Mapinduzi makubwa duniani yameletwa na matumizi ya zana za madini ya chuma, ni heri uache vyote ili uchimbe chuma kama unayo

25 January 2021

Joe Biden atangaza mpango kabambe wa kufufua viwanda mama, kusaini waraka wa dhararu kuinusuru Marekani

Rais wa 46 wa USA Joe Biden ameapa kuhakikisha kuwa viwanda vya vyuma, aliminium, glasi, viwanda vya tekenolojia ya kisasa kama biotekinoloji n.k vinabaki Amerika huku malighafi / mashine/ utaalamu pia uwe wa kutoka ndani ya Marekani na serikali yake (Joe Biden) kuwa mkali zaidi ya Donald Trump kisera kuhusu "Marekani Kwanza" kwa kuhakikisha kila kitu kinazalishwa ndani ya Amerika na kuwa atasaini waraka wa dharura (executive order/decree) mapema kutimiza ndoto hiyo ya " Amerika Kwanza".

Rais Joe Biden anasisitiza sera ya "Marekani Kwanza" ni hakikisho la kuwa Marekani inabaki kuwa na viwanda mama, viwanda vidogo, vyuo vikuu vitakavyo fanya tafiti zitumike ktk sekta za viwanda / kilimo/ Afya vya Marekani, uchumi mkubwa, ajira nyingi za ndani na usalama ktk kandarasi za kijeshi na vifaa tiba madawa, chanjo afya za waMarekani.

Serikali yake imeunda Kurugenzi Maalum itakayokuwa chini ya Ofisi ya Rais kuhakikisha kandarasi zote zinakwenda kwa waMarekani. Pia itakuwa lazima Kurugenzi hiyo kutangaza kwa umma fursa hizo za kandarasi na uzalishaji ktk vyombo vya habari ili kuhakikisha Kurugenzi hiyo haiwapiti waMarekani kwa bahati mbaya.

Maana serikali haifahamu kila kitu hivyo "Uwazi" kupitia taarifa kwa umma anaweza kutokeza Mmarekani akasema anaweza kuifanya kazi hiyo kabla ya makampuni ya kigeni kupewa fursa hiyo pia kutakuwepo mfuko maalum kuwasaidia waMarekani wenye makampuni yenye ujuzi lakini wenye mtaji mdogo kuweza kuchukua kazi za kandarasi kubwa ili waMarekani wafaidike kwanza.

Biden gives remarks on strengthening American manufacturing
Source : PBS NewsHour

January 25, 2021

Biden signs ‘Buy American’ order​

WASHINGTON (AP) — President Joe Biden signed an executive order Monday to boost government buying from U.S. manufacturers, as talks with Congress over a $1.9 trillion stimulus package that he considers essential to the nation's recovery showed few signs of progress.

Watch Biden's remarks in the player above.

The executive order is among a flurry of moves by Biden during his first full week to publicly show he's taking swift action to heal an ailing economy. Biden reiterated Monday that he believes the country is in a precarious spot and and that relief is urgently needed, even as he dismissed the possibility of embracing a scaled-down bill to secure passage faster. Among the features of the stimulus plan are a national vaccination program, aid to reopen schools, direct payments of $1,400 to individuals and financial relief for state and local governments.

"Time is of the essence," Biden said. "I am reluctant to cherry-pick and take out one or two items here."

Biden, meanwhile, was growing more bullish on vaccine distribution in the U.S., after he and his aides face criticism for their caution in setting vaccination targets for the virus-weary nation. Biden told reporters that he believes 150 million shots in arms may be achievable in his first 100 days in office — up from 100 million doses — and that he expects widespread availability of the vaccines for Americans by spring, with the U.S. "well on our way to herd immunity" by summer.

Biden's comments come after his team held a call Sunday to outline the stimulus plan with at least a dozen senators, while the president has also privately talked with lawmakers.

"There's an urgency to moving it forward, and he certainly believes there has to be progress in the next couple of weeks," White House press secretary Jen Psaki said Monday. She warned that action needed to be taken before the U.S. reaches an "unemployment cliff" in March, when long-term unemployment benefits expire for millions of Americans.

But Republicans on Capitol Hill were not joining in the push for immediate action.

