Mkutano Mkuu wa Wadau wa Tasnia ya Chai 2024

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,909
946
Kauli Mbiu- “Changamkia Fursa, Ongeza Kasi ya Maendeleo ya Tasnia ya Chai Tanzania”

Wilaya ya Ludewa kama wazalishaji wa Zao la Chai- tumeshiriki kikamilifu mkutano huu jijini Dodoma

Wilaya ya Ludewa ina jumla ya Hekta 16,300 zinafaa kwa Kilimo cha Chai katika vijiji vya kata za Madilu, Madope na Milo.

✅ Eneo linalolimwa limeongezeka kutoka Hekta 33 mwaka 2019 mpaka Hekta 380 mwaka 2024.

✅ Jumla ya wakulima 661 wanaolima chai 2024 kutoka wakulima 85 mwaka 2019.

✅ Mashamba ya pamoja (blockfarms) 13 zilizopimwa zenye ukubwa wa jumla ya Hekta 165.
Upandaji katika maneo ya mashamba ya pamoja unaendelea Kwa kushirikiana na kampuni ya NOSCI.

✅ Katika kuboresha Kilimo cha Chai na kuongeza tija ya uzalishaji wa majani tuna mpango wa skimu za umwagiliaji katika blockfarms ili kuongea tija ya uzalishaji.

✅ Kutoa elimu kwa wakulima na wataalamu katika kuongeza uzalishaji na kushirikiana na wadau katika kuendeleza Kilimo cha Chai.

✅ Msimu wa 2023/24 jumla ya miche 1,000,000 imesambazwa Kwa wakulima kwa kushirikiana na kampuni ya NOSCI ambayo imepandwa katika eneo la hekta 72.

🇹🇿 Tunazidi Kumshukuru Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kufungua milango ya uwekezaji kwenye Sekta ya Kilimo- nasi kama Wilaya ya Ludewa tunawakaribisha kuwekeza katika zao hili la Biashara la Chai.

Victoria Mwanziva
Mkuu wa Wilaya ya Ludewa
26/03/2024

#Ludewa #LudewaYetu

WhatsApp Image 2024-03-26 at 20.48.46.jpeg
 
Back
Top Bottom