwa kuondoka na Bwana Ahmed Omar Jahadhmy. Wamasri waliishauri serikali ya Zanzibar wasubiri mpaka watakapokuwa na wanafunzi wa kutosha ambao wataweza kufundishwa kwenye Chuo hicho. Fikra iliyoona mbali kwa wakati huo ni hii ambayo leo inaitwa Open University. Redio na televisheni vilikuwa viwe ndiyo vyombo viwiili vikubwa vya kufundishiya kote Afrika Mashariki na Kati. Majaribio ya kwanza yalifanywa kabla ya mapinduzi lakini yalifeli.8
Baada ya kuvunjwa kwa East African Muslim Welfare Society ambazo khabari zake zinapatikana kwa urefu kwenye kitabu cha Kiswahili cha Bwana Mohamed Said cha Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes, taasisi na mali zake zote zikataifishwa na badala yake pakaundwa BAKWATA Tanzania, SUPKEM Kenya na UMSC Uganda. Hali ya Waislam chini ya utawala wa Kiingereza ilikuwa ni ya kuridhisha zaidi kuliko hali waliyokuwa nayo baada ya kupatikana uhuru Tanganyika, Kenya na hata Uganda.
Waingereza Walijuwa Nini Kuhusu Mapinduzi?
Ukiangaliya kwa makini utakuja kuona kuwa walikuwepo Waingereza na mamishionari ambao walikuwa hawana chuki dhidi ya Wazanzibari wenye asili ya Kiarabu lakini kwa bahati mbaya sauti zao sio zilizokuwa zikisikilizwa na kupewa nafasi. Kwa mfano alikuwepo Dk. Gerald Broomfield ambaye alikuwa ni mmishionari wa Kianglikani aliyekuwa na uzowefu mkubwa Zanzibar. Dk. Broomfield alinukuliwa na Arab Association ya Zanzibar kutoka kitabu chake Colour Conflict in Africa kwa maneno yake yafuatayo:
Afrika iliyobakiya ina jambo la kujifunza kutoka Zanzibar…Zanzibar inaonyesha uwezekano wa kuwepo amani na kuhishimiana baina ya makabila. Huenda likawa ni jambo zuri kwa roho zetu kukumbuka [Zanzibar] inafanya hivyo kwa sababu Sultan wa Kiarabu ndiye mkubwa wa Dola.9
Hilo halistaajabishi kwa sababu Ukristo uliingiya Zanzibar na bara kwa kupewa hishma na Masultani waliokuwa ni Waarabu na Waislamu. Lakini Muingereza mtawala alipoona kuwa Ufalme umegeuka na kuiunga mkono siasa ya kizalendo ya chama cha Zanzibar Nationalist Party (ZNP) ambayo ilikuwa karibu sana na siasa ya uzalendo wa Kiarabu (Pan-Arabism au Arab Nationalism) wa Gamal Abdel Nasser wa Misri, akaamua kuwatupa mkono ZNP-ZPPP na kuubwaga uhuru wa Zanzibar ambao ulikuwa hauna salama kwa Waingereza au kwa Mwalimu Nyerere kwa sababu, na kama alivyoelezeya Sheikh Abdillahi:
Siri Nzito 5
Zanzibar ilikuwa ni nchi pekee katika Afrika nzima ambayo isingelihitajiya Mzungu hata mmoja. Zanzibar ilikuwa ina watu wa kuendesha nchi na kuwaazima majirani kuendesha nchi zao.10
Sababu kubwa ya Wazanzibari wenye asili ya Kiarabu kuwageuka watawala wa Kiingereza na watawala hao kupanga kuwakomowa Wazanzibari wenye asili ya Kiarabu, kulianza kwa kupigwa mabomu Misri na Muingereza mwaka 1956.11 Wazanzibari wenye asili ya Kiarabu walihisi kuwa Uingereza haiaminiki na kuwa ilikuwa dhidi ya Waarabu. Hisia hii ilisababisha kudai uhuru kamili bila ya kungojea maendeleo zaidi ya baadae.
Mwisho wa mivutano Muingereza alikataa kuisaidiya serikali ya Zanzibar ilipopinduliwa tarehe 12 Januari 1964 na sababu kubwa iliyowafanya kukataa ni imani yao kuwa Mapinduzi ya Zanzibar yalikuwa ni suala la ndani ya Zanzibar na kuwa hakukuwa na mkono au uvamizi kutoka nje ya Zanzibar. Kwa upande wa Tanganyika Muingereza aliamuwa kuzuwiya fujo na kumrejesha kitini Mwalimu Nyerere pale jeshi la Tanganyika lilipoasi tarehe 20 Januari 1964 na Nyerere akakimbilia mafichoni siku tisa tu baada ya mapinduzi ya Zanzibar.12 Viongozi wa Serikali ya Tanganyika haraka walikwenda kuomba msaada kutoka kwa wakubwa wa Kiingereza. Anaelezeya Brigadier Douglas:
Kambona, akifuatana na [Paul] Bomani, Waziri wa Fedha, akionekana ana jambo ameficha, na ana khofu zaidi kuliko kabla, walikuja nyumbani kwangu na barua kutoka kwa Naibu Raisi Kawawa ilosema: Nimeelekezwa na Raisi wa Jamhuri ya Tanganyika kuiletea ombi la msaada wa kijeshi serikali ya Kiingereza ili utuwezeshe kuweka sheria na amani ndani ya nchi.13
Mara nyingi uasi wa jeshi la Tanganyika umekuwa ukihusishwa na mapinduzi ya Zanzibar kwa kuwa wanajeshi wa Tanganyika, Kenya na Uganda waliingiwa moyo wa kuasi kutokana na kufaulu kwa Mapinduzi ya Zanzibar ingawa hakukuwa na uhusiano wowote baina ya matukio hayo mawili. Uamuzi huu unatokana na kukosekana kuyafahamu Mapinduzi ya Zanzibar kwanza, na pili, kukosekana huko kufahamika kwa mapinduzi ya Zanzibar kumeondowa hoja ya kufanywa utafiti wa mahusiano baina ya mapinduzi na uasi wa kijeshi wa Tanganyika.
Suala moja muhimu ambalo linavutiya hoja ya uhusiano baina ya mapinduzi ya Zanzibar na uasi wa kijeshi wa Afrika Mashariki ni suala la kukamatwa kwa viongozi wa vyama vya wafanyakazi baada ya kutokeya uasi huo Tanganyika. Tarehe 29 Januari 1964 Balozi wa Kiingereza kwa niaba, alipeleka ujumbe wa telegram kwa Commonwealth Relations Office, London, uliopitiya Ubalozi wa Kiingereza Kampala, Nairobi, Aden na Washington:
Matokeo ya kuasi kwa jeshi la Tanganyika ni kundi kubwa la viongozi wa vyama vya wafanyakazi kukamatwa Jumapili usiku Tanganyika nzima pamoja na
 
