SoC01 Mwanamke mjamzito afanye hivi kuondoa mazoea ya kula udongo kutokana na madhara yake.

Stories of Change - 2021 Competition

ROJA MIRO

Member
Jul 19, 2021
52
56
Watu maarufu waliowahi kula udongo.
Mwaka 2014, Muigizaji mashuhuri wa Hollywood nchini Marekani, Shailene Woodley, aliwashangaza watu alipofichua kuwa yeye hula udongo kila siku kwa kupima kijiko kimoja.

Muigizaji huyo, aliyewahi kucheza filamu mashuhuri ya Descendants akishirikiana na George Clooney, alisema kuwa udongo ni moja ya vitu vyenye afya kwa mwili ambavyo yeye mwenyewe anaweza kula.

"nimegundua kuwa udongo unaweza kukupa afya nzuri mwilini. Najua wengi wanadhani kuwa mimi ni kichaa ninaposema kwmaba , udongo una uwezo wa kusaidia kusafisha mwili wako kutokana na madini mazito mwilini,'' alisema Woodley.

Anasema alijifunza kula udongo kutoka kwa dereva mmoja mwafrika. Baadhi ya marafiki zake hutengeza dawa ya kusugua meno kutoka kwa udongo ambao unaweza kumeza. Hata hivyo alisema ni muhimu kuwa udongo huo kabla ya kuliwa uwe safi.

Tabia ya kula mchanga au udongo inajulikana kwa kiingereza kama Geophagy.

1629790806401.jpeg


Shailene Woodley,Picha kutoka Mtandaoni.



SABABU YA WATU KULA UDONGO HUSUSANI WAJAWAZITO.


1.Kutamani kula udongo huashiria upungufu wa madini mwilini.
Daktari Bingwa wa magonjwa ya damu hapa nchini Clara Chamba anasema, takwimu zinaonesha kuwa takriban asilimia 25 ya watu ulimwenguni wana upungufu wa damu.

Anaeleza makundi yaliyo athirika zaidi kwa upungufu wa damu ni watoto wenye umri chini ya miaka mitano na wanawake walioko kwenye umri wa kuzaa. Anasema tafiti zilizofanyika nchini, mwaka 2017 zinaonyesha kuwa, asilimia 60 ya watoto chini ya umri wa miaka mitano wana tatizo la upungufu wa damu, huku Shinyanga ikiongoza.

Anasema ingawa sababu za kupungukiwa damu ni nyingi, zinaweza kugawanywa katika makundi makuu matatu ambayo kundi la kwanza ni upungufu wa damu utokanao na kuvuja damu. Daktari huyo anasema kuvuja damu huko hutokea kwenye ajali, vidonda vya tumbo, wakati wa hedhi kwa wanawake, saratani ya utumbo au wakati wa upasuaji.

Dk Chamba anasema upungufu mwingine wa damu unatokana na uboho kushindwa kuzalisha damu au kuzalisha damu kwa uhafifu, hali am bayo husababishwa na upungufu wa virutubisho vinavyohitajika kuzalisha damu yaani madini chuma, vitamin B12 na folic acid. Vile vile anasema magonjwa ya maambukizi kama vile ukosefu wa kinga mwilini, kifua kikuu na magonjwa sugu kama saratani, kisukari, shinikizo la damu la juu na magonjwa ya figo, huchangia tatizo.

Anaelezea kuwa kwa kawaida seli nyekundu za damu huishi kwa muda wa siku 120 hivyo hitilafu zinapotokea kwenye seli hizi, mwili hulazimika kuzitoa mapema kwenye mzunguko wa damu kabla ya kutimiza siku hizo 120. Lakini pia anasema baadhi ya magonjwa hayo, mtu huzaliwa nayo. Mfanoo mzuri ni ugonjwa wa selimundu.