One key Republican, Sen. Susan Collins of Maine, said after Sunday's call that "it seems premature to be considering a package of this size and scope." Collins described the additional funding for vaccinations as useful while cautioning that any economic aid should be more targeted.

Senate Minority Leader Mitch McConnell, R-Ky., said Monday that "any further action should be smart and targeted, not just an imprecise deluge of borrowed money that would direct huge sums toward those who don't need it."

Biden sought to downplay the rhetoric from GOP lawmakers, saying, "I have been doing legislative negotiations for a large part of my life. I know how the system works."

"This is just the process beginning," he added. "No one wants to give up on their position until there's no other alternative."

Monday's order will likely take 45 days or longer to make its way through the federal bureaucracy, during which time wrangling with Congress could produce a new aid package. That would be a follow-up to the roughly $4 trillion previously approved to tackle the economic and medical fallout from the coronavirus.

The order was aimed at increasing factory jobs, which have slumped by 540,000 since the pandemic began last year.

"America can't sit on the sidelines in the race for the future," Biden said before signing the order in the Eisenhower Executive Office Building. "We're ready, despite all we're facing."

Biden's order would modify the rules for the Buy American program, making it harder for contractors to qualify for a waiver and sell foreign-made goods to federal agencies. It also changes rules so that more of a manufactured good's components must originate from U.S. factories. America-made goods would also be protected by an increase in the government's threshold and price preferences, the difference in price over which the government can buy a foreign product.

It's an order that channels Biden's own blue-collar persona and his promise to use the government's market power to support its industrial base, an initiative that former President Donald Trump also attempted with executive actions and import taxes.

"Thanks to past presidents granting a trade-pact waiver to Buy American, today billions in U.S. tax dollars leak offshore every year because the goods and companies from 60 other countries are treated like they are American for government procurement purposes," said Lori Wallach, director of Public Citizen's Global Trade Watch and a critic of past trade agreements.

While Trump also issued a series of executive actions and tariffs with the goal of boosting manufacturing, he didn't attempt to rewrite the guidance for what constitutes a U.S.-made component or tighten the process for granting exemptions to buy foreign goods, a key difference from Biden's agenda, Biden's administration said.

The order also has elements that apply to the separate Buy America program that applies to highways and bridges. It aims to open up government procurement contracts to new companies by scouting potential contractors. The order would create a public website for companies that received waivers to sell foreign goods to the government, so that U.S. manufacturers can have more information and be in a more competitive position.

Past presidents have promised to revitalize manufacturing as a source of job growth and achieved mixed results. The government helped save the automotive sector after the 2008 financial crisis, but the number of factory jobs has been steadily shrinking over the course of four decades.

The number of U.S. manufacturing jobs peaked in 1979 at 19.5 million and now totals 12.3 million, according to the Labor Department
Source : WATCH: Biden signs 'Buy American' order, pushes for urgent COVID-19 relief

Hii itakuww pigo kubwa sana kwa China.
 
Ndiyo, hayo madini yanaitwa "Iron ore" au kwa kiswahili ndiyo makinikia. Hayo madini yapo Liganga, Mchuchuma , Morogoro nk, Mamilioni ya tani.

Kinachotakiwa ni kujenga au kununua jiko la kufanyia "Smelting", smelting ni kitendo cha kuchuja chuma na udongo na kitendo hicho hufanyika ndani ya hiyo smelter inayoitwa "Blast furnace"--- humo ndani ya hiyo smelter wanaweka Coke (makaa ya mawe yaliyosafishwa) na limestones mawe ya chokaa kiasi fulani ndipo huwashwa kwa moto mkali ndipo hatimaye chuma hukingwa kutoka katika hiyo smelter kikiwa kama maji mekundu, chuma hicho huitwa "Pig iron", hicho chuma huwa bado ni "ghafi" yaani kimejaa uchafu hasa Carbon na hivyo kinatakiwa kupitishwa kwenye chungu kingine kiitwacho "Bessemer convertor" humo hicho chuma hupashwaa joto kali na Oxygen hupitishwa ili kuondoa hiyo Carbon, hapo sasa ndipo unapata aina mbalimbali za Chuma cha pua "steels" na chuma cha udongo cast irons kulingana na mahitaji, katika steels ndipo utapata Nondo, Shafts, Mabati ya kutengenezea mageti a grills , vyuma vya reli nk.