Btw according to mtunzi yeye hakuweka lawama kwa Wakristo kwa sababu amesema kuwa Waislam tele wamehusika. Waislam wa TANU walihusika pamoja na Wakristo wengi ikiwa ni pamoja na Kambona na kina Mkello na wengine.

Huyu mtu Kama blame ameweka basi ni kwa Tanganyika and Pan-africanism


Okello ameelezewa alikuwa anafanya kazi wapi (kwa Mazrui) aliyeenda kum-scout amezungumza moja kwa moja na kutoa sababu zake za kwanini Okello

Pia zimethibitishwa na report za balozi mbali mbali

Hicho kitabu watunzi walimuuliza Nyerere, Okello, Karume na wengine juu ya Mapindizi ya Zanzibar au ni one sided story? Je, kuna document zozote mithili ya zile za WikiLeaks juu ya tukio zima au ni masimilizi ya wazee wanaokunywa kahawa kule Mji Mkongwe?
 
We Buchanan ni mtu wa kupinga pinga uislamu tu kila siku.Lakini safari hii nakushauri hichi kitabu ukitafute kwa gharama yoyote na ukisome huenda ukaona yale uyapendayo wakifanyiwa waislamu yako humo ndani,utafurahi tu.
John Okello ;yule mchonga mawe alitumika tu kufanikisha ajenda ya siri halafu wabaguzi wakamwita ni mganda na wakamfukuza.

Kumbe Okello alikuwa raia wa wapi maana nimewahi kusoma kitabu alichoandika Okello mwenyewe, Chapter inayosema, Nine Hours Revolution, pamoja na historia nzima ya maisha yake! Ukiamua kupika majungu utatumia means zozote kuchanganya story zikaonekana za kweli!
 
Kumbe Okello alikuwa raia wa wapi maana nimewahi kusoma kitabu alichoandika Okello mwenyewe, Chapter inayosema, Nine Hours Revolution, pamoja na historia nzima ya maisha yake! Ukiamua kupika majungu utatumia means zozote kuchanganya story zikaonekana za kweli!

Sasa tutajuaje kama Okello sie aliyedanganya?

Ni muhimu kusoma vitabu tofauti ili kupata ukweli.

Kwenye Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru amezungumzwa kuwa ni Mganda. Hilo ni dhahiri kuwa halina mgogoro.
 
Btw according to mtunzi yeye hakuweka lawama kwa Wakristo kwa sababu amesema kuwa Waislam tele wamehusika. Waislam wa TANU walihusika pamoja na Wakristo wengi ikiwa ni pamoja na Kambona na kina Mkello na wengine.

Huyu mtu Kama blame ameweka basi ni kwa Tanganyika and Pan-africanism


Okello ameelezewa alikuwa anafanya kazi wapi (kwa Mazrui) aliyeenda kum-scout amezungumza moja kwa moja na kutoa sababu zake za kwanini Okello

Pia zimethibitishwa na report za balozi mbali mbali

Ukisoma hizo page chache ulizoweka ni kwamba kuna lawama dhidi ya Wakristo, kwa kudai eti historia ya mapambano ya uhuru ya Waislamu ilifichwa, hivi kuna haja kila mtu akifanya jambo jema atajwe na dini yake?
 
Sasa tutajuaje kama Okello sie aliyedanganya?

Ni muhimu kusoma vitabu tofauti ili kupata ukweli.

Kwenye Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru amezungumzwa kuwa ni Mganda. Hilo ni dhahiri kuwa halina mgogoro.

Ndio maana nikasema wangeulizwa akina Nyerere, Okello, Karume na wote waliohusika directly, sio kuacha watangulie mbele ya haki then tunaanza kuambiwa afterthoughts! Well, unaamini inawezekana Okello anadanganya lakini unaamini yaliyoandikwa na ndugu zako, strange indeed!
 
Back
Top Bottom