Anasema miongoni mwa mambo yote hayo yanayosababisha upungufu wa damu, upungufu wa madini chuma una mchango mkubwa katika upungufu wa damu. Asilimia kubwa ya watu wenye upungufu wa damu mara nyingi hukutwa na upungufu wa madini chuma. Upungufu wa madini chuma hutokana na lishe hafifu, matumizi makubwa ya madini chuma ndani ya mwili hususani wajawazito, watoto na kuvuja damu muda mrefu.

Hedhi zisizo za kawaida na vidonda vya tumbo, huchangia tatizo. Anasema watu wengi husumbuliwa na upungufu wa damu kutokana na kutokuwa na mazoea ya kula mlo kamili anasema madini chuma hupatikana kwa wingi kwenye mboga za majani, dagaa, nyama na maini. Anaelezea dalili mojawapo ya upungufu wa madini chuma ni kuwa na hamu ya vitu visivyo vya kawaida, mfano, hamu ya kula udongo au hamu ya kula barafu.

1629790931876.jpeg

Picha kwa hisani ya mwananchi.co.tz ikimuonesha mfanyabiashara wa Udongo.


MADHARA YA KULA UDONGO.
Wanawake wanaopenda kutafuna udongo maarufu kwa jina la pemba na hasa wakati wa ujauzito wanapaswa kufikiria mara mbili kabla ya kufanya hivyo.Hii ni kutokana na watafiti nchini kubaini kuwa viwango vya madini ya kemikali katika udongo huo nchini vimezidi kipimo kilichowekwa na Shirika la Afya Duniani (WHO).

Utafiti uliofanywa katika mikoa 12 ya Tanzania na wanasayansi kutoka Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Bugando (Cuhas-Bugando) wakishirikiana na wenzao kutoka Canada na Marekani, umebaini madini kama vile lead (risasi), arsenic, cadmium, nickel na aluminiamu katika udongo huo yanahatarisha afya za akinamama hao na watoto ambao hawajazaliwa.

Utafiti huo ambao umekamilika umefanywa kwa kipindi cha miaka mitano katika mikoa ya Singida, Rukwa, Lindi, Dodoma, Mbeya, Kusini Pemba, Mara, Morogoro, Kigoma, Kilimanjaro, Tanga na Ruvuma.

Hata hivyo, mtafiti mkuu katika utafiti huo, Elias Nyanza kutoka Cuhas amesisitiza kuwa wao wamejikita katika kuchanganua udongo unaouzwa katika masoko.

Alisema utafiti huo uko katika mchakato wa kuchapishwa katika majarida ya kisayansi kimataifa.

“Tunashauri ulaji wa udongo huu uzuiwe hadi pale walaji watakapohakikishiwa usalama wao kiafya,’’ alisema Nyanza ambaye ni mtaalamu wa afya ya mazingira kutoka Shule Kuu ya Afya ya Jamii, Cuhas-Bugando. Nyanza alishirikiana na wataalamu kutoka Chuo Kikuu cha Colorado Denver cha Marekani na cha Calgary, Canada. Alisema madini waliyoyabaini kama vile risasi, cadmium na arsenic tayari yameorodheshwa na shirika la Marekani la viambata vyenye sumu na magonjwa.



Mtafiti huyo alisema madini hayo yanajulikana kwa kusababisha madhara kiafya na hasa kwa mama na mtoto, hata yakiwa katika kiwango kidogo. “Madini mengi ya kemikali, hasa yale tuliyochanganua kutoka kwenye udongo unaoitwa pemba yako katika viwango vya juu kuliko inavyotakiwa katika miongozo ya Shirika la Afya Duniani,’’ alisema.

Nyanza alisema, “Kuna wanawake tulikuta wanakula udongo wenye viwango vya madini hayo kufikia 50 micrograms per litre hadi 60 micrograms per litre, lakini WHO inasisitiza kuwa madini haya yanakuwa salama pale yanapotumika katika viwango vya 10 micrograms per litre.’’