Hapo nimeandika kwa ufupi ili upate picha kidogo.
Eeenh, Sawa mkuu 'Mokaze'.

Wewe ni 'mhunzi'?

Nimependa ulivyoeleza jinsi ya kupata hivyo vyuma vya aina mbalimbali,... hebu endelea hadi kule kwa 'graphine basi; kwa vile naona una mwelekeo wa kuyafahamu haya mambo!

Nimesoma hii mada hadi nilipofikia mchango wako nikaona kuna urahisishaji wa mambo mengi yahusuyo chuma.
Ndiyo, pamoja na kuendelea kuwepo na umuhimu wa madini haya katika matumizi mengi, tusisahau kwamba teknologia imekwishakuwa kubwa na kupanuka zaidi. Hatuwezi kukiona chuma katika mwonekano uleule uliokuwepo miaka mia mbili iliyopita.

Ndio, nadhani Tanzania ingefaidika zaidi kama ingeweka mikakati ya kuchimba na kuendeleza utumiaji wa chuma chake katika kutengeneza bidhaa mbalimbali zitokanazo na mali ghafi hiyo hasa katika wakati huu. Tungeunganisha madini yetu mbalimbali kama 'nickel' na 'graphite', madini ambayo sasa yanachimbwa na kusafirishwa nje na kutengeneza aina mbalimbali za vyuma vyenye thamani kubwa na kutengeneza bidhaa mbalimbali kama mafriji, majiko na vitu vingine chungu nzima.

Pamoja na yote hayo, tukumbuke pia tunapojadili bidhaa ya chuma kama anayoiongelea mleta mada, tujiulize bei ya chuma duniani sasa hivi ikoje.? Ni nani watengenezaji wakubwa wa bidhaa hii na wameshikilia soko kwa kiasi gani. Tutaweza kushindana ndani ya soko hilo analotamba nalo mChina?
 
Mtoa mada atakuwa hajasoma kitu kinachoitwa "DEMAND AND SUPPLY" how price is affected by Dd & Ss😆
Haya sasa!

Si hivyo tu. Inabidi tuangalie pia tunataka kuitumia chuma yetu kwa bidhaa zipi. Je teknologia ya kuvitengeneza hivi vitu tunayo?

Hii 'dhana' yetu mbovu ya "hatuwezi" tutaiweka pembeni na kudhamiria kufanya kweli?

Soko la bidhaa za chuma lipo sana. Hivi vi-nchi vya Afrika vyote, hata kama vinakwenda taratibu, lakini vinaendelea. Vitahitaji bidhaa hizi katika maendeleo yao. Kwa nini chuma kitoke China kiuzwe rahisi kuliko hiki chetu kitakachotengenezwa hapa hapa Afrika? Kama AfCFTA itafanya kazi, kwa nini sisi tusiwe ndio nchi ya kuwapatia chuma hawa wengine wote katika umoja wetu?

"Kupanga ni kuchagua"; kama tukipanga na kudhamiria kwa dhati kufanya hilo ndilo liwe mchango wetu mkuu katika umoja huo, kwa nini isiwezekani? (kama tutaweza kupata uongozi wenye uthubutu), na sisi sote tutakuwa na 'mindset' hiyo hiyo ya uthubutu.
 
Ujuzi wa kuunda Vitu mbalimbali ndiyo changamoto. Ili nchi iendelee inatakiwa iweze kuunda angalau asilimia 50 ya mashine za viwanda vyake hapa hapa nchini na pia kuvifanyia ukarabati.

Kuwepo na "mnyororo" wa kuvipatia viwanda vya ndani mashine na vipuri vinavyotengenezwa na makampuni ya hapa hapa nchini vinavyoweza kuyeyusha Madini ya chuma, vioo glass chupa, nati skrubu, kudizani mashine, vifaa kazi na ujuzi wa kukamilisha kitu kizima kiweze kutumika viwandani ili viweze kuzalisha au kusindika. Yaani viwanda viwe walaji "customer " wa mashine, vipuri na service vinavyofanywa na viwanda vingine vya ndani ya Tanzania.

