mstaafrika
Member
- Jan 3, 2017
- 10
- 2
Sisi kama wa Tanzania, tumejikwaa kiakili na kimtazamo pale tulipodhani Mapinduzi pekee na ya mwisho ni yale yaliyofanyika Zanzibar miaka kadhaa iliyopita.*
*Mtizamo huu kwa kiasi kikubwa umetuathiri sana, umeweka ukomo wa kufikiri, tumesahau Kuwa Mapinduzi ni lazima yaendelee, tumebaki kuyaenzi mapinduzi kwa kupumzika majumbani mwetu leo na wengine kuhudhuria katika viwanja kadhaa kusikiliza hotuba za 'Watawala'.*
*Hii si sahihi bado tunahitaji Mapinduzi zaidi ya kifikra, Mapinduzi dhidi ya 'mkoloni Mweusi',*
*Tumesherekea Mapinduzi tukiwa na fikra ambazo hazijapinduliwa kuutambua ubaya na udhalimu wa 'Mkoloni mweusi'*
*moize_zoisite*