“Ulaji wa udongo huu unaongeza hatari ya wanawake kuzaa watoto wafu, wenye uzito mdogo, njiti na hata wakati mwingine kusababisha watoto kuzaliwa wakiwa na hitilafu za kimaumbile,’’ alitahadharisha Nyanza.

Mkemia mkuu wa Serikali, Profesa Samwel Manyere amependekeza watafiti hao wachukue sampuli walizozipata katika utafiti na kuziwasilisha katika ofisi yake ili hatua za kuingilia kati suala la udongo huo zitekelezwe ipasavyo na mamlaka zinazohusika.

“Sisi katika maabara ya mkemia mkuu bado hatujafanya utafiti kama huo. Ila tuna teknolojia ya kuweza kubaini hicho wanachodai wamekuta katika udongo huo. Wataarifu walete sampuli walizokusanya ili nasi tujiridhishe kwanza,’’ alisema Profesa Manyere alipozungumza na mwandishi wa gazeti hili ofisini kwake jijini Dar es Salaam kuhusu utafiti huo.

“Mojawapo ya madini yanayotajwa hapo ni risasi ambayo kweli ni hatari kwa afya. Sisi tuko katika mchakato wa kuyawekea miongozo lakini si katika ulaji wa udongo.”

1629791103337.jpeg


Picha kwa hisani ya Mwananchi.co.tz
Muandaaji wa udongo akionekana akiandaa udongo huku amekaa hapohapo,akionekana amevaa nguo ambazo sio safi na jasho huenda likawa linamtiririka hali inayoonesha usalama wa afya ni mdogo.


MAENEO YA UCHIMBAJI DHAHABU.

“Hatari zaidi tuliibaini kwa wanawake wanaokula udongo unaotengenezwa kutoka ardhi iliyopo maeneo ambayo kuna shughuli za wachimbaji wadogo wa dhahabu,’’ alisema Nyanza.

Mwaka 2014, utafiti mwingine uliofanywa katika maeneo yenye shughuli za uchimbaji madini ulionyesha kati ya wanawake 115 walioshirikishwa, asilimia 69 walinunua udongo (pemba) huo kutoka kwenye maduka na asilimia 31 walikula udongo maarufu kama kichuguu. “Kwa pemba na kichuguu, utafiti huo uligundua viwango vikubwa vya arsenic, chromium, shaba, chuma, manganizi, nickel na zinki. Viwango vya cadmium na zebaki vilikutwa zaidi katika sampuli za kichuguu,’’ watafiti walisema katika Jarida la BMC Pregnancy and Childbirth utafiti ulikochapishwa.

Katika utafiti huo, watafiti walishauri hatua za kiafya zichukuliwe kunusuru afya za akinamama wanaokula udongo unaozalishwa kutoka maeneo ya migodi.

“Hatua za kisera na programu za kuelimisha zichuliwe katika mazingira ya wachimbaji wadogo, wanawake wanazidi kula udongo na wanajiweka katika hatari kiafya,’’ wanaeleza watafiti katika mapendekezo yao.

Pia, walisema sababu zinazowafanya wanawake kula udongo zichunguzwe na elimu itolewe katika kukabiliana na hatari za kiafya.

Wengi wanaamini ulaji wa udongo huwasaidia kutatua changamoto za ujauzito kama vile kichefuchefu, upungufu wa madini ya chuma na wakati mwingine wanakuwa na hamu tu ya kuula.

Dk Latifa Kalinga kutoka Hospitali ya Mkoa ya Songwe, alisema kwa uzoefu wake wa kidaktari na mwanamke aliyewahi kuwa mjamzito, kula udongo ni kati ya changamoto zinazowakumba wengi. “Ujauzito huwa na changamoto nyingi. Wakati mwingine wanawake hupenda tu kula udongo. Wanaweza kula hata barafu katika jokofu, kutafuna mchele kilo nzima na mengine. Hii tabia inaitwa pica katika lugha ya kitaalamu,’’ alisema huku akisisitiza inapaswa washauriwe waache kwa kujiweka katika hatari ya kupata minyoo inayosababisha upungufu wa damu


Kipi kifanyike kuzuia kula Udongo na vitu vingine wakati wa ujauzito kwa wanawake?