Tuondokane na "utegemezi"/ dependency yaani kuzalisha tusichotumia na kutumia tusichozalisha iwe katika level ya vitambaa vya nguo (matumizi ya watu) au mashine za viwandani (matumizi ya wenye viwanda).
Hawa jamaa unaowaona wanashinda 'vijiweni' kila kona ya Tanzania,..., hawa ni 'vipuli' tele tunavyotakiwa kuvitumia, lakini kwa ushamba wetu, tunaviacha vinaozea hapo hapo.
Akitokea mtu (kiongozi), aseme anataka kuvitumia ipasavyo 'vipuli' hivi..., kwa nini visiweze kutumia kutimiza hayo uliyoandika hapa. Vyuo vya ufundi vipo, na vingi vingine vinaweza kujengwa kwa muda mfupi tu! Ndani ya miaka mitano, tunaweza kuwa na hali tofauti kabisa na ilivyo sasa. Ni swala la 'UTHUBUTU' tu na kuwa na dhamira halisi ya kutaka kutekeleza jambo. Hizi sifa kwa bahati mbaya viongozi wetu na sisi wenyewe hatujafanikiwa kuzitumia ipasavyo.
 
Mbarikiwe sana

Uzi wangu bora wa siku
 
Tunazo faculties za uhandishi vyuo vikuu, tunavyo vyuo vya kati vya ufundi, tuna SIDO, VETA, TIRDO, COSTECH, Nyumbu na wahunzi Tanzania. Sisi tulipaswa kuunda 80% ya viwanda vyetu vinavyozalisha bidhaa zetu na za kuexport. Brother hata vijiko na masufuria tunayaagiza kutoka nje. Nani katuroga?

Nickel haiwezi kutufikisha popote sisi kuliko chuma.
 
Quenched steel yenyewe vipi.
Ila nashukuru umefanunua Poa sana. Ile kemia f4 ilinitoaga nishai mana haikuwaga na kanuni ni full maelezo. Niliichukiaga sana. Sijui ni inorganic chemistry.extraction of metals and its oxides. Yaani kemia Nilikuwa naiona mchawi natamani ningekuwa na uwezo Wa kukomaa na fizikia and maths only.

Ndiyo, hayo madini yanaitwa "Iron ore" au kwa kiswahili ndiyo makinikia. Hayo madini yapo Liganga, Mchuchuma , Morogoro nk, Mamilioni ya tani.

Kinachotakiwa ni kujenga au kununua jiko la kufanyia "Smelting", smelting ni kitendo cha kuchuja chuma na udongo na kitendo hicho hufanyika ndani ya hiyo smelter inayoitwa "Blast furnace"--- humo ndani ya hiyo smelter wanaweka Coke (makaa ya mawe yaliyosafishwa) na limestones mawe ya chokaa kiasi fulani ndipo huwashwa kwa moto mkali ndipo hatimaye chuma hukingwa kutoka katika hiyo smelter kikiwa kama maji mekundu, chuma hicho huitwa "Pig iron", hicho chuma huwa bado ni "ghafi" yaani kimejaa uchafu hasa Carbon na hivyo kinatakiwa kupitishwa kwenye chungu kingine kiitwacho "Bessemer convertor" humo hicho chuma hupashwaa joto kali na Oxygen hupitishwa ili kuondoa hiyo Carbon, hapo sasa ndipo unapata aina mbalimbali za Chuma cha pua "steels" na chuma cha udongo cast irons kulingana na mahitaji, katika steels ndipo utapata Nondo, Shafts, Mabati ya kutengenezea mageti a grills , vyuma vya reli nk.

Hapo nimeandika kwa ufupi ili upate picha kidogo.
 
Ni kweli tuna mabilion ya tani za chuma zipo ardhini...hizi ndiyo zingetumika kujengea reli yetu ya kisasa ili kupinguza gharama; kama tungeamua kuanza kuchimba madini haya ya chuma kwanza hiyo reli ingetumia chuma hiki hiki cha Mchuchuma na Liganga!! Tena chenye ubora mzuri

Sasa kwa kuwa bunge letu limebakia kibigoyo basi tena!! Hizi hoja hakuna wa kuziibua...kwa sasa ni utekelezaji wa miradi mizigo kwa wananchi ndiyo inayopewa kipaombele... maisha yanazidi kuwa magumu...ajira kwa vijana wetu ndiyo kabisaa!!
 
