mapinduzi ya kifikra,mapinduzi ya kimaendeleo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

mapinduzi ya kifikra,mapinduzi ya kimaendeleo

Discussion in 'Nafasi za Kazi na Tenda' started by Jpinduzi, Nov 14, 2011.

 1. Jpinduzi

  Jpinduzi Senior Member

  #1
  Nov 14, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 136
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Habari marafiki, Katika ulimwengu wa sasa kuna mabadiliko ya namna mbalimbali,kwa viumbe na mazingira yake.Mabadiliko haya hutokana na na tabia asilia na pia za mpito au sababishi au tegemezi.Mfano wa tabia asilia ni mabadiliko ya majira na viambatanishivyake.Masika-kilimo,kiangazi-mavuno&ukame,ukuaji wa viumbe hai nk.mfano wa mabadiko tegemezi ni kama mabadiko ya hali ya hewa(kutokana na mahitaji ya viumbe hai),ustawi wa mimea nk.

  Lakini pia kuna mabadiliko tegemezi/asilia,na mfanowe ni mabadiliko ya kifikra.Kila kiumbe chenye uhai ulimwenguni kina mfumo wake wa kufikiri na kuishi.Nitazungumzia kiumbe hai,binadamu!!Mimi ninaamini kuwa asili ya mwanadamu ni Mungu,na katika uumbaji Mungu alimpa kiumbe huyu uwezo wa kipekee wa kufikiri/kuchanganua mambo au mahitaji yake na viumbe wengine.NI UWEZO HUU ULIOASILI YA MAFANIKIO/ANGUKO LA KIUMBE HUYU PAMOJA NA VINAVYOMZUNGUKA.Unavyofikiri ndivyo ulivyo.Kama unafikiri wewe ni masikini basi ndivyo unavyojitengenezea mazingira ya kuwa masikini,na pia kinyume chake.

  ​Lakini pia kuna uwezekano wa kuiga tabia asilia,labda kutoka kwa wazazi.Wahenga walisema ;mtoto wa nyoka ni nyoka;.Ninaamini kwamba wengi wetu tunaelewa walimaanisha nini.Pia kuna mabadiliko tegemezi,ambayo hutokana mazingira pamoja na viumbe vinavyomzunguka.Unaweza kubadilika kifikra kutokana na kujifunza kutoka kwa mwenzako au ushauri nasaha.

  Mabadiliko ya kifikra ni mapinduzi halisi ya kimaendeleo.Huwezi kuwa tajiri katika lindi la mawazo ya kimasikini.Kama unafikiri kwamba ulizaliwa masikini na utakufa masikini,ndivyo itakavyokuwa.au kama unafikiri kuwa kwa kukosa kwako elimu,pesa,kazi na mahitaji mengine kunakupotezea uhalali wa kuheshimiwa,kuthaminiwa basi ndivyo itakavyokuwa.Kwa kifupi ni kwamba tunahitaji mabadiliko ya kifikra kwanza kabla ya yote,ukijumuisha mali.Ni baada ya hapo,ndipo tutakapoweza kujiletea mapinduzi halisi ya kimaisha.Ni hayo tu kwa leo.
   
Loading...