VYAKULA


Ili kuepuka kuwa na upungufu wa damu anasema ni muhimu kuhakikisha mtu anakula mlo uliokamilika. Pia anashauri iwapo mtu ana dalili zozote za upungufu wa damu, aende hospitali kwa ajili ya uchunguzi zaidi.



MAJANI YA MABOGA.

Mboga za maboga zinatokana na mmea wa maboga. Mboga za maboga huliwa sana na wanyakyusa na wasafwa mkoani Mbeya. Watu wengi wanakula bila kujua faida zake kiafya. Waingereza huita pumpkin leaves.Mboga za maboga zina virutubisho vifuatavyo vitamin A, C, E, B6, calcium, Thiamine, Riboflavin, Niacin, Chuma, Protini, Shaba, Potassium, Magnesium, Phosphorus, manganizi, Nyuzi Lishe na Folic acid.

Wataalamu husema kwamba madini ya chuma yanahitajika sana kwa mama mjamzito na ndio maana hupelekea kula udongo,kwa sababu kwenye udongo kunapatikana madini hayo,hivyo kwa vile madini hayo pia yanapatikana kwenye majani ya maboga basi akila hupunguza uwezekano wa kula udongo.

1629791257172.jpeg

Picha kutoka muaandaaji wa makala hii.


JINSI YA KUPIKA MAJANI YA MABOGA.

MaHITAJI:

1.Majani ya maboga fungu hata 2 kutegemeana na ukubwa wa familia.

2.Hoho.

3.Kitunguu maji

4.Karoti

5.Mafuta ya kupikia

6.Karanga za kusaga(kipome) kwa wenzangu wa nyanda za juu kusini.

7.Chumvi



JINSI YA KUPIKA:


Chambua,osha vizuri halafu katakata mboga zako.

Chukua sufuria weka mboga yako,weka na mafuta ya kupika kiasi ukitakacho.

Andaa kitunguu,hoho,karoti pia weka vyote kwa pamoja juu ya mboga.

Weka chumvi na maji kiasi yatakayo tosha kuivisha mboga na karanga utazoweka baadae,ila yasizidi mboga,maana mboga ya majani INA tabia ya kunywea au kusinyaa ikichemka.

Bandika jikoni,baada ya dk 8 angalia kama viungo ulivoweka vimesinyaa.

Geuza mboga yako iache iive kama dk 5 tena.

Baada ya hapo weka karanga zako kulingana na wewe unavopenda(kama Mimi napenda karanga nyingi kwenye hii mboga).unapoweka unakoroga mpka zichanganyike na mboga vizuri.

Iache mboga iendelee kuchemka kama dk 5 usiifunike,maana karanga INA tabia ya kushika chini ya sufuria,koroga ili zisishike chini.

Hakikisha harufu ya karanga ile mbichi haisikiki,mboga yako itakuwa tayari kwa kuliwa.

1629791306393.jpeg




MATUMIZI YA DAWA.

Iwapo mhusika ana magonjwa sugu, afuatilie matibabu yake na kufanya uchunguzi wa mara kwa mara. “Unapokutwa na upungufu wa damu, hakikisha unafanya uchunguzi zaidi kujua chanzo, na usitumie dawa ovyo bila kujua chanzo kwa kuwa si kila upungufu wa damu unatibika kwa kutumia dawa za kuongeza madini chuma,” anasema .

Dk Chamba anashauri kwamba, endapo mgonjwa amepewa dawa za kuongeza damu, afuate masharti na azitumie kama inavyotakiwa
 
Back
Top Bottom