Kesho tunazindua shamba la miti chato hiyo habari ya chuma haituhusu karibuni sana chato
Ni kweli tuna mabilion ya tani za chuma zipo ardhini...hizi ndiyo zingetumika kujengea reli yetu ya kisasa ili kupinguza gharama; kama tungeamua kuanza kuchimba madini haya ya chuma kwanza hiyo reli ingetumia chuma hiki hiki cha Mchuchuma na Liganga!! Tena chenye ubora mzuri

Sasa kwa kuwa bunge letu limebakia kibigoyo basi tena!! Hizi hoja hakuna wa kuziibua...kwa sasa ni utekelezaji wa miradi mizigo kwa wananchi ndiyo inayopewa kipaombele... maisha yanazidi kuwa magumu...ajira kwa vijana wetu ndiyo kabisaa!!
 
Haya sasa!

Si hivyo tu. Inabidi tuangalie pia tunataka kuitumia chuma yetu kwa bidhaa zipi. Je teknologia ya kuvitengeneza hivi vitu tunayo?

Hii 'dhana' yetu mbovu ya "hatuwezi" tutaiweka pembeni na kudhamiria kufanya kweli?

Soko la bidhaa za chuma lipo sana. Hivi vi-nchi vya Afrika vyote, hata kama vinakwenda taratibu, lakini vinaendelea. Vitahitaji bidhaa hizi katika maendeleo yao. Kwa nini chuma kitoke China kiuzwe rahisi kuliko hiki chetu kitakachotengenezwa hapa hapa Afrika? Kama AfCFTA itafanya kazi, kwa nini sisi tusiwe ndio nchi ya kuwapatia chuma hawa wengine wote katika umoja wetu?

"Kupanga ni kuchagua"; kama tukipanga na kudhamiria kwa dhati kufanya hilo ndilo liwe mchango wetu mkuu katika umoja huo, kwa nini isiwezekani? (kama tutaweza kupata uongozi wenye uthubutu), na sisi sote tutakuwa na 'mindset' hiyo hiyo ya uthubutu.
Kama tunataka maendeleo ya kweli ambayo yatawaudhi wazungu hatuna budi kutumia our uncommon sense, maana common sense ya hatuwezi, hatuna mtaji, hatuna technolojia ndiyo iliyotufikisha hapa tulipo. Lazima tuseme tunaweza na tuanze sasa. Viongozi wetu ni rahisi sana kuelekea kwenye dhahabu na almasi kwakuwa ni rahisi kupewa tofali la madini hayo kama zawadi binafsi. Kwenye chuma mambo hayo hakuna hivyo hayawavutii viongozi kuelekea huko. Lakini ni heri pesa yote ya dhahabu, almasi, germstones na nickel tukaitumia kwenye kwenye kusomesha watoto wetu kokote duniani kuhusu chuma na matumizi ya chuma, technolojia ya kutengeneza bidhaa za chuma na uchimbaji wa chuma. Baba wa taifa alishaianza hiyo kazi pale UFI ubungo, Mang'ula na arusha, SIDO nk lakini hatukumuelewa hata kidogo. Leo hii hata jembe la chapa jogoo linaagizwa kutoka china.
 
Hawa jamaa unaowaona wanashinda 'vijiweni' kila kona ya Tanzania,..., hawa ni 'vipuli' tele tunavyotakiwa kuvitumia, lakini kwa ushamba wetu, tunaviacha vinaozea hapo hapo.
Akitokea mtu (kiongozi), aseme anataka kuvitumia ipasavyo 'vipuli' hivi..., kwa nini visiweze kutumia kutimiza hayo uliyoandika hapa. Vyuo vya ufundi vipo, na vingi vingine vinaweza kujengwa kwa muda mfupi tu! Ndani ya miaka mitano, tunaweza kuwa na hali tofauti kabisa na ilivyo sasa. Ni swala la 'UTHUBUTU' tu na kuwa na dhamira halisi ya kutaka kutekeleza jambo. Hizi sifa kwa bahati mbaya viongozi wetu na sisi wenyewe hatujafanikiwa kuzitumia ipasavyo.
Kiongozi yuko tayari kuleta mzungu afundishe timu ya mpira kuliko kuleta mtaalamu wa kufundisha namna ya kutengeneza bidhaa za chuma kama matrecta. Badala ya kuuza bidhaa za dhahabu kama pete, mikufu, bangili, mikanda ya saa, makombe na mikanda ya mashindano mbalimbali sisi tunafurahia kuuza matofali ya dhahabu na malipo ya milabaha.
 
Ni kweli tuna mabilion ya tani za chuma zipo ardhini...hizi ndiyo zingetumika kujengea reli yetu ya kisasa ili kupinguza gharama; kama tungeamua kuanza kuchimba madini haya ya chuma kwanza hiyo reli ingetumia chuma hiki hiki cha Mchuchuma na Liganga!! Tena chenye ubora mzuri

Sasa kwa kuwa bunge letu limebakia kibigoyo basi tena!! Hizi hoja hakuna wa kuziibua...kwa sasa ni utekelezaji wa miradi mizigo kwa wananchi ndiyo inayopewa kipaombele... maisha yanazidi kuwa magumu...ajira kwa vijana wetu ndiyo kabisaa!!
Iko siku watu watalipa kodi ya kuvaa chupi. Wanakamua ng'ombe asiyelishwa wapate maziwa ya nunualia vyuma toka china.
 
7 Dec 2020

Western Australian iron ore exports remain strong in the face of the China row | ABC News

The bust that followed our mining boom will be on more than a few minds as the spat between Beijing and Canberra plays out. But dig a little deeper and it seems there's little to worry about.
Source : ABC News ( Australia)

Tafuta sasa na documentary za railroads Australia uone how remote wanapotoa hizo iron ore, line ya reli inayofuata chuma ina kilometa ngapi na ukubwa wa train zenyewe ili kupata advantages za economy of scales: wakati sisi kujenga kilometre 500 za reli tu hela mtaani aionekani kila mtu analia.

Ujafika kwenye investment za heavy metal na zenyewe zinahitaji umeme wa uhakika, supporting infrastructure kama reli jumlisha na gharama za kiwanda chenyewe. Ukishafanikisha hayo inabidi uwe nafuu ili uweze ku import maana uzalishaji wenyewe unaweza jikuta unahitaji tonne elfu kadhaa kwa mwaka ili ufikie break even point si ajabu ni kiwango ambacho Tanzania pekee akiwezi tumia kwa hali ya leo.

Mteja wako mkubwa kwa sasa ni serikali ya Tanzania ambae ndio huyu huyu kujenga SGR deni la nchi limeongezeka maradufu.

In other words kujenga kiwanda cha chuma unamwambia serikali akakope kiasi karibu na ujenzi wa phase mbili za SGR, halafu akitoka hapo atafute na hela ya kununua hiyo chuma ili ajenge SGR (wakati kuisha haraka kwa SGR kuna benefit zingine kubwa za kiuchumi).

Hakuna nchi itaikopesha Tanzania kujenga icho kiwanda cha chuma kwa uchumi wake wa sasa na kwa upande wa soko la dunia Tanzania aiwezi zalisha chuma ya ku populate ata soko la Kenya na Uganda tu kwa ushindani wa bei kutoka kwa wazalishaji wakubwa.

We Tanzanians need to be realistic kuliko kutoa demands tu.
 
Quenched steel yenyewe vipi.

Quenching ni mchakato wa kufanya steels ziwe ngumu na imara (hard and tough), hii inahusisha kuchoma steels hasa iron based steels, katika curie temperature na kisha kupozwa kwa haraka kwenye coolant, coolant inaweza kuwa maji, brine (salt water), oil, nk.

Sio Quenching tu bali kuna njia nyingi za ku treat steel ili kupata sifa zinazohitajika, mfano kuna Annealing--- ni kuchoma steel ngumu katika joto la Curie na kisha kuachwa ipoe polepole yenyewe ili iwe laini kwa ajili ya machining nk.

Kuna Tempering-- hii ni kuchoma steel iliyokuwa Quenched ili kupunguza internal stresses zilizojijenga ndani ya Chuma ili kisivunjike kama glass wakati wa matumizi.

Kuna Normalising--- huu ni mchakato wa kurejea tabia ya asili ya chuma baada ya kuchomwa na kupondwa wakati wa forging (forging ni upondsji wa steel kupata shape inayotakiwa). Katika Normalising chuma huchoma katika joto husika baada ya forging.

Njia zote hizo na zingine nyingi zinaitwa steel heat treatments. Elimu hii ipo deeper katika "metallurgy".

Sijui Watanzania na Waafrika kwa jumla tumekwama wapi, Mababu zetu wa zamani walikuwa wakitengeneza majembe, visu nk, duni katika zama zao, walichukua Iron ore na kuichoma pamoja na mkaa wa miti migumu kama mpingo nk, na hapo walipata chuma ghafi (pig iron) na baadaye chuma hicho walifukuta na kukifua (forging) kupata vifaa walivyohitaji, kama katika zama za giza za 1800 wazee wetu waliweza vipi zama zetu hizi za Mwanga na maendeleo ya Elimu sisi vitukuu tunashindwa kufukuta hata jembe kutokana na iron ore??, leo wahunzi wetu wanafukuta mashoka, majembe nk, kutokana na Steels kutoka ulaya, mfano utakuta muhunzi anachukua Spring ya gari na kuifukuta kupata panga nk, malighafi zote hizo ni kutoka nje, kifupi tumelemazwa na wazungu kwa kila kitu hadi kifikra.
 
Tafuta sasa na documentary za railroads Australia uone how remote wanapotoa hizo iron ore, line ya reli ina inayofuata chuma ina kilometa ngapi na ukubwa wa train zenyewe ili kupata advantages za economic scales: wakati sisi kujenga kilometre 500 za reli tu hela mtaani aionekani kila mtu analia.

Ujafika sasa kwenye investment za heavy metal na zenyewe zinahitaji umeme wa uhakika, infrastructure kama za reli jumlisha na gharama za kiwanda chenyewe. Ukishafanikisha hayo inabidi uwe nafuu ili uweze ku import maana uzalishaji wenyewe unaweza jikuta unahitaji tonne elfu kadhaa kwa mwaka ili ufikie break even point si ajabu ni kiwango ambacho Tanzania pekee akiwezi tumia kwa hali ya leo.

Mteja wako mkubwa kwa sasa ni serikali ya Tanzania ambae ndio huyu huyu kujenga SGR deni la nchi limeongezeka maradufu.

In other words kujenga kiwanda cha chuma unamwambia serikali akakope kiasi karibu na ujenzi wa phase mbili za SGR, halafu akitoka hapo atafute na hela ya kununua hiko chuma ili ajenge SGR (wakati kuisha haraka kwa SGR kuna benefit zingine kubwa za kiuchumi).

Hayo ni matumizi ya common sense, kuwa huwezi huwezi huwezi huna huna huna. Hata Rais ilimbidi atumie his uncommon sense kuhamia Dodoma kulikomshinda Nyerere, Mwinyi, Mkapa na Kikwete.
 
Tafuta sasa na documentary za railroads Australia uone how remote wanapotoa hizo iron ore, line ya reli ina inayofuata chuma ina kilometa ngapi na ukubwa wa train zenyewe ili kupata advantages za economic scales: wakati sisi kujenga kilometre 500 za reli tu hela mtaani aionekani kila mtu analia.

Ujafika sasa kwenye investment za heavy metal na zenyewe zinahitaji umeme wa uhakika, infrastructure kama za reli jumlisha na gharama za kiwanda chenyewe. Ukishafanikisha hayo inabidi uwe nafuu ili uweze ku import maana uzalishaji wenyewe unaweza jikuta unahitaji tonne elfu kadhaa kwa mwaka ili ufikie break even point si ajabu ni kiwango ambacho Tanzania pekee akiwezi tumia kwa hali ya leo.

Mteja wako mkubwa kwa sasa ni serikali ya Tanzania ambae ndio huyu huyu kujenga SGR deni la nchi limeongezeka maradufu.

In other words kujenga kiwanda cha chuma unamwambia serikali akakope kiasi karibu na ujenzi wa phase mbili za SGR, halafu akitoka hapo atafute na hela ya kununua hiko chuma ili ajenge SGR (wakati kuisha haraka kwa SGR kuna benefit zingine kubwa za kiuchumi).

Hakuna nchi itaikopesha Tanzania kujenga icho kiwanda cha chuma kwa uchumi wake wa sasa na kwa upande wa soko la dunia Tanzania aiwezi zalisha chuma ya ku populate ata soko la Kenya na Uganda tu kwa ushindani wa bei kutoka kwa wazalishaji wakubwa.

We Tanzanians need to be realistic kuliko kutoa demands tu.

Hivi ndugu unajua kiwanda cha chuma ni nini??--- na kitu gani kinafanyika humo kupata chuma??

Wazungu wanatuaminisha kwamba kujenga hicho kiwanda ni gharama kubwa na ni impossible lakini Wachina wanasomba tons of Iron ores kisha wanazalisha chuma kisha wanatuletea tena steels na bidhaa za chuma (machineries) kutoka katika hizo ores walizochukua/kupora huku kwetu.

Chuma ndiyo mapinduzi ya mechanizations na wazungu hawataki kamwe sisi waswahili tuzalishe chuma kwasababu tutapata maendeleo na tutaacha kuwategemea wao.
 
Quenching ni mchakato wa kufanya steels ziwe ngumu na imara (hard and tough), hii inahusisha kuchoma steels hasa iron based steels, katika curie temperature na kisha kupozwa kwa haraka kwenye coolant, coolant inaweza kuwa maji, brine (salt water), oil, nk.

Sio Quenching tu bali kuna njia nyingi za ku treat steel ili kupata sifa zinazohitajika, mfano kuna Annealing--- ni kuchoma steel ngumu katika joto la Curie na kisha kuachwa ipoe polepole yenyewe ili iwe laini kwa ajili ya machining nk.

Kuna Tempering-- hii ni kuchoma steel iliyokuwa Quenched ili kupunguza internal stresses zilizojijenga ndani ya Chuma ili kisivunjike kama glass wakati wa matumizi.

Kuna Normalising--- huu ni mchakato wa kurejea tabia ya asili ya chuma baada ya kuchomwa na kupondwa wakati wa forging (forging ni upondsji wa steel kupata shape inayotakiwa). Katika Normalising chuma huchoma katika joto husika baada ya forging.

Njia zote hizo na zingine nyingi zinaitwa steel heat treatments. Elimu hii ipo deeper katika "metallurgy".

Sijui Watanzania na Waafrika kwa jumla tumekwama wapi, Mababu zetu wa zamani walikuwa wakitengeneza majembe, visu nk, duni katika zama zao, walichukua Iron ore na kuichoma pamoja na mkaa wa miti migumu kama mpingo nk, na hapo walipata chuma ghafi (pig iron) na baadaye chuma hicho walifukuta na kukifua (forging) kupata vifaa walivyohitaji, kama katika zama za giza za 1800 wazee wetu waliweza vipi zama zetu hizi za Mwanga na maendeleo ya Elimu sisi vitukuu tunashindwa kufukuta hata jembe kutokana na iron ore??, leo wahunzi wetu wanafukuta mashoka, majembe nk, kutokana na Steels kutoka ulaya, mfano utakuta muhunzi anachukua Spring ya gari na kuifukuta kupata panga nk, malighafi zote hizo ni kutoka nje, kifupi tumelemazwa na wazungu kwa kila kitu hadi kifikra.
Ndo mana mtu akileta hoja nyepesi na dumavu za demand and supply, hatuna technologia, hatuna mitaji, nk. Babu zetu hawakuwaza kivivu namna hii.

Kupanga ni kuchagua lazima tuumie leo kwaajili ya kesho. Kinachoniuma hadi kesho ni kupoteza rasilimali zetu kuhamia Dodoma kwa sababu ambazo zingetatuliwa na uwekezaji kwenye mawasiliano, internet, whatsapp, simu, zoom, nk
 
Hivi ndugu unajua kiwanda cha chuma nini??--- na kitu gani kinafanyika humo kupata chuma??

Wazungu wanatuaminisha kwamba kujenga hicho kiwanda ni gharama kubwa na ni impossible lakini Wachina wanasomba tons of Iron ores kisha wanazalisha chuma kisha wanatuletea tena steels na bidhaa za chuma (machineries) kutoka katika hizo ores walizochukua/pora huku kwetu.

Chuma ndiyo mapinduzi ya mechanizations na wazungu hawataki kamwe sisi waswahili tuzalishe chuma kwasababu tutapata maendeleo na tutaacha kuwategemea wao.
Tena wachina wanakuwekea chuma kidogo sana kwenye bidhaa zao na kuchakachua na mafibers, plastics na maplastics. Yaani wanatufanya mazezeta. Unanunu gari la kichina lisilodumu
 
Back
Top Bottom